A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, October 15, 2024

ZAIDI YA SH800 BILIONI KUPANUA, KUJENGA KIWANDA KIPYA CHA SARUJI MKOANI TANGA


Dar es Salaam. Serikali, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, na kampuni ya AMSONS, wameingia makubaliano ya kuwekeza $320 milioni (zaidi ya Sh800 bilioni) katika upanuzi wa kiwanda cha saruji Mbeya na kuanzisha kiwanda kipya cha saruji Tanga.  

 

Hayo yamesemwa leo (Oktoba 15) jijini Dar es Salaam na Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

 

Bw. Mchechu alisema kati ya fedha hizo, $190 milioni ( yapata Sh513 bilioni) zitatumika kwaajili wa ujenzi wa kiwanda kipya Tanga na $130 milioni (Sh351 bilioni) ni kwaajili ya upanuzi wa kiwanda cha Saruji Mbeya.

 

“Hivi ninavyozungumza tayari tumeshafanya maamuzi ya kimsingi. Kazi zilizobakia ni za kimenejimenti, ikiwemo kumalizia mpango wa biashara na hatua nyingine za kifedha,” alisema Bw. Mchechu.

 

 

Alisema mradi huu wa upanuzi wa kiwanda cha saruji Mbeya na ujenzi wa kiwanda kipya Tanga, unaotarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili hadi mitatu, utapelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa klinka mara kumi.

 

Kwa kiwanda cha Mbeya, alifafanua, uzalishaji wa klinka, malighafi muhimu katika utengenezaji wa saruji, unatarajiwa kuongezeka kutoka tani 1,000 kwa siku hadi kufikia tani 5,000.

 

Aliendelea kufafanua kuwa kwa upande wa kiwanda kipya cha Tanga, kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 5,000 za klinka kwa siku, na hivyo kuleta jumla ya tani 10,000.

 

“Kuongeza kwa uzalishaji kutatufanya tuendelee kulikamata vizuri soko la nyanda za juu kusini ambalo tumekuwa tukilihudumia kwa zaidi ya asilimia 70 kwa muda mrefu,” alisema Bw. Mchechu.

 

Aliongeza: “Uwekezaji huu pia utakuwa mwanzo wa kupenye kwenye nchi jirani za Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.”

 

Bw. Mchechu alisema uwekezaji huo ni matokeo ya uboreshwaji wa mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais, Dr. Samia Suluhu Hassan.

 

“Uwekezaji huu ni sehemu ya mabadiliko ambayo Mhe. Rais amekuwa akitamani kuyaona katika mashirika ambayo Serikali ina hisa,” alisema.

 

Kwa upande wake Mkurugezi wa fedha wa AMSONS Bw. Ahmed Mhada alisema kukamilika kwa mradi wa upanuzi na ujenzi wa kiwanda kipya kutapelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa saruji kutoka tani milioni 1.1 kwa mwaka hadi kufikia tani milioni 4.2.

 

“Inatarajiwa kuongezeka kwa uzalishaji kutapelekea kuongezeka kwa gawio mara 10 ya lile ambalo Serikali ilipata mwaka jana,” alisema Bw. Mhada

  “Inatarajiwa kuongezeka kwa uzalishaji kutapelekea kuongezeka kwa gawio kuongezeka kwa gawio mara 10 ya lile ambalo Serikali ilipata mwaka jana,” alisema Bw. Mhada.

 

Serikali, ambayo inamiliki asilimia 25 ya hisa, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, mwaka jana ilipata gawio la Sh3 bilioni, ikiwa ni miaka 10 ipite bila kampuni hiyo kutoa gawio.

 

Kama ongezeko la uzalishaji linatarajiwa kuongeza gawio mara 10, tafsiri yake ni kuwa serikali inatarajia kuanza kupata wastani wa Sh30 milioni kama gawio baada ya mradi kukamilika.

 

Kwa upande wa ajira, Bw. Mhada, alisema kuwa kukamilika kwa upanuzi wa kiwanda cha Saruji cha Mbeya na ujenzi wa kiwanda kipya Tanga, kutazalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja 12,000.

 

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Kiwanda cha Saruji Mbeya, Prof. Siasa Mzenzi, alimshukuru Mhe. Rais kwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji nchini.

 

“Anachofanya Mhe. Rais, kinavutia wawekezaji kuwekeza nchini. Tuko tayari kusimamia uwekezaji huu ipasavyo kwa maslahi mapana ya Taifa letu na watu wake,” alisema Prof. Mzenzi.

 

Kadri siku zinavyozidi kwenda, idadi ya watu inazidi kuongezeka, na hatimaye mahitaji ya saruji yanazidi kupaa.


Mpaka kufikia mwezi Disemba mwaka jana, uzalishaji wa saruji Tanzania ulikuwa tani milioni 11 ikilinganishwa na mahitaji ya tani milioni 7.5.

 

Kiwanda cha Saruji cha Mbeya kinamilikiwa kwa ubia kati Kampuni ya Amsons kutoka Holcim ya Uswisi (65%), Serikali ya Tanzania kupitia kwa Msajili wa Hazina (25%) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wenye hisa (10%).

 

Share:

Monday, October 14, 2024

Customer service: KCB Bank (T) planting trees across eight regions

.com/img/a/
KCB Bank (T) is championing sustainability as a responsible corporate citizen, advancing the Sustainable Development Goal (SDGs) no. 14 by extensive tree planting around the country.

Paschal Machango, a senior official, stood in for Cosmas Kimario, the group regional businesses director and country managing director, at an event to commemorate Customer Service Week.

.com/img/a/

He said KCB Bank has undertaken a significant environmental initiative by planting 1,500 trees across its operational regions in Tanzania, part of a strategic focus on economic, social, and environmental pillars.

The bank executive appreciated staff at the Mbagala Annex Primary School, one of the beneficiaries of the initiative, for their acceptance to host the project in the city.

This had helped to boost the bank’s participation in this crucial environmental cause, he said, asserting that the bank’s commitment extends beyond business success.

“We are dedicated to environmental conservation. Today, we are proud to have planted over 1,500 trees in schools across Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Geita, Kahama, Mwanza, and Morogoro,” he stated.

.com/img/a/
Ruth Mussa, an assistant head teacher, expressed gratitude to KCB Bank for their engagement in the initiative, while Phina Bernard, an environmental officer with Temeke municipality, commended the bank for its impactful contribution.

Focus should also be placed on nurturing the planted trees, she stated, with the bank executive urging communities and organizations to join hands in promoting environmental stewardship and sustainability for the well-being of future generations

Share:

Sunday, October 6, 2024

Rais wa Zanzibar aipongeza Benki ya Absa Tanzania kuboresha afya ya mama na mtoto

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kuwezesha kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha’ iliyoanzishwa na Shirika la Amref Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Zanzibar. Ilikuwa ni katika hafla ya shukurani na uchangishaji fedha iliyofanyika katika Ikulu ya Zanzibar, jana. Wengine kutoka kushoto ni, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui, Mwenyekiti wa Bodi ya Amref, Bw. Anthony Chamungwana na Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dk. Florence Temu.

Na mwandishi wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Benki ya Absa Tanzania kwa mchango wake wa shs milioni 150 kuchangia kampeni ya ‘Uzazi ni Salama’ yenye lengo la kuboresha afya ya mama na mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua.

Mheshimiwa Rais Mwinyi alitoa pongezi hizo katika hafla ya tatu ya shukurani na uchangishaji fedha wa kampeni hiyo, iliyoandaliwa na Shirika la Amref Tanzania, Wizara ya Afya Zanzibar, kwa udhamini mkuu wa Benki ya Absa Tanzania na kufanyika katika Ikulu ya Zanzibar, jana.

Leo tumekusanyika hapa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kuokoa maisha kupitia kampeni hii, iliyoanzishwa mwaka 2020 ikiwa na lengo la kukusanya fedha kiasi cha shs Bilioni 1."

Aidha nimefahamishwa, mwezi juni mwaka huu, Amref, wizara yetu ya afya pamoja na Benki ya Absa Tanzania wakiungwa mkono na wadau kadhaa walitoa vifaa tiba vyenye thamani ya shs milioni 262.6 kwa ajili ya vituo vya afya 28 katika mikoa mitano ya Zanzibar, niwashukuru Amref Tanzania, wadhamini wakuu Benki ya Absa Tanzania na wadau wote kwa kujitolea kuunga mkono jitihada ya serikali ya Zanzibar katika kuboresha huduma za afya”, alisema Rais Mwinyi.

Pamoja na hayo alisema ni jambo la kutia moyo kuona Zanzibar ikiwa kwenye njia sahihi ya kufikia malengo endelevu (SDG) 2030 ya kupunguza vifo vya wajawazito hadi chini ya vifo 70 kwa vizazi hai 100, vifo vya watoto wachanga hadi kufikia 12 kwa kila vizazi 1000 na vifo vya watoto chini ya miaka mitano hadi 25 kwa kila vizazi hai 1000 kufikia 2030.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser alisema wametoa msaada kuunga mkono juhudi zinazofanywa za serikali za mbili za, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwekeza katika sekta ya afya hususan katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto.

Benki ya Absa Tanzania tunaenda sawa na lengo la taasisi yetu lisemalo ‘Kuiwezesha Afrika na Tanzania ya kesho kwa pamoja, hatua moja baada ya nyingine’ hapa tukihakikisha jamii yetu inapata huduma za afya stahiki."

Lakini pia msaada huu unaenda sambamba na ahadi yetu ya chapa tuliyoizindua hivi karibuni isemayo ‘Stori yako ina thamani’, hivyo kwa kuunga mkono juhudi hizi, tunaamini tunazisaidia serikali zetu katika kuandika stori zake zile zinazohakikisha watanzania wote wanapata huduma bora za afya”, alisema Bw. Laiser.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dk. Florence Temu alimshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa kukubali, kujitoa na kuunga mkono kampeni ya Uzazi ni Maisha tokea ilipoanzishwa mwaka 2020.

Niwashukuru pia wadhamini wakuu, Benki ya Absa pamoja na wafadhili wetu wengine waliokuwa nasi tokea mwanzo kufanikisha malengo ya kampeni hii yenye kauli mbiu ya ‘Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama’ ambapo kati ya malengo yetu ya kukusanya kiasi cha shs Bilioni 1, hadi sasa tumeshapokea ahadi zenye thamani ya shs 989,831,145, Zaidi ya asilimia 98.9 ya malengo yetu tukipokea kiasi cha shs 740,457,422 sawa na asilimia 75”, alisema Dk. Florence.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassoro Mazrui, Naibu Waziri, Mhe. Hassan Khamis Hafidh, Katibu Mkuu, Dk. Mngereza Mzee Miraji, mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na kitaifa ya maendeleo, watendaji na watumishi wa serikali na mashirika ya umma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) na wengine kutoka kushoto; Mwenyekiti wa Bodi ya Amref Tanzania, Bw. Anthony Temu, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dk. Florence Temu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, wakifanya dua katika hafla ya shukurani na uchangishaji fedha wa kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha’ iliyofanyika katika Ikulu ya Zanzibar, jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akihutubia katika hafla ya shukurani na uchangishaji fedha ya kampeni ya Uzazi ni Maisha iliyofanyika katika Ikulu ya Zanzibar, jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akizungumza kuhusu udhamini na malengo ya benki hiyo katika kuiwezesha kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha’ iliyoanzishwa ma Shirika la Amref Tanzania pamoja na Wizara ya Afya Zanzibar, katika hafla ya shukurani na uchangishaji fedha kwa ajili ya kampeni hiyo katika Ikulu ya Zanzibar, jana. Kampeni hiyo ina lengo la kuboresha afya ya mama na mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati),akipozi kwa picha ya kumbukubu na baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Absa Tanzania, pamoja na viongozi wengine, mara ya baada ya hafla ya shukurani na uchangishaji fedha ya kampeni ya 'Uzazi ni Salama' iiyofanyika Ikulu ya Zanzibar, jana.
Share:

Thursday, October 3, 2024

Benki ya DCB yatenga shs bilioni 30 mikopo ya wafanyabiashara wa masokoni

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Songoro Mnyonge (wa tatu kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi huduma ya mkopo uliopewa jina la Sokoni (Sokoni Loan), unaolenga wafanyabiashara wa masokoni katika hafla iliyofanyika katika soko la Magomeni, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Pamoja naye ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi na Meneja Mahusiano Taasisi za Kiserikali wa benki hiyo, Bi. Dalilla Issa (wa pili kulia).

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Songoro Mnyonge, ameipongeza Benki ya Biashara ya DCB, kwa kutenga kiasi cha shs bilioni 30 kwa ajili ya mikopo ya wafanyabiashara ndogo ndogo, wanaoendesha biashara zao katika masoko yaliodhinishwa jijini Dar es Salaam na Dodoma.

Pongezi hizo alizitoa wakati akizindua huduma ya mkopo uliopewa jina la Sokoni (Sokoni Loan), unaowalenga wafanyabiashara wadogo wadogo wanaofanya biashara zao masokoni katika Soko la Magomeni, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo.

Mstahiki Meya alisema uamuzi wa DCB wa kuamua kutenga kiasi hicho unapaswa kupongezwa kwani unaunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha uchumi wa wananchi wa kipato cha chini unaimarika.

Serikali ilianzisha mikopo ya asilimia 10 kupitia Halmashauri, mikopo hii haitoshi kuwafikia wajasiriamali wadogo wote ambao ndio kundi kubwa, Halmashauri ya Kinondoni inawaunga mkono na itaendelea kushirikiana nanyi katika kuhakikisha mikopo hii inaleta tija katika masoko mbalimbali yalipo Kinondoni”, alisema Meya Songoro.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema uzinduzi wa huduma hiyo unaendana na misingi ya kuanzishwa kwa benki hiyo, miaka 22 iliyopita ambayo ni kuwakomboa kiuchumi wananchi wenye kipato cha chini.

DCB imeendelea kusimamia vizuri misingi ya kuanzishwa kwake, tokea kuanza kwa huduma hii ya mikopo ya wafanyabiashara wa masokoni, zaidi ya wafanyabiashara 1500 wamenufaika kwa kupata mikopo ya takribani shs bilioni 3 huku tukiwa tumetenga zaidi ya shs bilioni 30 kwa mikopo hii.

Tunaamini tukishikiriana kwa pamoja, sisi kama benki, serikali, wafanyabiashara na wadau wengine tunaweza kupunguza umasikini kwa kiwango kikubwa.

DCB tutaendelea kuweka fedha zaidi kwa ajili ya mikopo ya wafanyabiashara, kuongeza nguvu kazi yetu ili tuwafikie wateja wetu mahali walipo, niwapongeze pia wale ambao tayari wamepata mikopo hii kwani mpaka muda huu hakuna mkopo kichefuchefu hata mmoja”, alisema Bw. Moshingi.

Awali akizungumza mahali hapo, Meneja wa Mikopo ya Wajasiriamali, Bi. Sheila Nicas Banzi alisema uzinduzi wa huduma hiyo umelenga kuondoa usumbufu wanaoupata wafanyabiashara hao wanapoenda kukopa katika mikopo kandamizi, maarufu kama ‘Kausha Damu’.

