Mchambuzi
wa maswala ya Kibiashara wa Benki ya CBA Yessie Yassin (katikati), akichezesha
droo ya tano ya miaka mitano ya Kampeni ya M-PAWA, iliyofanyika hivi karibuni
jijini Dar es Salaam wanaoshuhudia ni (kushoto), ni Mwakilishi kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Abdallah Hussein pamoja na Afisa kutoka CBA
Maria Marballa.
Benki ya CBA ikishirikiana na kampuni ya Vodacom imefanya
droo yake ya 5 ya kuadhimisha miaka 5 ya huduma ya MPawa yenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa
wateja wake kwenye makao makuu ya benki hiyo Dar es salaam.
Katika kusherehekea maadhimisho hayo, promosheni hiyo
inajumuisha droo za kila wiki zilizohusu kuwekeza na kukopa na MPawa huku ukitoa washindi zaidi ya 340
walioibuka na mara mbili ya akiba zao kuanzia kiwango cha Tsh 1000-200,000, simu janja na muda wa maongezi.
Katika kuongelea kuhusu huduma hii ya MPawa, Meneja Masoko wa
benki hiyo Bw Solomon Kawiche aligusia
mambo 3 muhimu kwenye maadhimisho hayo.
M-Pawa inasherehekea miaka 5, ni mafanikio gani yameonekana
tangu kuanzishwa kwa huduma hii?
Mpawa ilianza na wateja 4 tu ila hadi leo hii
imefikisha wateja Mil 8.5 na imefanikiwa kurahisisha Maisha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za
kibenki kwa kuwapatia huduma nafuu.
Ikiwemo kukopa kiasi kidogo cha hadi 1000 ambacho hauwezi
kupata kupitia huduma za benki. M-Pawa imefanikiwa kutoa huduma ya kuhifadhi akiba kwa kiwango cha chini cha
hadi Tsh 1, hakuna benki nyingine
ndani ya Tanzania inayotoa huduma kama hii na kurahisisha huduma za kibenki
bila ya kuwa nautaratibu mrefu kukamilisha miamala.
Watumiaji wa M-Pawa hawana haja ya kutembelea
matawi yetu na kupitia huduma hii, wateja wetu wanapata faida kupitia akiba
zao. Akiba za wateja wa MPawa pia zipo kwenye usalama wa hali ya juu kwasababu hakuna makato wala gharama
zilizofichika.
MPawa imeinua hali ya Maisha ya mamilioni ya watanzania
hususani wafanyabiashara wadogo na bila kusahau kuwa imekuwa ikitoa uhakika wa kifedha wakati wa dharura; mteja
anaweza kukopa muda wowote na
wakati wowote ule.
Nini malengo ya baadae ya M-Pawa?
Ikiwa ni huduma ya kwanza ya kidigitali Tanzania, MPawa
itaendelea kugusa miasha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za kibenki na itaendelea
kujidhatiti kwenye kuwajumuisha kifedha wateja wake.
Kama
benki, tuna maleno ya kuwekeza zaidi kwenye huduma hii kuhakikisha kuwa
inaendana na maendeleo ya sasa ya kisayansi
na Teknolojia na kuwezesha huduma hii kwenye application.
Nini maoni yako kwenye huduma za kifedha za kiditali hususani
M-Pawa?
Huduma za kifedha za kidigitali kwenye dunia ya leo ni sio kitu
ya kupuuza hususani huduma kama MPawa
kwa sababu ya urahisi wake kwenye gharama, uaminifu wake na urahisi wake katika
kuitumia.
MPawa inapatika kupitia simu yoyote ya mkononi,
ni huduma ya kibenki iliyorahisishwa kutumia mahalipopote kwa gharama
nafuu na humpatia mteja faida kupitia akiba anayoweka bila kuwa na gharama zilizofichwa.
Hili linaupa upekee
huduma hii ya M-Pawa Mshindi mkubwa wa maadhimisho
haya ya Miaka 5 ya MPawa ataibuka na zawadi ya Million 15 za kitanzania kwenye droo ya mwisho ya promosheni hiyo.
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii, wateja wanaweza
kutembelea mitandao ya kijamii ya benki ya CBA/Vodacom au kutembelea menyu ya MPawa kwa kubonyeza
*150*00# kupitia mtandao wa vodacom
0 comments:
Post a Comment