A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, May 6, 2021

WAKAZI WA MKOA WA KATAVI WAIPOKEA BENKI YA NBC KWA SHANGWE

 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Juma Zuberi Homera (katikati), akikata keki wakati wa uzinduzi Ofisi ya wakala mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi hivi karibuni. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Theobald Sabi, Meneja wa Huduma za NBC Wakala Robert Madaki, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya hiyo Elibariki Masuke, na kulia ni na Wakala wa ofisi hiyo Emmanuel Atimili, Hafla hiyo imefanyika hivi jana .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Juma Zuberi Homera (katikati), akikata keki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya wakala mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi hivi karibuni kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Theobald Sabi, pamoja na maofisa wengine kutoka Benki hiyo na Wakala wa Ofisi hiyo Emmanuel Atimili.

Taarifa kwa Umma Mei 5 mwaka huu 2021 Wakazi wa Mkoa wa Katavi wameipongeza Benki ya NBC kwa kuzindua NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda kwani kwa kuwepo kwa wakala mkuu huyo kutafungua fursa za kiuchumi, kuziendeleza pamoja na kuinua uchumi wa wafanyabiashara katika Mkoa huo.

Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi wa tawi hilo la NBC Wakala Plus, Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Komredi Juma Zuberi Homera ameupongeza uongozi wa Benki ya NBC kwa kuja kuwekeza katika Mkoa huu ambapo watu zaidi ya elfu moja wamefungua akaunti katika tawi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Homera aliupongeza uongozi wa Benki ya NBC kwa kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Katavi. Mafunzo hayo yalifanyika kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda. Komredi Homera pia aliusihi uongozi wa Benki ya NBC kutoa mikopo kwa wajasiriamli wa Katavi ili matunda ya mafunzo hayo yaonekane kwa haraka.

Aidha Homera ameishukuru Benki ya NBC kwa kutoa msaada mifuko 300 ya saruji, Bati 60 sambasamba na ndoo 5 za rangi katika Cho Cha Afya huku benki hiyo ikiahidi kusimamia ujenzi wa madarasa mawili katika chuo hicho.

Homera pia amewapongeza Benki ya NBC kwa kufika Mkoani Katavi japo alisema kuwa wamefika kwa kuchelewa kwani fursa zipo nyingi katika Mkoa huu wa Katavi kwani uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara upo juu pamoja na mazao ya kimkakati.

Pia Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliuhakikishia uongozi wa Benki ya NBC kwamba huduma ya NBC Wakala Plus waliyoifungua katika Mkoa wa Katavi inakuwa na kuwa tawi kamili Ili huduma kubwa za kibenki zaidi ziweze kutolewa.

Kuzunduliwa kwa NBC Wakala Plus hapa Katavi maana yake ni kwamba wapo wafanyakazi, Wakuu wa Taasisi pamoja wananchi ambao akaunti zao zilikua zimelala sasa kupitia NBC Wakala Plus wakazifufue na kuanza kutumika na kuungana na benki nyingine zilizopo katika Mkoa wetu Ili uwekezaji huu wa Benki ya NBC uweze kuleta maendeleo katika Mkoa wetu," alisisitiza Homera.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi alisema kuwa wameamua kufungia NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda kwani manispaa hiyo inakuwa kwa haraka kiuchumi na miradi mingi ya kimakakati iliyoanzishwa na awamu ya tano inaendelea katika awamu ya sita na ni Mkoa wenye fursa nyingi za kiuchumi wa nchi yetu na ukanda huu.

"Na sisi NBC tumeona ni muhimu kuwa hapa tushirikiane na wananchi wa Katavi pamoja na wafanyabiashara katika kuhakikisha kwamba fursa hizi za kiuchumi tunaziendeleza ukizingatia nchi yetu ipo katika mkakati wa kukuza viwanda na kuongeza thamani katika mazao hivyo hiyo ni fursa kubwa ambayo tumeiona kwa hiyo uwepo wetu hapa utatuwezesha kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wakulima Ili waweze kuongeza thamani katika mazao yao na kununua pembejeo kama matreka na nk na kuongeza uzalishaji.

Naye Meneja wa huduma na bidhaa kutoka Benki ya NBC, Nd Jonathan Bitababaje amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Katavi kwa Benki ya NBC ina akaunti mbalimbali zinazomfikia kila mmoja kwa upande wake Kama Shambani Akaunti, Kuwa Nasi Akaunti, Johari akaunti kwa ajili ya wanawake, Akaunti za watoto, wanafunzi na Bima za kulinda Mali zao.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive