Thursday, December 15, 2022
Wafanyakazi Wa Absa Wasaidia Madawati Kwa Watoto Wenye Mahitaji
Thursday, December 8, 2022
Absa yazindua Ripoti ya Viashiria vya Masoko ya Fedha Afrika
Monday, December 5, 2022
Benki ya DCB yafunga mwaka ikiendelea kubeba tuzo lukuki
Monday, November 21, 2022
TANGA CEMENT YASHINDA TENA MZALISHAJI BORA TUZO ZA RAIS
Thursday, November 10, 2022
Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi yazinduliwa jijini Dar
Thursday, October 13, 2022
SWISSPORT YAKABIDHI MSAADA WA ULTRASOUND CCBRT
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi akipokea kifaa tiba - mashine ya Ultrasound kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania Mrisho Yassin katika hafka iliyofanyika leo Hospitalini hapo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi (kulia), akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya kifaa tiba cha Ultrasound kilichotolewa na Swissport kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto chenye thamani ya shilingi Milioni 68.
Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania Mrisho Yassin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi kifaa tiba cha Ultrasound kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya mama ma mtoto katika Hospitali ya CCBRT leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi
KATIKA kuhakikisha sekta ya afya inazidi kukua na jamii ya watanzania inakuwa na afya bora kampuni ya Swissport Tanzania PLC imeendelea kuwa karibu na jamii na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Sama Suluhu Hassan kwa kutoa msaada wa kifaa tiba ‘Ultrasound’ chenye thamani ya shilingi milioni 68 katika taasisi ya CCBRT.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania PLC Mrisho Yassin amesema mchango huo umeelekezwa kuwasaidia akina Mama wajawazito.
‘’Tunatambua kuna changamoto ya vifaa tiba na sisi kama kampuni tumeliona hili na kuona kutoa mchango huu, kwa taarifa tuliyopewa kifaa hiki kitasaidia sana kutokana na uhiitaji wa mashine hii hapa CCBRT ili kusadia jamii ya watanzania akina Mama wajawazito.’’ Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi ameishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kuchangia kifaa tiba hicho cha Ultrasound kitakachoongeza nguvu ya kuwahudumia akina Mama wajawazito wengi zaidi na kwa ufasaha.
‘’Sisi kama CCBRT asilimia 87 ya wagonjwa wanaokuja hapa ni aidha wanapata huduma za bure kabisa au wanachangia….Tunahitaji kushikwa mkono katika maeneo makuu matatu ya huduma za kibingwa na bobezi za afya, mafunzo kwa wafanyakazi na watoa huduma na eneo la vifaa na vifaa tiba na tunawashukuru Swissport na tuendeleze uhusiano huu.’’ Amesema.
Amesema, tangu kuanza kutolewa kwa huduma katika kitengo cha Mama na Mtoto mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu wamewahuduma akina Mama wapatao 225.
‘’CCBRT tunatoa shukrani zetu za dhati kwa SwissPort kwa kututembelea na kutoa kifaa hiki kwa umoja huu iko siku ambayo tutaona kila mwanamke anayepata ujauzito anajifungua salama na kwa furaha….Tunashukuru sana kwa msaada wenu na ushirikiano wenye kwenye huduma hizi za kuokoa maisha ya watu.’’ Amesema.
Aidha amesema, mwezi Julai mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu alizindua rasmi kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto ambacho kimepewa jina la ‘CCBRT- Samia Suluhu Hassan Maternity Wing’ kutokana na juhudi binafsi na Serikali anayoiongoza katika kupigania afya za akina Mama wajawazito na watoto wachanga pamoja na maboresho makubwa ya sekta ya afya nchini kote.
‘’Lengo la kuanzishwa kwa kitengo hiki ni cha uzazi ni kutaka kuwahakikishia akina Mama wote uzazi salama, kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi sambamba na kuzuia ulemavu….kitengo hiki kimedhamiria kuwahudumia akina Mama wajawazito wenye ulemavu, wenye historia hatarishi za uzazi, akina Mama wenye historia ya fistula na mabinti wanaopata mimba katika umri mdogo.’’ Amesema.
Monday, October 10, 2022
Benki ya Absa kutoa huduma bora zaidi zinazokidhi mahitaji ya wateja
Sunday, October 9, 2022
Benki ya DCB yang'ara ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja
- Benki ya kwanza kufuzu kutoka benki ya kijamii kwenda Benki ya Biashara.
- Benki ya kwanza Tanzania kusajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
- Benki inayoongozwa na watanzania kuanzia Bodi ya Wakurugenzi hadi Menejimenti.
- Benki imewanyanyua wajasiriamali wanawake zaidi ya 400,000 kupitia mikopo ya vikundi.
- Benki inatoa huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja.
- Benki ina Wateja kuanzia wajasiriamali wadogo, wafanyabiashara wa kati na wakubwa, wateja binafsi, waajiriwa, mashirika na makampuni.
- Benki ipo sambamba na waajiriwa na inatoa mikopo yenye riba nafuu.
- Benki ipo sambamba na wazazi kuwawezesha watoto elimu hadi chuo kikuu kupitia akaunti ya Skonga na mkopo wa ada.
- Benki inatoa mikopo ya nyumba yenye masharti nafuu.
- Fanya miamala na malipo mahali popote kupitia DCB Pesa, DCB Wakala, Visa, Master Card QR, DCB Malipo na Internet Banking.
- Kufanya miamala nje ya nchi kupitia International money transfer na Western Union.
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAJIVUNIA KUSHEREHEKEA HUDUMA BORA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo Bi Janemary Rutahoile ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga, Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki hiyo Jema Msuya na kushoto ni Meneja wa TCB Tawi la Mlimani City Happy Ernest.Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo Bi Anna Philemoni ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga. Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy ErnestAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga pamoja na wateja wa wa benki hiyoAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki Deodarus Nkeyera ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga na Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy Ernest.
Tanzania Commercial Bank (TCB) imewahakikishia wateja wake kuwa inabuni mipango madhubuti ya kuzindua bidhaa mpya zinazoendana na mahitaji ya watumiaji wa huduma za kibenki kote nchini.
Akizungumza na wateja wake waalikwa wakati wa wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commercial Bank lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi, alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatoa huduma bora na yenye kumdhamini mteja.
"Thamani yetu kuu iko katika uhakika kwamba tunamjali na kuvutiwa na mteja, tunataka kuwahakikishia wateja wetu wapendwa kuwa tumejitolea kufanya uzoefu wako wa kibenki kuwa wa kufurahisha zaidi," alisema.
Anna Philemon, mteja wa Tanzania Commercial Bank alisema Benki ya TCB imeweka huduma zake na bidhaa ziko mikononi mwa mteja, na hivyo kuwasaidia wateja kufanya miamala kwa njia rahisi zaidi.
Anna alitoa wito kwa Watanzania kutoka nyanja mbalimbali kujiunga na Tanzania Commercial Bank na kufurahia baadhi ya huduma bora na bidhaa za kipekee zinazotolewa na benki hiyo.