A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Wednesday, April 20, 2022

BENKI YA ABC YATOA VIFAA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 2 KUSAIDIA UJENZI WA CHOO CHA WAALIMU SHULE YA MSINGI MTAWALA MANISPAA YA MOROGORO.

 


Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga,(katikati), akikabidhi vifaa vya ujenzi wa Choo kwa Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya (wapili kutoka kulia), kulia Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati.

Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akimkabidhi taarifa ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi , Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.

Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.akizungumza katika hafla hiyo.

Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga akizungumza katika hafla hiyo.

Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati akisalimiana na waalimu waliojitokeza katika hafla hiyo.

Waalimu wa shule ya Msingi Mtawala. 

BENKI ya ABC Kanda ya  Morogoro, imekabidhi vitu vyenye thamani ya  zaidi ya milioni 2 katika kusaidia ujenzi wa Choo cha Waalimu katika Shule ya Msingi Mtawalaa Manispaa ya Morogoro ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia kuondoa changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu hususani katika upande wa vyoo.

Hafla hiyo fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, imefanyika leo Aprili 20/2022 katika shule hiyo huku tukishuhudia Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro , Chausiku masegenya ,akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Masegenya, ameishukuru Benki ya ABC  huku akibainisha kuwa msaada huo utagusa maisha ya Waalimu  wengi kwa miaka mingi ijayo.

“Wadau wetu muhimu na washirika kama Benki ya ABC ndio nguzo muhimu kwa mafanikio yetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao utasaidia katika kuweka mazingira rafiki kwa waalimu ya kupata huduma ya choo , lakini pia kuwaondolea adha ya kutoka nje kwa ajili ya kufuata huduma ya choo" Amesema Masegenya.

Mwisho, Masegenya, ametoa wito kwa taasisi zingine za kifedha na wadau wanaopenda kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya vyoo pamoja na mazingira ya kujifunzia katika shule za umma zilizopo Manispaa ya Morogoro  kujitokeza kwa wingi katika jitihada hizo.

Naye Diwani wa Viti Maalum anayetokana na Kata ya Mwembesongo, Mhe. Hadija Kibati, ameishukuru Benki ya ABC Kwa kuwaunga mkono kwenye sekta ya elimu kwa kuwapa vifaa hivyo  ambayo yatasaidia kuondosha changamoto ya choo cha walimu shuleni hapo.

Kwa upande wa Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo, amesema kwamba  utoaji wa misaada kwa jamii  ni sehemu ya dhamira endelevu ya benki hiyo katika kusaidia sekta za elimu na kuona benki hiyo inachukulia kwa uzito sana suala la uwekezaji kwenye sekta ya elimu.

Kalinga, amesema wametoa msaada huo ili kuunga mkono Serikali na  juhudi za wananchi na kurudisha kwao ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa na hamasa ya kutenegeneza miundombinu ya elimu kwa manufaa ya sasa na kizazi cha baadae.

“Benki yetu inajivunia kuona Taifa linapiga hatua kubwa kwenye sekta ya elimu ambapo kupitia sera ya serikali elimu bure imeongeza idadi ya wanafunzi lakini pia ufaulu ambao maendeleo yake yanaakiisi hadi kiwango chetu cha uchumi ambapo mwaka jana nchi iliingia kwenye uchumi wa kati” Amesema Kalinga.

“Tumejitolea kuhudumia watu, biashara na jamii kwa ujumla. Benki yetu ya ABC, tumeguswa na changamoto ambayo iliwasilishwa kwetu , dhamira yetu kwa jamii ni kuona ni kuona tunaunga mkono na  kusaidia juhudi za kielimu na ustawi wa wanafunzi wetu na shule kote nchini na sio kwa Manispaa hii ya Morogoro pekee,  hivyo ni muhimu zaidi tukiweka jitihada katika kuboresha mazingira ya vyoo shuleni ili sasa Waalimu waweze kuwa na mahala rafiki kwa kutumia na kuacha kutoka eneo lao kwenda mbali  na shule zao,  ABC tutaendelea kushirikiana na Serikali kwa kadri tunavyoweza kuguswa na changamoto katika jamii ” Ameongeza Kalinga.

Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mtawala, Mwl. Godfrey Binagwa , ameishukuru Benki ya ABC kwa msaada huo ambao wameutoa ambao utasaidia kuondoa changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo za uhaba wa choo cha walimu.

Vifaa hivyo vya ujenzi ambayo walikabidhi benki hiyo ni Mifuko 50 ya saruji, mchanga Lori 1, Kokoto Lori 1, Mawe Lori 1, Milango 2 ya mbao, Fremu 2 za milango, Tofali za block 400 pamoja na Mabati 70.

Share:

Wednesday, April 13, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKIANA NA TRC KUZINDUA UJENZI WA RELI TABORA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi  akiweka udongo kwenye jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora leo ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbalawa akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanian Mh Samia Suluhu.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Makame Mbalawa  akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi  alipotembelea banda laBenkihiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbalawa  akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi (kulia), wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Makame Mbalawa akiwa katikapicha ya pamojana wakuu wa idara kutoka taasisi mbalimbali


Tanzania Commercial Bank TCB) imesema itaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo  ili kuboresha uchumi wa Tanzania.


TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora mpaka Makutupora Mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa na Afisa  Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi  wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya tatu leo Mkoani Tabora

 Moshingi amesema, Tanzania Commercial Bank  ni benki kubwa nchini  na  wamejitoa na wameshiriki kwa hatua kubwa katika kuhakikisha shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanikisha mradi wa SGR Lot 4 kwa mafanikio makubwa.

“Tanzania commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC ni wenzetu hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio kwa mkoa wa Tabora,”amesema

“Kufanikiwa kwa mradi huu kutarahisha usafiri wa kutoka Tabora hadi Dar es Salaam kwa masaa sita, na treni ya mizigo kwa masaa kumi pia kutafungua fursa za kiuchumi kwa mikoa ya Tabora, Dodoma, Singida , Shinyanga hadi Mwanza,”amesema

Moshingi amesema, wananchi wa Tabora kwa sasa wataanza kukua kiuchumi, kwa kusafirisha mazao yao kwenda Dar es Salaam ambapo ndio soko kuu la biashara na usafiri utakuwani ni wa uhakika zaidi.

Amewahimiza wakazi wa Tabora kujipatia huduma Bora zinazopatika Tanzania Commercial Bank ili waweze kwenda na kazi ya Uchumi kupitia mradi huo "amesema

Moshingi ameeleza kuwa kwa Sasa Tanzania Commercial Bank ina matawi kila pembe ya Tanzania hivyo imejipanga vema kutoa huduma kwa watanzania pamoja na wageni kutoka nje
Share:

Sunday, April 10, 2022

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI RUANGWA

  
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Mkoani Lindi, Upendo Mfilinge akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Likunja Barnabas Kwangu wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka. Msaada huo ukiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kujitolea kusaidia jamii yenye uhitaji. Hafla ya kukabidhi msaada huo imefanyika katika Shule ya Msingi Likunja hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Mkoani Lindi, Upendo Mfilinge akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mwanafunzi wa Darasa la Sita wa Shule ya Msingi Likunja Shadia Mbochele wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka. Msaada huo ukiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kujitolea kusaidia jamii yenye uhitaji. Hafla ya kukabidhi msaada huo imefanyika katika Shule ya Msingi Likunja hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Mkoani Lindi, Upendo Mfilinge (wa pili kushoto) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mwalimu wa Afya wa Shule ya Msingi Likunja Happiness Amlima wakati benki hiyo ilipotembelea shule hiyo na kutoa msaada huo wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka. Msaada huo ukiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kujitolea kusaidia jamii yenye uhitaji. Hafla ya kukabidhi msaada huo imefanyika katika Shule ya Msingi Likunja hivi karibuni. Wengine pichani ni Meneja Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB tawi la Ruangwa, Mwichande A. Mwichande, mwengine ni Msimamizi wa Sheria na Miongozo wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Faraja Haule pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Barnabas Kwangu.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Mkoani Lindi, Upendo Mfilinge (wa pili kushoto) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ruangwa, Esha Chama wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka. Msaada huo ukiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kujitolea kusaidia jamii yenye uhitaji. Hafla ya kukabidhi msaada huo imefanyika katika Shule ya Msingi Likunja hivi karibuni.
Msimamizi wa Sheria na Miongozo wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Faraja Haule akikabidhi moja ya msaada wa taulo za kike kwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ruangwa wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Mkoani Lindi, Upendo Mfilinge akikabidhi moja ya msaada wa taulo za kike kwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ruangwa wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka.
Afisa Uhusiano wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Mkoani Lindi, Francis Saini akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ruangwa Zainabu Madina wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka. Msaada huo ukiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kujitolea kusaidia jamii yenye uhitaji. Hafla ya kukabidhi msaada huo imefanyika katika Shule ya Msingi Likunja hivi karibuni.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB tawi la Ruangwa, Mwichande A. Mwichande akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Ruangwa Monica Chacky wakati benki hiyo ilipotembelea shule hiyo na kutoa msaada huo wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka. Msaada huo ukiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kujitolea kusaidia jamii yenye uhitaji. Hafla ya kukabidhi msaada huo imefanyika katika Shule ya Msingi Likunja hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Mkoani Lindi, Upendo Mfilinge (wa tatu kulia) akikabidhi moja ya msaada wa taulo za kike kwa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Ruangwa Mwisio Tuyanje wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipotembelea shuleni hapo na kutoa msaada huo wakati wafanyakazi hao walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka. Wengine pichani ni Maafisa wa Benki ya CRDB, Walimu pamoja na Wanafunzi wa Shule hiyo.
Msimamizi wa Sheria na Miongozo wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Faraja Haule akikabidhi ya msaada wa taulo za kike kwa Mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Ruangwa Safina Omary Ally wakati wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Ruangwa walipoadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka.

Na Mwandishi wetu, Ruangwa

BENKI ya CRDB kupitia Wafanyakazi wa Benki hiyo Tawi la Ruangwa mkoani Lindi imetoa msaada wa taulo za kike katika kuazimisha siku ya Wanawake Duniani ambayo huazimishwa tarehe 8 ya mwezi wa tatu katika Shule ya Sekondari Ruangwa na Shule ya Msingi Likunja za wilayani humo.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Mkoani Lindi, Upendo Mfilinge alisema wametoa msaada huo ili kuwasaidia watoto wa kike kusoma kwenye mazingira salama hali itakayowasaidia kuongeza bidii kwenye masomo yao.

"UPATIKANAJI wa Taulo za Kike ni muhimu kwa maudhurio ya mtoto wa kike shuleni katika kuwawezesha wanafunzi wa kike kuhudhuria shule kikamilifu na kupata haki msingi ya elimu sawa na vijana wa kiume," alisema Bi Upendo.

Meneja huyo alisema kwamba ndani ya benki yao wamefanya hivyo wakiamini kuwa ukimuwezesha mwanamke umeiwezesha jamii na hivyo ndio moja ya siri kubwa ya mafanikio kwenye benki hiyo.

Nae Mwalimu wa Afya wa Shule ya Msingi Likunja, Happiness Amlima akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa uzinduzi wa Taulo za Kike shuleni hapo alisema wanafunzi wengi wa kike shuleni hapo huvaa vitambaa ambavyo sio salama kwa afya zao wawapo hedhini.

Pamoja na jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali bado mahudhuria ya watoto wa kike mashuleni hayaridhishi na hivyo kupelekea kutokufanya vizuri katika masomo yao, changamoto hiyo kwa kiasi kubwa imechangia watoto wengi wa kike wakati wanapoingia kwenye kipindi chao cha hedhi kutokuwa na uwezo wa kuwa na taulo bora za kike nakuwalazimu kukaa nyumbani na kushindwa kuja shuleni mpaka watakapomaliza." alisema Mwalimu Happiness.

Awali Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Ruangwa Mwisio Tuyanje amewashukuru wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Ruangwa kwa kuitembelea shule hiyo na kutoa msaada huo wakati ikiadhimisha siku ya mwanamke duniani inayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka.

Kwa kweli niwashukuru sana na kuwapongeza uongozi wa Benki ya CRDB tawi la Ruangwa kwa kutambua umuhimu wa huduma hii kwa mtoto wa kike kwenye shule zetu, nimefurahishwa sana kwa kujali na kutoa mahitaji haya ambayo ni muhimu kwa vijana wetu wa kike”Alisema Mwalimu Tuyanje.

Naye Msimamizi wa Sheria na Miongozo wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa Faraja Haule amezikumbusha taasisi mbalimbali kushiriki kusaidia shule ambazo zipo pembezoni zinazokosa fursa ya kupata misaada ya mara kwa mara ukifananisha na zile zilizopo mijini.

"Mara nyingi taasisi nyingi hushiriki kutoa misaada kwa shule zilizo mijini na kuzisahau shule zilizopo vijijini, ambazo wanafunzi wake wanatoka kwenye mazingira duni wenye uhitaji," alisema Bi Faraja Haule.
Share:

Wednesday, April 6, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK LAUNCHES NEW BRANCH MBAGALA CHARAMBE

Temeke District Commissioner Jokate Mwegello with Acting Chief Executive Officer of Tanzania Commercial Bank Moses Manyatta opening the curtain to mark the official launch of the Bank's new Branch opened at Mbagala Charambe in Dar es Salaam today.

Temeke District Commissioner Jokate Mwegello addressing various stakeholders and users of financial services during the Official Launch of the new Tanzania Commercial Bank Branch opened today in Mbagala Charambe, others pictured are Acting Chief Executive Officer of Tanzania Commercial Bank Moses Manyatta, Branch Manager Edward Mwoleka along with other Bank officials.

Acting Chief Executive Officer Moses Manyatta addressing various stakeholders, customers and users of financial services during the Official Launch of the new Tanzania Commercial Bank Branch opened in Mbagala Charambe.


Temeke District Commissioner Jokate Mwegello receiving a commemorative gift during the Official launch of the new Tanzania Commercial Bank Branch opened in Mbagala Charambe.


Temeke District Commissioner Jokate Mwegello receiving an ATM card during the Official Launch of the new Tanzania Commercial Bank Branch opened in Mbagala Charambe today.


Tanzania Commercial Bank Mbagala Charambe New Branch Manager Edward Mwoleka talking to various stakeholders, customers and users of financial services during the Official launch of the Branch







TANZANIA COMMERIAL BANK goes live in Mbagala with 12th branch in Dar es Salaam.


By A Special Correspondent

National lender Tanzania Commercial Bank (TCB) has upped presence in Dar es Salaam by opening the 12th branch in the country’s commercial capital and economic hub that went live yesterday in Mbagala.

Temeke DC Jokate Mwegelo graced the ceremony to unveil the newest outlet in the TCB stable that now comprises an extensive network of 85 branches across the country.

Speaking before its inauguration, Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi said the TCB Mbagala Branch is the fifth outlet to be launched by the oldest lender in Tanzania so far this year.

He said the financial inclusion investment in one of the most populous suburbs in Dar es Salaam makes the branches the bank has opened in the city this year to be two. The TCB Kigamboni Branch, which opened for business in March, was the first and the lender’s 11th in the region.

Apart from a blossoming population, which no operations expert can ignore, Mbagala also has a thriving and enterprising economy that lured TCB to come up with the mortar and brick presence idea in the area.

The venture is part of the transformation agenda of the bank and a key aspect of its endeavour to become fully fledged universal bank. Before the transformation journey kicked off in 2011, TCB had a limited branch network that mostly comprised dilapidated outlets.

“This is our 12th branch in Dar es Salaam that gives Mbagala residents the opportunity to join mainstream banking and conveniently enjoy our top notch services,” Mr Moshingi said.

He said the new outlet consolidates TCB position of being among the banks that have the widest branch networks in the market.

The ongoing transformation efforts have also made TCB to be among the ten top performing banks in the country. Its latest financials put the assets base at around TZS 1.18 trillion as to the end of 2021 and customers’ deposits, which the new branch will help to mobilise, standing at 729,137.

The lender said another four branches are lined up for opening before this year ends as part of the operational scheme to take its services closer to the people and strategically position itself to better and competitively serve the country.

“The Mbagala branch is the fifth we have launched in 2022. Branches already opened this year are Kigamboni, Mbinga, Usa River and Mpanda. Our plan is to expand our outreach in four new locations this year,” TCB noted in a presser.

DC Jokate lauded the bank for its inclusive finance zeal and championing financial inclusion for all saying it was in line with the government’s grand mission to make life better for all.

According to her, TCB should be emulated for its continued in-roads into the underserved areas like Mbagala and going for un-banked populations in many parts of the country.

Share:

Sunday, April 3, 2022

WAKAZI WA RUANGWA WAASWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI


Na Mwandishi wetu, Ruangwa

Tanzania itafanya Sensa ya Watu na Makazi mwezi Agosti mwaka 2022 katika siku itakayotangazwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yametanabaishwa na Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Mchumi-Tumsime Lazaro Mutta kwenye mahojiano maalumu na mwandishi wetu katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi.

Mchumi-Tumsime amesema "Kabla ya zoezi la kuhesabu watu wote watakaolala ndani ya mipaka ya nchi usiku wa kuamkia Siku ya Sensa, shughuli mbalimbali za maandalizi hufanyika ambazo hujumuisha utoaji elimu kwa lengo la kuuelimisha umma juu ya umuhimu wa Sensa ili kuhakikisha kila mmoja anatambua umuhimu wa kuhesabiwa na kuhamasika kuhakikisha kwamba anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu."

Aidha, Mchumi-Lazaro Muta ametumia fursa hiyo kuieleza jamii kuhusu lengo la Sensa ya Watu na Makazi, "Lengo la Sensa ya Watu na Makazi ni kupata taarifa sahihi za kidemografia, kijamii, kiuchumi na hali ya mazingira kwa lengo la kupata takwimu sahihi zitakazoiwezesha Serikali na wadau wengine kupanga kwa usahihi mipango ya maendeleo ya watu wake katika sekta mbalimbali za elimu, afya, hali ya ajira, miundombinu kama barabara, nishati na maji safi".

Ikumbukwe Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa katika moja hotuba zake kwa wadau wa Sensa ya Watu na Makazi amewataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na Kata kuhakikisha wanaongeza kasi katika uratibu wa maandalizi ya zoezi hili.

"Zoezi hili linatakiwa kutekelezwa kwa operesheni na kwa kipindi maalum kama ilivyokuwa katika miradi iliyojengwa kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19," alisema Mhe.Majaliwa.

Awali, Mchumi-Lazaro Mutta amewaasa wakazi wa Ruangwa kushiriki ipasavyo zoezi hilo "Wakati wa Sensa ya Watu na Makazi tunachotakiwa kufanya ni kumpa ushirikiano wa kutosha Karani wa Sensa atakapotembelea katika kaya kwa kujibu maswali yote atakayouliza kwa usahihi".
Share:

Friday, April 1, 2022

Absa Tanzania yahamasisha watanzania kuchanja chanjo ya Covid-19

Mkurugenzi wa Makampuni Makubwa na Uwekezaji wa Benki ya Absa Tanzania, Hugo Chilufya (wa tatu kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Shirika la Kimataifa la Mambo ya Afya la Fhi360 kusaidia kampeni ya kuhamasisha watanzania kupata chanjo ya Covid 19. Kutoka kushoto ni Mshauri Mwandamizi wa Fhi360, Theresia Mrema, Meneja Mahusiano ya Jamii wa Absa, Hellen Siria, Mkurugenzi Mkazi wa Fhi360, Waziri Nyoni, Mkurugenzi wa fedha wa Fhi360, Anselm Mmassy na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Masoko ya Kigeni wa Absa, Irene Rwegalulira.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Mambo ya Afya la Fhi360, Waziri Nyoni (wa tatu kulia) akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati Benki ya Absa Tanzania ikikabidhi msaada wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kusaidia kampeni ya kuhamasisha watanzania kupata chanjo ya Covid 19. Kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Masoko ya Kigeni wa Absa, Irene Rwegalulira, Mkurugenzi wa fedha wa Fhi360, Anselm Mmassy, Mkurugenzi wa Makampuni Makubwa na Uwekezaji wa Benki ya Absa Tanzania, Hugo Chilufya, Meneja Mahusiano ya Jamii wa Absa, Hellen Siria na Mshauri Mwandamizi wa Fhi360, Theresia Mrema.
Meneja Mahusiano ya Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria (wa pili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam leo kabla ya benki hiyo haijakabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Shirika la Kimataifa la Mambo ya Afya la Fhi360 kusaidia kampeni ya kuhamasisha watanzania kuchanja chanjo ya Covid 19. Kutoka kushoto ni Mshauri Mwandamizi wa Fhi360, Theresia Mrema, Mkurugenzi wa Makampuni Makubwa na Uwekezaji wa Benki ya Absa Tanzania, Hugo Chilufya, Mkurugenzi Mkazi wa Fhi360, Waziri Nyoni, Mkurugenzi wa fedha wa Fhi360, Anselm Mmassy na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Masoko ya Kigeni wa Absa, Irene Rwegalulira.
Mkurugenzi wa Makampuni Makubwa na Uwekezaji wa Benki ya Absa Tanzania, Hugo Chilufya (wa tatu kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Mambo ya Afya la Fhi360, Waziri Nyoni kwa ajili ya kuhamasisha watanzania kuchanja chanjo ya Covid 19. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria, Mshauri Mwandamizi wa Fhi360, Theresia Mrema, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Masoko ya Kigeni wa Absa, Irene Rwegalulira na Meneja Uhusiano wa Absa, Neema Athanas.
Mkurugenzi wa Makampuni Makubwa na Uwekezaji wa Benki ya Absa Tanzania, Hugo Chilufya (kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Mambo ya Afya la Fhi360, Waziri Nyoni kusaidia kampeni ya kuhamasisha watanzania kuchanja chanjo ya Covid 19. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wa Makampuni Makubwa na Uwekezaji wa Benki ya Absa Tanzania, Hugo Chilufya (wa pili kushoto), Meneja Mahusiano ya Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria, Meneja Uhusiano wa Absa, Neema Athanas, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Mambo ya Afya la Fhi360, Waziri Nyoni, Mshauri Mwandamizi wa Fhi360, Theresia Mrema, Mkurugenzi wa fedha wa Fhi360, Anselm Mmassy na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Masoko ya Kigeni wa Absa, Irene Rwegalulira wakipiga picmara baada ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Sunday, March 27, 2022

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA USIMAMIZI WA FEDHA YANAYOTOLEWA NA DCB FOUNDATION KUENDELEA KUWANUFAISHA WATANZANIA

  
Ofisa Mikopo Vikundi vidogo vidogo wa Benki ya Biashara ya DCB, Leticia Nyato akizungumza na wajasiriamali jijini Dar es Salaam jana wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation.
Ofisa Mikopo ya Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, Odilia Johnson akizungumza na wajasiriamali jijini Dar es Salaam jana wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation.
Ofisa Masoko na Huduma kwa Wateja Benki ya Biashara ya DCB, Elizabeth Ntulu (kulia) akikabidhi cheti kwa Shafii Njayo wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Masoko na Huduma kwa Wateja Benki ya Biashara ya DCB, Elizabeth Ntulu (kulia) akikabidhi cheti kwa Amina Ally wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Masoko na Huduma kwa Wateja Benki ya Biashara ya DCB, Elizabeth Ntulu (kulia) akikabidhi cheti kwa Baraka Jeremia wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Wednesday, March 23, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK DEBUTS POPOTE VISA CARD, VOWS TO SUPPORT DIGITAL TANZANIA AGENDA




VISA Card East Africa Vice President Corine Nana (right), and Tanzania Commercial Bank Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi press a button to mark the official launch of the Popote Visa Card launched by Tanzania Commercial Bank to facilitate the Bank's customers access to any services and wherever they are in and out of the country the launch event took place today in Dar es Salaam






VISA card East Africa Vice President Corine Nana (center) with Tanzania Commercial Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi second left showing the POPOTE VISA CARD model during the official launch of the card launched by Tanzania Commercial Bank. and Tanzania Commercial Bank Telecommunications and Operations Director Jema Mssuya, CEO of UBX Tanzania LTD, Seronga Wangwe and TCB Internet Banking Senior Manager Allen Manzi at the event held today in Dar es Saam.





Tanzania Commercial Bank Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi, speaking during the official launch of the Popote Visa Card launched by Tanzania Commercial Bank to facilitate the Bank's customers accessing any services and anywhere in the country and abroad. today in Dar es Salaam


Vice President of VISA card East Africa Corine Nana (right), presenting the POPOTE VISA CARD card to one of the customers who attended the official launch of the Popote Visa Card launched by Tanzania Commercial Bank to facilitate the Bank's customers accessing any services and In any part of the country and abroad, the launch took place today in Dar es Salaam (center) by Tanzania Commercial Bank Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi.


Tanzania Commercial Bank customer showing the VISA CARD card of Tanzania Commercial Bank launched today




The government’s aspiration for a less cash economy got yet another vital digital finance shot in the arm yesterday following the official debut of an internationally accepted electronic payments card in the market by Tanzania Commercial Bank (TCB).

The bank has partnered with Visa International to introduce the new service that elevates its commercial clout in international trade finance circles and enables its customers to transact anywhere any time in the world.

Speaking at the launching ceremony of the Popote Visa Card, the Chief Executive Officer of TCB, Mr Sabasaba Moshingi, said the debit card has all it takes to make universal financial services to be within reach in Tanzania.

The Popote debt card partners vowed to support efforts for a less cash national economy by championing and promoting responsible and innovative digital payment solutions that are more convenient, safe and offer better money management options.

“Any efforts like the international debit card that we have launched today and our partnership with Visa are mportant to the government’s digital economy and cashless society ambitions,” Mr Moshingi noted.

He said the bank opted for the Visa partnership because the American multinational was the giant of digital payments in the world with an unmatched network of 61 million merchants.

Speaking at yesterday’s event in Dar es Salam, Visa East Africa officials said the company is committed to expand digital payments not only in Tanzania but across the world by working closely with partners like TCB to also bring the benefits of digital finance to consumers and government partners.

The Visa Vice President and Managing Director for East Africa, Ms Corine Mbiaketcha Nana, said Tanzania has all the ingredients for a cashless society.

The official was upbeat of the benefits the partnership with TCB will deliver and the added values that will be accrued from it, including cost savings through greater payments efficiency and speed.

“Like all innovative digital payment solutions, adoption and use of the Popote Visa Card offers significant benefits to individuals, business entities and the government,” Ms Nana pointed out emphatically noting that the impactful advancement of financial inclusion will make the most difference in the lives of many people.

The launch of TCB Popote Visa Card comes a week after the government revealed its plans and the investments to create a digitally empowered national economy.

The ICT minister Nape Mnauye said that already a US$150 million World Bank soft loan has been secured to advance the Digital Tanzania Project, whose ultimate goal is to stir the national digital transformation efforts.

He said already a blueprint is being drawn to chart out the roadmap for executing the grand digital economy venture.

Speaking yesterday at Hyatt Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam, TCB customers and other sectoral stakeholders said the Popote debit card rollout augurs well with ongoing local initiatives to accelerate digital payments.

The debut of TCB Popote Visa Card, they emphasised, was also a boon for supporting the government and national efforts to make Tanzania a digitally supported cashless society.

“The strategic partnership between TCB and Visa international does not only expand benefit the two organisations but will also greatly help to expand the local digital payments space and enhance commercial fortunes across the national payments value chain,” the General Manager of dt card Tanzania told this reporter.







Share:

BENKI YA CRDB YAJA NA MUAROBAINI KWA WAJASILIAMARI

 
Maafisa wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa wakitoa elimu ya utunzaji wa fedha na kuwafungulia akaunti wanakijiji wa Naunambe wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi.

Na Mwandishi Wetu, Ruangwa | Benki ya CRDB katika kuendeleza juhudi za Serikali katika kuhakikisha wajasiriamali wanafanikiwa katika biashara zao.

Hivi karibuni CRDB imezindua huduma ya utunzaji wa Fedha za wajasiriamali kupitia Akaunti iitwayo Hodari ambayo ni mahususi kwa wafanyabiashara wenye mitaji isiyozidi Milioni 300.

Akiongea na mwandishi wetu Kiongozi wa Mauzo na Huduma za Kibenki wa CRDB Tawi la Ruangwa, Lilian Makawa amesema Akaunti hiyo haina makato ya utunzaji wa fedha wala makato wakati wa kutoa pesa kutoka kwenye Akaunti hiyo.

"Hodari Akaunti ni akaunti sahihi kwa Wajasiriamali kwani ni akaunti rahisi kutumia kwasababu ni akaunti isiyo na makato iwe ni wakati wa kutoa hela au makato ya kila mwisho wa mwezi"

"Mteja wa Akaunti hii ana uwezo wa kutoa pesa zake wakati wowote kwenye ATM, Wakala au ndani ya Benki dirishani," aliongeza Bi Lilian.

Musa Mpue mmoja wa waendesha Bodaboda katika Kituo cha Mabasi Ruangwa anasema kupitia Akaunti ya Hodari ameweza kuhifadhi makusanyo yake ya kila siku anayoyapata kutokana na biashara yake ya usafirishaji kwa kutumia Bodaboda.

Akaunti ya hodari imenisaidia kuhifadhi makusanyo yangu ya kila siku yatokanayo na biashara yangu ya Bodaboda, na fedha hizo nazipata kwa wakati pale ninapozihitaji kufanya marejesho ya mkopo wangu wa Bodaboda,” alisema Musa.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa na wakati mgumu wanapozitunza pesa zao Benki, pale wanapozihitaji huhitajika kutumia taratibu kadhaa ambazo husababisha kutoweza kufanya miamala ya kibiashara kwa wakati. Benki ya CRDB imeondoa kikwazo hicho kupitia Akaunti hii ya Hodari kwani inawawezesha wafanyabiashara hawa kufanya miamala ya kipesa muda wowote kupitia CRDB Wakala.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive