A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, June 5, 2020

RC MAKONDA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI WILAYA YA TEMEKE


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wakazi wa mbagala alipofanya ziara yakukagua miradi mbalimbali iliyotelekezwa na Raisi Magufuli katika Wilaya ya Temeke leo jiji humo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikagua mitaro inayojengwa katika shule ya sekondari Kibasila ambayo imekuwa korofi wakati wa kipindi cha mvua.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa katika kituo cha afya kukagua maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizindua Majengo ya Madarasa 124, Matundu 124 ya Vyoo na Madawati 7,179 kwenye Shule ya Sekondari Mbagala na Shule nyingine 16 Wilayani humo jambo linalokwenda kusaidia zaidi ya Wanafunzi 5,000 waliofaulu na kukosa nafasi kupata uhakika wa kuendelea na masomo.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makondaa akiendasha mtambo wakufyatulia matofali. Picha zote na Brian Peter...



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemuelekeza Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuhakikisha wanawashughulikia ipasavyo baadhi ya vijana walioanza tabia ya kupora na kuiba Mali za Watu jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya Watu.

RC Makonda amesema operesheni maalumu ya kushughulikia Vibaka hao imeanza rasmi jana ambapo amemtaka kila mzazi kuhakikisha anamchunga mwanae kwakuwa hakuna kibaka atakaesalimika katika msako huo.

Mhe. Makonda ametoa agizo hilo wakati wa Ziara ya ukaguzi miradi ya maendeleo Wilaya ya Temeke iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Majengo ya Madarasa 124, Matundu 124 ya Vyoo na Madawati 7,179 kwenye Shule ya Sekondari Mbagala na Shule nyingine 16 Wilayani humo jambo linalokwenda kusaidia zaidi ya Wanafunzi 5,000 waliofaulu na kukosa nafasi kupata uhakika wa kuendelea na masomo.

Aidha RC Makonda ametembelea Ujenzi wa kituo cha Afya Buza na Hospital ya Yombo Vituka yenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 2,000 kwa Siku ambapo amesema kuongezeka kwa Zahanati, Vituo vya Afya na Hospital vinakwenda kurahisisha upatikanaji wa Huduma za Afya kwa wananchi.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema ifikapo Juni 20 ataanza Ziara ya Siku 10 na Kamati ya Siasa ya Mkoa kwenye kila jimbo kwa lengo la kukabidhi miradi iliyokamilika ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Vitendo.

Katika Ziara hiyo RC Makonda pia ametembelea *Ujenzi Mitaro yenye urefu wa Km 9 Wilayani humo ikiwemo mtaro mkubwa kabisa unaojengwa eneo la Serengeti kuelekea Shule ya Sekondari Kibasila na Maradi na Mradi wa uwezeshaji wa vijana kupitia 10% ya mikopo inayotolewa kwenye halmashauri ambapo ameipongeza Manispaa hiyo kwa namna inasimamia miradi ya maendeleo.

MATUKIO KATIKA PICHA










Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive