Friday, August 27, 2021
JENGA HUB NA KIDS FINANCE NA TRACY YAWAFUNDISHA WATOTO NAMNA BORA NA MATUMIZI YA FEDHA
Wednesday, August 25, 2021
Vodafone renews its relationship with Workplace to build bridges in a hybrid world
Tuesday, August 24, 2021
Facebook Marketplace Rolls Out to 37 Countries & Territories Across Sub-Saharan Africa
PROF:KITILA MKUMBO ATANGAZA FURSA ZA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA
23 Agosti, 2021 – DAR ES SALAAM.
Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara Mhe. Prof Kitila Mkumbo (Mb) ametangaza fursa za uwekezaji katika Viwanda 20 vilivyokuwa vimebinafsishwa na kurejeshwa Serikalini.
Mkumbo ameyasema hayo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu fursa za kuwekeza katika Viwanda vilivyobinafsishwa na kurejeshwa Serikalini leo tarehe 23 Agosti 2021 katika ukumbi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) jijini Dar es salaam.
Akiongea na Waandishi hao, Prof. Mkumbo amefafanua kuwa Serikali ilifanya tathimini mwaka 2017 katika Viwanda 156 vilivyobinafsishwa tangu mwaka 1990 na kubaini kuwa Viwanda 88 vinafanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya mikataba husika na Viwanda 68 vilikuwa havifanyi kazi kwa mujibu wa mikataba husika.
Akiendelea kufafanua zaidi, Prof. Mkumbo amesema Serikali ipo katika hatua ya kurudisha Viwanda 48 kati ya Viwanda 68 visivyofanya kazi kwa mujibu wa mikataba husika kwa hatua zingine za uwekezaji ambapo hadi sasa Viwanda 20 havina mgogoro wa kisheria na viko katika hatua ya uwekezaji.
Prof. Mkumbo pia amefafanua utaratibu wa kuwekeza katika Viwanda hivyo 20 kwa kuvigawa Viwanda 10 kwa wawekezaji kutoka Sekta binafsi ili waviendeleze, Viwanda nane (8) vimekabidhiwa kwa Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje EPZA kwa ajili ya wawekezaji katika maeneo hayo na Viwanda viwili (2) vitakabidhiwa mashirika ya umma ili waviendeleze kwa kuingia ubia na wawekezaji wa sekta binafsi.
Viwanda 10 vitakavyokabidhiwa kwa Sekta Binafsi kwa ajili ya uwekezaji ni pamoja na Kiwanda cha Kilimanjaro Paddy Hauling kilichopo Kilimanjaro, Polysacks Company Ltd kilichopo Dar es salaam, NMC Isaka Rice Mill Company Limited kilichopo Shinyanga na Multpurpose Oil seed Processing Co.ltd (MOPROCO). Alitaja Prof. Mkumbo.
Vingine vilivyotajwa na Prof. Mkumbo ni pamoja na CDA Intergrated Concrete Industry Kilichopo Dodoma, Manawa Generies Ltd kilichopo Mwanza, NMC Tabora Rice Mill kilichopo Tabora, Musoma Textikes Mills kilichopo Musoma, NMC Mzizima Maize Mill kilichopo Dar es salaam na Pesticides Manufacturers limited - Moshi kilichopo Kilimanjaro.
Viwanda nane (8) vinavyokabidhiwa kwa EPZA ni pamoja na Mwanza Tanneries kilichopo Mwanza, TPL Shinyanga Meat Plant kilichopo Shinyanga, Mafuta Ilulu kilichopo Lindi, Nachingwea Cashewnut kilichopo Lindi, TPL Mbeya kilichopo Mbeya, Sikh Sawmill Limited kilichopo Tanga na National Steel Corporation kilichopo Dar es salaam. Alitaja Prof. Mkumbo.
Prof Mkumbo pia alibainisha Viwanda viwili (2) vitakavyokabidhiwa Mashirika ya Umma ni pamoja na Mag’ula Mechanical MachineTolls kilichopo Mororgoro kitakabidhiwa kwa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mbeya Ceramics Co. Ltd kitakabidhiwa kwa Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo (SIDO).
Aidha amesema Wawekezaji wenye nia na uwezo wa kuwekeeza katika Viwanda hivyo wawasilishe maombi yao Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo zoezi la kuwapata wawekezaji litafanyika kwa uwazi na ushindani na taratibu za maombi hayo zitatolewa katika vyombo vya habari.
Wakati huohuo, Prof Mkumbo amesema kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana Ofisi Taifa ya Takwimu (NBS) imekamilisha utafiti wa awali wa kutathimini ya maendeleo ya viwanda nchini ambapo kwa sasa Tanzania ina viwanda 80,969 kati ya hivyo Viwanda Vidogo sana vevye uwezo wa kuajili mtu 1 - 4 na mtaji usiozidi milioni tano (5), ni 60,463, Vidogo vyenye uwezo wa kuajiri watu 5 hadi 49 na mtaji wa milioni tano (5) hadi milioni 200 ni 17, 267, vya Kati venye uwezo wa kuajiri watu 50 hadi 99 na mtaji wa milioni200 hadi milioni 800 ni 684 na Vikubwa vyenye uwezo wa kuajiriwatu 100 na zaidi na mtajizaidi ya milioni 800 ni 618.
Vievile, wakati wa Mkutano huo Prof Mkumbo alisema Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) limebuni mitambo midogo itakayotumika kuzalisha sukari kwa wakulima wadogo katika mikoa yenye uwezo wa kulima miwa ya sukari ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa sukari nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TEMDO Prof. Fredrick Kahimba amesema utengenezaji wa mitambo hiyo yenye uwezo wa kuchakata tani 10 za miwa na kuzalisha tani 1 ya sukari aina ya “brown sugar’ utakamilika kabla ya mwezi Disemba 2021 na kuanza kutumika kabla yam waka wa Fedha 2021/22 kuisha.
Kutokana na ubunifu huo, Prof. Kahimba amewasihi wakulima wadogo katika mikoa yenye mabonde yanayoweza kulimwa miwa ya sukari kulima na kuungana ili kuanzisha Viwanda vidogo vya kuzalisha sukali katika maeneo yao.
Saturday, August 21, 2021
BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI SHULE YA MSINGI NAZARETH MKOANI RUVUMA
“Serikali pamoja na wazazi tutaongeza nguvu kwenye ujenzi wa madarasa 20 ambayo yatakamilisha lengo la kuwa na jumla ya vyumba 30 vya madarasa pamoja na ofisi.” Amesema Grace.
Aidha Mkuu wa Shule ya Msingi ya Nazareth, Mwalimu Anitha Agustino Mbungo amesema kwamba jitihada za ujenzi zilianza mwaka 2020 kwa ushirikiano baina ya wazazi, kamati ya shule na uongozi wa kata lakini kushindwa kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo kutokana na changamoto za kifedha.
“Uhaba wa madarasa ni mkubwa sana na muda mwengine hupelekea wanafunzi hadi 200 kutumia chumba kimoja hivyo naomba taasisi zingine kuiga mfano wa Benki ya NBC kwa kuchangia katika ujenzi wa madarasa ili kuendelea kuboresha elimu nchini.” Amesema Mbungo.
Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Elibariki Masuke aliwasihi wanafunzi wa shule hiyo kuendelea kusoma kwa bidii na kushikilia wanayofunzwa walimu ili kuja kuwa viongozi wakubwa nchi hapo baadaye.
Aidha Masuke pia amewapongeza wazazi na uongozi wa shule kwa jitihada zao za kuchangia na kuanza ujenzi wa madarasa shuleni hapo.
KLABU YA BIASHARA YA NBC YAINGIA MKOANI RUVUMA
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando pamoja na maofisa wa Benki ya NBC na wateja wake wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara iliyozinduliwa na Benki ya NBC Mkoani Songea. |
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando pamoja na maofisa wa Benki ya NBC na wateja wake wakiserebuka mara baada ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara iliyozinduliwa na Benki ya NBC Mkoani Songea. |
Benki ya Taifa ya Biashara imezindua NBC Biashara Club, Mkoa wa Ruvuma katika hafla ya uzinduzi ilifanyika katika hoteli ya Heritage Cottage Wilaya ya Songea na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Songea, DC Pololet Komando ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, RC John Ibuge.
NBC Biashara Club ni sehemu ya mkakati mpana wa benki hiyo wa kuwainua wajasiriamali kwa kuwajengea uwezo wa kibiashara kupitia semina za mafunzo, kuwasogezea huduma za kibenki, kuwajengea mitandao ya kibiashara pamoja na kuwapa mbinu za kurasimisha biashara zao ili waweze kukopesheka. Jitihada hizi za Benki ya NBC zinaonekana kuzaa matunda kwani benki hiyo ilifanikiwa kuzindua klabu ya biashara kwa Mkoa wa Kigoma miezi michache iliyopita.
Zaidi ya kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara, NBC Biashara Club pia inatoa fursa ya kuwakutanisha wanachama wake na watoa huduma mbali mbali katika sekta ya biashara zikiwemo taasisi za serikali kama TRA ili kujadili na kutatua changamoto na kupata mafunzo zaidi kwenye masuala ya kodi, uagizaji malighafi na bidhaa kwenda na kutoka nje.
Uzinduzi wa NBC Biashara Club mkoani Ruvuma unakuja siku chache baada ya benki hiyo kuanzisha huduma ya NBC Wakala Plus wilayani Mbinga. Benki hiyo pia iliendesha semina za mafunzo kwa makundi mbali mbali ya wajasiriamali wilayani humo kwa dhumuni la kuwajengea uwezo katika kuendesha biashara. Pamoja na semina kwa wajasiriamali benki ya NBC kupitia huduma ya NBC Shambani, ilikutana na viongozi na wanachama wa vyama vya ushirika (AMCOS) Mkoani Ruvuma ili kujadili fursa zinazotokana na kushirikiana kwa sekta za kilimo ya kibenki.
Benki ya NBC kupitia klabu yake ya biashara pia iliandaa semina maalum kwajili ya wajasiriamali wanawake wa Wilaya ya Songea ambapo pia walitoa mafunzo na kupata fursa ya kutambulisha huduma zake za kibenki na kuwaelimisha wajasirimali hao juu ya faida na manufaa ya huduma hizo.
Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, mgeni rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Songea, DC Pololet Komando aliwahikishia wafanyabiashara wa Ruvuma kuwa Benki ya NBC ni benki kongwe nchini ambayo inaelewa changamoto na mahitaji ya wafanyabiashara. DC Sololet pia aliipongeza benki hiyo kwa kutoa elimu kwa wajasiriamali wa mkoa huku akiwasihi kutumia fursa za mikopo inayotolewa na Benki ya NBC kukuza biashara. zao.
“Tunawapongeza kwa kufunga safari kuja kuonana na wananchi wa Ruvuma ambao ni wafanyabiashara na wakulima wa mazao ya chakula na biashara, huu ni uthibitisho kwamba benki yen uinathamini wateja wake.” Alisema DC Pololet
Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC,Nd ElibarikiMasuke alisema kamba mafanikio makubwa ya klabu ya biashara ya NBC yametokana na ushikiano kutoka kwa serikali kupitia taasisi zaidi ya 15 zikiwemo TRA, BRELA, SIDOna TABWA. Ushirikiano ambao umesaidia benki hiyo kufikia dhumuni la kuongeza ukaribu baina ya Benki ya NBC na wateja wake kupitia na mafunzo ya ujasiriamali.
“Mpaka sasa tumeweza kufungua NBC Biashara Club katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Mbeya, Moshi, Morogoro, Singida Kahama, Lindi, Mtwara, Masasi, Tanga , Kigoma, Dar es Salaam na leo tunazindua hapa Songea. Kupitia jukwaa la NBC Biashara Club, wafanyabiashara zaidi ya 6,300 wamenufaikana mafunzo tunayotoa na safari za kibiashara kwenda nje ya nchi.” Alisema Nd Elibariki.
Aidha Nd Elibariki alisema kwamba pamoja na changamoto ya gonjwa la Uviko-1, benki hiyo ina azma ya kufikia mikoa yote ya Tanzania hivyo benki hiyo inachukua tahadhari zote za kujikinga na gonjwa hilo wanapoendesha makongamano na wajasiriamali.
Thursday, August 19, 2021
AKIBA COMMERCIAL BANK YAZINDUA AKIBA WAKALA
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Akiba Commercial Bank Webster Kaunga (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa benki hiyo ilipozindua huduma za Akiba Wakala katika Tawi la Makao Makuu barabara ya Ohio jijini Dar es Salaam jana wengine pichani n Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Dora Siria na Mkuu wa Kitengo cha mikopo wa Benki hiyo Charles Kamoto.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Akiba Commercial Bank Dora Saria amesema benki hiyo imeanzisha huduma ya Wakala ijulikanayo kwa jina la Akiba Wakala.
Huduma hii itawasaidia wateja wa benki hiyo kupata huduma kwa urahisi zaidi popote pale walipo kupitia mtandao mpana wa huduma za Wakala unaopatikana nchi nzima.
Dora Saria ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo kwenye tawi la benki hiyo ililopo baeabaea ya Ohio mkabala nahoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana.
Amesema Mteja anaweza kupata huduma ya kutoa na kuweka fedha mahali popote penye tangazo la Akiba Wakala Kupitia huduma hii tutawafikia Watanzania wengi popote pale walipo na wataweza kunufaika na huduma zetu.
Pia ameongeza kuwa kwamba, kupitia huduma hii ya Akiba Wakala Benki watakuwa washiriki wazuri katika kuunga mkono harakati za Serikali za kuhakikisha uwepo wa huduma jumuishi za kifedha yaani (Financial inclusion) kwa Watanzania wote.
Tumeingia sokoni na jumla ya Wakala wapatao 200 na lengo letu ni kuendelea kuongeza Wakala wengi kadri iwezekanavyo kwa lengo la kukidhi kiu ya upatikana wa huduma za Akiba nchi nzima, kwa urahisi na ukaribu kwa kumfata mteja popote alipo au kwa urahisi waweza kusema pasipo na ulazima kwa kufika tawini.
Aidha, Benki itaendelea kuboresha huduma hizi za Akiba Wakala kwa kuhakikisha upatikana wa mahitaji mengi ya kibenki kadri iwezekanavyo kwa Wakala wetu kwa lengo la kuleta urahisi na huduma zaidi kwa wananchi kama tulivyoainisha kwenye kauli mbiu ya huduma hii ya Akiba Wakala ambayo inasema Huduma Zaidi.
“Tunategemea kutoa huduma za kufungua akaunti na nyinginezo nyingi hapo mbeleni. Vile vile Benki imeanzisha mkakati rasmi wa kuhakikisha kuingia rasmi katika mfumo wa kidigitali katika mchakato wa kutoa huduma.”. Amesema Dora Saria
Mfumo huu utaendelea kuleta unafuu na kuokoa gharama za upatikananji wa huduma zetu.Pia tunazo huduma za Akiba Mobile, ambazo zinawawezesha wateja wetu kupata mahitaji mbali mbali ya Kibenki na mengineyo mathalani kununua LUKU, ving’amuzi, muda wa maongezi pamoja na malipo yote ya Serikali kupitia simu zao za mikononi.
Ameongeza kuwa wateja wote wa Benki ya Akiba wanaomiliki akaunti binafsi wanakuwa wameunganishwa na huduma hii na wanaweza kufanya miamala popote pale walipo. Huduma ya Akiba Mobile inaptikana kupitia mfumo wa USSD na App kwa wale wanoatumia simu janja.
Pia huduma ya Akiba Mobile inamuwezesha mteja kufanya miamala yake ya kibenki kupitia Akiba Wakala vile vile.Kabla ya hitimisho naomba pia niwadokeze ndugu wnahabari kuwa Benki ya Akiba inatoa huduma nyingine nyingi za Amana, Mikopo, kuuza na kununua float, kutuma na kupokea fedha kupitia Western Union n.k.
Ametoa rai kwa Watanzania wote watembelee matawi yetu yote pamoja na Akiba Wakala kwa ajili ya kuhudumiwa na ufafanuzi.Kwa kumalizia, ikumbukwe kwamba benki yetu imepata mwekezaji wa kimkakati, ambaye ni National Bank of Malawi (NBM).
Ni imani yetu kwamba ubia huu utasaidia kupanua wigo wetu wa kibiashara ikizingatiwa NBM ni moja ya benki kubwa kwenye ukanda wetu wa nchi kusini mwa Afrika.
Vile vile, tutaendelea kuboresha na kuanzisha huduma nyingi zikiwemo za kidijitali na hizi za Akiba Wakala imezinduliwa rasmi na tunawakaribisha Wateja wetu wote watumie huduma hiyo kwa mahitaji yako kibenki na wakumbuke kuwa hawana ulazima wa kufika matawini kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kwenye Akaunti zao, kufanya marejesho ya mikop
Thursday, August 5, 2021
TCB UPGRADES INTERNET BANKING TO UNRIVALLED NEW HEIGHTS
Tanzania Commercial Bank (TCB) has upgraded its
internet banking service to uniquely new heights in the market by fully
integrating the digital finance solution with all national payment systems.
Its Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi said the
revolutionary development is unrivalled in the industry and has been developed
internally at no cost.
“The TCB Internet Banking solution was developed
in-house at zero cost by our ICT experts and its edge over other online banking
services is being fully integrated with all national payment systems,” Mr
Moshingi said yesterday at its launch in Dar es Salaam.
“If we had bought its off shelf that would have cost
us between US$300,000 and US$500,000,” he noted highlighting its cost
effectiveness since those prices translate to about TSh 695.7 million and
almost TSh1.16 billion respectively.
According to him, the investment in the new service is
part of TCB strategic plan to continue offering quality banking solutions that
meet changing market demands. Mr Moshing said the service upgrading move also seeks to enhance the bank’s commercial clout
and its competitiveness in the market.
The digital development has impressed government,
which said TCB Internet Banking will add a lot of value to national payment
systems.
Gracing the inauguration of the fast and affordable
online banking service, Treasury Permanent Secretary Emmanuel Tutuba said its
convenience and reliability are worth the investment.
Mr Tutuba commended TCB for investing in the highly
secure proposition that facilitates local and international transfers as well
as easing transactions such as bulk processing of funds as well as government
and utility payments.
“I have been impressed to hear that this digital
service channel is also connected to the MUSE system in order to simplify payments
for government institutions without necessarily having to visit banks,” he
noted.
MUSE is the government payment system that is a key
aspect of the e-government initiative, which promotes the use of ICT for
improving public service delivery.