Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika (kushoto), akikaribishwa na Mkurugenzi wa
Biashara wa NBC, Alvis Ndunguru wakati akiwasili kwa ajili ya uzinduzi wa Klabu
ya Biashara ya NBC mkoani Mbeya. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NBC, William
Kallaghe. Uzinduzi huo ulitanguliwa na semina ya siku moja juu
ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati.
Mwakilishi
kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gabriel Mwangosi (kulia),
akifundisha masuala mbalimbali kuhusu kodi katika semina ya siku moja
iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake wadogo na wa kati mjini Mbeya. Semina hiyo
ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani Mbeya hivi
karibuni.
Mkurugenzi wa Biashara wa
NBC, Elvis Ndunguru akizungumza wakati
wa hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya NBC, mkoani Mbeya. Uzinduzi huo ulitanguliwa na semina ya
siku moja juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa
kati. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wateja wa NBC, wajasiriamali na maofisa
wa serikali mkoani humo.
Baadhi ya wateja wa
NBC mkoani Mbeya wakijipiga picha wenyewe ‘maaarufu kama selfie’
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya NBC mkoani humo hivi
karibuni. Uzinduzi huo ulitanguliwa na
semina ya siku moja juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha
wadogo na wa kati ilihudhuriwa na wateja wa NBC, wajasiriamali na
maofisa waandamizi wa serikali mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment