A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Saturday, October 14, 2023

ZAIDI YA MAWAKALA 1300 WA TANZANIA COMMERCIAL BENKI PLC WAPATIWA MAFUNZO YA UTOAJI HUDUMA BORA

 

Kaimu Mkurugenzi wa Tanzania Commercial Bank Jema Msuya akizungumza na mawakala wa benki hiyo wa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi  wa mafuzo kwaajili yakuwajengea uwezo wa ili kuhakikisha wanatoa huduma bora


Mawakala wa TCB wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo.


Tanzania Commercial Bank imetoa semina kwa mawakala wake zaidi ya 1300 wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha huduma na ufanisi kwa wateja wa TCB wanaojipatia huduma za kibenki kwa mawakala hao.


Akizungumza katika semina hiyo,Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw, Jema Msuya alisema semina hizo ni mwendelezo wa mafunzo kwa mawakala waTCB nchi nzima ili kuboresha huduma, kukuza biashara zao na kuleta ufanisi kuboresha katika kumuhudumia mteja.


Alisema TCB Hadi sasa tumekuwa na mwakalazaidi zaidi ya 5600 ambao hutoa huduma nchi nzima huku ikiwa na matawi 82 na mashine za ATM zaidi ya 400 lengo likiwa kusogeza huduma kwa wateja wake.


Jema alisema huduma ya TCB Wakala iliyoanzishwa  ili kusaidia na kuondoa kero mbalimbali  kwa wateja wa TCB ikiwemo foleni katika matawi mbalimbali ya benki hiyo huku ikitoa ajira kwa mawakala zaidi ya elfu 5600 ambao nao wameajiri vijana mbalimbali ambao wanajipatia kipato.


Mafunzo haya yanaenda sambamba na kuwapongeza mawakala waliofanya vizuri kwa mwaka huu katika kazi zao, ili kuleta chachu kwa wengine kufanya vizuri zaidi.


kwa upande wake mmoja ya mawakala Raqeeb Hamidu ameishukuru TCB kwakuandaa semina hizi marakwamara kwasababu wanazidi kunufaika nakuongeza uwezo wakuwahudumia wateja kwa uadilifu mkubwa na wepesi.

Tanzania commercial bank imekuwa Benki ya kwanza kwakutujali sisi mawakala na wateja wake maana hizi semina zinakwenda kumsaidia wakala wa zamani lakini pia wakala wapya



Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive