A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, May 26, 2020

WANYAMA 380 WAMEKUFA KWA KUGONGWA NA MAGARI NDANI YA MWAKA MMOJA 2019


WANYAMA 380 wamekufa kwa kugongwa na magari  ndani ya mwaka mmoja 2019 katika eneo la mapito ya wanyama kuanzia Magugu wilayani Babati hadi Makuyuni wilayani Monduli ambayo husaidia wanyama kwenda hifadhi ya tarangire na hifadhi ya Manyara.

Mtafiti wa wanyamapori katika mradi wa Simba Tarangire, Dk Bernard Kissui alitoa taarifa hizo juz katika kikao cha kujadili kuokoa eneo la mapito ya wanyama kwa kuchinja hadi Mdori ambalo linaendelea kuvamiwa .

Dk Kissui alisema kati ya januari hadi Desemba 2019, wamebaini wanyama 380 kugongwa katika barabara hiyo hali ambayo inatishia uhai wa hifadhi za taifa za Tarangire na Manyara.

Alisema katika eneo hilo ,licha ya wanyama kugongwa pia kuna uvamizi mkubwa wa wananchi, kulima na kuweka makazi ndani ya eneo hilo.
“Kama serikali isipochukuwa hatua sasa, wanyama wengi watapotea lakini pia tutaathiri ikolojia ya Tarangire na Manyara”alisema

Alisema wanyama hao, wanagongwa wengi nyakati za
usiku hasa kutokana na mwendokasi ya magari.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantite Kanyasu, aliagiza Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Wanyamapori(TAWA) na Taasisi ya Utafiti wanyamapori(TAWIRI), kuandaa mabango na kuweka katika eneo la barabara hiyo kutoka Arusha hadi Babati.

“naagiza kuwekwa mabango ya kuonesha faini ukigonga mnyama mfano simba dola 4000,pia yawekwe mabango ya kupunguza mwendo kwa kuonesha wanyama wanaovuka maeneo hayo”alisema

Alisema pia atazungumza na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,ili kuhakikisha zinawekwa alama za kupunguza mwendo za kisasa ambazo haziwezi kuisha kwa muda mfupi.

Mkurugenzi wa utafiti wa TAWIRI, Dk Julius Keyyu alisema ili kuokoa wanyama na mapito yao ni muhimu kuwepo ushirikiano baina ya wananchi, viongozi wa vijiji na wadau wa utalii.

Dk Keyyu alisema tayari taasisi kadhaa zimekuwa zikifadhili mradi wa kufatilia wanyama, ikiwepo taasisi ya Chemchem Foundation ambayo imegharamia mradi wa Tembo katika eneo hilo kufungwa vifaa vya mawasiliano kufatilia mapito yao.

Akizungumzia taaarifa hiyo,Mkurugenzi wa Wanyamapori
nchini, Dr Maurus Msuha alisema ni lazima sasa serikali kwa kushirikiana na wadau kuchukuwa hatua za kulinda eneo hilo la mapito ya wanyama.

Alisema Katika kulinda eneo hili ni lazima barabara kuwekwa alama na kutolewa adhabu kwa wanaogonga wanyama lakini pia katika kulinda mapito ya wanyama wananchi wanapaswa kushirikishwa ili kupisha maeneo ya mapito ya wanyama
Share:

Monday, May 25, 2020

RC MAKONDA AMUELEKEZA MKANDARASI WA UJENZI WA STAND MPYA YA MABASI YA MBEZI LUIS KUKABIDHI MRADI KWA MUDA ULIOPANGWA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda akizungumza wakati wa muendelezo wa ziara yake yakukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Ubungo ambapo ametembelea Mradi wa ujenzi wa Stand mpya ya mabasi inayojengwa mbezi jijini humo.
Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo, Mhe.Beatrice Dominic akitoa taarifa na maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za kisasa za Manispaa ya Ubungo wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ikiwepo barabara Stendi ya Mabasi inayojengwa mbezi katika Wilaya ya hoyo.



Mkuu wa mkoa akiendelea kukagua Ujenzi huo. (Picha zote na Brian Peter)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemuelekeza Mkandarasi wa Ujenzi wa Stand mpya ya mabasi ya Mikoani na nje ya nchi ya Mbezi Louis ambayo ujenzi wake kwa sasa umefikia 70% kuhakikisha Ujenzi huo unakamilika na kukabidhiwa kwa wakati.


RC Makonda amesema ujenzi wa Stand hiyo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 50.9 na itakuwa na uwezo wa kuegesha Mabasi Makubwa 700 na Magari Madogo yasiyopungua 300 ambapo ndani yake kutakuwa na Jengo la abiria, Jengo la utawala, Shopping mall's, Hotel, Hostel, kituo cha polisi, matawi ya bank, Migahawa na eneo la wafanyabiashara wa chakula.


Aidha RC Makonda ameelekeza Manispaa ya Ubungo kuhakikusha ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ubungo unaanza kabla ya Mwezi June na Mkandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kabla ya Mwezi September mwaka huu kwakuwa tayari Rais Dkt. Magufuli aliagiza kujengwa kwa Hospital hiyo lakini cha kushangaza baadhi ya wizara zimekuwa zikipiga danadana kutoa fedha hizo.


Pamoja na hayo RC Makonda ametembelea Ujenzi wa Jengo la Manispaa ya Ubungo linalogharimu kiasi cha bilioni 6 ambalo ujenzi wake umefikia 65% na kuwataka TBA kuhakikisha Jengo linaanza kutoa huduma kabla ya mwezi August mwaka huu kwakuwa wamekuwa wakisuasua licha ya kuongezewa muda.


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe.Kisare Matiku Makori akiripoti jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ikiwepo barabara Stendi ya Mabasi inayojengwa mbezi  katika Wilaya ya hoyo.
Share:

Sunday, May 24, 2020

RC MAKONDA AWAAGIZA MANISPAA YA ILALA KUHAKIKISHA HOSPITAL YA WILAYA INAANZA KUTOA HUDUMA KABLA JUNE MOSI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati alipofanya muendelezo wa ziara zake katika wilaya ya Ilala alipotembelea na kukagua ujenzi wa Hospital inayojengwa Chanika jijini humo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaelekeza Manispaa ya Ilala kuhakikisha Hospital mpya ya Wilaya hiyo iliyopo Kata ya Kivule inaanza kutoa huduma za kimatibabu kwa wananchi kabla ya June Mosi ambapo leo amewakabidhi magodoro 286 kwaajili ya Wagonjwa.


RC Makonda amesema kama majengo yote ya Hospital yamekamilika haoni sababu ya kutokutumika ambapo amesema miongoni mwa huduma zitakazoanza kutolewa ni pamoja na Huduma ya Mama na Mtoto, OPD, Uzazi na huduma ya Vipimo Mahabara huku akimuelekeza Mganga Mkuu kuhakikisha anapeleka Watumishi wa Afya 60 kwaajili ya kutoa huduma.


Aidha RC Makonda ameitaka Manispaa hiyo kuhakikisha Ujenzi wa Jengo la Gorofa nne la watu wenye uwezo wa kupata huduma binafsi linakamilika na kukabidhiwa ifikapo August 31 na ameelekeza katika hospital hiyo pawepo na Jengo la Wagonjwa wa dharura (ICU).


Katika hatua nyingine RC Makonda amesema Serikali inaendelea kutatua changamoto ya ubovu wa barabara za Banana, kitunda na Msongola zenye urefu wa Km 14.7 ambapo kwa sasa takriban Km 3.2 zinajengwa kwa kiwango cha lami.


Hata hivyo RC Makonda amesema ifikapo June Mosi ujenzi wa madaraja Mawili ya Ulongoni A na B utaanza ambapo gharama halisi ya mradi ni shilini Bilioni 7.


Katika hatua nyingine RC Makonda amewaelekeza TANESCO kuhakikisha wanawafikishia huduma ya Umeme wakazi wa Zingiziwa na Kazimzungu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilia na kero ya kutokufikishiwa umeme.



  
(Picha zote na Brian Peter)
Share:

Saturday, May 23, 2020

RC MAKONDA AMTAKA MKANDARASI WA UJENZI WA BARABARA YA SINZA KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa ziara yake yakukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Bamaga hadi Shekilango ambao ni moja ya miradi inayotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Ukaguzi Ukiendelea



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa maelekezo kwa baadhi ya watendaji wakati alipotembelea eneo la Sinza Mapambano kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Bamaga hadi Shekilango ambao ni moja ya miradi inayotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Brian Peter)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemtaka Mkandarasi anaejenga Barabara ya Sinza inayoanzia Bamaga hadi Shekilango kuhakikisha Ujenzi unakamilika kwa Wakati ili kupunguza kilio cha foleni kwa watumiaji wa njia hiyo.

RC Makonda amesema barabara hiyo inayojengwa ina urefu wa Km 3.7 na upana wa Mita 22 ambapo itakuwa na Njia nne za Magari pamoja na Barabara ya watembea kwa miguu, Taa za Kisasa, Mitaro ya Maji na Bustani.

Aidha RC Makonda amesema ujenzi huo unaenda sambamba na ujenzi wa Barabara unganishi ikiwemo ya Kuelekea Kebbys hotel, Chuo cha ustawi wa jamii, Mwenge TRA, Sinza Mapambano, Lion hotel, Sinza meeda na Barabara ya Sinza Makaburini.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza Viongozi wote wa Mkoa, Wilaya na Jiji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi na kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliokusudiwa.
Share:

Monday, May 18, 2020

WAKAZI WA VINGUNGUTI SASA WATAKIWA KUKAA MKAO WA KIBIASHARA

IMG-20200517-WA0045
IMG-20200517-WA0047%2B%25281%2529Ujenzi wa Machinjio ya kisasa yanayojengwa Vingunguti Jijini Dar es Salaam, yamefikia hatua za mwisho  wenye thamani ya shilingi  Billion 12.4, ambapo jengo Hilo lina vyumba 2 vya kufanyia ibada kwa Wakristo Pamoja na Waislam.

Akizungumza  mara Baada ya kufanya ziara katika Machinjio hayo, Meya wa Ilala ambae pia ni Diwani wa Vingunguti,  Omary Kumbilamoto,  amesema vyumba hivyo vimejengwa kutokana na agizo la Rais John Magufuli ambapo limetekelezwa na wafanyakazi katika machinjio hayo watasali kulingana na dini zao.

Aidha amesema jengo hilo litafungwa mafriji makubwa yenye uwezo wa kuhifadhi ng'ombe zilizochinjwa(Nyama) 1000 Pamoja na mbuzi 1000, na kuongeza kuwa uchinjaji utafanyika kwa saa 24, kutokana na kufungwa kamera za kusaidia usalama, Pamoja na mashine za kuchinjia za kisasa zitawekwa katika Machinjio hayo.

Ameongeza kuwa  machinjio yatakuwa ya kisasa na kuwavutia watu wengi hata watalii pia, kwani kutajengwa mabwawa ya maji taka ambayo yatachakatwa na kupata maji Safi kwa ajili ya umwagiliaji wa bustani zinazozunguka eneo Hilo.

Pia amewataka wafanyabiashara wa Vingunguti kutumia fursa kwani miguu, maini, ngozi, mikia ya ng'ombe ni tija hivyo waitumie vizuri kwani machinjio hayo yatakuwa Ni bora Tanzania nzima na ya kimataifa.

Mbali na hayo amewataka wafanyabiashara wa hoteli zinazozunguka machinjio hayo kuboresha zaidi Pamoja na wahudumu kuwa wakarimu Pindi wageni watakapofika ili kuwavutia zaidi.Ujenzi wa Machinjio ya kisasa yanayojengwa Vingunguti Jijini Dar es Salaam, yamefikia hatua za mwisho  wenye thamani ya shilingi  Billion 12.4, ambapo jengo Hilo lina vyumba 2 vya kufanyia ibada kwa Wakristo Pamoja na Waislam.

Akizungumza  mara Baada ya kufanya ziara katika Machinjio hayo, Meya wa Ilala ambae pia ni Diwani wa Vingunguti,  Omary Kumbilamoto,  amesema vyumba hivyo vimejengwa kutokana na agizo la Rais John Magufuli ambapo limetekelezwa na wafanyakazi katika machinjio hayo watasali kulingana na dini zao.

Aidha amesema jengo hilo litafungwa mafriji makubwa yenye uwezo wa kuhifadhi ng'ombe zilizochinjwa(Nyama) 1000 Pamoja na mbuzi 1000, na kuongeza kuwa uchinjaji utafanyika kwa saa 24, kutokana na kufungwa kamera za kusaidia usalama, Pamoja na mashine za kuchinjia za kisasa zitawekwa katika Machinjio hayo.

Ameongeza kuwa  machinjio yatakuwa ya kisasa na kuwavutia watu wengi hata watalii pia, kwani kutajengwa mabwawa ya maji taka ambayo yatachakatwa na kupata maji Safi kwa ajili ya umwagiliaji wa bustani zinazozunguka eneo Hilo.

Pia amewataka wafanyabiashara wa Vingunguti kutumia fursa kwani miguu, maini, ngozi, mikia ya ng'ombe ni tija hivyo waitumie vizuri kwani machinjio hayo yatakuwa Ni bora Tanzania nzima na ya kimataifa.

Mbali na hayo amewataka wafanyabiashara wa hoteli zinazozunguka machinjio hayo kuboresha zaidi Pamoja na wahudumu kuwa wakarimu Pindi wageni watakapofika ili kuwavutia zaidi.
Share:

Friday, May 15, 2020

KAMPUNI YA EVERWELL CABLE AND ENGINEERING CO. LTD YACHANGIA SH. MILIONI 100 KUKABILIANA NA CORONA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 100,000,000/= kutoka kwa kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kupokea hundi ya Sh. 100,000,000/=, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (Kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Tixon Nzunda wakati wa kupokea hundi ya Sh. 100,000,000/=, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi ya Sh. 100,000,000/=, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (Kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Tixon Nzunda wakati wa kupokea hundi ya Sh. 100,000,000/=, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb), amepokea msaada wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 100 iliyotolewa na kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, inayojishughulisha na uzalishaji wa nyaya za kusafirisha umeme kwenye miradi mbalimbali ya umeme hapa nchini, kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID- 19).

Waziri amepokea mchango huo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 13 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa kupokea mchango huo Waziri Mhagama ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

“Kwa niaba ya serikali nawashukuru sana kwa kuwa sehemu ya watanzania katika kipindi hiki cha mapambano ya janga la COVID-19. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa sehemu ya shida na raha za Taifa hili,” ameeleza Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amewahakikishia watanzania kuwa michango hiyo inasimamiwa vyema na serikali kwa kuitumia michango hiyo katika kushughulikia majukumu yaliyopangwa ya kupambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

Awali, Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani ameipongeza kampuni hiyo kwa mchango wao kwa Serikali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

“Kampuni hii ni moja ya wawekezaji waliojenga Kiwanda hapa nchini, lakini pamoja na shughuli za uwekezaji wameguswa katika kipindi hiki wakati serikali inapambana na janga hili la ugonjwa wa COVID-19, tunawashukuru sana kwa mchango wenu kwa watanzania ”amesema Dkt. Kalemani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, Bw. Jiaopeng Lu ameeleza kuwa Kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na watanzania katika uzalishaji wa bidhaa za kiwanda kabla ya Janga hili la Ugonjwa wa COVID-19, hivyo hawana budi kuhakikisha watanzania wanakuwa salama ili waendelee kushirikiana nao katika shughuli za uzalishaji.
Share:

Tuesday, May 5, 2020

Absa Tanzania yaunga mkono juhudi za serikali mapambano dhidi ya Covid-19

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, (katikati), akimshukuru Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utumishi wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick Foya (kushoto), baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuisaidia serikali katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayotokana na virusi vya Corona (Covid-19) kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Mabula Daudi Mchembe. Vifaa hivyo vikiwemo barakoa, vitakasa mikono na gloves vyenye thamani ya shs milioni 20 vimekabidhiwa katika ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Rasilimali watu na Utumishi wa Benki ya Absa Tanzania Patrick Foya (kushoto), akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba kusaidia juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa wa corona (Covid-19), kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya. Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Mabula Daudi Mchembe. Vifaa hivyo vikiwemo barakoa, vitakasa mikono na gloves vyenye thamani ya shs milioni 20 vimekabidhiwa katika ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya. Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza wakati akipokea vifaa tiba kutoka kwa Mkurugenzi wa Rasiliamali Watu na Utumishi wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick Foya (kushoto) ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika kusaidia juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19). Vifaa hivyo vikiwemo barakoa, vitakasa mikono na gloves vyenye thamani ya shs milioni 20 vimekabidhiwa katika ofisi za wizara, Dar es Salaam leo.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive