Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu
(aliepiga magoti), akizindua rasmi zoezi la upandaji miti lililopewa jina la
Kijanisha Dodoma na kudhaminiwa na Benki ya NBC katika mtaa wa Swaswa
Halmashauri ya jiji la Dodoma likiwa na lengo la kutunza mazingira katika mkoa
huo. Nyuma ya mheshimiwa waziri ni Meneja
wa Kanda ya kati wa NBC James Ndimbo, Afisa mauzo wa benki hiyo, Zachalia Lema
(kushoto), pamoja na Mkuu wa huduma kwa
Wateja, Anne Mwasaka. Upandaji miti huo umefanyika Dodoma hivi karibuni.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya NBC
James Ndimbo, akipanda miti huku wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na na
viongozi wa kata ya Swaswa wakiangalia wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya
upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma uliofanyika mkoani humo kwa udhamini wa Benki
ya NBC hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa
Azzan Zungu (kushoto), akishikana mikono na Afisa Mauzo
wa Benki ya NBC, Dodoma, Zachalia Lema wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya
upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma uliofanyika mkoani humo kwa udhamini wa Benki
ya NBC hivi karibuni.
Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa
taka ngumu Halmashauri ya jiji la Dodoma, Dickson Kimaro akipanda mti mara
baada Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu
kuzindua kampeni ya upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma na
kudhaminiwa na benki ya NBC katika mtaa wa Swaswa Halmashauri ya jiji la Dodoma
hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Azzan
Zungu (katikati), akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi waa NBC, wakazi wa
kitongoji cha Swaswa pamoja na wakai wengine wa Dodoma walishiriki hafla ya
upandaji miti lililodhaminiwa na benki hiyo.
0 comments:
Post a Comment