Akizungumza jinsi ya kupata mikopo hiyo, Bi Sheila alisema, sharti muhimu ni kuwa kuwa na kizimba cha biashara katika masoko yaliyoidhishwa na mteja kuwa mwanachama hai wa masoko hayo.

Mikopo ya DCB Sokoni inatolewa kwa dhamana ya kizimba pamoja na Umoja wa Soko husika kwa kiwango kinachoanzia shs 100,000 hadi shs 1,000,000. Zaidi ya milioni moja kutahitajika dhamana binafsi”, alisema Bi. Sheila.

Mwenyekiti wa Soko la Bw. Daudi Mohamed Dole aliishukuru DCB akisema kuingia kwa benki hiyo sokoni hapo kumewapunguzia uchungu wa tatizo la mitaji na pia muda wa kwenda katika taasisi zenye masharti yasiyo rafiki ya utoaji wa mikopo.

Wafanyabiashara wa Soko la Magomeni wanakopesheka, tunaishukuru DCB Kwa kutuletea mikopo hii, natoa ushauri kwa wafanyabiashara wa Magomeni na Masoko mengine kuchangamkia fursa hii”, alisema Bw. Dole.

Huduma ya mikopo ya DCB Sokoni imeanzia katika masoko ya Jiji la Dar es Salaam na Dodoma, inatarajiwa pia kupelekwa katika masoko mengine sehemu tofauti.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Songoro Mnyonge, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo uliopewa jina la Sokoni (Sokoni Loan), unaolenga wafanyabiashara wa masokoni uliofanyika katika Soko la Magomeni, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Mikopo ya Wajasiriamali Wadogo wadogo wa Benki ya DCB, Bi. Sheila Nicas Banzi na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Bw. Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mkopo wa Sokoni (Sokoni Loan), katika soko la Magomeni, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Mikopo ya Wajasiriamali Wadogo wadogo wa Benki ya DCB, Bi. Sheila Nicas Banzi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Songoro Mnyonge.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, Bw. Ramadhani Mganga, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mkopo wa Sokoni (Sokoni Loan), a unaolenga wafanyabiashara wa masokoni, katika Soko la Magomeni jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Meneja wa Mikopo ya Wajasiriamali Wadogo wadogo wa Benki ya DCB, Bi. Sheila Nicas Banzi, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Songoro Mnyonge.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Songoro Mnyonge akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara mara baada ya uzinduzi rasmi wa mkopo wa Sokoni (Sokoni Loan), uliofanyika katika soko la Magomeni jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Wednesday, October 2, 2024

Tanzania Breweries Plc (TBL) na WWF Wakabidhi Mradi wa Maji Kijiji Cha Minazi mirefu, Ruvu Stesheni

Katika hatua muhimu ya kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji kwa jamii za wenyeji na mazingira, Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) na WWF Tanzania wamekabidhi rasmi miundombinu ya mfumo wa maji unaotumia nishati ya jua, ikijumuisha kisima, sehemu ya kunyweshea mifugo, na kituo cha maji kwa matumizi ya nyumbani katika Wilaya ya Kibaha.
Katika tukio hilo hilo, washirika hao wawili pia walizindua mradi wa majaribio wa miradi ya urejeshaji wa mazingira chini ya mpango wa "Bankable Nature Solutions" (BNbS) ili kuimarisha usalama wa maji wa muda mrefu na ulinzi wa mazingira.

Hafla ya makabidhiano iliyofanyika Kijiji cha Minazimikinda, Wilaya ya Kibaha, ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Nickson Simon John, ambaye alisifu ushirikiano kati ya TBL na WWF. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za maji nchini, hususan katika maeneo yanayokua kwa kasi kama Pwani na Dar es Salaam.

"Maji ni rasilimali muhimu kwa ukuaji wa jamii zetu na uchumi. Ushirikiano huu unaonesha nguvu ya kufanya kazi kwa pamoja katika kutatua uhaba wa maji. Juhudi za TBL na WWF Tanzania za kuboresha usalama wa maji, hasa katika Dar es Salaam na maeneo jirani, ni za kupongezwa na ni hatua muhimu kuelekea kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji safi kwa wote," alisema Mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Nickson Simon John.

Mfumo mpya wa maji unaotumia nishati ya jua utatoa maji safi na ya kuaminika kwa jamii zinazozunguka, ukiwasaidia kaya na mifugo katika eneo hilo. Miundombinu hii inashughulikia changamoto za uhaba wa maji kwa sasa na kutumia teknolojia rafiki wa mazingira ili kuhakikisha matumizi endelevu kwa muda mrefu.
Mradi huu ni sehemu ya dhamira kubwa ya TBL kwa uendelevu, inayooana na mkakati wake wa kuleta athari chanya kwa jamii inazozihudumia huku ikiunga mkono uhifadhi wa rasilimali za asili za Tanzania. Ushirikiano na WWF Tanzania chini ya mpango wa BNbS unalenga kuhakikisha kuwa mifumo ya asili inabaki salama wakati changamoto za maji zinashughulikiwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Michelle Kilpin, alisisitiza umuhimu wa mradi huo: "Kwa TBL, uendelevu ni msingi wa shughuli zetu. Mfumo huu wa maji unaotumia nishati ya jua, pamoja na uzinduzi wa mradi wa majaribio wa Bankable Nature Solutions, ni hatua muhimu kuelekea kuhakikisha kwamba watu na mazingira wote wananufaika na juhudi zetu. Kwa kushirikiana kwa karibu na WWF Tanzania, tunahakikisha upatikanaji wa maji kwa jamii hii na kulinda mifumo muhimu ya ikolojia ambayo ni muhimu kwa mustakabali wetu."
Mbinu ya Bankable Nature Solutions (BNbS) inatumia rasilimali za asili kwa njia endelevu, ikigeuza juhudi za uhifadhi wa mazingira kuwa miradi inayoweza kujiendesha kifedha na kuleta manufaa kwa uchumi na jamii. Kupitia mpango huu, TBL na WWF Tanzania wanalenga kuunda mfano wa kurudiwa unaoweza kutekelezwa nchi nzima ili kukabiliana na uhaba wa maji na kuimarisha uhifadhi wa mazingira.

Mkurugenzi wa Nchi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusaru, alielezea umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji. “Ulinzi wa vyanzo muhimu vya maji ni muhimu kwa kudumisha maisha ya binadamu na usawa wa mazingira. Kupitia mbinu za ubunifu kama Bankable Nature Solutions, tunaweza kuunda suluhisho la muda mrefu kwa ajili ya watu na mazingira.”

"Ushirikiano wetu na TBL unaonesha jinsi biashara na mashirika ya uhifadhi wa mazingira yanavyoweza kushirikiana kufanikisha matokeo ya kudumu. Kwa uzinduzi wa mradi wa majaribio wa BNbS hapa Kibaha, tunaweka msingi wa suluhisho za muda mrefu na endelevu ambazo zinalinda rasilimali zetu za asili huku zikihakikisha jamii zinapata huduma muhimu kama maji." alisema Dkt. Ngusaru

Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi wa eneo hilo, wanajamii, na wadau muhimu ambao walipongeza mpango huo kwa kuwa na mtazamo wa mbali na manufaa ya muda mrefu kwa jamii. Kisima cha maji cha nishati ya jua, sehemu ya kunyweshea mifugo, na kituo cha maji kwa matumizi ya nyumbani vinatarajiwa kunufaisha moja kwa moja mamia ya kaya na mifugo yao.

Ushirikiano kati ya TBL na WWF Tanzania haukabiliani tu na upungufu wa maji, bali pia unaimarisha ulinzi wa vyanzo vya maji, muhimu kwa kuhifadhi bioanuwai na kudumisha huduma za mazingira kwa vizazi vijavyo.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive