Mkurugenzi Mtendaji wa Victoria Finance, Bw. Julius Mcharo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kuingia mkubaliano yakufanya kazi pamoja kuwaweesha wakulima kujipatia mikopo watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Pass Yohane Kaduma pamoja na maafisa wengine kutoka Taasisi hizo.
Dar es Salaam, 23 Oktoba 2023. Victoria Finance kwa kushirikiana na PASS Trust, inatoa mikopo kwa wajasiriamali wa kilimo (Kilimo Pesa) kupitia dhamana ya mikopo kwa njia ya kidijitali kupitia PASS Trust, lengo likiwa ni kutoa huduma muhimu ya mitaji kwa wajasiriamali wa kilimo.
Victoria Finance imeanzisha huduma hii ya kidijitali ili kukidhi mahitaji ya mitaji kwa wakulima na wafanyabiashara wadogo waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo, ikiwa ni pamoja na wale wanaojihusisha na biashara za mazao ya kilimo na mifugo. Kwa kutambua changamoto wanazokabiliana nazo wajasiriamali hawa, taasisi hiyo imeanzisha aina mbalimbali za mikopo ya muda mfupi ili kuimarisha biashara zao kwa ufanisi, urahisi na kwa uhakika zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayowasaidia wakulima, wafugaji na wajasiarimali wote kwenye sector ya. Kilimo Biashara, ikupata mitaji katika benki ili waweze kuwekeza Pass Yohane Kaduma (watatu kulia), akizungumza wakati wa hafla ya kuingia mkubaliano yakufanya kazi pamoja kuwaweesha wakulima kujipatia mikopowapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Victoria Finance, Bw. Julius Mcharo pamojana maafisa wengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Victoria Finance, Bw. Julius Mcharo akizungumza katika tukio hilo amesema, “Dhamira yetu ni kutoa mitaji kwa wajasiriamali wa kilimo itakayo saidia kustawi kwa sekta ya kilimo. Mikopo hii imeundwa kwa kusudi la kusaidia gharama za mavuno, gharama za usindikaji, na gharama za maghala/kodi za maghala, ili wajasiriamali waweze kunufaika zaidi katika shughuli zao.”
Wajasiriamali wanaweza kupata mikopo kuanzia Shilingi za Tanzania 100,000 hadi 1,000,000 kwa mtu binafsi au kikundi kulingana na mahitaji yao. Pia kiasi hiki cha mkopo kinaweza kutolewa kwa njia ya simu ya muombaji, ili kurahisisha malipo ya fedha kwa wakati na wakati huohuo kurahisisha urejeshwaji wake kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust, Bw. Yohane Kaduma, amesema, “Tunaamini kwa dhati kuwa sekta ya kilimo ndiyo nguzo ya uchumi wa nchi yetu, na ushirikiano wetu na Victoria Finance ni ushuhuda tosha wa kusaidia sekta hii ya kilimo. Ndiyo maana sisi PASS tunatoa dhamana za mikopo ya kidijitali kupitia simu za mkononi, kuruhusu wakulima kupata huduma ya mikopo kutoka kwa taasisi za kifedha tukianza na taasisi ya Victoria Finance.”
Hata hivyo ushirikiano huu kati ya PASS na Victoria Finance unaonyesha dhamira ya kuendelea kuwawezesha wajasiriamali wa kilimo, kukuza mnyororo wa thamani wa kilimo, na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania.
Kuhusu Victoria Finance
Victoria Finance ni taasisi ya kifedha yenye sifa njema inayojitolea kutimiza mahitaji ya kifedha kwa wakulima wadogo, biashara ndogo na za kati, na wajasiriamali waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo nchini Tanzania. Huduma nyingine za mikopo zinajumuisha mikopo ya biashara, ufugaji, elimu, nyumba, karadha na mikopo maalumu ya wajasiriamali wanawake. Taasisi ya Victoria Finance ina matawi Dar es Salaam, Dakawa-Morogoro na Madibira Mbeya.
0 comments:
Post a Comment