A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, October 8, 2020

Benki ya DCB yazindua wiki ya huduma kwa wateja ikiahidi kuendelea kutoa huduma bora

 
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro (wa tatu kushoto), akikata keki kuashiriki uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja wa benki hiyo katika hafla iliyofanyika katika Tawi la DCB Uhuru, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendajiwa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa, Mkuu wa Kitengo cha Mikopo, Isidori Msaki (wa pili kulia), na baadhi ya wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati), akisalimiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Joachim Kimanza, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano tawini hapo, Olen Misigaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo, Amir Amirali, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam jana. Anayeangalia ni mteja mwingine, Joachim Kimanza.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Zacharia Kapama (kulia), akisalimiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Joachim Kimanza, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam jana. Katikati ni maofisa uhusiano katika tawi hilo, Getrude Mziray (wa pili kushoto) na Olen Misigaro.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya DCB, Isidori Msaki (wa pili kushoto), akisalimiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Joachim Kimanza, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.
Menea Uhusiano wa Benki ya DCB wa Tawi la Uhuru, Olen Misigaro (katikati), akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya DCB, Rahma Ngassa (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto), akimpa keki mmoja wa benki hiyo, Theresia Lyimo, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Zawadia Nanyaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kulia), Mkurugenzi wa Biashara, Zacharia Kapama na Meneja Uhusiano wa DCB Tawi la Uhuru, Olen Misigaro, wakisaliana na baadhi ya wateja tawini hapo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo, Kariakoo, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Geofrey Ndalahwa akizungumza na baadhi ya wateja katika tawi la Temeke kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia muda wao kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali ya benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Geofrey (kulia), Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Francis Kafuku (wa tatu kulia) na Meneja wa benki hiyo tawi la Temeke, Anna Kasyupa (kushoto) wakikata keki pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia muda wao kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali ya benki hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa akizungumza na baadhi ya wateja katika tawi la Temeke kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia muda wao kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali ya benki hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive