A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, March 9, 2018

Tanga Cement yaendelea na udhamini wake Kilimanjaro Marathon

Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Bi. Mtanga Noor (kulia), akigawa maji kwa mmoja wa wakimbiaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika mjini Moshi hivi karibuni. Kampuni ya Tanga Cement ilitumia zaidi ya shs milioni 30 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Ofisa Mawasiliano wa Tanga Cement, Hellen Maleko (kulia) akimpooza kwa maji mmoja wakimbiaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika mjini Moshi hivi karibuni. Kampuni ya Tanga Cement ilitumia zaidi ya shs milioni 30 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Baadhi ya wakimbiaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon wakipita katika kituo cha maji cha Kampuni ya Tanga Cement wakati wa mashindano ya mwaka huu mjini Moshi, Kilimanjaro hivi karibuni.
Mmoja wa wafanyakazi wa Tanga Cement aliyeshiriki mbio hizo naye akipata maji kupooza koo wakati wa mashindano hayo mjini Moshi hivi karibuni.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Taga Cement akimpa maji mmoja wa wakimbiaji wa mbio hizo mjini Moshi mkoani  Kilimanjaro hivi karibuni.
Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Bi. Mtanga Noor (kushoto), akigawa maji na viburudisho vingine kwa baadhi ya wakimbiaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika mjini Moshi hivi karibuni. Kampuni ya Tanga Cement ilitumia zaidi ya shs milioni 30 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive