Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati alipofanya muendelezo wa ziara zake katika wilaya ya Ilala alipotembelea na kukagua ujenzi wa Hospital inayojengwa Chanika jijini humo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaelekeza Manispaa ya Ilala kuhakikisha Hospital mpya ya Wilaya hiyo iliyopo Kata ya Kivule inaanza kutoa huduma za kimatibabu kwa wananchi kabla ya June Mosi ambapo leo amewakabidhi magodoro 286 kwaajili ya Wagonjwa.
RC Makonda amesema kama majengo yote ya Hospital yamekamilika haoni sababu ya kutokutumika ambapo amesema miongoni mwa huduma zitakazoanza kutolewa ni pamoja na Huduma ya Mama na Mtoto, OPD, Uzazi na huduma ya Vipimo Mahabara huku akimuelekeza Mganga Mkuu kuhakikisha anapeleka Watumishi wa Afya 60 kwaajili ya kutoa huduma.
Aidha RC Makonda ameitaka Manispaa hiyo kuhakikisha Ujenzi wa Jengo la Gorofa nne la watu wenye uwezo wa kupata huduma binafsi linakamilika na kukabidhiwa ifikapo August 31 na ameelekeza katika hospital hiyo pawepo na Jengo la Wagonjwa wa dharura (ICU).
Katika hatua nyingine RC Makonda amesema Serikali inaendelea kutatua changamoto ya ubovu wa barabara za Banana, kitunda na Msongola zenye urefu wa Km 14.7 ambapo kwa sasa takriban Km 3.2 zinajengwa kwa kiwango cha lami.
Hata hivyo RC Makonda amesema ifikapo June Mosi ujenzi wa madaraja Mawili ya Ulongoni A na B utaanza ambapo gharama halisi ya mradi ni shilini Bilioni 7.
0 comments:
Post a Comment