A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, March 15, 2018

WADAU WAZIDI KUJITOKEZA KUCHANGIA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR ES SALAAMMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea Tani 120 za Saruji ambazo ni sawa na Mifuko 2,400 ya saruji kutoka kwa Vyama vya ushirika 27 vya Mkoa huo vilivyoguswa na kempeni ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Dar es salaam.
CEMENTMifuko hiyo 2,400 ina uwezo wa kufyatua Tofali 70,000 ambazo zitejenga ofisi 14 za kisasa kwaajili ya Walimu. 


Akipokea mifuko hiyo  Makonda amesema shughuli ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri  ambapo amewashukuru wadau wote wanaoendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi na mwisho wa siku tuwe na wataalamu wa kutosha.

IMG_9728
kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es salaam Bwana Tumaini Wilfred amesema wameguswa Sana na jitiada zinazofanywa na RC Makonda kwenye kuboresha mazingira ya walimu ndio maana wameona na hao Kama ushirika wasibaki Nyuma  jambo hilo jema linalolenga kuleta ukombozi wa fikra.


Aidha Bwana Tumaini amesema Ushirika utaendelea kuunga mkono kwa kila hali juhudi zinazifanywa na  Rc Makonda3Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive