A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, November 16, 2023

WASHINDI WA DROO YA SITA YA Y9 MICROFINANCE WAPATIKANA

Meneja masoko wa taasisi ya kifedha Y9 microfinance Bi. Sophia Mang’enya (katikati) akizungumza na mshindi wa pikipiki droo ya sita  kwa njia ya simu Baraka Barazae mkazi wa Dar es Salaam ambaye amejishindia pikipiki na Robert Keraryo mkazi wa Butiama ambaye amejishindia simu janja. Hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bi. Pendo Mfulu.


Washindi wa Droo ya sita ya Y9 Microfinance wapatikana mshindi wa pikipiki ni Baraka Barazae mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam na mshindi wa simu Robert Keraryo Mkazi wa Butiama mkoani Kagera.


Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Masoko ya taasisi ya kifedha Y9 microfinance Bi Sophia Mang'enya ameeleza kuwa huu ni muendelezo wa Y9 microfinance kuchezesha droo kila wiki na kupata washindi wawili.


Alisema "Matamanio makubwa ya Y9 microfinance ni kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma za kifedha popote alipo, hilo ndio lengo kuu la kuanzishwa kwa Y9 microfinance".


Aligusia kuwepo kwa wimbi kubwa  matapeli wa mtandaoni na amewasihi wateja wa Y9 microfinance kuwa makini na wizi huo wa mitandaoni, amewasihi watanzania kuitumia Tehama  kwa maendeleo sio kutumia Tehama kufanya uhalifu. 


Alieleza namna ya kushiriki ni rahisi hakikisha umepakua app ya Y9 microfinance kisha kujisajili na kuanza kukopa na moja kwa moja utaingia kwenye droo hii baada ya marejesho.  


Kwa upande wake afisa  kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Pendo Mfulu ameeleza "kama bodi ya michezo ya kubahatisha nchini tumeridhishwa na namna ya uchezeshwaji wa droo hii na upatikanaji wa washindi.

Share:

Takwimu sahihi nyenzo muhimu mapambano dhidi ya Ukimwi

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa (USAID) Bw. Craig Hart (katikati) akiangalia, wakati mmoja wa wenye VVU akijisajili katika mfumo wa alama za vidole mara baada ya mkurugenzi huyo kukabidhi msaada wa kifaa hicho kwa hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Mfumo huo unasaidia kupata takwimu sahihi za wenye VVU, jambo ambalo ni muhimu katika kufanikisha utoaji wa huduma bora. Hafla hiyo iliyofanyika mkoani humo jana inakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) unaofadhili miradi ya kupabana na Ukimwi inayosimamiwa na (USAID)
Mkurugenzi wa mradi wa USAID Afya yangu kanda ya Kusini unaoendeshwa na Shirika la Deloitte, Dk Marina Njekela, akielezea utendaji na mafanikio ya mradi huo katika kutoa huduma bora kwa wenye VVU katika hafla hiyo Mjini Iringa jana.
Mwakilishi wa mabinti wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Lucy Michael Mpwage, aliyezaliwa na maambukizi ya ugonjwa huo akitoa ushuhuda pamoja na changamoto za unyanyapaa alizokumbana nazo katika vipindi tofauti vya maisha yake na jinsi huduma za miradi ya USAID inayoendeshwa na Shirika la Deloitte ilivyookoa maisha yake. Ilikua ni wakati wawakilishi wa mfuko PEPFAR, USAID, mashirika yanayosimamia utoaji wa huduma kwa wenye VVU pamoja na waandishi wa wabari wakitembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa jana, kuangalia mafanikio ya miradi hiyo .
Baadhi ya wanawake waliowezeshwa na Mradi wa Hebu tuyajenge unaoendeshwa na Shirika la NACOPHA wakishangilia wakati wa ziara ya wawakilishi wa PEPFAR, USAID wakitembelea katika ofisi za shirika hilo mjini Iringa jana.

Na Zuhura Rashidi, Iringa.

UWEPO wa takwimu sahihi za wenye VVU unachangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya mipango mikakati katika uratibu wa miradi ya kupambana na ukimwi imeelezwa mkoani Iringa jana.

Hayo yalisemwa na Maganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dk. Mohamedi Mang’ula wakati wa ziara ya wawakilishi wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na ukimwi (PEPFAR), pamoja na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) hospitalini hapo ili kuangalia huduma mbalimbali za utoaji tiba kwa wenye VVU zinazofadhiliwa na mfuko huo kupitia USAID.

Dk Mang’ula alisema hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa msaada wa kifaa cha kufanyia usajili wa wenye VVU kwa kutumia mfumo wa alama za vidole kilichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Bwana Craig Hart akishukuru ufadhili wa USAID uliochangia uboreshaji wa huduma za afya kwa wenye VVU hospitalini hapo.

Tunaipongeza Kampuni ya Deloitte inayoendesha miradi hii inayofadhili na Mfuko wa PEPFAR katika mkoa wetu kwani imeweza kutusaidia kupata mafanikio makubwa katika kufikia malengo ya 95;95;95 katika kutambua wenye VVU, waliotambuliwa kuanza kupata tiba na suala la kufubaza virusi vya ukimwi”, alisema.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Afya Yangu Kusini, Dk. Marina Njelekela alisema wamekuwa na safari ndefu ila yenye mafanikio lukuki katika kutekeleza miradi inayofadhiliwa na PEPFAR kwa kupitia USAID.

Alisema misaada inayotolewa na PEPFAR kupitia Shirika la USAID imesainia kuokoa maisha ya watanzania wengi katika kipindi hiki cha miaka 20 huku kukishuhudiwa uimarikaji mkubwa wa huduma kwa wenye VVU katika vituo mbalimbali nchini.

USAID Afya Yangu Kusini tunasharehekea miaka 20 kwa kuboresha miradi ya PEPFAR USAID, tukipitia hatua mbalimbali za kimaendeleo moja ikiwa ni kuwajengea uwezo watoa huduma za afya katika vituo mbalimbali."

Tumeboresha ubora wa utoaji huduma bora za VVU na Kifua Kikuu katika ngazi ya jamii, mwaka 2004 tukiwa na vituo vya kutolewa huduma 33 lakini kwa msaada wa PEPFAR kwa hadi mwaka 2023 tumeweza kufikisha vituo 676."

Deloitte pamoja na washirika wake wa kiufundi wa MDH na T-marc tunajivunia sana kusimamia miradi inayofadhiliwa na PEPFAR, mwaka 2004 aina ya wagonjwa tulioanza nao kwa sasa imebadilika kabisa, sasa wapo na furaha na matumaini, wamewezeshwa, hawajisikii unyanyapaa”, alisema Dk. Marina.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraa la Taifa la Watu Wanaoishi na UVVU Tanzania (NACOPHA), Bwana Deogratius Rutwatwa wanaoendesha mradi wa ‘Hebu Tuyajenge’ alisema moja ya mikakati ya malengo ya mradi huo ni kuhakikisha pamoja na mambo mengine watu wenye maambukizi ya VVU wanatambua hali zao.

Ofisa mtendaji huyo alizungumzia suala la unyanyapaa kuwa moja ya changamoto inayosababisha watu wengi wenye VVU kushindwa kujitokeza kupata huduma za upimaji na kuunganishwa kwenye vituo vya tiba.

Baadhi ya huduma tunazozitoa ni pamoja na elimu kwa wenye VVU kuhusu namna bora ya kujzuia maambukizi mapya, kutambua wenza na watoto wenye VVU hivyo kuwaunganisha kwenye huduma za upimaji na kutoa usaidizi juu ya matumizi sahihi ya dawa za ARV’s."

Kwa namna ya kipekee niupongeze Mfuko wa PEPFAR kupitia USAID kipindi hiki unapotimiza miaka 20 kwa mafanikio na jitihada zake katika kupambana na janga la ugonjwa wa ukimwi hapa Tanzania”, alisema.
Share:

BENKI YA MWANGA HAKIKA YAJA NA “PINK MWANAMKE ACCOUNT” KUWAWEZESHA WANAWAKE KUTIMIZA MALENGO YA KIFEDHA

 -Wateja kupata uhakika wa kuweka akiba na kufurahia faida kwenye amana zao


Benki ya Mwanga Hakika Limited imekuja na huduma ya Pinki Mwanamke Account ambayo itawawezesha wateja wanawake kuweka akiba huku wakipata faida mbalimbali ikiwamo kupata faida ya kwenye amana zao.

Akaunti hii ni rafiki kwa wanawake wa aina zote na ni mahususi kwa wanawake wenye ndoto za muda mfupi na mrefu ambapo itawawezesha kuyafikia malengo hayo bila kutumia nguvu kubwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja wa Biashara wa Mwanga Hakika Bank, Judith Halinga alisema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasogeza huduma za kibenki karibu na wateja ili kuboresha Maisha ya watanzania.

“Benki yetu toka ilipopata hadhi ya kuwa benki rasmi ya biashara, tumekuwa mstari wa mbele kuendeleza ajenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwa kuja na huduma za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya kifedha,” alisema na kuongeza;

“Hii inathibitika leo ambapo tunazindua Pinki Mwanamke Account ambayo itaboresha huduma za kibenki kwenye soko.Kwa kupitia akaunti hii, wanawake nchini bila kujali kipato chao wanapata fursa ya kuhifadhi fedha zao kwa uhakika zaidi huku amana zao zikiwasaidia kupata faida mbali na kutunza fedha,” alisema.

Huduma hii imekuja wakati ambapo watanzania wengi wamekuwa na muamko mkubwa wa kufuatilia matumizi yao ya fedha. Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa Fin Scope ya mwaka 2023 inaonesha asilimia 77 ya watanzania wanafuatilia matumizi ya pesa zao.

Hii ina maana kwamba uelewa juu ya umuhimu wa kuwa na taarifa za mapato na matumizi umeongezeka hivyo ni muhimu kwa taasisi kuja na suluhu za kifedha zitakazowasaidia kufanikisha malengo yao.

Huduma hii inakuja na manufaa mbalimbali kama kufungua akaunti bure, hakuna makato ya mwezi na riba itakokotolewa na kulipwa kila mwezi.

Zaidi ya hilo, akaunti hiyo itawawezesha wateja kupata mikopo bila riba ambayo itawasaidia kufanikisha malengo ya muda mfupi bila kuharibu au kugusa amana zao (savings).

“Kama benki inayokua kwa kasi, tumeenda mbali zaidi na kuja na suluhu ambayo itakidhi mahitaji ya watanzania wengi zaidi.Tunaamini kwamba kupitia akaunti hii watanzania wengi zaidi bila kujali kipato chao watakuwa na uwezo wa kupatan huduma za kibenki na kufungua milango ya mafanikio,” alisema Mkurugenzi Mtendaji Jagjit Singh.

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu ya https://mhbbank.co.tz/





Ofisa Mtendaji Mkuu Kampuni ya JSG Travellers, Venancia Msita (kushoto), akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa akaunti ya Mwanamke Pinki na Kadi ya Pinki ya Mwanga Hakika Benki. Wapili Kushoto ni Meneja Mwandamizi Biasahara Benki ya Mwanga Hakika, Judith Halinga, Mwanasaikolojia, Sadaka Saidi na Mteja wa Benki hiyo, Graciana Mgeni.
Meneja Mwandamizi Biasahara Benki ya Mwanga Hakika, Judith Halinga (wapili kushoto),akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa akaunti ya Mwanamke Pinki na Kadi ya Pinki ya Mwanga Hakika Benki. kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu Kampuni ya JSG Travellers, Venancia Msita, Mwanasaikolojia, Sadaka Saidi, na Mteja wa Benki hiyo, Graciana Mgeni.
Share:

BARAZA LA FCT LARIDHIA UUNGANISHWAJI WA KAMPUNI YA SARUJI YA TANGA CEMENT NA TWIGA

 Mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Tanga cement PLC, Patrick Rutabanzibwa (katikati), akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam jana.Wengine ni Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Tanga Cement PLC, Pieter De Jager (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (wa pili kulia) na Raymond Mbilinyi, ye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi wa Tanga Cement pamoja na Katibu wa kampuni ya Tanga Cement , Quresh Ganijee

Mkurugenzi Mtendaji  wa  Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (wapili kushoto), akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam Wengine ni Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Tanga Cement PLC, Pieter De Jager (kushoto) Mwenyekiti wa bodi ya Tanga cement, Patrick Rutabanzibwa, (wa tatu kulia) na Raymond Mbilinyi, ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi wa Tanga Cement na Katibu wa kampuni ya Tanga Cement Quresh Ganijee

Baraza la ushindani nchini FCT limeridhia mchakato wa uunganishaji kampunu ya saruji ya tanga na ile ya twiga huku wanahisa wa kampuni ya saruji ya tanga nao wakipitsha maamuzi ya kuruhusu uuzaji hisa asilimia 73 za kampuni hiyo kwenda kwa mwekezaji heidberg ambaye ndiye mmiliki kiwanda cha twiga cement.

Maamuzi hayo yamepitishwa jijini Dare esl saam wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa  hisa wa kampuni ya saruji ya tanga Cement ambapo akizungumza Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo patrick rutabanzibwa amesema maamuzi ya wana hisa hao yametokana na hali ngumu inayo ipitia kampuni ya tanga cement ambayo imeshindwa kutoa gawio kutokana na deni ambalo lipo kwenye kampuni hiyo.

Kampuni hiyo pia ilielemewa na gharama kubwa za uzalishaji hivyo kujikuta wakihitaji zaidi uwekezaji kutoka kampuni ya heidelberg inayo miliki kampuni ya scancem ambaye ndie mmiliki wa kiwanda cha twiga cement ili kuingiza nguvu nakuhakikishia wateja kuwa na uhakika wakupata bidhaa hiyo bila kuwa na mashaka.

Kwa upande wake mmiliki wa kampuni ya african mauritus ambaye anamiliki hisa zaidi ya asilimia 73 ya kiwanda cha tanga cement reinhardt swart ambaye ndie mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha tanga cement amesema mchakato wa upatikanaji wa mwekezaji huyo utakamilika haraka iwezekanavyo ili kuongeza nguvu ya uzalishaji wa saruji ambapo pia ameiomba serikali kuimarisha upatikanaji wa nishati kwa uhai wa viwanda nchini

Hata  baadhi ya wana hisa wa kiwanda cha tanga cement ambao wameeleza kusikitishwa na kukosa gawio kwa muda mrefu huku wakibariki kuuzwa kwa hisa hizo na kuunganishwa kwa kiwanda cha tanga cement na twiga cement ili kuwa kiwanda kimoja kitakacho kuwa imara.


WARAKA WA MWEYEKITI
Utangulizi
Wanahisa,
Tuko hapa kuwasilisha taarifa ya biashara iliyokaguliwa ya Tanga Cement Public Limited Company (“Tanga Cement” au “Kampuni”) na kampuni zake tanzu (kwa pamoja “Kundi”) kwa mwaka unaoshia tarehe 31 Disemba 2021.

 Licha ya athari za janga la kimataifa la UVIKO-19, kundi limefanya vizuri kwenye viashiria vyake muhimu vya utendaji wa kifedha kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Disemba 2021 kama ilivyofafanuliwa kwenye eneo la mapitio ya Kifedha na Kiutendaji hapo chini.

Tunathibitisha kujitolea kwetu kwa wadau wote kupitia simenti yetu yenye ubora wa hali ya juu na klinka na pia usambazaji wetu ambao ni mchango wetu katika ukuaji endelevu na maendeleo ya Tanzania, kama ilivyo kauli mbiu yetu, “STRENGTH WITHIN”. 

Kampuni imeweka viwango vya juu sana vya afya na usalama katika maeneo yake yote ya utendaji na inaendelea kutekeleza sera za usalama katika sehemu ya kazi ili kulinda wafanyakazi wake na wakandarasi.

Mapitio ya Uchumi.
Ukuaji wa kampuni (Kundi) unaendelea kujikita kwenye ukuaji wa mahitaji ya simenti kwaajili ya soko la ujenzi Tanzania.

Wastani wa kiwango cha mfumuko wa bei kimeongezeka na kufikia asilima nne nukta mbili (4.2%) mwaka 2021 kutoka asilimia tatu nukta tatu (3.3%) mwaka 2020. Makadirio ya ukuaji wa pato ghafi la taifa la asilimia nne nukta tatu (4.3%) kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia nne nukta nane (4.8%) iliyorekodiwa mwaka 2020 (kama ilivyochapishwa na shirika la takwimu la taifa). 

Japo ongezeko la pato ghafi la taifa linaridhisha, uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na uimarishaji wa msingi wa wateja, vinabaki kuwa vichocheo vya msingi vya ufanisi wa biashara. Mpango wa Serikali wa kati wa sera za kifedha wenye lengo la asilimia tano (5%) umesaidia kuongeza uhitaji wa bidhaa zetu. 

Kampuni (Kundi) inabaki kuwa na matumaini chanya ya maendeleo chini ya mipango ya maendeleo ya miundo mbinu iliyopo kwenye dira ya Mpango wa Maendeleo wa Serikali wa mwaka 2025 na inategemewa
miradi itashika kasi mwaka 2022. 


Kampuni inaimani na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 na imedhamiria kufanya kazi pamoja na Serikali kwenye kukuza uchumi. Kampuni inao uwezo wa kufikia kiwango maalum cha mahitaji ya simenti nchini na kuendelea kujizatiti na uzalishai wa bidhaa za simenti zenye ubora wa hali ya juu. 

Mapitio ya Fedha na Utendaji Mapato ya kampuni kutokana na mauzo yaliongezeka kwa kiasi cha asilimia tisa (9%) na kuwa TZS 231bn kutoka TZS 213bn iliyopatikana mwaka 2020.

Sambamba na ongezeko la mapato, faida ghafi iliongezeka kwa asilima kumi na nne (14%) na kufikia TZS61.7bn kutoka TZS 54.2bn iliyopatikana mwaka 2020.

 Licha ya miradi mikubwa ya matengenezo ya mitambo yaliyofanyika
mwaka 2021 na kukatika kwa umeme mara kwa mara
kulikopelekea ongezeko la gharama za uzalishaji, pato la jumla
liliongezeka kufikia asilimia ishirini na saba (27%)
ikilinganishwa na asilimia ishirini na tano (25%) ya mwaka
2020.


Kampuni (Kundi) iliingia gharama za mara moja za
marekebisho yaliyosababisha kupungua kwa pato linalotokana
na uendeshaji kwa asilimia kumi na tatu (13%) na kufikia TZS
15bn kwa mwaka 2021 kutoka TZS 17bn kwa mwaka 2020.
Marekebisho hayo ni pamoja na kurekebisha Tanuri (Kiln) na
gharama zilizoambatana na marekebisho hayo ili kurudisha
uzalishaji katika hali ya kawaida.


 Gharama za kuachana na
operesheni za machimbo/migodi na kuanza kukodi huduma
hizo kutoka kampuni nyingine pia zimechangia kwenye
gharama hizo. 


Mapato kabla ya Riba, Kodi, Gawio na
Uchakavu (EBITDA) yalipungua kwa asilimia mbili (2%) kufikia
TZS 40.8bn kutoka TZS 41bn iliyopatikana mwaka 2020
iliyosababishwa haswa na gharama za kusitisha mikataba ya
wafanyakazi na gharama za matengenezo ya mitambo.


Kampuni (Kundi) ilirekodi faida kabla ya kodi ya TZS 3.8bn
mwaka 2021 ambayo imeongezeka kutoka hasara iliyopatikana
kabla ya kodi ya TZS 0.63bn iliyopatikana mwaka 2020.


Kuongezeka kwa faida kabla ya kodi ilitokana na kuongezeka
kwa faida ghafi na kupungua kwa hasara zitokanazo na
ubadilishaji wa fedha za kigeni na hasara ya thamani ya fedha
ambazo zinahusiana na deni la mkopo wa ujenzi wa kiln mpya
kuthaminishwa kwa Dola ya Kimarekani (USD) na riba
itokanayo na kukodisha vifaa na mali mbalimbali.

 Kampuni iliingia kwenye mkataba mpya uitwao ‘Standstill agreement’
kwenye mkopo wa PIC ambao ulizuia hasara zitokanazo na
ubadilishaji wa fedha za kigeni.


Matokeo hayo mazuriyamechagizwa na kuboreka kwa usimamizi wa hazina, mikakatiya ununuzi wa fedha za kigeni na viwango vya udhibiti wa mitaji
ya kazi. Kampuni (Kundi) ilipata faida baada ya kodi ya TZS
3.5bn mwaka 2021 ambayo imeboreka kutoka hasara baada
ya kodi ya TZS 2.1bn iliyopatikana mwaka 2020.


Fedha taslimu zilizotokana na shughuli za biashara zilipungua kwa asilimia
hamsini na nane (58%) kutoka TZS 48bn zilizorekodiwa mwaka
2020 na kufikia TZS 20bn mwaka 2021.

 Mtiririko wa fedha zilizotokana na shughuli za uendeshaji pia ulipungua kwa
asilimia hamsini na saba (57%) na kufikia TZS 18bn kutoka
TZS 43bn iliyo rekodiwa mwaka uliopita. 

Mapungufu yamtiririko wa fedha yamechangiwa na kushuka kwa faida ya
uendeshaji kwa asilimia kumi na tatu (13%) kutokana na
gharama za mara moja kama zilivyoainishwa hapo juu.


Kuongezeka kwa wadaiwa kwa TZS 5bn, kuongezeka kwa
malighafi kwa TZS 11bn, kupungua kwa madeni ya kibiashara
na madeni ya kimkataba kwa TZS 4bn na TZS 1bn kwa mwaka
2020 na 2021 mtawalia.

Kampuni inaendelea kujitoakuhakiksha mauzo, ufikishaji bidhaa sokoni na mipango yake ya kupunguza gharama za uendeshaji vinaendelea kuwa
suluhisho la kuongeza thamani ya wadau wake.

 Kampuni inabaki kuwa na matarajio chanya kwa mwaka 2022 licha ya
ushindani mkali na athari za UVIKO-19.

Mipango ya Serikali yakukuza uchumi kupitia maendeleo ya miundombinu na ukuzajiwa viwanda vya ndani vinatarajiwa kuchochea uzalishaji wa
ndani wa simenti na matumizi huku ikiendelea kuzuia utitiri wa
uingizaji wa simenti kutoka nje.
Gawio.


Kampuni haikutangaza gawio la muda mfupi au la mwisho wa
mwaka kwa wanahisa kwa mwaka 2021 na 2020. Maamuzi
hayo yamefanyika kwa kusudi la kua makini na rasilimali fedha
zilizopo ili kampuni iweze kujikimu na mahitaji mbalimbali katika
kipindi hiki cha kujikwamua kiuchumi kutoka kwenye athari
zilizosababishwa na UVIKO-19.


 Bodi imeamua kuendelea kutenga fedha zilizopo kwa ajili ya uendeshaji wa kampuni Bodi pia itafanya tathmini ya mwenendo wa kifedha katika
kipindi chote cha mwaka wa fedha wa 2022 kabla ya kufanya
uamuzi wa kutangaza gawio.

Pendekezo la kununuliwa kwa
kampuni na Scancem International DA Wanahisa
wanakumbushwa kuhusu tangazo la tarehe 27 Oktoba 2021 la
pendekezo la Scancem International DA kununua asilimia
68.33% ya hisa za Tanga Cement PLC kutoka Afrisam
Mauritius Investment Holdings Limited.

Taratibu zote zinazohusisha mamlaka mbalimbali zimekwisha fanywa. Pande
zote mbili zinasubiri maamuzi ya mamlaka hizo. Wanahisa
wataendelea kupewa taarifa za mchakato huu kadiri muda
unavyoenda.

Hitimisho
Katika kufanyia kazi malengo yake ya muda mfupi na mrefu,
kampuni inaendelea kuwashukuru wafanyakazi wake kwa
mapenzi yao na kujitoa walikokuonesha katika kipindi hiki licha
ya kuwepo kwa changamoto, na pia kwa wateja wake kutokana
na uaminifu wao kwa chapa yetu ya Simba simenti. Pamoja na
Tanzania kubaki kuwa mshirika mkuu katika Jumuia ya Afrika
Mashariki kwenye soko la ujenzi, uzalishaji wa simenti
unategemewa kuongezeka na Kampuni imejiweka tayari
kuchukua fursa hizo za ukuaji wa soko kwenye kanda.
Kwaniaba ya Bodi ya Wakurugenzi
Patrick Rutabanzibwa
Share:

Wednesday, November 15, 2023

Serikali yaupongeza Mfuko wa PEPFAR ukitimiza miaka 20 ya kurudisha matumaini ya wenye VVU nchini

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Halima Dendego, akipokea cheti cha shukurani kwa kutambua mchango wake katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na unyanyapaa kwa wenye VVU katika Mkoa wa Iringa, kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la maendeleo ya Kimataifa (USAID), Bwana Craig Hart, wakati wa ziara ya waandishi wa habari mkoani humo leo ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha miaka 20 ya Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR). Ziara hiyo, ililenga kuangalia mafanikio ya miradi inayohudumia wenye VVU na kusimamiwa na mashirika ya Deloitte, Nacopha na FHI360.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la maendeleo ya Kimataifa (USAID), Bwana Craig Hart, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi wa mradi wa USAID Afya Yangu Kanda ya Kusini Dk. Marina Njelekela, kwa kutambua mchango wa shirika hilo, likiwa ni moja ya Mashirika yanayofadhiliwa na Shirika la USAID katika kutoa huduma bora kwa wenye VVU. Hii ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha miaka 20 ya mfuko wa PEPFAR Mkoani Iringa leo. Wa kwanza kushoto ni muwakilishi wa PEPFAR nchini, Bi. Jessica Greene na Mkurugenzi Msaidizi wa USAID kitengo cha afya nchini, Bi. Anna Hofmann.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Bwana Craig Hart, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kusini, Bi. Dorothy Matoyo (kulia) kwa kutambua mchango wa shirika hilo, likiwa ni moja ya Mashirika yanayofadhiliwa na Shirika la USAID katika kutoa huduma bora kwa wenye VVU. Hii ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha miaka 20 ya mfuko wa PEPFAR Mkoani Iringa leo. Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa PEPFAR nchini, Bi. Jessica Greene na Mkurugenzi Msaidizi USAID kitengo cha afya nchini, Bi. Anna Hofmann.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la maendeleo ya Kimataifa USAID Craig Hart, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi wa mradi wa Rise project, Maende Makokha, kwa kutambua mchango wa shirika hilo, likiwa ni moja ya Mashirika yanayofadhiliwa na Shirika la USAID katika kutoa huduma bora kwa wenye VVU. Hii ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha miaka 20 ya mfuko wa PEPFAR Mkoani Iringa leo. Kushoto ni mwakilishi wa PEPFAR nchini, Jessica Greene na Mkurugenzi Msaidizi USAID Kitengo cha Afya nchini, Bi. Anna Hofmann.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la maendeleo ya Kimataifa (USAID), Bwana. Craig Hart, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi wa Shirika la FHI360, Bwana Bernard Ogwang, kwa kutambua mchango wa shirika hilo, likiwa ni moja ya Mashirika yanayofadhiliwa na Shirika la USAID katika kutoa huduma bora kwa wenye VVU. Hii ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha miaka 20 ya mfuko wa PEPFAR Mkoani Iringa leo
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Bwana Craig Hart, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi wa Shirika wa Nacopha, Bwana Deogratius Rutatwa, kwa kutambua mchango wa shirika hilo, likiwa ni moja ya Mashirika yanayofadhiliwa na Shirika la USAID katika kutoa huduma bora kwa wenye VVU. Hii ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha miaka 20 ya mfuko wa PEPFAR Mkoani Iringa.
Mratibu wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR) nchini, Bi. Jessica Greene akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Bw Craig Hart (katikati), akipozi kwa picha ya kumbukumbu mjini Iringa leo, na baadhi ya wawakilishi kutoka mfuko wa PEPFAR, USAID na Mashirika yanayoratibu miradi ya Ukimwi inayofadhiliwa na PEPFAR kwa usimamizi wa USAID.

*Zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 6 zatumika

*Mwaka 2022 pekee ikitumia Dola 450 milioni kupambana na maambukizi ya ukimwi nchini

Na Zuhura Rashidi, Iringa

SERIKALI ya Tanzania imeupongeza Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR), kwa jitihada zake katika kuleta matumaini mapya katika mikoa iliyoelemewa na mzigo mkubwa wa maambukizi ya ugonjwa wa HIV na Kifua Kikuu.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Halima Dendegu wakati wa ziara ya wawakilishi wa mfuko wa PEPFAR, Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), mashirika yanayotekeleza miradi ya ukimwi pamoja na waandishi wa habari mkoani humo wakitembelea miradi na vituo vinavyotoa huduma za ukimwi ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa mfuko huo.

Mkuu wa Mkoa huyo alisema Iringa ni mmoja wa mikoa iliyoathiriwa sana na maambuki ya VVU lakini kwa msaada wa PEPFAR chini ya Shirika la USAID imewawezesha kuwa na vituo vya huduma na tiba (CTC) 261 kutoka vinane vilivyokuwepo awali, huku 136 vikiendeshwa na USAID vilivyosaidia kuleta mabadiliko chanya katika utoaji elimu na huduma bora kwa kutumia vifaa vilivyoboreshwa na wahudumu wa afya wenye elimu na ujuzi katika utoaji wa huduma bora za afya.

Tafadhali pokeeni pongezi za dhati kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani, tunashukuru sana kwa misaada tunayoipokea kwani tunatarajia kushuka kwa maambukizi mapya kwa magonjwa ya ukimwi, kifua kikuu huku tukiendelea kupunguza unyanyapaa kwa wenye VVU."

Awali akizungumza mafanikio miradi ya PEPFAR inayosimamiwa na USAID, Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo nchini, Bwana Craig Hart alisema tokea mwaka 2003 serikali ya Marekali imetoa zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 6 ikiwa ni pamoja na Dola 450 Milioni kwa mwaka 2022 pekee katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi chini Tanzania.

Mwaka 2003 ni watanzania 1000 tu waliokuwa wakipokea dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV), leo wakati tukiadhimisha miaka 20 ya PEPFAR zaidi ya watanzania milioni 1.5 wananufaika na mpango huu wa tiba wa kuokoa maisha yao ikiwa ni asilimia 98 ya watu wanaoishi ya VVU."

Misaada yetu kwa watu wa Tanzania ni uwekezaji wa baadae, kwani kufikia mwaka 2050 robo ya watu wote duniani wataishi Afrika, nchini Tanzania theluthi mbili ya idadi ya watu wakiwa ni vijana chini ya umri wa miaka 25, hivyo kufanya uwekezaji katika kizazi kijacho kuwa ni jambo muhimu mno na lisiloepukika”, anasema Bwana Hart.

Naye Mratibu wa Mfuko wa PEPFAR nchini Bi. Jessica Greene alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kugusia maeneo manne ambayo mfuko huo umekuwa ukiyapa kipaumbele akiyataja kama; tiba, utoaji huduma bora, vituo vya afya na dawa za kupunguza makali ya VVU.

Tumeungana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha vipaumbele hivi vinafanikiwa na tutandelea kuhakikisha watu wenye VVU wanapata huduma boza za matunzo na tiba”, alisema Bi. Jessica.

Baadhi ya miradi inayofadhiliwa na PEPFAR chini ya usimamizi wa USAID ni USAID Afya Yangu Kanda ya Kusini unaolenga utoaji huduma jumuishi za matunzo, matibabu na kuzuia maambukizi ya VVU na kifua kikuu na kuboresha mazingira wezeshi ya utoaji wa huduma bora za afya katika mikoa sita ya kusini mwa Tanzania, huku mradi wa USAID Kizazi Hodari Kusini unaoangalia utoaji wa huduma jumuishi za watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na walezi wao ili kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima pamoja na vijana katika mikoa 11, miradi hii ikiendesha na Shirika la Deloitte.

Mradi mwingine ni ‘Epic’ unaotekelezwa na Shirika la FHI360 uKjjikita katika kufikia na kuendeleza udhibiti wa janga la VVU huku ukijihusisha katika kutoa msaada wa kitaalamu na huduma za moja kwa moja katika kuondoa vikwazo kufikia malengo ya 95-95-95 ukilenga makundi maalumu wakiwemo wasichana, wamama vijana, wanaume na wanawake walio katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU.

Aidha mradi wa ‘Hebu Tuyajenge’ ukishirikisha watu wanaoishi na VVU, unalenga katika kuongeza matumizi ya huduma za upimaji VVU, tiba na uzazi wa mpango mongoni mwa vijana balehe na wenye VVU ukitekelezwa na Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU Tanzania (NACOPHA).
Share:

Monday, November 13, 2023

Benki ya Absa yajizatiti katika kuwawezesha watoto wa kitanzania

Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Esther Maruma (wa pili kulia) akikabidhi fomu baada ya kusaini makubaliano yanayoashiria makabidhiano ya msaada wa fedha kiasi cha shilingi Milioni 10 kutoka benki hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Malezi mbadala ya Watoto wenye uhitaji la SOS Children’s Villages, Bi. Dorothy Ndege jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki yaAbsa, Bi. Nellyana Mmanyi na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.

ILI kuhakikisha watoto wa kitanzania wanafikia malengo yao ya kimaisha, Benki ya Absa Tanzania imetoa msaada wa kiasi cha Sh Milioni 10 ili kusaidia shughuli za uendeshaji wa Shirika la kimataifa linalojihusisha na malezi mbadala ya watoto lijulikanalo kama SOS Children’s Village.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya msaada huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa benki hiyo, Bi. Esther Maruma alisema msaada huo unaenda sambamba na lengo kuu la Benki ya Absa ambalo ni kuiwezesha Tanzania ya Kesho Pamoja, Hatua Moja Baada ya Nyingine ikiwa ni pamoja na kulikomboa Bara la Afrika Kiuchumi.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo katika hafla hiyo, Bi. Esther alisema, “Lengo la Benki ya Absa Tanzania ni kumuwezesha mtoto wa kitanzania kielimu, kiafya na kiuchumi hivyo ni imani yetu msaada huu utaleta chachu kubwa katika kuboresha maisha ya watoto wanaopata huduma mbalimbali katika kituo hiki”.

Akipokea msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la SOS Children’s Village, Bi. Doroth Ndege alisema shirika lao litaendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wa mtoto katika ngazi zote za jamii na hivyo kuwezesha ustawi endelevu wa jamii

Msaada tunaoupokea utasaidia juhudi za shirika letu katika uanzishwaji wa vikundi vya hisa 210 na kugusa takribani wananchi 3150 katika mkoa wa pwani na Dar es salaam na hivyo kuboresha uchumi wao na hatimaye kuboresha malezi katika ngazi ya familia”, alisema Bi. Doroth.

Naye Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bwana Aron Luhanga alisema benki ya Absa Tanzania imejidhatiti katika kubuni miradi mbalimbali inayolenga kuzifikia jamii zenye mahitaji na pia kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kijamii.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive