A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, August 2, 2024

UINGEREZA KUENDELEA KUFADHILI MIRADI YA UKIMWI NCHINI

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki wenye umri mdogo wa Kampeni ya kupanda mlima kilimanjaro ya GGM Kili Challenge, Regina Enos Baraka (kulia), mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda na kushuka mlima huo, mjini Moshi, Kilimanjaro, hivi karibuni. Kampeni hiyo ya kila mwaka ina lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki. Regina anaishi katika Kituo cha Moyo wa Huruma cha Geita kilichoanzishwa kwa msaada kutoka Mfuko wa Kili Challenge.

Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi Ili kutimiza malengo ya Kimataifa ya muda wa kati na mrefu ili kuona hakuna maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vinavyohusiana na VVU .

Balozi Concar aliyasema hayo wakati wa mapokezi ya wapanda mlima Kilimanjaro 71 walikuwa wakishiriki Kampeni ya kila mwaka ya GGM Kili Challenge mjini Moshi, Kilimanjaro, inayoandaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kupambana na Ukimwi (TACAIDS)

Njia kuu ambayo Uingereza inafanya ni kuwa mmoja wachangiaji wakubwa wa Mfuko wa Kimataifa wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, kwa miaka mitatu kutoka 2024 hadi 2026, Uingereza itatoa pauni bilioni 1 kwa mfuko huo, ambao kwa jumla utatoa dola milioni 602 kwa Tanzania."

Nitoe pongezi kwa AngloGold Ashanti na Bodi ya Wadhamini ya Geita Gold Mining Limited Kilimanjaro Challenge dhidi ya HIV/AIDS pamoja na TACAIDS kwa kuifanya Kili Challenge kuwa tukio la kila mwaka la kupendeza likileta ujumbe wa nguvu kwa wanaoishi na VVU”, alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi ukutoka Geita Gold Mining, Mhandisi Nzuamkende alisema kampeni hiyo inayofanyika Kwa mwaka wa 22, inalenga kukusanya fedha kuchangia jitihada za Serikali ya Tanzania kufikia malengo ya sifuri tatu ( Maambukizi mapya Sifuri, Unyanyapaa Sifuri na vifo vinavyohusiana na UKIMWI Sifuri).

Tunapokusanyika hapa ili kusherehekea mafanikio yenu, ninatoa shukrani zangu za dhati kwa kila mmoja wenu kwa kukabiliana na hofu zenu, na kushinda mojawapo ya milima mirefu zaidi na yenye changamoto duniani."

Juhudi zenu, kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro na kwenye njia tambarare za baiskeli, hazijadhihirisha tu nguvu ya uamuzi na umoja lakini pia zimeleta athari kubwa katika dhamira yetu ya pamoja ya kupambana na VVU na UKIMWI, mmetuonyesha kwamba hakuna changamoto isiyoweza kuzuilika tunapokutana kwa sababu moja na kwa hilo, nawapongeza nyote”, alisema.

Aidha aliwashukuru wafadhili na washiriki wote kutokana na michango yao inayoendelea kufanikisha Kampeni hiyo hadi kuufanya Mfuko wa Kili Challenge Against HIV/AIDS Trust kuwa mfuko wa kimataifa, unaohusisha wapanda mlima na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela alisema Tanzania inafanya vizuri kueleka malengo ya kimataifa ya muda mrefu na wa kati ambayo ni kufikia 95 tatu kufikia mwaka 2025 ambazo kama tawimu za karibuni zinavyoonesha kuwa kuna watu milioni 1.7 wanaishi na VVU, hivyo 95 ya kwanza ni kuona watu hao wanatambuliwa na kujua hali zao ambapo sasa imefika asilimia 83, huku 95 ya pili ni wale wanaoishi na VVU watumie dawa za kufubaza makali ya ukimwi (ARV) ambapo Tanzania imevuka lengo kwa kufikisha asilimia 98 na 95 ya tatu wale wanaotumia ARV asilimia 95 wawe wamefubaza virusi, utafiti wa mwisho unaonyesha maambukizi mapya yakipungua.

Nao baadhi ya washiriki wenye umri mdogo waliopanda Mlima Kilimanjaro, Regina Baraka na Baraka Erasto, kutoka kituo cha Moyo wa Huruma cha mkoani Geita, kilichoanzishwa kupitia mfuko wa Kili Challenge walielezwa kufurahishwa kwa uzoefu walioupata Kwa mara ya kwanza wakipanda mlimani hivyo kutoa hamasa Kwa vijana wadogo wenye umri kama wao kujitokeza kushiriki katika Kampeni hiyo Ili kuweza kuleta mabadiliko kwa wenye VVU.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki wenye umri mdogo wa Kampeni ya kupanda mlima kilimanjaro ya GGM Kili Challenge, Baraka Erasto (kulia), mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda na kushuka mlima huo, mjini Moshi, Kilimanjaro, hivi karibuni. Kampeni hiyo ya kila mwaka ina lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki. anaishi katika Kituo cha Moyo wa Huruma cha Geita kilichoanzishwa kwa msaada kutoka Mfuko wa Kili Challenge.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akihutubia katika hafla ya kuwapokea wapanda mlima Kilimanjaro waliokuwa wakishiriki kampeni ya kila mwaka ya GGM Kili Challenge yenye lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi. Kampeni hiyo imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki zoezi hilo lilioanza Julai 19 kufikia tamati yake mjini humo hivi karibuni.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive