Meneja Rasilimali Watu wa
Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi, akishikana mikono na mlezi wa
watoto katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia
(Nyumba ya Furaha), Sista Irene Kafuka (kushoto) wakati akikabidhi msaada wa
magodoro 20 ambapo pia walilipia bima za
afya ya NHIF kwa watoto wote 46 wa kituo
hicho ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha
Siku ya Wanawake Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha
watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), wakibeba
moja ya magodoro 20 waliyopewa msaada na Kampuni ya Tanga Cement katika hafla
ambayo pia kampuni hiyo ililipa bima za afya ya NHIF kwa watoto wote 46 wa kituo hicho kwa muda wa
mwaka mmoja ikiwa ni sehemu ya matukio
ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
kituoni hapo mjini Tanga jana. Katikati kushoto ni mlezi wa kituo, Sista Irene
Kafuka na Meneja Rasilimali Watu wa Tanga Cement, Diana Malambugi.
Mmoja wa wafanyakazi wa
Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Nancy Mkoyogo (kulia) akishikana mikono na
mlezi wa watoto katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della
Gioia (Nyumba ya Furaha), Sista Irene Kafuka (kushoto) wakati wakikabidhi msaada
wa magodoro 20 pamoja na kulipia bima za afya ya NHIF kwa watoto 46 wa kituo hicho ikiwa ni sehemu
ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake
Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana.
Ofisa Masoko na Mawasiliano
wa Tanga Cement, Hellen Maleko (kulia), akigawa chakula kwa watoto kituoni hapo
jana katika hafla hiyo.
Meneja Rasilimali Watu wa
Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi (wa pili kulia), akizungumza
na baadhi ya watoto wanaolelewa katika
kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya
Furaha), huku mlezi wa watoto kituoni hapo Sista Irene Kafuka (kulia),
akiangalia.
Mmoja wa wafanyakazi wa Tanga
Cement, Changwa Mjella, akisaidia kumlisha chakula mmoja wa watoto wanaolelewa
katika kituo hicho wakati wa tukio hilo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa
katika kituo hicho akionyesha umahiri wake wa kusakata muziki wa kizazi kipya
katika hafla hiyo. (Picha zote na Mgongos Photography)
0 comments:
Post a Comment