A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, September 6, 2017

Halotel FINCA launches Halo Yako service

         
Commissioner in the Finance and Planning Ministry, John Rubaga (centre) presses a button to officiate at the official launching of ‘Halo Yako’ service in Dart es Salaam yesterday. Looking on left is Halotel Managing Director, Le Van Dai and FINCA Managing Director,  Issa Ngwegwe. Halo Yako designed by Halotel and Finca will enable customers to save their money. Photo by Brian Peter
Commissioner in the Finance and Planning Ministry, John Rubaga (centre), Halotel Managing Director, Le Van Dai (left) and  Finca Microfinance Bank Managing Director, Issa Ngwegwe applauses during the official launching of ‘Halo Yako’ service in Dart es Salaam yesterday. Halo Yako designed by Halotel and Finca will enable customers to save their money. Photo by Brian Peter
     JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
      WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO                                                                                                                 
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO (MB), WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO KATIKA UZINDUZI WA HUDUMA YA HALO YAKO MALENGO INAYOENDESHWA  KATI YA KAMPUNI  YA
HALOTEL NA FINCA TANZANIASERENA HOTEL DAR ES SALAAM,
 5 SEPTEMBA , 2017

Ndugu Le Van Dai, Mkurugenzi wa Halotel Tanzania,

Ndugu Issa Ngwegwe, Mkurugenzi wa FINCA Tanzania,

Menejimenti na Wafanyakazi wa Kampuni ya Halotel na FINCA,

Wawakilishi wa Vyombo vya Habari,

Wageni Waalikwa,

Mabibi na Mabwana.
Kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, napenda kuushukuru Uongozi wa Hallotel na FINCA kwa kumualika katika hafla hii ya uzinduzi wa huduma mpya ya HALO YAKO ambayo nimeambiwa italeta faraja ya kweli kwa wananchi, hususan wa kipato cha chini kwa kuwawezesha kujiwekea akiba ili kufikia malengo yao kiuchumi na hali ya maisha kwa ujumla.

Hata hivyo, kutokana na majukumu mengine ya Kitaifa aliyonayo, hususan katika kipindi hiki cha vikao vya Bunge vilivyoanza leo hii Dodoma, Mhe. Waziri ameshindwa kuhudhuria katika tukio hili muhimu na hivyo amenituma nimwakilishe. Ninamshukuru sana kwa dhamana hiyo na natumaini kwamba nitaifanya kazi hiyo ipasavyo.

Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana, Serikali inatambua kwamba jitihada za Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini haziwezi kuwa na mafanikio bila kushirikisha Sekta Binafsi, hususan Makampuni ya Mawasiliano ya simu.

 Vilevile, Serikali imekuwa ikifanya mageuzi mbalimbali kwa mtazamo wa kuiwezesha Sekta Binafsi kuwa Injini ya Ukuaji wa Uchumi wetu, ambapo tangu kuingia kwa Mfumo wa Soko Huria hapa Nchini, Sekta Binafsi imeweza kuchukua nafasi yake na kuwekeza katika huduma mbalimbali zikiwemo huduma za simu hususan huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi.

Sisi kama Serikali tutaendelea kuhakikisha kuwa uhusiano wa karibu uliopo kati ya Serikali na Sekta Binafsi zikiwemo Kampuni za mawasiliano ya simu unadumishwa. Aidha, tutaendelea kuheshimu mchango wa Sekta Binafsi ambao ni kichocheo kikubwa  kwa  Uchumi  na  maendeleo ya Taifa letu. Vilevile, Serikali itaendelea na jukumu lake la kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuhamasisha wawekezaji zaidi Nchini.

            Ndugu Wageni Waalikwa, ninaitambua Halotel Tanzania kuwa ni miongoni mwa kampuni za simu hapa Tanzania zinazoongoza kwa kutoa huduma za kibunifu za mawasiliano zenye wigo mpana na kuchangia katika shughuli mbalimbali za maendeleo na Taifa kwa ujumla; hali kadhalika, FINCA kwa kutoa huduma mbalimbali za kibenki kwa watanzania wengi mijini na vijijini.  Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango, ninaomba mniruhusu nichukue fursa hii kuwapongeza Halotel Tanzania na FINCA kwa jitihada zao za kuiunga mkono Serikali yetu katika kutoa huduma za mawasiliano, kifedha na kuongeza ajira ndani ya jamii yetu.

            Ndugu Wageni Waalikwa, huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi  zimekuwa ni muhimu na kichocheo kikubwa katika maendeleo ya nchi yetu. Serikali tunaunga mkono jitihada hizi kwani zinaleta mapinduzi na maendeleo huku zikichangia kubadili maisha ya watanzania wengi na kuwawezesha kuwa na mifumo rasmi ya kutuma na kupokea pesa. Maendeleo ya kiuchumi yamechochea watanzania wengi kutumia simu zao za mkononi kwa kufanya miamala mbalimbali ya kifedha katika akaunti zao mahali popote walipo.
 Asanteni sana Halotel kwa kufika kila kona ya Nchi yetu, hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma hizi.
Niwapongeze tena Halotel na FINCA kwa kuingia katika ushirikiano huu; ninaona faraja kubwa sana kutambua kuwa sekta ya fedha inaendelea kupata mdau mwingine katika kuhakikisha huduma za fedha zinasambaa kote nchi nzima.


Mabibi na Mabwana, wengi wetu kama sio wote hapa tunatumia huduma za simu katika kutuma na kupokea fedha na hata kujiwekea akiba, pengine mniruhusu kwa uchache tu kuizungumzia huduma ya HALOPESA. Nimeelezwa kuwa, huduma hii ya HALOPESA tangu ilipoanzishwa imeleta mapinduzi makubwa, jinsi tunavyotuma na kupokea pesa kwa ndugu jamaa na marafiki popote pale nchini kwa urahisi, uharaka na kwa usalama zaidi.

 Huduma hii imekuwa mkombozi mkubwa kwa wajasiliamali wengi na wananchi wanaoishi vijijini. Niipongeze tena kampuni ya HALOTEL pamoja na kampuni zingine kwa kazi hii kubwa mnayoifanya kuhakikisha huduma ya fedha kupitia mitandao ya simu inabakia kuwa ya uhakika na ya kuaminika; na pia kwa namna mnavyoshirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kwamba kuna mafanikio makubwa sokoni ambayo kwayo yanaleta tija kwa wananchi wetu.

 Aidha, nitoe wito kwa makampuni yote ya simu kuendelea kutoa huduma zenye gharama nafuu kwa wananchi na kwa uwazi zaidi. Mkumbuke kuwa mamilioni ya wananchi wanawaamini na kuthamini ubora wa bidhaa na huduma zenu.

            Mabibi na Mabwana, napenda kuwaasa kidogo Kampuni ya HALOTEL kwamba, japo mmekuwa wabunifu katika huduma za mawasiliano, msibweteke! Bali sasa ni muda muafaka wa kuendelea kuongeza juhudi katika mambo yafutayo:

·         Endeleeni kuwa  wabunifu zaidi na kuboresha  huduma kwa wateja ili Kampuni iweze kupata faida kubwa zaidi na hivyo kulipa kodi kubwa kwa Serikali na kuchangia maendeleo ya Taifa;

·         Endeleeni kutimiza wajibu wenu ili huduma mnazozitoa ziweze kuwafikia wananchi wengi zaidi na kwa gharama nafuu; na

·         Endeleeni kuhamasisha wananchi  wajiunge na huduma hii mpya ya HALO YAKO na wasaidieni wananchi wa kipato cha chini  kufikia malengo yao na hatimaye waweze kuongeza kipato chao na cha taifa kwa ujumla.

Kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, nimalizie kwa kuwashukuru nyote mliofika hapa kushuhudia uzinduzi huu. Nina imani kwamba kwa pamoja sote tutakuwa mabalozi wazuri wa huduma hii ya HALO YAKO. Wito wangu kwa Wananchi wote ni kwamba, tumieni kikamilifu huduma hii mpya ya HALO YAKO inayozinduliwa leo ili muweze kuendeleza shughuli zenu za maendeleo. Mwisho kabisa, nawatakia Halotel na FINCA ufanisi zaidi katika shughuli zenu za kila siku ili kwa pamoja tusaidiane kujenga Taifa letu.

Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana, kabla sijahitimisha hotuba hii, naomba niyaseme machache kwa lugha ya kigeni kwa manufaa ya wale ambao hawajabahatika kuijuwa lugha hii adhimu ya Kiswahili:

Ladies and Gentlemen:
Allow me to share with you few messages in English for the benefit of some of us:Let me express my sincere gratitude for the honor accorded to the Minister for Finance and planning, Hon. Philip I. Mpango (MP) at this auspicious occasion of launching HALO YAKO Service by Halotel and Finca. I am really humbled and privileged to represent him, since he could not make it due to other pressing public service responsibilities, particularly at the time when Parliamentary Sessions start today. Kindly accept his apology. I trust I will be able to represent him well.
The role of the financial sector is to transfer funds from surplus units to deficit units, thereby promoting greater efficiency and economic growth by channeling funds from people who do not have productive use for them to those who do.
This includes among others, mobilizing savings from the population, guarding against uncertainty, assessing risks and providing credit.  Along these lines, the financial sector finds itself capable of linking economic agents in the manner that supports expansion of economic opportunities, creates jobs, and generates revenue for the Government
. This is what Halotel and Finca Tanzania are trying to achieve!On behalf of Hon. Minister, may I take this opportunity to congratulate them for joining forces to create a service such as this one which we are about to launch today; the service is geared towards assisting millions of Tanzanians, who may have no easy access to conventional banking facilities; indeed this is financial inclusion at work
!One of the biggest challenges we face today is the ability to mobilize savings and access to credit at affordable prices. However, there is enough evidence to show that technology can significantly help to reduce some of the barriers to access, such as remoteness and cost of providing financial services.
 It is our sincere hope that, the product we are about to launch today will meet our expectations on what technology can facilitate to achieve!Finally, while efforts need to be sustained to further increase inclusion and access, there is a need to expand and sustain digital financial services ecosystem, including money transfer platforms, payment solutions, savings, financing, micro-insurance, financial planning and access to capital markets securities.
 I trust that Halotel and Finca Tanzania, and indeed all stakeholders in the financial system will continue to be innovative in designing various products that can cater for long-term needs of customers at affordable prices.The Government recognizes the role of the private sector in Tanzania’s economic growth endeavours, and will therefore continue to support it.

Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana, baada ya kusema hayo, sasa napenda kutamka kwamba niko tayari Kuzindua rasmi huduma ya HALO YAKO inayomwezesha hasa mwananchi wa kipato cha chini kuweza kujiwekea akiba na kufikia malengo yake.


Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive