A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, August 27, 2021

JENGA HUB NA KIDS FINANCE NA TRACY YAWAFUNDISHA WATOTO NAMNA BORA NA MATUMIZI YA FEDHA

 

IMG-20210824-WA0058%2B%25281%2529
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jenga Hub ambae pia ni Miss Tanzania wa zamani Nancy Sumari (kushoto), wakitiliana saini na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Kids Finance na Tracy zilizoanzishwa na msichana wa miaka 11, Tracy Rabi, kwaajili ya makubaliano ya kufanya kazi pamoja yenye lengo la kuwasaidia watoto wa Kitanzania namna bora yamatumizi ya fedha na ujasiliamali wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Programu ya Mipango Lilian Makoi, Mwanzilishi wa program ya Natokaje kidigitali Gertrude Mligo, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam | Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Kids Finance na Tracy, zilianzishwa na msichana wa miaka 11, Tracy Rabi ambaye leo ametia saini mkataba wa makubaliano na Miss Tanzania wa zamani na mwanzilishi wa Jenga Hub, Nancy Sumari, kwa ajili ya ushirikiano wa kufanya kazi pamoja kwa kuwapa elimu ya kisasa watoto wa Kitanzania juu ya ujasiriamali nan a matumizi mazuri ya fedha.

Ushirikiano huo pia umejumuisha Natokaje Kidigitali, iliyoanzishwa na Getrude Mligo. Natokaje Kidigitali imekuwa ikijihusisha na watoto wenye umri wa kuanzia miaka 8 hadi 17 kwa kushirikiana na mfanyabiashara aliyepata mafanikio makubwa Mohammed Dewji na wakongwe kama Gillsant Mlaseko.

Wamekuwa wakiwapa watoto fursa ya kujifunza kutoka kwa watu wenye vipaji nchini.Nancy alisema kuwa amekuwa akiendesha taasisi yake kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu sasa na kuwasaidia kujifunza masuala mbalimbali ya kibiashara yanayokwenda sambamba na teknolojia ya kisasa.

Msichana mwenye umri wa miaka 11, Tracy Rabi, sio tu anaandika vitabu vya kifedha na ujasiriamali kwa watoto lakini pia alianzisha Maonyesho ya Uzoefu wa Ujasiriamali kwa Vijana wa Tanzania ambayo hukusanya pamoja watoto wenye miradi ya ujasiriamali ili kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa watoto wengine, kama njia ya watoto ya kujaribu na kujifunza ujuzi wa ujasiriamali tangu wakiwa na umri mdogo.

Taaisi hizi tatu zimeungana pamoja ili kutoa fursa ya aina yake kwa watoto wa Tanzania kuongeza nafasi ya kujifunza ujasiriamali na kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa nchini.

Hii pia inakwenda sambamba na lengo la Serikali la kuhakikisha kuwa kizazi kijacho kinapata teknolojia na vifaa muhimu vya kisasa ili kuendanana na kasi ya teknolojia. Kuboresha upatikanaji wa teknolojia ni moja ambayo ni ajenda kuu ndani ya sekta ya mawasiliano haswa, kwa njia ambazo zinafaidisha vizazi vipya.

Kampeni hiyo inayoitwa Children Bootcamp, imeanzishwa mwaka huu ambapo inatarajia kusaidia watoto zaidi ya 200 kutoka katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Ninaamini kwamba sio mapema kwa vijana kuanza kujifunza kuhusu biashara na fedha kama watoto, tunatumia zaidi ya miaka 16 shuleni kupata ujuzi wa kutusaidia kupata pesa, ni muhimu watoto wawezeshwe kupata pesa, kuweka pesa na ujuzi wa kukuza pesa, kuwasaidia kuepukana na umaskini au mitego ya madeni inayosababishwa na ukosefu wa elimu ya kifedha,” alisema Tracy Rabi.

Watoto wanatakiwa kuelewa hatua za awali za kuhifadhi fedha, thamani ya fedha, kuanzisha biashara na kujua mbinu za kuendesha biashara ambazo ni hatua muhimu kwa haki za binadamu,” alisema Rabi.

Tunafurahi pia tutakuwa na program za watoto na zinazopatikana Tracy Kids Finance ambaye zinaonyesha kuwa hata watoto wadogo wanaweza kupata ujuzi na kuwajengea mazingira ya kuwa wafanyabiashara wenye mafanikio. Ujuzi upo wa unapatikana katika ulimwengu tunaoishi kwa njia ya za kidijitali,” aliongeza.

Nancy Sumari aliongeza “Tumejipanga kuleta mapinduzi katika kuwajengea uwezo watoto kwenye vitengo vifuatavyo:

● Elimu ya Fedha
● Elimu ya Kidijitali
● Ujasiriamali
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive