A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, May 25, 2020

RC MAKONDA AMUELEKEZA MKANDARASI WA UJENZI WA STAND MPYA YA MABASI YA MBEZI LUIS KUKABIDHI MRADI KWA MUDA ULIOPANGWA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda akizungumza wakati wa muendelezo wa ziara yake yakukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Ubungo ambapo ametembelea Mradi wa ujenzi wa Stand mpya ya mabasi inayojengwa mbezi jijini humo.
Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo, Mhe.Beatrice Dominic akitoa taarifa na maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za kisasa za Manispaa ya Ubungo wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ikiwepo barabara Stendi ya Mabasi inayojengwa mbezi katika Wilaya ya hoyo.



Mkuu wa mkoa akiendelea kukagua Ujenzi huo. (Picha zote na Brian Peter)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemuelekeza Mkandarasi wa Ujenzi wa Stand mpya ya mabasi ya Mikoani na nje ya nchi ya Mbezi Louis ambayo ujenzi wake kwa sasa umefikia 70% kuhakikisha Ujenzi huo unakamilika na kukabidhiwa kwa wakati.


RC Makonda amesema ujenzi wa Stand hiyo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 50.9 na itakuwa na uwezo wa kuegesha Mabasi Makubwa 700 na Magari Madogo yasiyopungua 300 ambapo ndani yake kutakuwa na Jengo la abiria, Jengo la utawala, Shopping mall's, Hotel, Hostel, kituo cha polisi, matawi ya bank, Migahawa na eneo la wafanyabiashara wa chakula.


Aidha RC Makonda ameelekeza Manispaa ya Ubungo kuhakikusha ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ubungo unaanza kabla ya Mwezi June na Mkandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kabla ya Mwezi September mwaka huu kwakuwa tayari Rais Dkt. Magufuli aliagiza kujengwa kwa Hospital hiyo lakini cha kushangaza baadhi ya wizara zimekuwa zikipiga danadana kutoa fedha hizo.


Pamoja na hayo RC Makonda ametembelea Ujenzi wa Jengo la Manispaa ya Ubungo linalogharimu kiasi cha bilioni 6 ambalo ujenzi wake umefikia 65% na kuwataka TBA kuhakikisha Jengo linaanza kutoa huduma kabla ya mwezi August mwaka huu kwakuwa wamekuwa wakisuasua licha ya kuongezewa muda.


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe.Kisare Matiku Makori akiripoti jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ikiwepo barabara Stendi ya Mabasi inayojengwa mbezi  katika Wilaya ya hoyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive