Monday, July 29, 2019
THOUSANDS OF PEOPLE BENEFITED FROM LSF's "SIYO TATIZO TENA CAMPAIGN"
Zanzibar-based paralegal, Donald Msechu educating residents in Unguja on legal and related matters, including accessibility and accessibility of free legal aid services during “Sio Tatizo Tena campaign” which is funded by the Legal Services Facility (LSF) in Zanzibar. (Photo by Correspondent)
Around 2000 people have been reached with legal aid services, legal and human rights education through a focused and strategic campaign dubbed “Msaada wa Kisheria Siyo Tatizo Tena (Legal Aid is not a problem anymore in Tanzania)”—which has been designed to help needy and disadvantaged people out of various forms of injustices and violence.
Commenced officially late last year, the drive “Legal aid is not Problem Anymore in Tanzania” was meant to make it easier for poor women and men facing legal problems to access justice and secure their rights –through free legal aid services offered by paralegals. A six-month campaign (December 2018-June 2019) is implemented and sponsored by the Legal Services Facility (LSF)—a non-governmental and non-profit organization which provide financial and technical support to legal aid organizations involved in the implementation of paralegals and legal aid projects on Tanzania mainland and Zanzibar.
The campaign covered some wards across Temeke, Kinondoni and Ilala municipalities and several wards in Zanzibar—Unguja and Pemba, according to an official report issued by LSF. “Among other things, Msaada wa Kisheria Siyo Tatizo Tena crusade, seeks to broaden and enhance public awareness on the availability and accessibility of free legal aid services offered by paralegals across all districts of Tanzania,” noted LSF report in part.
Thousands of residents in Dar es Salaam (1, 1000) and Zanzibar (789) have benefited from the campaign; they received free legal aid services and got their legal and related problems (related to land, early-marriage, early-pregnancies, divorce, gender-based violence etc) resolved through quality legal aid services provided by paralegals.
In an exclusive interview with this paper, Coordinator of Kinondoni paralegal unit, Anthony Isakwi said “Of course, ‘Msaada wa Kisheria Siyo Tatizo Tena’ has produced impressive results in our municipality, as many people in two wards (Kigogo Mkwajuni and Kawe Sokoni) were counseled and received relevant education on legal and other related affairs.”
Elias Mkapa, Coordinator of Temeke paralegal centre said the campaign benefited thousands of needy people in the municipality, some of them had their problems solved (on the spot) peacefully by Temeke paralegals in three wards Fenesini, Mangengeni and Mtongani. He, however, suggested that “such campaigns should be conducted on regular basis, at least once in a month in order to produce greater results.”
Residents in Ilala municipality received free legal assistance (counseled and advised) during the “Msaada wa Kisheria Siyo Tatizo Tena Campaign” conducted in two wards—Bungoni-Mafuriko and Buguruni, according to Salumu Kindokomile, Coordinator of Ilala paralegal centre.
“It’s undeniable fact that approaches of the campaign (which included drama and music performances, public shows etc), is good and results-oriented, as it attracts and allow many people to get legal aid education at a go. But we still need to expand the drive, covering all wards of the Dar es Salaam municipalities,” noted Kindokomile.
For his part, Jovin Rugambo, an official from Paladin & Associates, a media agency which provided technical support in the implementation of the campaign, said large number of people turned up and benefited (in terms of legal and related education and their problems resolved) during the campaigns conducted in some parts of Zanzibar—Kwerekwe market at West B, Fuoni at West B, Kinyasini market, Matemwe wards in Unguja and two wards in Pemba--Muwambe-Mkoani and Mchangamdogo-Chwale.
“As a matter of fact, ‘Sio Tatizo Tena’ campaign has managed to raise public awareness on availability and accessibility of free legal services in different parts of Dar es Salaam—through different platforms—drama, music and public performances/shows, radio jingles, mentions, interviews, social media networks.
“Basically, this crusade was meant to ensure that the messages of free legal aid services, how to access these services, are aggressively taken across the country, down to the rural settings,” said Rugambo.
NBC yadhamini Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyaya (kulia), akisalimiana na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale, wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Maonyesho hayo yalifanyika katika viwanja vya Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akisaini kwenze kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki ya NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Maonesho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Majimaji mjini Songea MKoani Ruvuma mwishoni mwa wiki. Wengine kushoto kwa waziri ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale, Ofisa Mauzo, Jennifer Peter, pamoja na Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC, Hilaria Mhagama.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana mikono na Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Hilaria Mhagama alipotembelea banda la Benki ya NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea Simon Ntwale, na Ofisa Mauzo wa benki hiyo, Jennifer Peter
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana mikono na Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Jennifer Peter alipotembelea banda la NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Wa pili kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale pamoja na Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC Songea, Hilaria Mhagama.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana mikono na Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Jennifer Peter alipotembelea banda la NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Wa pili kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale pamoja na Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC Songea, Hilaria Mhagama.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema Maonesho ya Viwanda na kongamano la uwekezaji Ruvuma litaleta fursa nyingi za kibiashara na uchumi mkoani humo imeelezwa mjini Songea mwishoni mwa wiki.
Alisema Mkoa wa Ruvuma umejaliwa kuwa na fursa nyingi sana na kwa muda mrefu hawakuwa wakifanya tukio kama hilo lakini sasa kupitia kongamano hilo litawafungua kuwafahamisha watu mbalimbali kuwa nini kinapatikana mkoa huo wa Ruvuma.
Alisema changamoto zinazowakabili wawekezaji wadogo ni pamoja na upatikanaji wa mitaji lakini kwa sasa mkoa wa Ruvuma umepata mkombozi hususani Benki ya NBC ambayo inatoa mikopo mikubwa na midogo kwa masharti nafuu sana kinachotakiwa ni uaminifu.
"Nawakaribisha sana wawekezaji na wadau wote ambao wana nia thabiti ya kuja kuwekeza Ruvuma kwani mkoa huu umekuwa na nishati ya umeme ya kuridhisha inayoweza kukidhi mahitaji," alisema.
Kwa upande wake Meneja wa Tawi la NBC Songea,Simon Ntwale amesema kuwa maonesho hayo yamekuwa fursa nzuri kwa Benki ya NBC kwa sababu wameweza kukutana na wadau mbalimbali watakaoweza kufungua fursa mbalimbali za kibiashara.aziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa huo amesema kuwa Ruvuma itakuwa na wawekezaji mbalimbali .
Alisema NBC imepata faida ya kuingia mkataba na taasisi ya PASS ambapo wanakwenda kuwawezesha wakulima kupata mikopo ya kilimo ambapo mkopaji anaweza kupata pembejeo za kilimo.
Ntwale pia amewatoa shaka wakulima wakubwa na wadogo pamoja na wachakataji na wawekezaji wadogo kujitokeza kwa wingi ili kupata mkopo endapo kampuni ya PASS itakuwa imeadhinisha kwa mteja husika kupata mkopo huo.
"Wawekezaji na wakulima wadogo msiogope kuitumia Benki ya NBC kwani ni benki yenu ambayo ipo tayari kuwasaidia ili mtimize malengo yenu kwani wengi wamenufaika na mikopo hiyo hadi sasa wanafanya biashaza za mazao yao hadi nje ya nchi," alisema.
Monday, July 22, 2019
Sanlam yakabidhi madarasa na ofisi za walimu Kondoa
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakishikana mikono baada ya kufungua pazia la jiwe la msingi katika uzinduzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma (wa pili kulia) na Meneja wa Mamlaka hiyo kanda ya kati, Stella Rutaguza (kulia).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakati wa hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Katikati ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), DK. Mussa Juma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam Kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakifungua pazia la jiwe la msingi kuzindua madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam yenye thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kati, Stella Rutaguza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili na Ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima Sanlam kwa gharama ya shilingi Milioni 49. Makabidhiano yalifanyika shuleni hapo, Pahi, Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akihutubia katika hafla ya uzinduzi pamoja na makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa gharama ya shilingi Milioni 49. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman akihutubia katika hafla ya uzinduzi pamoja na makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Sanlam kwa gharama ya shilingi Milioni 49. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Katikati waliokaa ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Ashatu Kijaji na kushoto kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma.
Watanzania hawana budi kuchukulia bima kama hitaji muhimu na kujifunza aina mbalimbali za bidhaa za bima zilizopo sokoni ili wazitumie kujikinga, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Ashatu Kijaji amesema hivi karibuni akiwa ziarani wilayani Kondoa, Mkoani Dodoma.
Waziri huyo alitoa wito huo wakati wa hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya madarasa mawili, ofisi ya walimu na madawati 40 vyenye thamani ya jumla ya Tsh 49m kwa shule ya Msingi Lusangi iliyopo wilayani Kondoa, vilivyojengwa kwa msaada wa kampuni ya bima ya Sanlum, ambayo ndiyo mtoaji mkubwa wa bima barani Afrika.
“ Huduma ya bima inahitajika sana ili kuwawezesha watu kujikinga na majanga yasiyotabirika ya siku za usoni,” alisema Dr. Kijaji, na kuongeza kuwa ishara iliyoonyeshwa na kampuni ya Sanlam ya kurudisha sehemu ya faida yake kusaidia miradi ya jamii ichukuliwe kama ishara ya namna gani bima ni muhimu kwa uhakika wa maisha.
Akiongea katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda – Afrika Mashariki wa Sanlam Pan-Afrika, Julius Magabe, alisema kampuni hiyo itaendelea kusaidia miradi ya jamii nchini Tanzania.
“ Naomba nichukue fursa hii kuwahakikishia kuwa Sanlam tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutoa fedha kwa miradi mbalimbali ya jamii”, alisema Magabe, nakuongeza kuwa kampuni hiyo – ambayo imesherehekea mwaka 2018 imesherehekea miaka 100 tangu kuanziswha kwake, iko thabiti katika kurejesha sehemu ya faida yake kusaidia jamii.
Awali akiongea katika hafla hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lusangi, Josephine Paul, alisema shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madarasa, kwa kuwa madarasa matano yaliyokuwepo kabla hayakuweza kutosheleza idadi ya wanafunzi ambayo ni 348.
“Kutokana na mradi huu kukamilika, utakuwa umepunguza changamoto ya upungufu wa madarasa na oofoso ya walimu uliokuwepo,” alisema mkuu huyo wa shule.
Na katika hali ya kuonyesha ufanisi nadra katika matumizi ya fedha za wafadhili kitendo ambacho kilimvutia waziri Dr. Kijaji na vilevile ujumbe wa Sanlam, ujenzi huo siyo tu ulikamilika ndani ya muda uliopangwa, bali zaidi ya Tsh 2.7m zimeokolewwa kutokana na kupunguza gharama, fedha ambazo zimewekezwa katika ujenzi wa vyoo wa wanafunzi wa kike na wa kiume.
“ Sisi Sanlam hatujawahi kushuhudia mradi tunaoufadhili ukisimamiwa kwa umakini wa hali ya juu kiasi hiki,” Alisema Magabe, ambayo kampuni anayotumikia ina matawi ndani ya nchi 38 barani Africa, huku huduma zake zikiwa zimesambaa mabara ya Amerika, Asia na Australia
Friday, July 19, 2019
BENKI YA NBC YATOA SHILINGI BILLION 2.1 KUKOPESHA WASTAAFU
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la benki hiyo la Tegeta katika jengo la Kibo Complex jijini Dar es Salaam. |
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) nchini imetoa mikopo yenye jumla ya kiasi cha shilingi Billioni 2.1 kwa wastaafu tokea ilipozindua huduma ya mikopo ya wastaafu Juni mwaka jana.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Theobald Sabi, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bw Gaudence Shawa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Benki hiyo la Tegeta Kibo Commercial Complex alisema kwamba benki hiyo imewatambua wastaafu kama kundi muhimu la kiuchumi.
“NBC tumewatambua wastaafu wanaopokea pensheni kama kundi la kiuchumi ambalo lina uwezo wa kuchangia katika uchumi wa taifa letu kwa kuwezeshwa kifedha,”
Tuesday, July 16, 2019
MAMBO MATATU MUHIMU YATAJWA MIAKA MITANO YA M-PAWA
Mchambuzi
wa maswala ya Kibiashara wa Benki ya CBA Yessie Yassin (katikati), akichezesha
droo ya tano ya miaka mitano ya Kampeni ya M-PAWA, iliyofanyika hivi karibuni
jijini Dar es Salaam wanaoshuhudia ni (kushoto), ni Mwakilishi kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Abdallah Hussein pamoja na Afisa kutoka CBA
Maria Marballa.
Benki ya CBA ikishirikiana na kampuni ya Vodacom imefanya
droo yake ya 5 ya kuadhimisha miaka 5 ya huduma ya MPawa yenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa
wateja wake kwenye makao makuu ya benki hiyo Dar es salaam.
Katika kusherehekea maadhimisho hayo, promosheni hiyo
inajumuisha droo za kila wiki zilizohusu kuwekeza na kukopa na MPawa huku ukitoa washindi zaidi ya 340
walioibuka na mara mbili ya akiba zao kuanzia kiwango cha Tsh 1000-200,000, simu janja na muda wa maongezi.
Katika kuongelea kuhusu huduma hii ya MPawa, Meneja Masoko wa
benki hiyo Bw Solomon Kawiche aligusia
mambo 3 muhimu kwenye maadhimisho hayo.
M-Pawa inasherehekea miaka 5, ni mafanikio gani yameonekana
tangu kuanzishwa kwa huduma hii?
Mpawa ilianza na wateja 4 tu ila hadi leo hii
imefikisha wateja Mil 8.5 na imefanikiwa kurahisisha Maisha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za
kibenki kwa kuwapatia huduma nafuu.
Ikiwemo kukopa kiasi kidogo cha hadi 1000 ambacho hauwezi
kupata kupitia huduma za benki. M-Pawa imefanikiwa kutoa huduma ya kuhifadhi akiba kwa kiwango cha chini cha
hadi Tsh 1, hakuna benki nyingine
ndani ya Tanzania inayotoa huduma kama hii na kurahisisha huduma za kibenki
bila ya kuwa nautaratibu mrefu kukamilisha miamala.
Watumiaji wa M-Pawa hawana haja ya kutembelea
matawi yetu na kupitia huduma hii, wateja wetu wanapata faida kupitia akiba
zao. Akiba za wateja wa MPawa pia zipo kwenye usalama wa hali ya juu kwasababu hakuna makato wala gharama
zilizofichika.
MPawa imeinua hali ya Maisha ya mamilioni ya watanzania
hususani wafanyabiashara wadogo na bila kusahau kuwa imekuwa ikitoa uhakika wa kifedha wakati wa dharura; mteja
anaweza kukopa muda wowote na
wakati wowote ule.
Nini malengo ya baadae ya M-Pawa?
Ikiwa ni huduma ya kwanza ya kidigitali Tanzania, MPawa
itaendelea kugusa miasha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za kibenki na itaendelea
kujidhatiti kwenye kuwajumuisha kifedha wateja wake.
Kama
benki, tuna maleno ya kuwekeza zaidi kwenye huduma hii kuhakikisha kuwa
inaendana na maendeleo ya sasa ya kisayansi
na Teknolojia na kuwezesha huduma hii kwenye application.
Nini maoni yako kwenye huduma za kifedha za kiditali hususani
M-Pawa?
Huduma za kifedha za kidigitali kwenye dunia ya leo ni sio kitu
ya kupuuza hususani huduma kama MPawa
kwa sababu ya urahisi wake kwenye gharama, uaminifu wake na urahisi wake katika
kuitumia.
MPawa inapatika kupitia simu yoyote ya mkononi,
ni huduma ya kibenki iliyorahisishwa kutumia mahalipopote kwa gharama
nafuu na humpatia mteja faida kupitia akiba anayoweka bila kuwa na gharama zilizofichwa.
Hili linaupa upekee
huduma hii ya M-Pawa Mshindi mkubwa wa maadhimisho
haya ya Miaka 5 ya MPawa ataibuka na zawadi ya Million 15 za kitanzania kwenye droo ya mwisho ya promosheni hiyo.
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii, wateja wanaweza
kutembelea mitandao ya kijamii ya benki ya CBA/Vodacom au kutembelea menyu ya MPawa kwa kubonyeza
*150*00# kupitia mtandao wa vodacom
Monday, July 15, 2019
WATANZANIA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WA MITAA WANAOWEZA KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTON
Wakati Taifa linajiandaa kwenda katika Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Wito umetolewa kwa wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi kwa kupiga kura za kuchagua Viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaojali haki za Watoto wa Kike.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Shirika la utetezi wa haki za mtoto wa kike la New Hope Tanzania Bi. Elizabeth Ngaiza ambapo amesema Katika Kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" anayoendesha amebaini uwepo wa baadhi ya viongozi wa Ngazi za mitaa wasiokuwa na weledi, wasiowajibika na hawawezi kusimama katika nafasi yao kutetea haki za mtoto wa kike.
Aidha Bi. Elizabeth Ngaiza amesema lengo la Kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" ni kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa kike na kuhakikisha anawekewa mazingira wezeshi ya kusoma pasipo changamoto wala vikwazo vyovyote.
Hata hivyo Bi.Ngaiza amewaomba wadau na wananchi kuendelea kumuunga mkono katika Kampeni ya Kumlinda mtoto wa kike apate elimu Bora kwakuwa anaamini ukimwezesha mwanamke kupata elimu itasaidia kuinua kipato cha Familia na Taifa kwa ujumla.
Friday, July 12, 2019
LIGI YA PROPHET SUGUYE YAFIKIA HATUA YA ROBO FAINALI UKIPIGWA NJE
Beki wa machimbo FC Ekson Kavali, (katikati), akijaribu kumtoka Mshambuliaji wa Magereza FC, Frank William (kushoto), wakati wa mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule, ambapo katika mchezo huo Magereza iliibuka na ushindi wa 1-0 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mlinda mlango wa Machimbo FC, Dotto Doto, akikamata mpira wakati wamchezo wao dhidi ya Magereza FC katika mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule, ambapo mchezo huo umemalizaka Magereza ikiibuka na ushindi wa 1-0 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Monday, July 8, 2019
BENKI YA BIASHARA YA DCB YAJIKITA KWENYE VIWANDA NA KILIMO YAJA NA BIDHAA MAHUSUSI IJULIKANAYO DCB SOKONI KUWAWEZESHA WATANZANIA KIUCHUMI.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, James Ngaluko (kulia) na Mkurugenzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kayuni, Callington Kayuni (kushoto) wakiangalia mchele baada ya kutoka katika mashine wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichojengwa kwa mkopo kutoka DCB. Uzinduzi huo ulifanyika pamoja na uzinduzi wa huduma ya DCB Sokoni, kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani Songwe mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, James Ngaluko, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kayuni uliofanyika pamoja na uzinduzi wa bidhaa ya DCB Sokoni kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani Songwe mwishoni mwa wiki. Kiwanda hicho kimejengwa kwa mkopo kutoka DCB. Kushoto ni kurugenzi wa kiwanda hicho, Callington Kayuni na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mikopo Midogo wa DCB, Haika Machaku na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rahma Ngassa.
Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Mbozi, Richard Mwailanga (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kayuni kilichojengwa kwa mkopo kutoka Benki ya DCB. Uzinduzi huo uliofanyika pamoja na bidhaa ya DCB Sokoni, kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani Songwe mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda, Kallington Kayuni na Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, James Ngaluko. Mkurugenzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kayuni, Callington Kayuni akionyesha Mchele baada ya kutoka katika mashine kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, James Ngaluko (kulia) na kwa wahudhuriaji wegine, wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichojengwa kwa mkopo kutoka DCB. Uzinduzi huo ulifanyika pamoja na uzinduzi wa bidhaa ya DCB Sokoni, kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani Songwe mwishoni mwa wiki.Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara DCB, Rahma Ngassa (kutoka kushoto waliosimama), Mkurugenzi wa Mikopo Midogo, Haika Machaku na Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, James Ngaluko wakiangalia mchele baada ya kutoka katika mashine yan kukoboa wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichojengwa kwa mkopo kutoka DCB. Uzinduzi huo ulifanyika pamoja na uzinduzi wa bidhaa ya DCB Sokoni, kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani Songwe mwishoni mwa wiki.Mkurugenzi wa Mikopo Midogo wa DCB, Haika Machaku (kushoto), akisalimiana na mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Mbozi waliohudhuria uzinduzi wa kiwanda hicho uliofanyika paoja na uzinduzi wa bidhaa ya DCB Sokoni ya benki hiyo.
KATIKA kuhakikisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo Mwaka 2025 inatimia, Benki ya Biashara ya DCB imeingia na mpango kabambe wa kuviwezesha viwanda vya kilimo kwa kuja na bidhaa maalum ya DCB SOKONI ambayo inatoa suluhisho la kudumu kwa wakulima na wenye viwanda huku ikilenga kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kiuchumi.
Bidhaa hii mpya itamuwezesha mfanyabiashara mwenye azma ya kufungua viwanda vya kilimo kupata mikopo ya kuanzisha viwanda vya kilimo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo ukiofanyika pamoja na uzinduzi wa kiwanda kipya cha kukoboa mpunga cha mteja wao Bwana Callington kayuni, kilichopo katika kijiji cha Mlowo Mbozi Mkoa wa Songwe juzi, Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko alisema ‘tunayo furaha kubwa leo kushiriki kwenye uzinduzi huu muhimu na wa tija wa kiwanda hichi kikubwa na cha kisasa cha kukobolea mpunga kilichojengwa kwa uwezeshwaji mkubwa wa Benki ya biashara ya DCB, tunaamini kiwanda hichi kitakuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima wanaofanya shughuli zao za kilimo katika kijiji hichi na vijiji vilivyopo karibu na hapa.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa kuleta bidhaa hii mahususi ya DCB Sokoni, itawawezesha wafanyabiasha na wakulima sasa kufanya mapinduzi ya kweli kiuchumi kwa kutegemea kilimo pamoja na minyororo ya thamani kwani kupitia DCB tunakuongezea thamani ya mazao ya mkulima.
Alizitaja njia ambayo bidhaa ya DCB Sokoni itamuwezesha mteja kuwa ni pamoja na Kujenga kiwanda, kununua na kusafirisha mazao kutoka shambani, kuuza mazao ghafi au Kuchakata mazao na kuyaongezea thamani, usambazaji kwenda sokoni kwa wateja, ulinzi kutokana na bima ya maisha, kiwanda, pamoja na mazao ghalani katika kipindi chote cha mkopo, ununuaji wa nyumba ya makazi (Mortgage loan) utakaomwezesha kulipa taratibu kwa kipindi kirefu, ununuaji wa pembejeo kwa wafanyabiashara wa pembejeo na zana za kilimo, ubadilishaji wa fedha za kigeni zitokanazo na mauzo ya mazao na uwekezaji wa fedha kwa faida nzuri kupitia huduma ya DCB Lamba Kwanza.
“Natoa wito kwa wateja na wasio wateja kujiunga na DCB sokoni kwani tunatoa mikopo ya bei nafuu sana ambapo mkulima, mfanya biashara hawezi kushindwa kulipa na pia tunatoa thamani kwa mazao yako ili mteja aweze kushindana kwenye soko na bidhaa zake zinufaike na mnyororo wa thamani”, aliongeza Bwana Ngaluko.
Pamoja na hayo alisema uwezeshwaji wa viwanda vya kilimo kama ilivyo katika kiwanda hichi cha mteja wetu cha kukoboa mpunga, utachangia kwa kiasi kikubwa kasi ya uwekezaji kwa watanzania. Vilevile uwezeshaji huu utasaidia pia kuongeza kiasi cha mazao ya biashara yanayouzwa nje ya nchi, mazao ya biashara kama pamba, kahawa, korosho na mengineyo, hivyo kutuletea fedha za kigeni na kuinua pato la Taifa.
“Ni matumaini yetu wakulima na wafanyabiashara wa mkoa wa Songwe na maeneo jirani wataleta mazao yao katika kiwanda hiki hivyo kuweza kupata chakula na biashara itakayowaongezea kipato na kuinua maisha yao.
“Benki inaunga mkono juhudi za serikali katika kuiwezesha sekta ya kilimo kifedha, sekta hii inakabiliwa na changamoto nyingi, baadhi ikiwa ni ukulima unaotegemea mvua za msimu na changamoto za upatikanaji wa masoko, kupitia DCB Sokoni ni imani yetu tutaweza kuleta ufumbuzi wa baadhi ya changamoto hizo,” alisema mkurugenzi huyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi na Mmiliki wa kiwanda hicho, Callington Kayuni aliishukuru Benki ya DCB kwa uwezeshaji wa kifedha alioupata uliowezesha ujenzi wa kiwanda hicho kutoka hatua ya awali mpaka mwisho kiwanda chenye uwezo wa kukoboa hadi magunia 350 kwa siku.
“Nilipeleka michanganuo ya kuomba msaada wa kifedha katika Taasisi nyingi za Fedha, naishukuru DCB kwasababu walilipokea andiko langu kwa mikono miwili na matokeo yake ndio haya ambayo kila mmoja wenu anashuhudia kwa macho yake uwekezaji huu tulioufanya hapa Karacha, wilayani Mbozi,” alisema.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo alitaja changamoto ya masoko kuwa ni moja ya mambo yayozorotesha ufanisi wa kiwanda kwani wakulima wanaoleta mpunga kukobolewa kiwandani hapo hutegemea kupata soko hapo hapo la mchele hivyo wapo mbioni kuomba mkopo wa kifedha kutoka DCB utakaowezesha suala hilo.
Naye Richard Mwailanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi katika hafla hiyo alisema serikali katika wilaya ya Mbozi inaunga mkono juhudi za Taasisi za Fedha Kama DCB katika uwezeshaji wa viwanda kwani viwanda hivyo vinasaidia kuongeza mapato na pia kukuza uchumi kwa wakazi wa eneo hilo.
Pamoja na hayo aliongeza uanzishwaji wa viwanda kama hivyo utapunguza changamoto iliyopo sasa ya wakulima kuuza mazao yao yakiwa hayajatayarishwa jambo linalofanywa mazao yao kuuzwa kwa bei ya chini.
“Wakulima wengi wa Mbozi wangependa pia kuchukua mikopo kama alivyofanya Bwana Kayuni baadhi wanaogopa kutokana na hofu ya urejeshaji wa mikopo na riba, natoa wito kwa taasisi za fedha kuweka utaratibu rafiki katika eneo hilo hususani katika mikopo inayowahusu wakulima na kilimo,”. Aliongeza
Sunday, July 7, 2019
TANZANIA INA FURSA KUBWA YA KUVUNA UMEME WA NGUVU YA JUA
Waziri Mkuu Mtaafu Mh. Mizengo Peter Pinda na Mkurugenzi wa TANTRADE, Edwin Rutageruka (kushoto), wakimsikiliza Afisa Masoko wa Mobisol Farid Abdallah, wakati walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana.
Mfanya kazi wa kampuni ya Mobisol akitoa maelekezo kwa baadhi ya wateja waliotembelea banda lao wakati walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana.
Kama msambazaji wa huduma za vifaa vinavyotumia umeem unaotokana na nishati ya jua kwa maeneo ambayo hayana umeme, Mobisol inachukua fursa hii ya Maonyesho ya Sabasaba ya mwaka 2019 kupaza sauti kufikisha ujumbe kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa kubwa kupindukia ya kuzalisha umeme unaotokana na nishati ya jua, ikizingatiwa kuwa nchi hii ipo katika ukanda wa Tropiki, na kwa hiyo inapata nishati ya jua kwa kipindi kirefu cha mwaka. Tunatambua kuwa dhana ya matumizi ya umeme unaotokana na nishati ya jua ni jipya nchini Tanzania.
Hata hivyo, kwa kuzingatia inayotawala ulimwenguni ya kuvuna vyanzo vya nishati endelevu, ni muda muafaka sasa kwa watanzania kuanza kuwa na mtazamo chanya kuhusiana na manufaa ya muda mrefu ya nayotokana na matumizi ya nishati hiyo.
Umeme wa jua ni chanzo kinachofaa cha nishati mbadala majumbani. Nchi nyingi zimekwishagundua ukweli huo, na zimeachana na vyanzo vya kuzalisha nishati ya umeme vilivyozoeleka kama vile makaa ya mawe, ambavyo vinaitwika dunia mzigo mkubwa wa uharibifu wa mazingira, mzigo ambayo umegeuka changamoto kubwa.
Sisi Mobisol tunaitambua haja hiyo, na ndiyo maana tumeingiza sokoni mifumo inayokwendsa mbali zaidi ya ile ya kukidhi haja ya upatikanaji wa mwanga majumbani. Tumekuja na vifaa ambavyo vinakidhi haja nyingii. Bidhaa hizi ni bora ikilinganishwa vile vinavyotumiwa majumbani kwenye maeneo ambayo hayana umeme, kama mshumaa na taa za chemli.
Wigo wetu wa bidhaa ni mpana na una uwezo wa kukidhi mahitaji lukuki ya wateja, na bei zetu ni za chini kabisa miongoni mwa watoaji wa huduma ya umeme wa jua kwa maeneo yasiyofikiwa na umeme unaotoka kwenye Gridi ya Taifa.
Tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuwapa wateja elimu sahihi kuhusu uwezo mkubwa wa vifaa vyetu katika kukidhi haja zao mbalimbali.
Hii inajidhihirisha wazi kwa mifumo yetu ya 200W na 120W iliyopo sokoni, ambayo ina uwezo matumizi mengi majumbani.
Mifumo hii miwili ni madhubuti, ikiwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa jua wa kiwango kiwango cha juu kuliko ilivyo kawaida, na imeundwa kuhakikisha inakidhi haja mbalimbali majumbani.
Katika siku za usoni, tunapanga kuzindua bidhaa zanye uwezo mkubwa zaidi ili kupanua wigo wa matumizi, ambazo kwa sasa zipo katika hatua ya usanifu.
Swala la kuwa na bidhaa zenye ubora wa juu , vyenye uhakika gharama nafuu, na huduma zilizotapakaa kila mahali, kwa ujumla wake ndio vinafanya wateja wa Mobisol kujipatia thamani halisi ya pesa zao.
Uwezo huu wa kuzingatia thamani halisi ya pesa unatokana na uzoefu wetu ndani ya soko, tukiwa nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka minne sasa. Si ajabu tunafahamu vyema mahitaji hata ya mtu anayeishi maeneo ya ndani kabisa mashambani yasiyofikika kwa urahisi .
Mobisol ni mdau wa maendeleo wa kudumu nchini Tanzania kwenye jitihada za kufikisha huduma za umeme unaotokana na nguvu ya jua kwa maeneo yasiyokuwa na umeme, na tupo tayari kuwekeza zaidi katika kupanu wigo wa huduma zetu.
Dhamira yetu ya kusambaza umeme wa jua katika kila sehemu nchini inajidhihirisha wazi kwa jinsi ambavyo tumekita shughuli zetu hadi maeneo mengi ya mashambani, ambapo kipato ni cha msimu na kufanya malipo kutioka kwa wateja yawe ni ya kusuasua.
Licha ya mazingira hayo magumu kibiashara , tumejitahidi na kufanikiwa kufikisha huduma zetu maeneo mengi nchini.
Kiasi kwamba hivi sasa mteja anayelipa pesa taslimu kununua bidhaa zetu, anaweza kupata huduma sehemu yoyote nchini kupitia mtandao wetu wa huduma uliosambaa kote.
Jambo la kutia faraja zaidi ni kuwa pamoja na kuwa bidhaa zetu zinatumia teknologia ya kisasa kabisa ya mawasiliano, mfumo wetu hauna ugumu wowote kuutumia, na tunawatoa hofu kuhusu hilo wateja wote wanaotarajia kujiunga.
Mfumo wetu ni rahisi kutumia, na kila mteja amepewa namba maalum anayotumia kufanya miamala yote ya malipo na ile ya kukagua salio la mkopo wake.
Matumizi ya mfumo wetu ni rahisi kama ilivyo kufanya miamala kwenye simu za mkononi. Kuna manufaa ya ziada pale ambapo mteja anajiunga na huduma zetu za kulipa kwa awamu, kwa kuwa halipii umeme anaotumia bali analipia vifaa tu, kwa sababu umeme huo unatokana na nishati ya jua inayopatikana bure bure.
Na tungependa kuwahakikishia wateja wa umeme wa jua, waliojiunga na huduma zetu na wale wapya, kuwa Mobisol si wapiti njia na uwepo wetu ni wa kudumu.
Hii ni kwa sababu tunatambua ukweli kuwa umeme wa jua siyo suluuhisho la muda mfupi analokimbilia mtu wakati anasubiria kuunganishiwa umeme nyumbani kwake kutoka kwenye gridi ya Taifa.
Vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua vitaendelea kuwa ni vitu muhimu kwa takriban kila kaya wakati wote.
Tuwakumbushe wateja wa umeme unaotokana na nishati ya na wananchi wote wanaohudhuria maonyesho haya ya Sabasaba 2019 kuwa wakati ambapo uhaba wa nishati ya umeme lumekuwa ni changamoto kwa nchi nyingi duniani, ni baraka iliyoje kuwa Watanzania tunaweza kujichotea kadri tunavyohitaji nishati ya jua isiyokauka.
Kuigeuza umeme, na kama wasambazaji wa huduma ya vifaa vinavyotumia umeme huo, tunapendekeza swala la kutumia umeme huu lipigiwe debe na kila mdau wa nishati na litekelezwe ipasavyo.
Kwa sababu licha ya manufaa mengi ya umeme unaotokana na nishati ya jua, ugeni wa dhana hii nchini unatoa changamoto kwa wateja ambao wanakuta bidhaa za aina tofautitofauti zimejazana sokoni.
Matokeo yake, wengi wanajinunulia bidhaa kwa kubahatisha kwa kuwa wanashindwa kubainisha zipi ni bora kwa kuwa hawana taarifa sahihi na uzoefu.
Hali hii katika soko si rafiki sana kwa walaji. Tunakiri kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikiunga mkono kwa dhati mikakati ya kukuza matumizi ya nishati endelevu, jambo ambalo linatutia moyo.
Hata hivyo bado kuna mambo ya ziada yanayostahili kufanywa ili kujenga usimamizi dhabiti wa soko la bidhaa zinazotumia umeme wa jua ili kuhakikisha kuwa wateja wanapata bidhaa bora.
Tunaishauri serikali iende hatua ya mbali zaidi katika usimamizi wa soko la bidhaa za zinazotumia umeme wa jua, ili kuhakikisha kuwa walaji wanajipatia thamani halisi ya pesa yao. MWISHO. Kwa Malelezo Zaidi Wasiliana na : Seth Gerald Matemu Meneja Masoko Mobisol UK Ltd Simu: + 255 949 281