Meneja Mpya wa Hoteli
ya Park Hyatt ya Zanzibar, Nicolas Cedro, akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana kuzungumzia mipango ya hoteli hiyo katika kuinua
vipaji vya vijana walio katika shule zinazofundisha masomo ya hoteli. Kushoto ni
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Park Hyatt Zanzibar, Milvas Burnice.
Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar imemtambulisha Nicolas
Cedro kama meneja mpya atakayeendesha hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano
iliyopo katika eneo la hifadhi malum ya UNESCO kisiwani humo katika mji wa
Stone Town.
Cedro ambaye analeta uzoefu mkubwa kutoka katika sekta
ya hoteli amefanya kazi katika hoteli zenye chapa maarufu duniani kama Hyatt,
Melia, La Manga and Marriott na pia ni mwanachama wa shirikisho la kimataifa la
wahusika wa masuala ya vyakula linalojulikana kwa kifaransa kama “La Confrerie
de la Chaine des Rotisseurs.” Cedro
ambaye ana Shahada mbili za masuala ya vyakula na uendeshaji hoteli kutoka chuo
kikuu cha hoteli kilichopo Nice nchini Ufaransa pia ana Shahada ya uzamili ya
uendeshaji wa hoteli kutoka katika chuo kikuu cha E Cornel.
Cedro alianza kazi kama mpishi akiwa nchini Hispania
na toka wakati huo ameshafanya kazi katika nchi mbali mbali duniani zikiwemo
Hispania, Ufaransa, Qatar, Yordani na Tanzania bara na kisiwani Zanzibar.
Meneja huyo anasifika kwa uadilifu wake katika uongozi na kuhamasiha ubora
katika kazi na pia anazungumza lugha za kifaransa, kiingereza na kihispania.
Katika kipindi cha miaka 25 ambacho amekuwa akifanya
kazi amewahi kupata tuzo mbali mbali za ubora za kimataifa ikiwemo ya “Mkahawa
Bora” Hoteli ya La Manga nchini Hispania na pia amewahi kupika kwa ajili ya
watu maarufu wakiwemo Rais wa zamani wa Ufaranza Jacques Chirac na Mfalme wa
Malaysia. Uzoefu wa Cedro, elimu, ujuzi wa lugha pamoja na ubunifu ni vitu
muhimu ambavyo meneja huyo atatumia katika kujenga sifa na ubora wa hoteli hiyo
na pia kwa wafanyakazi.
“Napenda kufanya kazi katika bara la Afrika na hasa
katika kisiwa cha Zanzibar. Ni mahali ambapo kuna mazingira mazuri na watu
wenye upendo. Nimeshafanya kazi Tanzania kwa zaidi ya miaka mitatu sasa katika
hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro kama mkurugenzi wa chakula na vinywaji,
Melia Zanzibar na sasa hapa Park Hyatt Zanzibar. Nikiwa Tanzania nimefanya kazi
katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro ya Dar es Salaam kama. Nimesikia
furaha kubwa sana kupata nafasi hii ya kuendesha hoteli hii na nategemea
kutumia ujuzi na uzoefu wangu ili kuleta ladha ya kipekee katika chakula na pia
huduma tutakazowapatia wateja wetu,” alisema Cedro.
Cedro ambaye alizaliwa mjini Nice nchini Ufaransa,
alianza kazi ya upishi akiwa kijana wa miaka 17 na hivyo anatambua umuhimu wa
kuibua na kulea vipaji vya vijana. Akiwa kisiwani Zanzibar Cedro anategemea
kushiriki katika shughuli za kijamii kwa kushirikiana na shule mbali mbali za
kisiwani hapo za mapishi ili kusaidia vijana wenye vipaji vya upishi waweze
kupata ujuzi wa kimataifa alio nao na hivyo waweze kujiendeleza katika fani
hiyo na kuitumia kama njia ya kujiinua kiuchumi.
Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar ni Hoteli ya kipekee na
yenye historia ndefu hasa kwa kuwa katika eneo maalum lililotengwa kama urithi
na shirika la kimataifa la UNESCO. Hoteli hiyo inatumia majengo mawili
moajawapo ni jengo ambalo lililojengwa
katika miaka ya 1847 hadi 1850 na aliyekuwa rafiki wa mtawala wa wakati huo
Sheikh Seyyid Said. Jengo hilo linalojulikana kama ‘Mambo Msiige’ ni mfano
mzuri wa majengo ya kitamaduni ya Zanzibar likiwa na mandhari ya kiarabu na
linasadikika kuwa ni imara kutokana na udongo wake uliotumika kujenga uliokuwa
umechanganywa na maelfu ya mayai.
Hoteli hiyo iliyosheherekea miaka mitatu toka kuanzishwa
kwake tarehe 8 Machi mwaka huu, imejijengea umaarufu mkubwa kwa kipindi kifupi kwa
wageni wa kimataifa na nchini. Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar inashiriki
ipasavyo katika kukuza sekta ya utalii kisiwani humo na kutangaza kisiwa cha
Zanzibar kama moja ya maeneo ya kipekee kwa utalii.
0 comments:
Post a Comment