A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, May 27, 2019

Uzinduzi wa Prophet Suguye Cup wafana

Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la WRM, Nabii Nicholaus Suguye, ambaye pia ndio Muanzilishi wa Mashindano ya ligi ya Mchezo wa mpira wa miguu iliyopewa jina la PROPHET SUGUYE CUP, akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo katika viwanja vya Misitu vilivyopo Kivule matembele ya pili jijini Dar es Salaam jumamosi tarehe 25.5.2019




Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la WRM, Nabii Nicholaus Suguye, ambaye pia ndio Muanzilishi wa Mashindano ya ligi ya Mchezo wa mpira wa miguu iliyopewa jina la PROPHET SUGUYE CUP, akimlisha keki mmoja wa wageni waliohudhuria ufunguzi wa mashindano hayo Diwani wa Rukoma na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mh. Murshidi Hashimu Ngeze wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo katika viwanja vya Misitu vilivyopo Kivule matembele ya pili jijini Dar es Salaam jumamosi ya tarehe 25.5.2019

Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la WRM, Nabii Nicholaus Suguye, ambaye pia ndio Muanzilishi wa Mashindano ya ligi ya Mchezo wa mpira wa miguu iliyopewa jina la PROPHET SUGUYE CUP akipiga penati kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindsano hayo yaliyoanza rasmi jumamosi ya tarehe 25.5.2019
Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la WRM, Nabii Nicholaus Suguye, ambaye pia ndio Muanzilishi wa Mashindano ya ligi ya Mchezo wa mpira wa miguu iliyopewa jina la PROPHET SUGUYE CUP akipiga penati kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindsano hayo yaliyoanza rasmi jumamosi ya tarehe 25.5.2019
Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la WRM, Nabii Nicholaus Suguye, ambaye pia ndio Muanzilishi wa Mashindano ya ligi ya Mchezo wa mpira wa miguu iliyopewa jina la PROPHET SUGUYE CUP akipiga penati kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindsano hayo yaliyoanza rasmi jumamosi ya tarehe 25.5.2019
Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la WRM, Nabii Nicholaus Suguye, ambaye pia ndio Muanzilishi wa Mashindano ya ligi ya Mchezo wa mpira wa miguu iliyopewa jina la PROPHET SUGUYE CUP akitoka kupiga penati kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindsano hayo yaliyoanza rasmi jumamosi ya tarehe 25.5.2019
Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la WRM, Nabii Nicholaus Suguye, ambaye pia ndio Muanzilishi wa Mashindano ya ligi ya Mchezo wa mpira wa miguu iliyopewa jina la PROPHET SUGUYE CUP, akimlisha keki mmoja wa wageni waliohudhuria ufunguzi wa mashindano hayo Diwani wa Rukoma na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mh. Murshidi Hashimu Ngeze wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo katika viwanja vya Misitu vilivyopo Kivule matembele ya pili jijini Dar es Salaam jumamosi ya tarehe 25.5.2019
Mamia ya mashabiki na wananchi wa Kivule waliomiminika viwanjani hapo kushuhudia mtanange huo. Mchezo ambao Kivule Forest Wametoka kidedea kwa magoli matatu dhidi ya magoli mawili ya Professional FC.
Mamia ya mashabiki na wananchi wa Kivule waliomiminika viwanjani hapo kushuhudia mtanange huo. Mchezo ambao Kivule Forest Wametoka kidedea kwa magoli matatu dhidi ya magoli mawili ya Professional FC.
Mamia ya mashabiki na wananchi wa Kivule waliomiminika viwanjani hapo kushuhudia mtanange huo. Mchezo ambao Kivule Forest Wametoka kidedea kwa magoli matatu dhidi ya magoli mawili ya Professional FC.
Baadhi ya viongozi wa mchezo referee pamoja na raise woman wakiwa kazini katika mchezo wa ufunguzi kati ya Kivule fc pamoja na Professional fc. Mchezo ambao Kivule wameibuka na ushindi wa magoli ma 3 kwa ma 2 ya Professional FC.
Baadhi ya viongozi wa mchezo referee pamoja na raise woman wakiwa kazini katika mchezo wa ufunguzi kati ya Kivule fc pamoja na Professional FC. Mchezo ambao Kivule wameibuka na ushindi wa magoli ma 3 kwa ma 2 ya Professional FC.
Baadhi ya viongozi wa mchezo referee pamoja na raise woman wakiwa kazini katika mchezo wa ufunguzi kati ya Kivule fc pamoja na Professional FC. Mchezo ambao Kivule wameibuka na ushindi wa magoli ma 3 kwa ma 2 ya Professional FC.
Baadhi ya viongozi wa mchezo referee pamoja na raise woman wakiwa kazini katika mchezo wa ufunguzi kati ya Kivule fc pamoja na Professional FC. Mchezo ambao Kivule wameibuka na ushindi wa magoli ma 3 kwa ma 2 ya Professional FC.
Manahoza wa timu ya Kivule Forest pamoja na Professional FC wakiwa katika picha ya pamoja na waamuzi siku ya kwanza ya mashindano ya Prophet Suguye Cup.
Manahoza wa timu ya Kivule Forest pamoja na Professional FC wakisalimiana kuonyesha tendo la Fair Play huku waamuzi kwakishuhudia kitendo hicho siku ya kwanza ya mashindano ya Prophet Suguye Cup.
Baadhi ya wachezaji wa Professional FC wakiwa ndani ya uwanja wa misitu ama kerezange tayari kuanza mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Prophet Suguye Cup.
Mtanange kati ya Kivule Forest dhidi ya Professional FC ndani ya viwanja vya Misitu. Kivule forest wameshinda 3 dhidi ya 2 ya Professional FC.
Mtanange kati ya Kivule Forest dhidi ya Professional FC ndani ya viwanja vya Misitu. Kivule forest wameshinda 3 dhidi ya 2 ya Professional FC.
Baadhi ya wachezaji wa Kivule Forest FC pamoja wakiwa ndani ya uwanja wa misitu ama kerezange tayari kuanza mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Prophet Suguye Cup.

Mtanange kati ya Kivule Forest dhidi ya Professional FC ndani ya viwanja vya Misitu. Kivule forest wameshinda 3 dhidi ya 2 ya Professional FC.

Mwangalizi mkuu wa WRM Church na Mwanzilishi wa Prophet Suguye Cup akiwasalimia wachezaji siku ya Ufunguzi wa mashindano.
Share:

Friday, May 24, 2019

Tanga Cement yasaidia ujenzi wa madarasa Holili

Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Godwin Kamando (kushoto), akikabidhi msaada  wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya  shs Milioni 3,388,488 kwa  Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze (Ward Executive Officer) (watatu kulia) na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2  na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano  ilifanyika  kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana. Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo.
Meneja Afya, Usalama na Mazingira wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Emmanuel Ntoma (wa pili kushoto) akikabidhi msaada  wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya  shs 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola (kulia) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2  na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano  ilifanyika  kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana. Wapili kulia ni Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze na Wengine ni maofisa wa kampuni hiyo. 

Meneja Ugavi wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Livin Masawe  (wa pili kushoto), akikabidhi msaada  wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya  shs Milioni 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola (wapili kulia) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2  na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano  ilifanyika  kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana.Watatu kulia ni Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze na Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo. 

Meneja Meneja Mauzo wa Mkoa wa Tanga wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Issa Ndomondo(wa pili kushoto), akikabidhi msaada  wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya  shs 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola (kulia) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2  na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano  ilifanyika  kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana.Wapili kulia ni Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze na Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo.
Share:

Wednesday, May 22, 2019

WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA JIMBO LA XUZHOU LA CHINA

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na ujumbe kutoka Mji wa Xuzhou Nchini China uliokuja kufanya tathmini ya Madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanya kazi Zanzibar Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiagana na Kiongozi wa ujumbe kutoka Mji Xuzhou Nchini China Zhou Guangchum baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ofisini kwake.
Na Ramadhani Ali - Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed ameiomba Jamhuri ya Watu wa China kurejesha utaratibu wa madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanyakazi Zanzibar kukaa miaka miwili badala ya mwaka mmoja wa sasa.
Alisema tokea kuanzisha uhusiano wa madaktari wa China kuja Zanzibar mwaka 1965 walikuwa wakikaa kipindi cha miaka miwili lakini utaratibu huo ulibadilika miaka ya hivi karibuni na hivi sasa wanakaa mwaka mmoja.
Waziri wa Afya alitoa ombi hilo alipokutana na Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka Mji wa Xuzhou ambao upo nchini kufanya tathmini ya Madaktari wanaokuja kufanyakazi Zanzibar katika hospitali ya Abdlala Mzee Mkoani na Mnazimmoja.
Aliueleza ujumbe huo kwamba utaratibu wa zamani wa timu za madaktari wa China kukaa miaka miwili ulikuwa unatoa fursa nzuri kwa madaktari wa Zanzibar kujenga uzoefu na kujifunza mambo mengi ya kitaalamu kutoka kwao.
Alisema madaktari wa Zanzibar wanapopata uzoefu kwa vitendo kutoka kwa madaktari wa China inawasaidia kufanya vizuri wanapopata nafasi ya masomo ya juu nje ya nchi.
Waziri Hamad aliushauri ujumbe huo kuwaelekeza madaktari wa China waliopo Zanzibar kuwapa mafunzo madaktari wa Hospitali ya Abdalla Mzee ya kutumia mashine mpya zilizowekwa katika hospitali hiyo na kuitafsiri teknolojia iliyotumika ili baada ya kuondoka waweze kuzitumia.
Aidha Waziri wa Afya aliwahimiza madaktari wazalendo kuwa tayari kujifunza utaalamu kutoka madaktari wa China ambao wamekuwa wakifanya matibabu ya kitaalamu na kuwashirikisha.
Kiongozi wa ujumbe huo Zhou Guangchum alimuhakikishia Waziri wa Afya kwamba nchi yake itaendelea kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuongeza msaada wake hasa katika sekta ya afya.
Aliahidi kuwa atalifikisha nchini kwake ombi la kurejesha utaratibu wa zamani wa madaktari wanaokuja Zanzibar kukaa kwa kipindi cha miaka miwili ili waweze kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ndugu zao.
Share:

Tuesday, May 21, 2019

Barclays Bank organizes an Iftar dinner for customers in Dar

 Dar es Salaam Regional Sheikh,  Alhad Mussa Salum addresses the audience during an iftar hosted by Barclays Bank Tanzania to its customers in Dar es Salaam at the weekend.
Dar es Salaam Regional Sheikh,  Alhad Mussa Salum (right), Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (second right) together with some invited guests serving food during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam.
Barclays Bank Head of Communications and Corporate Relations, Aron Luhanga (left) chats to Dar es Salaam Regional Sheikh, Alhad Mussa Salum (right), during and iftar hosted by BBT to its customers in Dar es Salaam recently. Second right is the Information Director at the regional sheikh office, Tabu Kawambwa.
Barclays Bank Citizenship Manager, Hellen Siria (right) serves an iftar meal to some invitees at a function hosted by BBT to its customers in Dar es Salaam.
Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (centre), together with some invited guests, breaking the fast at an occasion hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam recently
Some invite guests breaking the fast at an occasion hosted by Barclays Bank Tanzania in Dar es Salaam recently.
Share:

Friday, May 17, 2019

SERIKALI YAIPONGEZA BENKI YA DCB KWA KUFANIKISHA ZOEZI LA UUZAJI WA HISA KWA UFANISI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya Uorodheshwaji wa Hisa za Benki ya Biashara ya DCB katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hii inatokana na kukamilika kwa zoezi la uuzwaji wa hisa hizo kwa umma na kwa wanahisa lililokamilika hivi karibuni kwa ufanisi. Wengine kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka, Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Nicodemus Mkama na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.

Share:

Tuesday, May 14, 2019

BENKI YA DCB YAWASHUKURU WAHESHIMIWA WABUNGE NA SPIKA KWA KUFANIKISHA UUZWAJI WA HISA.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa pale ugeni kutoka benki hiyo ulipomtembelea  ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kushoto), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka (katikati) pale ugeni kutoka benki hiyo ulipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Ndg. Godfrey Ndalahwa
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Katikati), akizungumza na ujumbe kutoka benki ya DCB ukiongozwa na  Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Lucian Msambichaka (kushoto kwake) ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Meneja wa Tawi la Benki ya DCB Dodoma, Joseph Njile wakati yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni, Dodoma jana. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, James Ngaluko  wakati yeye Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka na  Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa (kulia kwake), wakimtembelea mheshimiwa Spika, osifini kwake Dodoma jana.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na ofisa Uhusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Nuru Ashraf, wakati yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni, Dodoma juzi. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha  Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa, wakati yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni, Dodoma juzi. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Katikati), akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Benki ya Biashara ya DCB ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka (wa tatu kulia) walipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana.

Benki ya Biashara ya DCB imetoa shukurani kwa waheshimiwa wabunge pamoja na mheshimiwa spika kwa kufanikisha zoezi la uuzwaji wa hisa zao lililofanyika hivi karibuni kwa mafanikio. 


Akizungumza wakati wa mahojiano maalumu jijini Dodoma leo sambamba na ziara ya uongozi wa juu wa DCB ulioongozwa na Mwenyekiti wao wa Bodi bungeni juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema wabunge kama wawakilishi wa wananchi wamesaidia sana kwa taarifa za uuzaji wa hisa zao kuwafikia wananchi wengi. 

Alisema mafanikio ya uuzaji wa hisa yaliyoifanya benki kuongeza mtaji wake yatasaidia mpango mkakati wao wa kutanua wigo wa huduma zao wakitarajia ndani ya miaka mitano kuwafikia watanzania wengi huku wakiwekeza zaidi katika huduma za kidigitali. 

“DCB ilianza mpango wake wa kujitanua kutoka jijini Dar es Salaam miaka miwili iliyopita, safari ya kujitanua inaendelea, tumeshafika Dodoma na maeneo ya karibu, mfumo wetu unaotusaidia ni kutoa huduma bora kwa bei nafuu tukiwekeza zaidi katika mfumo wa kidigatali hivyo kuwa na matawi machache na kuweka vituo vingi vya huduma sehemu mbalimbali nchini,” alisema. 






Zoezi la uuzwaji wa hisa za dcb lilizinduliwa Novemba 12,2018 na kuhitimishwa Januari 31, 2019 ambapo hisa 36,635,435 ziliuzwa ikivuka kiwango cha hisa 33,913,948 zilizopangwa awali. 
Share:

Tuesday, May 7, 2019

WAZIRI MKUU AUTAKA UONGOZI WA BENKI YA DCB UIMARISHE KITENGO CHA ELIMU KWA UMMA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akipiga picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo, walipomtembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni Dodoma jana. Kutoka kushoto ni, Rahma Ngassa, Joseph Njile na Nuru Ashraf (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati) pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo,  walipomtegembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni Dodoma jana.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akisalimiana na Meneja wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, joseph Njile wakati Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa (katikati), akimtembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni Dodoma juzi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akisalimiana na Ofisa Mauzo wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, Nuru Ashraf, wakati Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa (katikati), akimtembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni, Dodoma  juzi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa, wakati Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa (katikati), akimtembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni juzi. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi benki ya DCB kwa kufanikiwa kubadili muundo kutoka benki ya jamii na kuwa ya biashara.

“Benki nyingi za jamii zimekufa baada ya kushidwa kujiendesha lakini ninyi DCB mmeweza kumudu kujiendesha hadi kufikia kuwa benki ya biashara.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa benki hiyo uimarishe kitengo cha elimu kwa umma ili jamii ifahamu huduma wanazozitoa.

“Nendeni kwa wananchi mkawape elimu juu ya umuhimu wa kufungua akaunti na pia rahisisheni mazingira ya kutolea huduma kwa wateja.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Mei 6, 2019) alipokutana na uongozi wa benki hiyo ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameitaka benki hiyo isogeze huduma kwa wananchi hususan maeneo ya pembezoni ambayo bado hayajafikiwa.

Amesema ni muhimu wananchi wakasogezewa huduma za kibenki ili waweze kuhakikishiwa usalama wao pamoja na fedha zao.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya DCB, Bw. Godfrey Ndalahwa alisema tangu benki hiyo ianzishwe imefanikiwa kukuza amana za wateja kutoka sh. bilioni mbili mwaka 2002 hadi sh. bilioni 75 Desemba mwaka jana.

“Pia mikopo imeongezeka kutoka sh. bilioni moja mwaka 2002 na kufikia sh. bilioni 90, Desemba 2018, faida ikiwa ni sh. bilioni 17.7 baada ya kodi.”

Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi cha miaka 16 ya utendaji wake, benki hiyo imeshatoa gawio la zaidi ya sh. bilioni 11 kwa wanachama wake.

Pia, Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuboresha maendeleo.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, wameona mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali nchini.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive