Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa ziara yake yakukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Bamaga hadi Shekilango ambao ni moja ya miradi inayotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Ukaguzi Ukiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa maelekezo kwa baadhi ya watendaji wakati alipotembelea eneo la Sinza Mapambano kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Bamaga hadi Shekilango ambao ni moja ya miradi inayotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Brian Peter)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemtaka Mkandarasi anaejenga Barabara ya Sinza inayoanzia Bamaga hadi Shekilango kuhakikisha Ujenzi unakamilika kwa Wakati ili kupunguza kilio cha foleni kwa watumiaji wa njia hiyo.
RC Makonda amesema barabara hiyo inayojengwa ina urefu wa Km 3.7 na upana wa Mita 22 ambapo itakuwa na Njia nne za Magari pamoja na Barabara ya watembea kwa miguu, Taa za Kisasa, Mitaro ya Maji na Bustani.
Aidha RC Makonda amesema ujenzi huo unaenda sambamba na ujenzi wa Barabara unganishi ikiwemo ya Kuelekea Kebbys hotel, Chuo cha ustawi wa jamii, Mwenge TRA, Sinza Mapambano, Lion hotel, Sinza meeda na Barabara ya Sinza Makaburini.
Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza Viongozi wote wa Mkoa, Wilaya na Jiji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi na kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliokusudiwa.
0 comments:
Post a Comment