A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, February 14, 2020

KAMPUNI YA TOTAL NA COCA COLA YATOA ZAWADI YA VALENTINE DAY KWA WATEJA WAO

Mkurugenzi wa Sheria  na Mahusiano wa Kampuni ya Total Tanzania,Marsha Msuya (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa siku ya Kusambaza Upendo katika siku ya wapendanao ambapo kampuni ya Total wakishirikiana na kampuni ya Coca cola wameanda zawadi maalumu kwaajili ya wateja wao hasa wanawake ambao watakuwa wamevalia mavazi yenye rangi nyekundu wengine (kushoto), ni Meneja Mauzo wa coca cola kanda ya Dar es Salaam Ruqaiya Alibhai pamoja na Meneja Msimamizi  wa Maduka , Chakula wa ToTAL Jane Mwita.   hafla hiyo imefanyika leo  katika kituo cha mafuta cha Total cha Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sheria  na Mahusiano wa Kampuni ya Total Tanzania,Marsha Msuya (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mteja wa kwanza aliefika katika kituo cha Total Bi. Sara Ndile wakati wa siku ya Kusambaza Upendo katika siku ya wapendanao ambapo kampuni ya Total wakishirikiana na kampuni ya Coca cola wameanda zawadi maalumu kwaajili ya wateja wao hasa wanawake ambao watakuwa wamevalia mavazi yenye rangi nyekundu wengine (kushoto), ni Meneja Mauzo wa coca cola kanda ya Dar es Salaam Ruqaiya Alibhai pamoja na Meneja Msimamizi  wa Maduka , Chakula wa ToTAL Jane Mwita.   hafla hiyo imefanyika leo  katika kituo cha mafuta cha Total cha Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa kampuni ya Total na Coca cola wakipiga picha wakati wa hafla hiyo

KAMPUNI ya Mafuta ya Total imeungana na Watanzania kusherehekea sikuku ya wapendanao ya Valentine kwa kuhamasisha upendo ambapo imetumia siku hiyo ya Februari 14 kutoa zawadi kwa kwa  kila mteja mwanamke aliyefika kuweka mafuta katika kituo cha Total.

Akizungumzungumzia kuhusu kuhamasisha upendo, Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Total, Marsha Msuya Kileo amesema kampuni ya Total inawapenda Watanzania na ina upendo siku zote ndio maana inawaletea mafuta bora yenye kiambata cha excellium na bidhaa  bora za vilainishi, na leo ndio imeamua kuwaonesha upendo kwa kuwapatia zawadi ya sikukuu ya Wapendanao ya Valentine kwa wateja wao, kwa kuonesha ishara ya upendo na kuwawezesha kusherehekea siku hiyo.

"Lengo la kutolewa kwa zawadi hizo ni ishara ya upendo na tumeamua kusambaza upendo kwa wateja wetu wote. Tumeamua kuwahamasisha Watanzania kuwa  na upendo kwa kupendana kama Total inavyowapenda Watanzania, na tunawakumbusha kuwa ukijaza mafuta kwenye kituo cha Total, haujazi mafuta tuu, bali unajaza mafuta ya Total Excellium ambayo ni mafuta yenye viambata vya kuifanya gari yako itumie mafuta kidogo, kwa kwenda umbali mrefu, huku mafuta hayo, yakiboresha injini ya gari yako,"amesema.

Amefafanua jumla ya vituo 16 vya mafuta vya Total ndivyo vimeteuliwa kuendesha zoezi hilo, katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanza Mbeya na Morogoro.

Kuhusu Total amesema ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi na kwamba ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati hiyo duniani kote na inawafanyakazi  100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama,  na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na  ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili  watu wengi waweze kuimudu.


Pia Total ipo katika nchi zaidi ya 130,  na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.

Baadhi ya wateja ambao wamepata upendo wa Total wameipongeza kampuni hiyo kwa kuonesha ishara ya kuwapenda kwa kuwapa zawadi  hiyo na kueleza ni jambo ambalo  linawaunganisha kati yao na kampuni hiyo.

 Kwa upande wa mmoja wa wateja waliojaza mafuta katika kituo cha Total kilichopo Mliman City jijini Dar es Salaam Leila Hassan amesema hakutarajia kupata Zawadi kutoka Kampuni ya Total ikiwemo ua lenye rangi nyekundu ambalo ni ishara ya upendo katika siku ya Valentine."Tunawapongeza Kampuni ya Total kwa kuonesha maana halisi ya Valetine Day kwa vitendo, Zawadi ambazo wametoa kwa wateja itabaki kuwa Kumbukumbu ya muda mrefu maishani,"


Total imeanzisha kampeni kabambe utafutaji na uzalishaji wa mafuta kwa kuongeza idadi ya visima vya mafuta huku ikijitahidi kupata nishati endelevu kwa ajili ya Bara la Afrika kwa sasa na baadae. Total imejikita katika uhamasishaji wa utafutaji vya vyanzo vipya vya nishati kutoa kipaumbele cha elimu ya nishati kwa vijana ili kuendeleza uwezo wa kipekee wa bara hili la Afika kujiletea maendeleo. Mbali na hilo,Kampuni ya Total   ndio sambazaji wa kwanza wa bidhaa za mafuta (mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa , lami,  na GPL, nk) katika bara la Afrika. Shukrani kwa mizizi yake ya kihistoria, ubora wa bidhaa na huduma zake, kutoka jumla ya vituo 4200 vya mafuta  katika nchi arobaini barani Afrika.  Vituo vya mafuta vya Total ni vituo tegemeo kwa wafanya biashara binafsi na wateja wake. Lengo letu ni kuwezesha upatikanaji mkubwa zaidi wa nishati, ambayo pia inahusisha kuendeleza upatikana wa vyanzo vingi na mbadala vya nishati na kwa gharama nafuu -  kama vile nishati ya jua, kwa kuuza vifaa vya nishati ya jua
Total tunasikiliza mahitaji ya wadau wetu, na sisi kwenda nao pamoja nao katika kuendeleza maendeleo ya kiuchumi, ajira, elimu na afya. www.total.com

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za  kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total Katika kujitanua kibiashara kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala, kampuni ya Total Tanzania Limited kupitia mradi wake wa 
Total Access to Solar (TATS) project, inasambaza taa za nishati jua zinazoitwa  AWANGO kwa jamii ya Watanzania.








Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive