Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Elibariki Masuke (wanne kulia), akikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vikiwemo mabati 240, mifuko 120 ya saruji na kilo 30 za misumari ya bati kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi, Grace Quintine kwaajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa 20 katika Shule ya Msingi Nazareth iliyopo Wilaya na Mbinga Mkoani Ruvuma wengine pichani ni maofisa wa Benki ya NBC pamoja na viongozi wengine kutoka Serikalini na Uongozi wa Kamati ya shule hiyo hafla ya makabidhiano hayo ya vifaa hivyo vya ujenzi

Benki ya Taifa ya Biashara imekabidhi mabati 240, mifuko 120 ya saruji na kilo 30 za misumari ya bati mkoani Ruvuma kwa dhamira ya kuunga mkono serikali katika juhudi zake za kuendeleza elimu kupitia ujenzi wa madarasa.
Msaada huo ulitolewa kwa Shule ya Msingi Nazareth iliyopo Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma na kupokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji huo, Grace Quintine.
“Serikali pamoja na wazazi tutaongeza nguvu kwenye ujenzi wa madarasa 20 ambayo yatakamilisha lengo la kuwa na jumla ya vyumba 30 vya madarasa pamoja na ofisi.” Amesema Grace.
Aidha Mkuu wa Shule ya Msingi ya Nazareth, Mwalimu Anitha Agustino Mbungo amesema kwamba jitihada za ujenzi zilianza mwaka 2020 kwa ushirikiano baina ya wazazi, kamati ya shule na uongozi wa kata lakini kushindwa kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo kutokana na changamoto za kifedha.
“Uhaba wa madarasa ni mkubwa sana na muda mwengine hupelekea wanafunzi hadi 200 kutumia chumba kimoja hivyo naomba taasisi zingine kuiga mfano wa Benki ya NBC kwa kuchangia katika ujenzi wa madarasa ili kuendelea kuboresha elimu nchini.” Amesema Mbungo.
Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Elibariki Masuke aliwasihi wanafunzi wa shule hiyo kuendelea kusoma kwa bidii na kushikilia wanayofunzwa walimu ili kuja kuwa viongozi wakubwa nchi hapo baadaye.
Aidha Masuke pia amewapongeza wazazi na uongozi wa shule kwa jitihada zao za kuchangia na kuanza ujenzi wa madarasa shuleni hapo.
“Benki yetu na NBC ni mdau mkubwa wa elimu, kwa kawaida kila mwaka tunatenga fungu kutoka katika faida yetu kwa ajili ya kurudisha katika jamii na tunaipa elimu kipaumbele. Kuwekeza kwenye kwani tukiwa kama benki elimu inatusiaida kupata wateja na wafanyakazi wa benki yetu wa baadaye. Tutaendelea kuchangia na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha elimu kwa kadri tunavyoweza na tunaahidi kwamba huu si mwisho.” Ameongeza Masuke
0 comments:
Post a Comment