A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, July 5, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA TAWI JIPYA BUKOBA

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Moses Machali (wapili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank lililozinduliwa katika Wilaya hiyo hivi karibuni ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuhakikisha inawafikia wateja wake kila kona ya nchi. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Mr. Sabasaba Moshingi, Mkurugenzi Rasilimali watu Bi. Diana Myonga pamoja na Mkurugenzi wa Mikopo Mr. Henry Bwogi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania TCB Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki hiyo lililozinduliwa katika Wilaya Bukoba hivi karibuni ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuhakikisha inawafikia wateja wake kila kona ya nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Moses Machali akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania TCB Sabasaba Moshingi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Benki hiyo mara baada ya uzinduzi wa Tawi hilo.
Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKI MAONESHO YA 46 YA BIASHARA SABASABA YAJIKITA ZAIDI KWENYE KUTOA HUDUMA BORA

Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB),Joanitha Deogratias (wapili kushoto), akizungumza na baadhi ya watejawaliotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalim Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo.

Afisa Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania TCB Cornel Mlay (kulia), akizungumza na mmoja wa mteja  alietembelea banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki, kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Jk Nyerere Barabara ya Kilwa. Katikati ni Afisa Uwendeshaji wa Benki hiyo Godbright Mlay.Afisa uwendeshaji wa Benki ya Biashara Tanzania TCB Salha Singano (wapili kushoto) akitoa maelekezo kwa moja ya mteja alipotembelea Banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki, kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Jk Nyerere Barabara ya Kilwa. kushoto ni Afisa wa kitengo cha ICT wa TCB Joseph BukuruMeneja Uhusiano wa wateja wakubwa wa Benki ya Biashara Tanzania TCB Shilla Senkoro  (kushoto), akizungumza na mteja kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki, kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Jk Nyerere Barabara ya Kilwa.

****************************************************

Benki ya Biashara Tanzania TCB imeshiriki maonesho ya 46 ya biashara Sabasaba ambapo benki hiyo imeeleza namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za kibenki hasa katika kuongeza matawi kila  mkoa na wilaya ili kusogeza huduma kwa wateja wake.

 

Akizungumza kwenye maonyesho hayo, Meneja Mwandamizi Udara ya Mikopo wa benki hiyo Bi. Joanitha Deogratias alisema benki imejidhatiti katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wengi kwa kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.

 

“Tunatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na wale wakubwa  pia mikopo kwa wastaafu kwaajili ya kuendeleza shughuli ndogondogo za kiuchumi.

 

Joanitha alisema katika kuboresha huduma TCB imefanikiwa kutoa huduma za kibenki za kidigitali ambapo wateja wanaweza kufanya malipo mtandaoni kwa urahisi zaidi.

 

alisema benki hiyo imechukua hatua mbalimbali ili kutoa unafuu kwa wateja wake kutokana  hali ya kiuchumina ikiwemo kutoa unafuu wa riba.

 

“Sisi kama benki  ya Biashara Tanzania TCB tumefungua milango kwa wateja wetu wote waliokopa na ambao hawajakopa, tunataka kuwaendeleza wateja hasa kwa kusikiliza changamoto zao na tumeendelea  kufungua matawi Karibia nchi nzima, ” alisema.

 

Vilevile benki hiyo imechukua hatua yakuwakumbusha nakuwahimiza watanzania wote kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti.

 

Aliwahimiza watu wote waendelee kutembelea katika banda la Tanzania Commerci Bank ili kujionea huduma mbalimbali zinazopatikana katika benki hiyo.

Share:

Thursday, June 30, 2022

VODACOM TANZANIA YAKABIDHI VIFAA KWA SHULE YA WASICHANA

 


Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis(wan ne kushoto) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa Mkuu wa shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam, Hollness Moshi (kushoto) ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom kwa shule hiyo, wafanyakazi hao wametoa viti 100, meza 100, vifaa vya kuzalisha umeme jua (solar power) 20 na vitabu 388. Kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria, Agapinus Tax na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.


Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza wakati wa Hafla ya kukabidhi misaada ya vifaa mbalimbali vya Elimu katika shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom kwa shule hiyo, wafanyakazi hao wametoa viti 100, meza 100, vifaa vya kuzalisha umeme jua (solar power) 20 na vitabu 388.


Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria wa kampuni yaVodacom Agapinus Tax akizungumza wakati wa Hafla ya kukabidhi misaada ya vifaa mbalimbali vya Elimu katika shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom kwa shule hiyo, wafanyakazi hao wametoa viti 100, meza 100, vifaa vya kuzalisha umeme jua (solar power) 20 na vitabu 388.


Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis(wa tano kushoto), akikata utepe wakati wa Hafla yakukabidhi misaada ya vifaa mbalimbali vya Elimu katika Shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom kwa shule hiyo, wafanyakazi hao wametoa viti 100, meza 100, vifaa vya kuzalisha umeme jua (solar power) 20 na vitabu 388. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria wa kampuni yaVodacom Agapinus Tax, uongozi wa shule pamoja na maofisa wengine wa Vodacom.


Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria wa kampuni yaVodacom Agapinus Tax akisalimiana na Mkuu wa shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam, Hollness Moshi wakati walipo kwenda kutoa msaada katika shule hiyo.


Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakitoa burudani ya ngoma za asili wakati wa kampuni ya Vodacom walipokwenda shuleni hapo kwa ajili ya kutoa misaada ya vifaa mbalimbali


Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria wa kampuni yaVodacom Agapinus Tax akikabidhi baadhi ya vitabu kwa wanafunzi shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom kwa shule hiyo, wafanyakazi hao wametoa viti 100, meza 100, vifaa vya kuzalisha umeme jua (solar power) 20 na vitabu 388.


Vodacom Tanzania Yakabidhi Vifaa kwa Shule ya WasichanaVodacom Tanzania Foundation leo imekabidhi vifaa na samani kwa Shule ya Wasichana ya Bethsaida mjini Dar es Salaam ambavyo kampuni ilishinda katika mashindano ya makampuni ya Vodacom duniani.


Akiongea wakati wa makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Vivienne Penessis alisema, “Elimu ni msingi pekee ambao unampatia mtu kianzio cha kujenga miasha bora.


Hii ni kweli zaidi kwa Watoto yatima ambao tegemeo lao ni elimu pekee.”Shule ya Wasichana ya Bethsaida ilichaguliwa kupokea msaada huu kwa kuwa ni moja ya shule chache zinazotoa elimu ya sekondari kwa Watoto yatima wa kike nchini.


Mkurugenzi wa Vodacom pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni waliikabidhi shule hiyo viti 100, vitabu Zaidi ya 300 pamoja na vifaa 20 vya kuzalisha umeme wa jua. Bi penessis alielezea Imani yake kuwa msaada huo utatumika ipasavyo kwani kampuni ya Vodacom ilijiridhisha juu ya utaalam na moyo wa kujitoa wa wafanyakazi wa shule ya Bethsaida.


Msaada huu unaendana na malengo ya Vodacom Tanzania kuongeza ujumuishwaji katika elimu. Hivi karibuni, kampuni ya Vodacom ilizindua mpango wa kupanua wigo wa mfumo wa E-Fahamu kufikia nchi nzima. E-Fahamu ni huduma inayotoa mawaidha ya elimu yenye viwango vya kimataifa na vyenye kukidhi miongozo ya serikali juu ya elimu.


Kuhusu Vodacom Tanzania FoundationThe Vodacom Tanzania Foundation ni sehemu ya kampuni ya Vodacom Tanzania PLC yenye mamlaka ya kutoa huduma za kijamii zikiwa zinawalenga zaidi wanwake na vijana. Foundation inajumuisha utoaji wa hisani na kutumia uwezo utakanao na teknolojia kuleta suluhisho kwa mahitaji ya kijamii.Ikishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, Vodacom Tanzania Foundationimesaidia zaidi ya miradi 120 hadi sasa ikiwa imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 15 kuboresha Maisha ya watanzania.Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://vodacom.co.tz/en/vodacom_foundation_aboutus/?SID=1u5nsmti8ahqks35k9tds71652
Share:

Wednesday, June 29, 2022

MAAJABU YA BIDHAA ZA LG SMART HOME , UOKOA NISHATI NA MUDA

 Na Mwandishi Wetu

• Faida kuu za vifaa Vya Nyumbani vya LG ni pamoja na kutoa urahisi na uharaka wa kutumia vifaa kama TV na friji, utendakazi ulioboreshwa kupitia teknolojia ya Upelelezi wa Artificial Intelligence (AI) kwa washer na kuokoa nishati kwa viyoyozi.

• Teknolojia mpya iliyobuniwa na Kampuni ya LG inayosifiwa kwa kusaidia kuhifadhi nishati na maji, kuwa rafiki wa mazingira huku ikitumika kwa urahisi, hivyo basi kukuza malengo muhimu ya maendeleo endelevu.

DAR ES SALAAM, TANZANIA, 29 JUNI 2022… Watanzania sasa wanaweza kuishi maisha rahisi, ya vitendo na rahisi zaidi wakiwa na Bidhaa za LG zilizoletwa hivi Karibuni, vifaa mahiri vya nyumbani vinavyolenga kukidhi mahitaji mengi, na kazi za kila siku zenye changamoto.

Bidhaa kama Majokofu, Microwave, televisheni na mashine za kufulia nguo, vifaa mahiri vya nyumbani vitakavyoweka muonekano wa kidijitali nyumba za Watanzania , kwa maana kwamba vifaa hivi kutoka kampuni ya LG havitoi kelele za aina yeyote wakati wa matumizi na kuifanya nyumba kuwa shwari na tulivu huku shughuli nyingine zikiendelea.

Akizungumzia ubunifu wa bidhaa bora za nyumbani za hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa LG Electronics Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema, "hatua ya kuweka vyumba vya kuishi, jikoni na vyumba vingine vyovyote katika nyumba za Watanzania kuwa za kidijitali imechochewa na dhamira yetu ya kuweka vipaumbele kwa urahisi na faraja kwa ajili ya wateja wetu. Ili sisi sote kufikia hili, lazima kuwe na usambazaji wa kutosha wa vifaa vya nyumbani ”.

Kulingana na uchunguzi wa hivi majuzi wa LG ThinQ Smart Home Report, 17.3% ya watumiaji waliohojiwa walichagua uokoaji wa nishati kama manufaa makubwa zaidi ya nyumbani. Faida nyingine kuu zilizotajwa katika utafiti huo ni pamoja na urahisi na usalama wa kutumia kwa TV na friji na utendakazi bora kupitia teknolojia ya Artificial Intelligence (AI) kwa washer na kuokoa nishati kwa viyoyozi.

Miongoni mwa vifaa muhimu vya nyumbani vilivyoletwa na LG nchini ni pamoja na Televisheni za Smart OLED zinazoendeshwa na teknolojia ya hali ya juu ya akili ya bandia ambayo hufanya nyumba kuwa nzuri na rahisi. Televisheni zimeunda vichakataji vya AI ambavyo huchanganua yaliyomo kwenye skrini ili kuyarekebisha kwa sauti, picha na video bora zaidi kulingana na mazingira ya mtumiaji .

Kando na hilo, TV zina kipengele cha akili cha utambuzi wa sauti ambacho huwezesha watumiaji kuzidhibiti kwa amri rahisi. Pia hutoa dashibodi ya nyumbani inayoonyesha hali ya vifaa vingine mahiri vya nyumbani na kuwaarifu watumiaji kuhusu hali yoyote ambayo watumiaji wanapaswa kufahamu, kama vile mlango wa friji kuwa wazi na muda uliosalia wa kuisha kwa mzunguko wa kuosha.
Ili kusaidia katika ufuaji, LG imehifadhi mashine mahiri za kufulia kama vile Mashine ya Kuosha ya Vivace na mashine nyinginezo (Ai DD™️/DD) mashine nyingine za kufulia za AI DD™️ / DD ambazo hutambua aina ya kitambaa cha watumiaji na kupendekeza kozi bora zaidi ya kufulia.


