A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, November 2, 2018

Gwiji wa zamani wa Arsenal Robert Pires atua nchini kunogesha kampeni ya Barclays ya Superfans


Gwiji wa  zamani wa timu ya Arsenal ya Uingereza Robert Pires akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  Dar es Salaam leo ikiwa ni mwaliko kwenye uzinduzi wa kampeni ya Benki ya Barclays Tanzania iitwayo Superfans inayozinduliwa leo inayompa mteja wenye akaunti ya biashara au anayetumia kadi kufanya manunuzi mara nyingi kipindi cha kampeni  fusra ya kujishindia bahati nasibu ya safari ya Uingereza kushuhudia mechi moja mubashara ya ligi Kuu ya Uingereza.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania Aron Luhanga akiongea na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere  Dar es Salaam leo baada ya kuompokea gwiji wa zamani wa timu ya Arsenal ya Uingereza Robert Pires (kushoto), aliyealikwa na benki hiyo nchini kuzindua kampeni ya wateja iitwayo Superfans, inayomwezesha mteja anayemiliki akaunti  ya biashara au anayetumia kadi ya Barclays kufanya manunuzi mara nyingi kuzawadiwa safari  ya Uingereza kushuhudia  mechi  mubashara ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Gwiji wa Zamani wa timu ya Arsenal ya Uingereza Robert Pires (kulia), akimsikiliza Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa BBT Aron Luhanga mara baada ya kuwasili. Katikati ni Meneja wa mchezaji huyo, Laura Smit.
Gwiji wazamani wa timu ya Arsenal ya Uingereza Robert Pires (kushoto ) akipokea maua mara bada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kiamataifa  wa  Mwalimu Nyerere jijini Dar es  Salaam leo ikiwa ni mwaliko kwenye uzinduzi wa kampeni ya Benki ya Barclays Tanzania (BBT iitwayo Superfans  inayompa mteja anayemiliki akaunti ya biashara au kutumia kadi ya Barclays kufanya manunuzi mara nyingi  kipindi cha promosheni fursa ya kujishindia safari ya kwenda Uingereza kushuhudia mechi moja mubashara ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Gwiji wa zamani wa timu ya Arsenal ya Uingereza Robert Pires (kulia) akiangali ngoma ya asili mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Dar es Salaam leo ikiwa ni mwaliko  kwenye uzinduzi wa kampeni ya Barclays iitwayo Superfans inayompa mteja anayemiliki akaunti ya  biashara au kutumia kadi ya Barclays kufanya manunuzi mara nyingi kipindi cha kampeni fursa ya kujjishindia bahati nasibu ya kusafiri kwenda uingereza kushuhudia mechi moja mubashara ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive