Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Nd Theobald Sabi. Hafla hiyo ilifanyika katika bustani za Serena Hotel jijini Dar es Salaam pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Nd Aboubakak Kunenge pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa huo Alhaj Mussa Salum, Wateja wa NBC na wadau wengine.Rais Mstaafu Jakaya mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Nd Theobald Sabi wakati akichukua chakula wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya hiyo. Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa Salum, pamoja na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Nd Aboubakak Kunenge.
Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wateja wa Benki ya NBC pamoja na wadau mabli mbali waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi wa wafanyakazi wa benki hiyo.
Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya
Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufuturisha
iliyoandaliwa na Benki ya NBC awataka wananchi wa Dar es Salaam,
kusherekea Sikukuu ya Eid il Fitr kwa amani bila kuharibu funga zao. Hafla
hiyo ya kufuturisha ilifanyika katika bustani za Serena Hotel jijini Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Nd
Aboubakar Kunenge, Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa
Salum, wateja wa Benki ya NBC na wadau wengine.
Akizungumza wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Banki ya Taifa ya Biashara,
NBC usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam, Rais Mstaafu Kikwete pia
aliipongeza Benki ya NBC kuwa na bidhaa maalum kwa makundi mbali
mbali bila kubagua imani za kidini hivyo kuongeza mshikamano ndani ya
jamii.
Pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa huduma hizo nzuri, Rais
Mstaafu Kikwete alisema kwamba Benki ya NBC iko mstari wa mbele katika
kujenga uchumi jumuishi kutokana na bidhaa ambazo zinalenga watu
wenye uwezo tofauti wa kifedha kuanzia yule wa juu mpaka wa hali ya chini
kabisa.
Aidha amewapongeza Bank ya Taifa ya Biashara, NBC kwa kuweza
kufuturisha waliofunga na kwamba wanapata thawabu sawasawa na
waliofunga. "Niwapongeze kwa kuweza kufuturisha na Mwenyezi Mungu
awabariki kwa mlichokifanya ni kitu kikubwa sana, kuna wengi hawajafikiria
kuweza kuwafuturi lakini ninyi mmeweza bila kuangalia.” amesema Kikwete
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya Taifa ya Biashara
NBC. Nd Theobald Sabi, aliwashukuru wateja na wageni waliofika kwenye
Iftari hiyo na kusema kwamba ni mmoja ya matukio muhimu katika kalenda
ya benki hiyo na ni sehemu ya kuongeza uhusiano na ushirikiano na wateja
wao.
“Kwa muda mrefu benki yetu ya NBC imekuwa na utaratibu wa kuandaa
futari kwa wateja wake Tanzania bara na visiwani Zanzibar wakati wa
mwezi mtukufu wa Ramadhani.” alisema Sabi
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Nd Theobald Sabi aliongeza kuwa
benki hiyo ina huduma za kibenki zinazofuata taratibu za Sharia. “Huduma
zetu za Islamic Banking zilianziswha. tangu mwaka 2010 na ni huduma za
mbadala kwa wateja wetu wanaopenda kufanya miamala kwa kuzingatia
sheria za Kiislamu.
Huduma hizi zinawalenga wateja wakubwa, wadogo na
wateja binafsi na zinapoatikaa katika matawi yote ya benki hiyo nchini.”
Baadhi ya huduma alizogusia ni mikopo isiokuwa na riba na inayofuata
sheria kwa wafanyabiashara na waajiriwa, huduma za amana za muda
maalum zenye gawio la faida halali na Akaunti ya Akiba ya La Riba
iliyounganishwa na mfuko wa bima wa Takahul inayochangia hadi 1m ya
rambi rambi kwa wanafamilia inpotokea mteja amefariki.
Kuhusu Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)
Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya kongwe kuliko zote nchini
Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma
mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na
misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha.
Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha
taasisi zote za fedha, zikiwamo benki.
Mwaka 1991, sheria ya mabenki
ilirekebishwa na miaka sita baadaye, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana
kama Benki ya Taifa ya biashara, iligawanywa katika tanzu tatu tofauti NBC
Holding Corporation, National Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997)
Limited. Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata
hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama
mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa
za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.
Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopatikana katika maeneo
mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 47 na mashine za ATM 180, Benki ya
NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine
za kibenki kwa wateja mbalimbali. Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi
takriban 1,200 nchi nzima.
Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22
2 1 9 3 0 0 0 | + 2 5 5 2 2 5 5 1 1 0 0 0 o r ema i l u s
NBC_MarketngDepartment@nbc.co.tz
0 comments:
Post a Comment