Pia hutatua masuala madogo haraka kabla hayajaongezeka.
Kwa watumiaji wanaotaka kuweka vyakula na matunda vikiwa vipya kwa muda mrefu, LG imethibitisha kundi la Friji mahiri zilizoundwa kuunganishwa kwenye simu janja ya mtumiaji ili kudhibiti halijoto ya friji, kudhibiti Express Freeze, na kupokea uchunguzi wowote wa friji na chakula cha mtumiaji, taarifa za tarehe ya kumalizika muda wake. Hii inajumuisha LG Net 426(L) | Fridge Slim French Door, pamoja na InstaView Door-In-Door™️ ambayo kwa simu mahiri inayooana iliyounganishwa kwenye programu ya LG SmartThinQ™️, watumiaji wanaweza kurekebisha mipangilio ya halijoto wakiwa mbali ili friji iwe tayari kuchukua mkondo mkubwa wa ununuzi.
Vipengele vingine bora ni pamoja na mlango wa kisasa wa Ufaransa wenye chaguo bunifu za kuhifadhi kama vile Rafu inayokunjwa ambayo inaweza kujikunja yenyewe kwa ajili ya kuhifadhi vitu virefu zaidi na Mfumo wa Barafu wa Slim SpacePlus™️ ambao umejengwa ndani ya mlango wa friji ili watumiaji waweze kutumia rafu nzima ya juu.
Kulingana na Sa Nyoung Kim, teknolojia hii ya hivi punde ya msingi inayoangazia programu mpya na za kijanja husaidia kaya kuhifadhi nishati, na maji na ni rafiki wa mazingira huku ikitumika kwa urahisi, hivyo basi kukuza malengo muhimu ya maendeleo endelevu.

 

Share:

Friday, June 17, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANKI YATANGAZA KUPATA FAIDA YA BILIONI 19.7

Mwenyekiti wabodiya Tanzania Commercial Bank Dkt. Edmund Mndolwa (katikati), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kupata faida ya shilingi Bilioni 19.7 kwa mwaka ulioishia Desemba 31 2021 hatua inayo tajwa kuwa yamafanikio na kuimarika kwa benki hiyo ambayo ni muunganiko wa iliyokuwa benki ya TPB na TIB Corparate.
Afisa MtendajiMkuuwa Tanzania Commercial Bank TCB, Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza faida ya shilingi Bilioni 19.7 kwa mwaka ulioishia Desemba 31 2021 hatua inayotajwa kuwa ya mafanikio na kuimarika kwa benki hiyo ambayo ni muunganiko wa iliyokuwa benki ya TPB na TIB Corparate.
Mwenyekitiwabodiya Tanzania Commercial Bank Dkt. Edmund Mndolwa (katikati), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kupatafaida ya shilingi Bilioni 19.7 iliyopata benki hiyo wa pilikulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB, Sabasaba Moshingi pamoja na maafisa wengine wa benki hiyo.

Tanzania Commercial Bank TCB imetangaza kupata faida ya shilingi Bilioni 19.7 kwa mwakaulioishiaDesemba 31 2021 hatua inayotajwa kuwa ya mafanikio na kuimarika kwa benki hiyo ambayo ni muunganiko wa iliyokuwa benki ya TPB na TIB Corparate.

Mwenyekitiwabodiya Tanzania Commercial Bank Dkt. Edmund Mndolwa ametoa taarifahiyo katika mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar esSalaam nakusema kuwa faida hiyo ni kabla ya kodi.

Faida iliyopatikana mwaka 2021 inatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kubwa kufuatia ile ya mwaka 2020 ambayo haijawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa Benki ya TCB takriban miaka 95 iliyopita.

Amepongeza uongozi pamoja na wafanyakazi wa Tanzania Commercial Bank kwakuchangia mafanikio hayo licha ya changamoto zamdororo wauchumi uliosababishwa na wimbi la ugonjwawa UVOKO-19 ambao pia umeathiri uchumi wamataifa mengi duniani.

Kwaupande wake Afisa Mtendaji Mkuuwa Tanzania Commercial Bank TCB, Sabasaba Moshingi amesema kufuatia mafanikio hayo, wanahisa wamekubaliana kutoa gawio la hisa na kuelekeza kwenye kuimarisha mtaji wa Benki.

Mafanikio hayo pia wamewezesha amana za wateja kuongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 1.18 mwaka 2021 kutoka shilingi trilioni 1.04 huku mikoponayo ikiongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 718.6 kutoka bilioni 617.81

Tanzania Commercial Bank TCB imekuwa ikifanya kazi na wafanyabiashara kuanzia mfanyabiashara mdogo, wakati na mkubwa nakuhakikisha kila mwananchi anapata huduma kutoka benki ya TCB kila kona ya Tanzania na mipaka yake.

Share:

BENKI YA ABSA TANZANIA YAJA NA MIKAKATI KUWANUFAISHA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI KIUCHUMI

   
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Kennedy Nyoni (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed (Kulia), Mkurugenzi wa Biashara wa Absa, Mervin Saprapasen na Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania kwenye Miradi ya Kimkakati wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Neema Mwakatobe wakibonyeza kitufe kuzindua kampeni ya uboreshaji wa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) wa Benki ya Absa, uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Kennedy Nyoni (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed (Kulia), Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Mervin Saprapasen na Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania kwenye Miradi ya Kimkakati wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Neema Mwakatobe wakimsikiliza Meneja Huduma za Jamii wa Absa, Hellen Siria wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uboreshaji wa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Ndabu Lillian Swere (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Mervin Saprapasen (katikati) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uboreshaji wa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Kennedy Nyoni (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed (Kulia) na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Mervin Saprapasen wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uboreshaji wa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Kennedy Nyoni akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uboreshaji wa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) wa Benki ya Absa Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Pass Leasing, Killo Lussewa akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uboreshaji wa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) wa Benki ya Absa Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya Absa wakishiriki uzinduzi wa kampeni ya uboreshaji wa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) wa benki hiyo pamoja na waalikwa wengine jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Kennedy Nyoni akipiga picha ya kumbukumbu na Wakurugenzi pamoja na baadhi ya wakuu wa idara za Benki ya Absa baada ya uzinduzi wa kampeni ya uboreshaji wa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) wa Benki ya Absa Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Thursday, June 16, 2022

SERIKALI YATOA VITAMBULISHO VYA BIMA YA AFYA KWA WAZEE 937,266 NCHINI

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Doroth Gwajima, akizungumza leo Juni 15/2022 wakati wa maadhimisho ya kupinga ukatili kwa wazee yaliyofanyika kitaifa katika Kijiji cha Kisharita Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Katibu Mkuu Wizara  wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Zainabu Chaula akizungumza kwenye hafla hiyo.

 Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Taifa, Lameck Sendo, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Doroth Gwajima, akisalimiana na Wazee mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho hayo.

Wananchi wa Kijiji cha Kisharita wakiserebuka katika sherehe hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisharita wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Pius Sangoma akizugumza kwenye maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Singida, Mugheni Sengi akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Doroth Gwajima, akitoa kwa Neema Msengi ambaye ni mmoja wa ndugu wa Wazee watatu waliouawa kikatili katika Kijiji cha Kisharita Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Doroth Gwajima, akizungumza na vijana wa SMAUJATA.

Afisa Mradi wa Sight Savers, Mradi wa Boresha Maisha, Edwin Barongo akizungumzia kuhusu shughuli mbalimbali zikiwemo za kuwapa huduma wazee.

Programu Meneja wa Shirika la HelpAge Tanzania, Joseph Mbasha, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.


Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Shabani Muhali kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri wa Wazee Manispaa ya Singida, Juma Mudida, alihoji kwanini watuhumiwa wa mauaji ya wazee wa Kijiji cha Kisharita hawajapatikana hadi leo.

Wazee wakiwa katika maadhimisho hayo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Pius Sangoma  akiserebuka na Wanafunzi wa Shule ya Msingi, Kisharita.
Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Singida Chifu Mughenyi Sengi (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Singida, Juma Mudida wakiserebuka na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kishirita.
Wananchi wa Kijiji cha Kishirita wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba, Ashery Samwel aakizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive