A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Friday, May 21, 2021

VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA TABORA WAISHUKURU BENKI YA NBC

 001Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Nd Raymond Urassa akizungumza na viongozi wa vyama zaidi ya 200 vya ushirika (AMCOS) Mkoani Tabora wakati wa kongamano lilioandaliwa na benki hiyo lenye lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi. Hafla hiyoimefanyika mkoani humo jana

02Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru (wapilikushoto) akikabidhi pikipiki kwa Mwenyekiti wa chama cha msingi Solelansabo Mary James wakati wa kongamano lilioandaliwa na Benki ya NBC lenye lengo la kuwapa mafunzo wanachama na viongozi wa vyama mbali mbali vya ushirika Mkoani Tabora yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Raymond Urassa pamoja na Katibu wa Chama hicho. Hafla hiyoimefanyika mkoani humo jana

03
Afisa Mauzo wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Tawi la Tabora Nuru Rajabu (kulia), akisimamia zoezi la kusajiri majina kwa wanachama mbalimbali vya Ushirika (AMCOS) Mkoani Tabora wakati wa kongamano lilioandaliwa na benki hiyo lenye lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao na huduma nyengine za kifedha ili waweze kukopesheka kwa urahisi. Hafla hiyoimefanyika mkoani humo jana
04
Viongozi mbalimbali wa vyama zaidi ya 200 vya ushirika (AMCOS) Mkoani Tabora wakifuatilia kwa umakini semina iliyoandaliwa na benki ya NBC lenye lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi. Hafla hiyoimefanyika mkoani humo jana


IMG_9389
Menejan Mahusiano Kitengo cha Bima wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Tawi la Tabora Abdul Farahan akitoa elimu juu ya matumizi sahihi ya bima wakati wa kongamano lilioandaliwa na benki hiyo lenye lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi


 

Benki ya NBC kupitia huduma yake ya #NBCShambani inayowalenga wateja wanaojishughulisha na kilimo imeongoza semina ya mafunzo kwa viongozi wa vyama zaidi ya 200 vya ushirika (AMCOS) Mkoani Tabora kwa lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni  pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi. Hafla hiyo ilifunguliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tabora, Nd Bosco Ndunguru na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali akiwemo Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora, Nd Absalom Cheliga na wakulima wa zao la tumbaku kutoka wilaya za Tabora Mjini, Sikonge na Uyui.

 

Pamoja na kuendesha mafunzo hayo Benki ya NBC kupitia Meneja wa Wateja Wadogo, Nd Raymond Urassa walitoa zawadi ya pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama  Cha Msingi Solelansabo, Bi Mary James Merrick ili kumsaidia katika shughuli za kuendesha chama na kuwatembelea wakulima. Pamoja na zawadi ya pikipiki hiyo, Benki ya NBC pia ilitoa baiskeli tatu kwa wakulima kutoka kwa vyama vya msingi mbali mbali kama pongezi kwa juhudi za kupata mazao mengikwa msimu uliopita.

 

Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mkurugenzi wa Manispaa ya hiyo, Nd Bosco Ndunguru aliipongeza Benki ya NBC kwa kuwawezesha na kuwapa mikopo na huduma za kibenki zenye gharama nafuu wakulima wa  zao la tumbaku ambalo kwa kiasi kikubwa linalochangia pato la mkoa huo. Aidha alitoa rai kwa benki hiyo kuingia kwenye mazao mengine ili kufungua fursa zaidi kwa wakulima wa mazao mengine. “Ni fursa kubwa sana kwa mkulima mmoja mmoja na ambao wako kwenye vyama mkoani kwetu kwa Benki ya NBC kuwa kwenye sekta ya kilimo na wakulima wanatakiwa kuichamgamki waanze kuzalisha kibiashara.” Aliongeza Nd Bosco.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa alisema kwamba Benki ya NBC kupitia NBC Shambani imejipanga vizuri kuwahudumia wateja wake kupitia matawi yake nchi nzima wakulima wa mazao mbali mbali yakiwemo tumbaku, kahawa, parachichi, pamba na chai. 

 

Akiongelea huduma za kibenki kwa mkulima mmoja mmoja, Nd Urassa alisema kuwa mkulima anaweza kufungua akaunti bila kuwa na kianzio na kuendesha akaunti bila kuwa na makato ya kila mwezi. “Pamoja na fursa ya akaunti za shilingi na dola, akaunti za vyama vya msingi pia hazina makato lakini pia zina gharama ndogo za uendeshaji kupeleka vyama vya msingi kuendesha shughuli zake kwa gharama nafuu na kuongeza ufanisi.” 

 

Kwa upande wake mnufaika wa zawadi ya pikipiki na Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi Solelansabo, Bi Mary James Merrick aliishukuru Benki ya NBC kwa zawadi hiyo na kusema kuwa itamsaidia katika kuendesha shuguli zake za chama kwa urahisi na ufanisi zaidi. Aidha alipongeza benki hiyo kwa kutoa huduma zilizo bora na mikopo yenye riba nafuu inayowawezesha wakulima kutimiza mahitaji yao ya pembejeo kwa wakati.

Share:

Thursday, May 20, 2021

Absa Bank Tanzania launches the first virtual branch engagement solution in the market

 
Absa Bank Tanzania Chief of Finance, Obedi Laiser (left), cuts a ribbon to inaugurate the bank’s first virtual branch engagement solution to be hosted on WhatSApp application. The brief event took place at Absa Mikocheni Branch in Dar es Salaam today. Watching (from right) are Absa Tanzania Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi and bank’s Head of Customer Experience, Samuel Mkuyu.

Absa Bank Tanzania Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi, addresses attendees during the launching ceremony.
Absa Bank Head of Customers Experience and Digital, Samuel Mkuyu, speaks during the launching ceremony.
Fasthub Solutions Business Manager, Hawa Mwakatundu, speaks at the launching event.
A cross-section of attendees fix their attention to the screen as Absa Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed, speaks over teleconferencing facility.
Absa Mikocheni Branch Manager, Prisca Daudi, demonstrates how to use the just-launched Absa's virtual branch engagement solution in Dar es Salaam today.
Absa Bank Tanzania Chie of Finance, Obedi Laiser (left), the bank’s Head of Customer Experience, Samuel Mkuyu, and Absa Tanzania Head of Retail Oscar Mwamfwagasi, in buoyant mood during the official launch of the bank’s first virtual branch engagement solution to be hosted on Whatsapp application. The occasion was held at Absa Mikocheni Branch in Dar es Salaam today.

Dar es Salaam, Tanzania | Absa Bank Tanzania has today launched its first ever virtual branch engagement solution to all customers. The new engagement solution is hosted on WhatsApp and will enable its customers to book their banking services and know the turnaround time per service prior to being attended to. The solution is aimed to fit into customers lifestyles and enhance their experience while at the branch.

Addressing the press to announce the system launch, the bank’s Managing Director, Abdi Mohamed said, “Absa’s aim is to become a digitally led bank while providing solutions which caters for our customers convenience and lifestyles. Our customers no longer need to wait aimless at the branch lobby, we are now in a position to engage them before they even arrive through their mobile phones.”

“We chose WhatsApp because it makes interacting with customers easy, private and personalized. Based off our market research at least 68% of WhatsApp users think using the platform is the easiest and most private way to connect. This system will also enable customers to share their feedback on their experience which will put more emphasis on how we can better improve our products and services. As a bank we are truly tapping into our customers lifestyles, by partnering with Fintech companies such as FastHub Solutions to provide more meaningful personalized moments for our customers”, said the Head of Customer Experience (CX) & Digital, Samuel Mkuyu.

The bank’s Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi also said, “We have not excluded our non-smartphone owning customers (Feature Phones). We guarantee them the exact same experience by sending a short message service (SMS) to our toll free acquired short code 15062. At Absa, we continue to aspire to help bring possibilities to life and we are now confidently placing our customers lifestyles and needs at the Centre of all we do. As an agile bank we are focused on empowering our customers and further revolutionizing the experience they have with us. We guarantee to serve them according to their needs and create the bank of the future now, which we call Africanacity".

Finance Director, Obedi Laiser concluded by saying "As Absa Bank Tanzania, we continue to harness technology and innovation to meet and anticipate our customers future demands. This platform was conceived from customers feedback that they wanted services to be hassle free and made easier according to the changing times. Our customers can trust that we will continue to evolve our role to become efficient and relevant in the market.

Furthermore, the solution is available to both existing customers with an account at Absa and new customers."
Share:

Tuesday, May 11, 2021

RAIS MSTAAFU IAMWAGIA SIFA BENKI YA NBC

Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Nd Theobald Sabi. Hafla hiyo ilifanyika katika bustani za Serena Hotel jijini Dar es Salaam pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Nd Aboubakak Kunenge pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa huo Alhaj Mussa Salum, Wateja wa NBC na wadau wengine.Rais Mstaafu Jakaya mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Nd Theobald Sabi wakati akichukua chakula wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya hiyo. Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa Salum, pamoja na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Nd Aboubakak Kunenge.
Mkurungezi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akizungumza wakati wa halfa hiyo.
Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wateja wa Benki ya NBC pamoja na wadau mabli mbali waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi wa wafanyakazi wa benki hiyo.



Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya
Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufuturisha
iliyoandaliwa na Benki ya NBC awataka wananchi wa Dar es Salaam,
kusherekea Sikukuu ya Eid il Fitr kwa amani bila kuharibu funga zao. Hafla
hiyo ya kufuturisha ilifanyika katika bustani za Serena Hotel jijini Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Nd
Aboubakar Kunenge, Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa
Salum, wateja wa Benki ya NBC na wadau wengine.



Akizungumza wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Banki ya Taifa ya Biashara,
NBC usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam, Rais Mstaafu Kikwete pia
aliipongeza Benki ya NBC kuwa na bidhaa maalum kwa makundi mbali
mbali bila kubagua imani za kidini hivyo kuongeza mshikamano ndani ya
jamii.


Pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa huduma hizo nzuri, Rais
Mstaafu Kikwete alisema kwamba Benki ya NBC iko mstari wa mbele katika
kujenga uchumi jumuishi kutokana na bidhaa ambazo zinalenga watu
wenye uwezo tofauti wa kifedha kuanzia yule wa juu mpaka wa hali ya chini
kabisa.


Aidha amewapongeza Bank ya Taifa ya Biashara, NBC kwa kuweza
kufuturisha waliofunga na kwamba wanapata thawabu sawasawa na
waliofunga. "Niwapongeze kwa kuweza kufuturisha na Mwenyezi Mungu
awabariki kwa mlichokifanya ni kitu kikubwa sana, kuna wengi hawajafikiria
kuweza kuwafuturi lakini ninyi mmeweza bila kuangalia.” amesema Kikwete
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya Taifa ya Biashara
NBC. Nd Theobald Sabi, aliwashukuru wateja na wageni waliofika kwenye
Iftari hiyo na kusema kwamba ni mmoja ya matukio muhimu katika kalenda
ya benki hiyo na ni sehemu ya kuongeza uhusiano na ushirikiano na wateja
wao.


“Kwa muda mrefu benki yetu ya NBC imekuwa na utaratibu wa kuandaa
futari kwa wateja wake Tanzania bara na visiwani Zanzibar wakati wa
mwezi mtukufu wa Ramadhani.” alisema Sabi
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Nd Theobald Sabi aliongeza kuwa
benki hiyo ina huduma za kibenki zinazofuata taratibu za Sharia. “Huduma
zetu za Islamic Banking zilianziswha. tangu mwaka 2010 na ni huduma za
mbadala kwa wateja wetu wanaopenda kufanya miamala kwa kuzingatia
sheria za Kiislamu.




Huduma hizi zinawalenga wateja wakubwa, wadogo na
wateja binafsi na zinapoatikaa katika matawi yote ya benki hiyo nchini.”
Baadhi ya huduma alizogusia ni mikopo isiokuwa na riba na inayofuata
sheria kwa wafanyabiashara na waajiriwa, huduma za amana za muda
maalum zenye gawio la faida halali na Akaunti ya Akiba ya La Riba
iliyounganishwa na mfuko wa bima wa Takahul inayochangia hadi 1m ya
rambi rambi kwa wanafamilia inpotokea mteja amefariki.
Kuhusu Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)


Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya kongwe kuliko zote nchini
Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma
mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na
misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.
Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha
taasisi zote za fedha, zikiwamo benki.


Mwaka 1991, sheria ya mabenki
ilirekebishwa na miaka sita baadaye, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana
kama Benki ya Taifa ya biashara, iligawanywa katika tanzu tatu tofauti NBC
Holding Corporation, National Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997)
Limited. Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata
hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama
mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa
za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.


Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopatikana katika maeneo
mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 47 na mashine za ATM 180, Benki ya
NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine
za kibenki kwa wateja mbalimbali. Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi
takriban 1,200 nchi nzima.



Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22
2 1 9 3 0 0 0 | + 2 5 5 2 2 5 5 1 1 0 0 0 o r ema i l u s
NBC_MarketngDepartment@nbc.co.tz
Share:

Monday, May 10, 2021

Absa Bank Tanzania co-sponsors FinTech & HealthTech youth entrepreneurs in the inaugural Wazo Challenge Tanzania Demo Day

  

Absa Bank Tanzania announced youth entrepreneurial winners of the Wazo Challenge Tanzania Demo Day. The program was managed and organized by Startup Réseau; an India-headquartered startup accelerator which kick-started its East Africa expansion with the inaugural edition of the "Wazo Challenge Tanzania", announced in February 2021.

Wazo Challenge Tanzania focussed on 5 thematic areas - Financial Services, Healthcare, Agriculture, Energy / Utility and Education. As a part of the program, Startup Réseau hosted a Venture Bootcamp, wherein 10 high-potential founders were selected for a 4-week venture mentorship and leadership development bootcamp, that was delivered by successful founders, industry leaders, domain experts and investors from Startup Réseau’s global network. The Venture Bootcamp also had a parallel track of “Office Hours” wherein 15 more startups from the application pool were mentored.

This one-month long venture development bootcamp operated from March - April 2021 having winners compete for a cash grant of USD 10,000 determined by the stage of startups, the founders’ vision, uniqueness, market opportunities and clarity of business model. The grant money was disbursed as Top-3 prizes of USD 5,000 (Kikoba App), USD 3,000 (Mipango App) and USD 2,000 (MedPack)

Awarding the winners during the Demo day event, the bank’s Managing Director, Abdi Mohamed said, “Wazo Challenge Tanzania was based on 12 startups selected from an application pool of 150 startups which focused on 5 themes. Absa being the co-sponsor saw the need to support youth with innovative ideas which are also aimed at impacting communities and bringing people’s possibilities to life, and this at Absa we say is Africanacity”.

Mr. Mohamed also added by saying that Absa Bank has a major role of being a force for good to the community and ensures that youth are highly supported considering there is a bright future instore for them and their daring spirit of making a business idea into reality marks ‘the dream come true’ for entrepreneurial footsteps in the business world.

“Our bank plays a big role in supporting enterprise development in the country and we ensure this impact flows down to the communities as we play a major role in the society by being a force for good. These youth will again set footprints in the business world as they aspire to not only expand from being just startups but to improving economies and adding value to the society” commented the bank’s Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga.

Mr. Luhanga also said that the bank maintains a strong relationship with organizations such as Startup Reseau with purpose of bringing change to the communities and providing support to the ongoing efforts the government still plays in developing the country from empowering youth to refining the economy.

Mr. Mohamed concluded by saying that Absa is a key role player in advancing several sectors in the country some of them being education, entrepreneurship, financial literacy, environment and social wellbeing. The bank ensures that every society investment is aligned with strengthening our relationship with the organizations, community and the government at large.
Share:

BENKI YA NBC YAZINDUA KLABU YA WAFANYABIASHARA MKOANI KIGOMA

Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta (wapili kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi wakifurahia baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa NBC Biashara Club kwa Mkoa wa Kigoma uliofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika wenye lengo la kuwakutanisha wateja wake wafanya biashara na wenye viwanda na wadau wengine. Wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanayabiashara Wadogo na wa Kati wa benki ya NBC, Mussa Mwinyidaho pamojana Mteja wa Benki hiyo, Marietha Patrick.
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Rashid Mchatta (wa sita kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa saba kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma baada ya uzinduzi rasmi wa NBC Biashara Club kwa Mkoa huo uliofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Benki ya NBC imezindua klabu ya wafanyabiashara wa benki hiyo mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya mipango ya benki hiyo kusogeza huduma kwa wateja wake sambamba na kujenga mtandao ambao utawasaidia wafanyabiashara wateja wa benki hiyo kufanya biashara zao kwa tija.

Theobald Sabi ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC,Theobald Sabi akizungumza kwenye uzinduzi wa klabu hiyo ya wafanyabiashara kwa mkoa Kigoma alisema kuwa lengo kubwa la klabu hiyo kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kwenye sekta ya biashara kuzungumza kwa pamoja changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao na kuzitatua.

“Kwenye business club pia tuna Business Clinic ambapo wateja licha ya kukutana wao kwa wao kujenga mtandao wa kubadilishana taarifa na uzoefu wa biashara pia watakutana na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama TCCIA, SIDO, BRELA, TRA, kampuni ya maswala ya ukaguzi wa fedha Delloitte na wadau wengine ambao watawasaidia kujua taratibu mbalimbali za kufanya biashara,” Alisema Sabi Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa klabu za wafanyabiashara pia zinawajenga wafanyabiashara na kuwapa uelewa wa namna ya kushiriki kwenye maonyesho mbalimbali kwa ajili ya kutangaza bidhaa zao na kufungua masoko ambapo biashara za kuvuka mpaka zimekuwa zikiangaliwa pia kupitia klabu hizo.

Alisema kuwa kupitia kwenye klabu za biashara benki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyabiashara hao ambao ndiyo msingi mkubwa wa kuwafanya wafanye biashara zao kwa tija ambapo mafunzo yanayotolewa yanazingatia taratibu mbalimbali za kuwafanya wapige hatua za maendeleo kwennye kusimamia biashara.

“Kuna watu wanafanya biashara hawana elimu ya usimamizi wa biashara (Business Management) hivyo kwa semina hizo tunawapa uelewa wa jambo hilo, mbinu za kutafuta masoko, mbinu za kujenga mtandao lakini pia tunawapa uelewa wa namba ya kuandika michanganuo ya biashara kwa ajili ya kuomba mikopo taasisi za fedha na kuwafanya waweze kumiliki mawazo yaliyopo kwenye michanganuo hiyo na kuifanyia kazi kwa faida,”Alisema.

Mkurugenzi huyo wa NBC alisema kuwa kubwa ambalo ndilo msingi wa kuanzishwa kwa klabu za wafanyabiashara ni kuwafanya wafanye biashara zao kwa faida na kukua kibiashara ambako kutaongeza mapato yao lakini pia kutaongeza mapato ya serikali na mwisho wa siku wafanyabiashara hao watakuwa na uwezo wa kukopa mikopo mikubwa na kurejesha jambo ambalo ndiyo msingi mkuu wa benki katika kujiendesha kwa faida.

Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Nd Rashid Mchatta akizindua klabu ya biashara kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Nd Thobias Andengenye alisema kuwa mafunzo na kujenga mtandao kwa wafanyabiashara ndiyo msingi mkubwa utakaowawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa faida.

Katika hotuba yake, Nd Mchatta alisema kuwa biashara ambazo zinaendeshwa kwa kufuata maelekezo ya watalaam zimekuwa zikifanyika kwa mafanikio na hata kunapotokea changamoto inakuwa rahisi kukabili changamoto hiyo.

Alisema kuwa kuwepo kwa vikao vya wafanyabiashara wao kwa wao, wao na wadau wengine na wao na serikali kuna faida kubwa katika kuifanya sekta ya biashara kuwa na tija lakini pia inasaidia kukabili changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na kila upande kwenye biashara.

“Tukikaa kwa pamoja na kujadili mambo yanayohusu biashara tutazipatia utatuzi changamoto zinazojitokeza maana wafanyabiashara wana malalamiko yao kwa taasisi za serikali zinazosimamia biashara na serikali nayo inalalamika kwa ukwepaji kodi, bidhaa duni na vitu vingine hivyo klabu za biashara zinatufanya kukutana pamoja na kuzungumza tofauti zetu,” Alisema Mkuu wa mkoa Kigoma.

Uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara mkoa wa Kigoma ulitanguliwa na semina kwa wafanyabiashara wa mjini Kigoma ambapo mada mbalimbali zilitolewa kuwezesha wafanyabiashara kuwa na uelewa wa mambo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki kwenye semina na uzinduzi wa klabu ya wafnyabiashara wameeleza faida kubwa ambayo wameipata kwa kuhudhuria semina kutokana na mada zilizotolewa kuishi ndani ya wafanyabiashara ambazo zitawafanya kufanya biashara zao kwa faida.

Kilahumba Kivumo ambaye ni mfanyabiashara mkoni humo akizungumza wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara wa mkoa Kigoma, alisema kuwa klabu hiyo ni wazo zuri la litawasaidia kupata mahali pa kuzungumza changamoto zao na namna ya kuzitafutia ufumbuzi.

Alisema kuwa changamoto kwenye biashara ni nyingi ikiwemo taratibu za kupata mikopo ambapo bado taarifa zake hazijawa wazi kwa wafanyabiashara lakini pia vikwazo katika biashara za kuvuka mpaka na vizuizi mbalimbali njiani ambavyo vinawakatisha tama wafanyabiashara hivyo Benki ya NBC imeingia Kigoma kwa wakati muafaka na imeleta matumaini mapya katika biashara zao.
Share:

Thursday, May 6, 2021

WAKAZI WA MKOA WA KATAVI WAIPOKEA BENKI YA NBC KWA SHANGWE

 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Juma Zuberi Homera (katikati), akikata keki wakati wa uzinduzi Ofisi ya wakala mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi hivi karibuni. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Theobald Sabi, Meneja wa Huduma za NBC Wakala Robert Madaki, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya hiyo Elibariki Masuke, na kulia ni na Wakala wa ofisi hiyo Emmanuel Atimili, Hafla hiyo imefanyika hivi jana .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Juma Zuberi Homera (katikati), akikata keki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya wakala mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi hivi karibuni kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Theobald Sabi, pamoja na maofisa wengine kutoka Benki hiyo na Wakala wa Ofisi hiyo Emmanuel Atimili.

Taarifa kwa Umma Mei 5 mwaka huu 2021 Wakazi wa Mkoa wa Katavi wameipongeza Benki ya NBC kwa kuzindua NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda kwani kwa kuwepo kwa wakala mkuu huyo kutafungua fursa za kiuchumi, kuziendeleza pamoja na kuinua uchumi wa wafanyabiashara katika Mkoa huo.

Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi wa tawi hilo la NBC Wakala Plus, Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Komredi Juma Zuberi Homera ameupongeza uongozi wa Benki ya NBC kwa kuja kuwekeza katika Mkoa huu ambapo watu zaidi ya elfu moja wamefungua akaunti katika tawi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Homera aliupongeza uongozi wa Benki ya NBC kwa kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Katavi. Mafunzo hayo yalifanyika kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda. Komredi Homera pia aliusihi uongozi wa Benki ya NBC kutoa mikopo kwa wajasiriamli wa Katavi ili matunda ya mafunzo hayo yaonekane kwa haraka.

Aidha Homera ameishukuru Benki ya NBC kwa kutoa msaada mifuko 300 ya saruji, Bati 60 sambasamba na ndoo 5 za rangi katika Cho Cha Afya huku benki hiyo ikiahidi kusimamia ujenzi wa madarasa mawili katika chuo hicho.

Homera pia amewapongeza Benki ya NBC kwa kufika Mkoani Katavi japo alisema kuwa wamefika kwa kuchelewa kwani fursa zipo nyingi katika Mkoa huu wa Katavi kwani uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara upo juu pamoja na mazao ya kimkakati.

Pia Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliuhakikishia uongozi wa Benki ya NBC kwamba huduma ya NBC Wakala Plus waliyoifungua katika Mkoa wa Katavi inakuwa na kuwa tawi kamili Ili huduma kubwa za kibenki zaidi ziweze kutolewa.

“Kuzunduliwa kwa NBC Wakala Plus hapa Katavi maana yake ni kwamba wapo wafanyakazi, Wakuu wa Taasisi pamoja wananchi ambao akaunti zao zilikua zimelala sasa kupitia NBC Wakala Plus wakazifufue na kuanza kutumika na kuungana na benki nyingine zilizopo katika Mkoa wetu Ili uwekezaji huu wa Benki ya NBC uweze kuleta maendeleo katika Mkoa wetu," alisisitiza Homera.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi alisema kuwa wameamua kufungia NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda kwani manispaa hiyo inakuwa kwa haraka kiuchumi na miradi mingi ya kimakakati iliyoanzishwa na awamu ya tano inaendelea katika awamu ya sita na ni Mkoa wenye fursa nyingi za kiuchumi wa nchi yetu na ukanda huu.

"Na sisi NBC tumeona ni muhimu kuwa hapa tushirikiane na wananchi wa Katavi pamoja na wafanyabiashara katika kuhakikisha kwamba fursa hizi za kiuchumi tunaziendeleza ukizingatia nchi yetu ipo katika mkakati wa kukuza viwanda na kuongeza thamani katika mazao hivyo hiyo ni fursa kubwa ambayo tumeiona kwa hiyo uwepo wetu hapa utatuwezesha kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wakulima Ili waweze kuongeza thamani katika mazao yao na kununua pembejeo kama matreka na nk na kuongeza uzalishaji.”

Naye Meneja wa huduma na bidhaa kutoka Benki ya NBC, Nd Jonathan Bitababaje amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Katavi kwa Benki ya NBC ina akaunti mbalimbali zinazomfikia kila mmoja kwa upande wake Kama Shambani Akaunti, Kuwa Nasi Akaunti, Johari akaunti kwa ajili ya wanawake, Akaunti za watoto, wanafunzi na Bima za kulinda Mali zao.
Share:

Tuesday, May 4, 2021

Waziri Ndugulile:Tunaandaa sheria ya faragha kulinda taarifa za mtumiaji

 NDUGULILE

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, TEHAMA Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa wadau wa sekta ya Tehama


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Faustine Ndugulile amesema katika kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi ya sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA, anakusudia kutunga sheria ya faragha.

Pia ametoa wito kwa wadau kupeleka mawazo, maoni au ushauri namna ya kuboresha sekta hiyo nchini.

Ndugulile ametoa kauli hiyo juzi katika mdahalo wa wadau wa sekta ya Tehama ambao pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili changamoto na suluhisho kuhusu sekta ya Mawasiliano na tekbnolojia nchini.

Akizungumza katika mdahalo huo uliokuwa na mada kuu kuhusu mapinduzi ya nne ya viwanda kwa uchumi wa dijitali wa ushindani, Dk. Ndugulile alisema wizara yake inakwenda kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali za sekta hiyo.

"Tunaenda kupitia sheria na kanuni zetu na tutafanya mabadiliko ili kukidhi mazingira ya sasa, tunakusudia kutunga sheria ya faragha na kulinda taarifa za mtumiaji(Data Privacy and Protection).

"Nimekuwa msikilizaji wa mdahalo kwa kweli tumepata mengi kutoka kwa wadau na kama serikali tunaenda kuyafanyia kazi kwa haraka.

"Muda wowote wadau leteni mawazo, maoni na ushauri ni namna gani tuboreshe na tusonge mbele uzuri hata mitandaoni nipo ukienda Twitter utanipata, Instagram nipo na twitter nipo na uzuri kwa sasa inapatikana vizuri na mnaipata vizuri pia.

"Kuhusu TCRA nimetoa maelekezo tayari wasifanye kazi kama polisi bali kama mlezi, mimi sio muumini wa faini kubwa kubwa lazima tubadilike na tumeanza kubadilika, alisema.

Akizungumza kwenye mkutano huo Dk Bello Moussa, Mkuu wa Ubunifu na Mikakati ya TEHAMA Huawei Kusini mwa Afrika alisema: "Mapinduzi ya Nne ya Viwanda yanakuja na maendeleo ya kiteknolojia yanaendesha maendeleo ya ulimwengu, ni wakati mzuri sasa kwa Tanzania kutosalia nyuma, bali kuungana na ulimwengu wote kwa kufanya kazi kwenye maeneo ambayo yataharakisha Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Tanzania katika Miaka 5 ijayo ”

Alitaja maeneo hayo ambayo ni pamoja na mpango wa kitaifa wa TEHAMA kwa uchumi wa kidigiti, mkongo wa taifa wenye kasi zaidi, ufikiwaji wa huduma ya internet maeneo ya vijijini na wataalamu wa wataalam wa TEHAMA.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dk. Godwill Wanga alisema Tehama imeleta matokeo chanya katika sekta mbalimbali ikiwamo kupunguza gharama za uzalishaji, kuongezeka uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi.

Share:

Thursday, April 29, 2021

Hivi ndivyo TEHAMA inaweza kupunguza uzalishaji wa kaboni na kuifikishaAfrika katika uchumi wa kijani.

 Smarter%2BEnergy%2Bfor%2Ba%2BBetter%2BLife

(Johannesburg, 21 Aprili 2021) Kampuni ya teknolojia ya kimataifa, Huawei inaamini kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano au TEHAMA, ina uwezo wa kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni kwa asilimia 20 katika muongo mmoja ujao.

William Xu, ni Mkurugenzi wa Bodi na Rais wa Taasisi ya Utafiti wa Mikakati wa Huawei, hivi karibuni alisema uendelevu wa nishati ni changamoto kubwa ambayo itazikabili nchi zote kwa muongo mmoja ujao.

“Matumizi ya nishati ulimwenguni yanaongezeka kwa kiwango cha asilimia 1.7 kila mwaka. Hivi sasa asilimia 85 ya nishati hutokana mabaki ya mimea na wanyama wa kihistoria yaani ”fossils”. Uendelevu wa nishati hii ni changamoto kubwa inayotukabili sisi sote. Kwa kuwezesha sekta mbalimbali, teknolojia ya TEHAMA ina uwezo wa kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni kwa asilimia 20 katika muongo mmoja ujao." Xu alisema.

Aliongeza kuwa wakati nchi nyingi zimejikita kupunguza uzalishaji wa kaboni, mahitaji ya nishati mbadala yameongezeka, na hapa ndipo TEHAMA inapotoa fursa mpya katika uzalishaji, uhifadhi na matumizi ya umeme.

"Kwa matumizi ya nishati, lazima tupendekeze mifumo jumuishi ya nishati kwa majumbani na viwandani na kuunda jamii, vyuo na miji isiyozalisha kaboni.” alisema Xu.

Hivi karibuni, Huawei ilitangaza kuwa itazingatia ubunifu na teknolojia mpya kusaidia viwanda kupunguza matumizi yao ya nishati ili kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni.

Barani Afrika pia, nchi nyingi zinazidi kuhamia katika matumizi ya nishati mbadala ili kusonga mbele katika nishati endelevu kwa siku zijazo.

Pamoja na algorithm yake ya muunganisho wa gridi inayoendeshwa na utashi wa kutengenezwa (Artificial Intelligence), Huawei imetoa zaidi ya mifano ya gridi 200 ya umeme kwa nchi zaidi ya 30. Hii imesaidia mitambo ya umeme kuunganishwa na gridi kwa uimara huku ikipelekea kuwepo na chanzo bora cha umeme wa jua.

Katika umeme wa jua pekee, Afrika imepata maendeleo makubwa katika miaka ya hivi karibuni. Zaidi ya gridi 6,200 ambazo hujumuisha gridi kubwa kabisa, za biashara na viwanda pamoja na zile ndogo zimethibitishwa kuwepo barani humo.

Kwa kuongezea, mataifa mengine tisa ya Kiafrika, mbali na Afrika Kusini na Misri, yapo njiani kujiunga na 'Gigawatt Club', lebo isiyo rasmi kwa kundi la nchi zilizo na uwezo wa kuzalisha gigawatt moja ya umeme kutokana na jua.

Huang Su, Mkurugenzi wa Huawei katika Biashara ya Umeme Dijitali Kusini mwa Africa, alisema kwamba karibu nusu ya idadi ya watu wasio na uwezo wa kupata umeme duniani wanaishi kusini mwa jangwa la Sahara.

 

"Kwa hivyo kuna haja kubwa na ya dharura ya kuharakisha ukuaji wa nishati mbadala kote katika eneo hilo ili kuhakikisha nishati ya kutosha, nafuu na ya kuaminika kwa Waafrika wote na kwa nchi kupata faida ya uchumi wa kijani." anasema.

Huawei imetumia zaidi ya miaka 30 ya utaalam na uzoefu katika teknolojia ya kidijitali ili kufanya uzalishaji wa umeme wa jua na matumizi kuwa bora zaidi na ya kuaminika kwa gharama ndogo.

Share:

Sunday, April 25, 2021

Uongozi wa juu wa Benki ya DCB washuhudia mheshimiwa Rais Samia akihutubia bunge kwa mara ya kwanza mjini Dodoma wiki hii

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (mstari wa mbele, katikati) akiwa na baadhi ya wakuu wa taasisi za fedha wakisikiliza hotuba ya Mheshiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakati ajikihutubia bunge kwa mara ya kwanza mjini Dodoma wiki hii. Viongozi hao walialikwa na Spika wa Bunge, Mhe.Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Mama Samia Suluhu hassan (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa taasisi za fedha ambapo Benki ya DCB iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Godfrey Ndalahwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi, Maharage Chande mara baada ya kulihutubia bunge kwa mara ya kwanza mjini Dodoma wiki hii.
Share:

Monday, April 19, 2021

Benki ya Absa yatoa msaada wa wheelchairs 20 kwa wanafunzi wenye ulemavu

  
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa (wa tatu kushoto), akikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) kwa mtoto mwenye ulemavu, Briton Andrew vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Absa, Aron Luhanga na wengine kutoka kushoto ni Mshauri kutoka Taasisi ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles; mama wa mtoto, Stella Philipo na Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania Aron Luhanga (wa tatu kushoto), akikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) Agnes Yohana, mama wa mwanafunzi mwenye ulemavu, Santieli Mduma (aliyekaa), vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa (katikati), akikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) Steven Francis, baba wa mwanafunzi mwenye ulemavu, Flora Steven (aliyekaa), vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Ofisa Elimu Maalum Manispaa ya Morogoro, Daniel Maganga. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa, Bakari Msulwa (wa pili kushoto), akiwa na, kutoka kushoto; Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa, Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania Aron Luhanga, Ofisa Elimu Maalum Manispaa ya Morogoro, Daniel Maganga na Mshauri kutoka Taasisi ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles, wakipiga picha na wanafunzi watano wenye ulemavu baada ya kukabidhiwa msaada wa viti mwendo vilivyotolewa na Benki ya Absa mkoani Morogoro leo. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania Aron Luhanga (kulia) na Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa wakikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) kwa mwanafunzi mwenye ulemavu, Hassan Moyo (aliyekaa), vilivyotolewa msaada na benki hiyo katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Mshauri wa masuala ya walemavu kutoka Taasisi ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles (wa pili kulia) akikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) Halima Liana, mama wa mwanafunzi mwenye ulemavu, Hassan Moyo (aliyekaa), vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga, Ofisa Elimu Maalum Manispaa ya Morogoro, Daniel Maganga na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa (kushoto kabisa). Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).

Benki ya Absa Tanzania imekabidhi vifaa vya usafiri 20 (wheelchairs) kwa wanafunzi walemavu waliopo shule za msingi katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya na Zanzibar.

Vifaa hivi vina thamani ya Tsh milioni 10 na vitagawiwa kwa wanafunzi hao kuanzia mkoa wa Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3) na Zanzibar (5).

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo mjini Morogoro jana, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga amesema “benki yetu inatambua umuhimu wa kuisaidia jamii katika kila nyanja na inasimama kidete kuhakikisha vijana wanafikia malengo yao kwa wakati na kwa kupata huduma stahili. Ndio maana leo tunashirikiana na shirika la Ikupa Trust Fund kwa kuwapatia wanafunzi hawa vifaa vya usafiri hivi ili waweze kufika shuleni kwa wakati na kuendelea na ratiba zao za masomo bila kukwamishwa”.

Bw. Aron alisisitiza kwamba Benki ya Absa ina lengo kuu la kuhakikisha vijana na watu katika jamii wananufaika zaidi kwa kufikia malengo yao ikiwa ndiyo moja ya nguzi kuu katika kuimarisha mchango wetu kwa jamii. Kwa kujali kwao ila pia kuzingatia vitu muhimu vya kuwasaidia vijana katika jamii kufikia malengo yao kwa upesi na kwa njia sahihi.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa alitoa wito kwa wazazi nchini kuwapekeka shuleni watoto wao wenye ulemavu ili kuweza kutambua vipaji vyao na kuviendeleaa.

Alisema kuzaliwa ama kupata ulemavu sio mwisho wa ndoto katika maisha kwani kuna walemavu wanaofanya vizuri katika njanja mbalimbali zikiwemo nafasi za uongozi serikalini, wanasiasa, wanamichezo na wataalamu mbalimbali.

"nachukua nafasi hii kuipongeza Benki ya Absa kwa kushirikiana na taasisi ya Ikupa Trust Fund na ni imani yangu tukio hili litaleta hamasa kwa taasisi na makampuni mengine kuiga Mfano wa Absa", alisema.

Kwa upande wake Meneja wa tawi la Absa mkoani Morogoro, Bw. Godfrey Chilewa pia amesema “kama benki tunazidi kuekeza nguvu katika jamii zinazotuzunguka huku tukishirikiana na wadau kama Ikupa Trust Fund na kwa kushikana mkono zaidi na uongozi mzima wa serikali yetu ili kuhakikisha tunaipa jamii huduma stahili na kufanikisha malengo ya watu pia”.

Mmoja wa wazazi wa wanafunzi waliokabidhiwa viti mwendo hivyo aliishukuru Benki ya Absa akisema kifaa hicho kitamrahisishia mtoto wake kwenda shuleni ukizingatia kuwa shule nyingi za msingi wilayani hapo ni za kutwa licha ya kuwa na vitengo maalumu vya wenye ulemavu.

"Naishukuru Absa, serikali na Ikupa, naona kama Absa imechukua jukumu la kuwa baba wa mtoto wangu kwani baba yake alishafariki, najua mtoto wangu anapoenda shule na ulemavu wake unapungua", alisema mama huyo.
Share:

HUAWEI YABORESHA UWEKEZAJI ILI KULINDA BIASHARA YAKE

  Eric%2BXuMwenyekiti wa kampuni ya Huawei Bw Eric Xu

Kampuni ya mawasiliano ya Huawei imebainisha mkakati wake wa kuboresha akaunti yake ya uwekezaji ili kukuza uthabiti na kukabiliana na hali ya mashaka katika biashara inayoletwa na mvutano wa kijiografia, kuibuka tena kwa virusi vya COVID-19 pamoja na kuzuiwa kufanya biashara Marekani.


Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw Eric Xu, wakati akiwasilisha hotuba kuu katika Mkutano  wa 18 wa Wachambuzi wa kidunia. Zaidi ya watu 400, ukijumuisha wachambuzi wa tasnia na wa kifedha, viongozi wa maoni na wawakilishi wa vyombo vya habari walishiriki katika mkutano huo wa siku 3 ulioanza liyoanza Aprili 12 hadi 14, kauli mbiu ikiwa "Ujenzi wa Ulimwengu Wa Maarifa na Uliounganishwa Kikamilifu."

“Uthibiti wa kibiashara ndio kanuni inayotuongoza. Tunataka kuongeza uimara wa biashara yetu yote, na tangu mwaka jana tumekuwa tukifanya kazi kuboresha uwekezaji letu tukiwa na lengo hili akilini.” alisema Eric Xu.

Ripoti ya mwaka 2020 ya Huawei inaonyesha mapato yaliotokana na mauzo ya kampuni hiyo mnamo 2020 yanafika CNY891.4 bilioni, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 3.8 kulinganisha na mwaka uliopita, huku faida yake kamili ilifikia CNY64.6 bilioni, ambayo ukilinganisha na ripoti ya mwaka 2019 ni ukuaji wa asilimia 3.2.

Eric Xu alisema moja ya vipaumbele ni kuongeza zaidi uwezo wa uhandisi wa programu za Huawei. "Tunatafuta fursa mpya za kibiashara katika sekta ya programu. Tunapopata kitu kinachotufaa, tutaongeza uwekezaji ili kuongeza ushiriki wa huduma za program katika vyanzo vyetu vya mapato. "alisema Eric Xu.

Mwisho wa Novemba 2018, Huawei iliamua kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani bilioni 2 katika kuboresha uwezo wao wa uhandisi wa programu. Eric Xu alisema kampuni hiyo "inafurahishwa na matokeo hadi sasa".

Programu kwa ajili ya magari kujiendesha ni mojawapo ya malengo makuu ya uwekezaji ndani ya kampuni. Kulingana na Eric Xu, programu hiyo ipo mbioni kufikia hatua ambapo magari yatajiendesha yenyewe bila dereva kujishughulisha kwa namna yoyote ile.

"Pamoja na uwekezaji mkubwa, matumaini yetu ni kusukuma mwenendo huu mbele kwani program hizi zinawezesha ujumuishaji wa tasnia ya magari na ICT, ambayo nayo hutengeneza fursa za kimkakati za muda mrefu kwa Huawei. Mara baada ya ukamilifu wa program hiyo, kutakua na mabadiliko katika sekta zote zilizo karibu ambayo yataleta mabadiliko makubwa zaidi katika miaka 10 ijayo.” Alisema Mwenyekiti huyo.

Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive