A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, February 7, 2018

WATEJA WA AIRTEL WALAMBA DUME

03Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania imezindua Promosheni ya Shinda na Smatika kupitia kifurushi cha yatosha chenye lengo la kuwazawadia Wateja watakaojiunga na huduma ya Bando za Yatosha Smatika Intaneti.

Akiongea leo katika uzinduzi wa Promosheni hiyo, Mkurugenzi wa  Masoko Airtel Tanzania ISACK NCHUNDA amesema promosheni hiyo inalenga wateja wa Intaneti ambao watanunua kifurushi cha bando ya Yatosha SMATIKA  Intaneti,ambapo watanufaika na huduma hiyo  hivyo ametoa hamasa kwa wateja kuendelea kutumia huduma za intaneti amabazo ni nafuu na rahisi.
04
Amesma huduma ya bando nafuu za Yatosha SMATIKA Intaneti ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana zilizolenga kutoa uhuru kwa mteja wa Airtel kote nchini kujiunga banddo la Intaneti KABAMBE wkati wowote.

"Mteja wa Airtel  anaweza kunufaika na Yatosha SMATIKA Internet kwa gharama nafuu zaidi ya hadi shilingi 200 na kujipatia MB 40,vilevile ofa hii inamwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elifu mbili pekee"Amesema Nchunda.
Nchunda amesema kuwa promosheni hiyo itakuwa ya  uwazi na wateja hawahitaji kujisajili ila anachotakiwa kufanya ni kuwa na laini ya Airtel na kuweza kujiunga na kifurushi hicho kwa kupiga *149*99# na kuweza kuchagua kifurushi.
02
"Mteja wetu anachotakiwa kufanya ni kuwa na laini ya Airtel tu halafu atajiunga kwenye kifurushi cha yatosha Smatika Intaneti kwa kupiga *149*99# halafu unachagua namba 5 Yatosha Smatika Intaneti,hapo utanunua bando ya siku au ya mwezi kadri uwezavyo na kuwa mmoja wa washndi wa zawadi zetu kabambe"Amesema mkurugenzi wa  Masoko Airtel Tanzania.

"Promosheni ya Sinda na Yatosha SMATIKA Inteneti itadumu kwa siku 30huku kukiwa na droo taatu kila wiki yaani Jumatatu,ajumatano na Ijumaa,ambapo droo za kila siku wateja 1000 wataweza kujishindia bando ya Intaneti yenye 1GB                 kila mmoja wakati kweye droo kubwa watakuwepo washindi 10 ambao watano kati yao watajishindia simu za Smatiphone na watano watajishindia moden"amesema Nchunda.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive