Wednesday, April 19, 2023
DCB Elimu Mpango Mzima Na Mama Samia Yazidi Kupaa
Monday, April 17, 2023
TANZANIA COMMERCIA BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI UKUTA WA CHUO CHA TIBA MTWARA
Friday, April 14, 2023
MAENDELEO BANK PLC YAJIVUNIA KUWEKA REKODI MPYA YA MAFANIKIO
Maendeleo Bank yaweka rekodi mpya ya mafanikio faida ya mwaka 2022 ni shilingi Bilioni 1.984 ambalo ni ongezeko la mara mbili Zaidi.
Akiungumza wakati akitangaza rekodi hiyo mpya Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Biashara wa Maendeleo Bank, Emmanuel Mwaya alieleza kuwa Maendeleo Bank Plc imeendelea kuwa benki yenye faida kwa miaka 8 mfululizo, kwa mujibu wa taarifa za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2022, ikiwa na mambo yafuatayo;
Ameeleza kuwa “Faida kabla ya kodi: TZS 1.984 bilioni, ukuaji wa mwaka 181%
Faida baada ya kodi: TZS 1.415 bilioni, ukuaji wa mwaka wa 141%
Jumla ya amapato: TZS 12. bilioni, ukuaji wa mwaka wa 5%
Amana: TZS 72.0 bilioni ukuaji wa 11%
Mikopo: TZS 61.0 bilioni ukuaji wa 5%
Ukuaji mzuri wa faida hizi umechangiwa Zaidi na timu iliyojitolea na ikiwa na lengo la kuifanya benki kuwa moja wapo ya wadau muhimu wa sekta ya kifedha katika uchumi. Ningependa kuangazia baadhi ya vichochezi vya faida ambavyo ni pamoja na; ukuaji wa jumla ya mapato kwa asilimia 26 mwaka hadi mwaka kutoka TZS 14.23 bilioni hadi TZS 17.97 bilioni mwaka 2022.
Benki pia imeendelea kuonyesha ufanisi mkubwa wa utendaji kazi, huku uwiano wa gharama kwa mapato ikiongezeka hadi 58% kutoka 74% katika kipindi kama hicho mwaka jana,ukiwa na nia ya kufikia kiwango elekezi kutoka benki kuu cha 55% ifikapo juni 2023.
Amana za wateja ziliongezeka kwa 11% kutoka TZS 70 bilioni mwaka 2021 hadi TZS 77.8 bilioni mwaka 2022 wakati mikopo ilongezeka kwa asilimia 5 kutoka TZS 57.7 bilioni hadi hadi TZS 60.6 bilioni mwaka 2022.
Mbinu iliyotumika katika uhamasishaji na ukuaji wa amana kwa wateja ulichangiwa kwa kiasi kikubwa uboreshaji wahuduma na bidhaa bunifu ambazo benki imekuwa ikitoa. Kuongezeka kwa bidhaa za kidijitali kama vile huduma za kibenki kwa simu, huduma za uwakala ambapo Zaidi ya benki mawakala 1300 (maendeleo Bank Wakala) Zimechangia ukuaji huu unaoshuhudiwa leo hii.
Akihitimisha wakati akitoa matokeo ya mwaka mzima ya benki hiyo mkuu wakitengo cha biashara Emmanuel Mwaya alisema”ninajivunia sana na ninashukuru kwa mafanikio yetu kama timu, nab ado nina Imani kubwa kwa ya utekelezaji wa mkakati wetu, kuongezeka kwa mahusiano ya wateja wetu, ari ya utendaji wa wafanyakazi, na uongozi thabiti tutadumisha kasi hii ya ukuaji wa biashara yetu kuu
Thursday, April 13, 2023
Absa Bank Tanzania Fetes its Dodoma Customers to Spice Ramadhan
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE JIJINI DAR ES SALAAM
Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (watatu kushoto), wakiwaongoza wateja wa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kupata mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium towerMkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (kushoto), akiongozana pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar na viongozi mbalimbali wa kidiniwa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium towerMkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na TCB kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium tower
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar akitoa neno la shukrani kwa Mkurungenzi Mtendaji waTanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, kwakujali na kuona umuhimu wa mfungo wa Ramadani na kuandaa mlo wa futari kwaajili ya wateja wake wa Dar es Salaam.hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la milenium tower.Maofisa wa Tanzania Commercial Bank (TCB) pamoja na wateja wa benki hiyo wakishiriki mlo huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB, Bi Chichi Banda (kushoto), akiwa kwenye picha ya pozi na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Benki hiyo Bi Gloria Mutta wakati wa hafla yakupata mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally