A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Saturday, October 17, 2020

BENKI YA DCB YATOA GAWIO KWA WANAHISA WAKE WAKUU

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe; Selemani Jafo, akikabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya shilingi 138,603,889 ikiwa ni gawio la wanahisa kutoka Benki ya DCB kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godrin Gondwe (wapilikushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Zawadia Nanyaro, hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe; Selemani Jafo (wa tatu kushoto), akikabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya shilingi 30,780,000 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga ikiwa ni gawio la hisa za shirika hilo kutoka Benki ya DCB. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Zawadia Nanyaro, hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, akiwakaribisha Mkuu Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri,na Mkurugenzi wa Jiji Bi Sipora Jonathan wakati wa hafla ya Benki ya DCB ilipokuwa ikitoa Gawio kwa wanahisa wake wakuu jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Uwekezaji (UTT) Simon Migangala wakati wa hafla ya benki ya DCB ya kutoa gawio kwa wanahisa wake wakuu jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Zawadia Nanyaro.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive