Mkurugenzi Mipango na Uendeshaji wa Taasisi ya Coconut Foundation Baraka Koukara, akizungumza na waandishi wa habari watika wa ufunguzi wa mashindano ya tahajia katika Shule za Msingi Tanzania (kushoto) ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Taasisi ya hiyo Zena Msonde (kulia) ni MenejaMradi wa Coconut Foundation Anna Mwalongo pamoja na Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Saluna Ally haflaya uzinduzi huo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Taasisi ya Coconut Foundation, Zena Msonde ( kushoto), akizungumza na waandishi wa habari watika wa ufunguzi wa mashindano ya tahajia katika Shule za Msingi Tanzania (katikati) ni Mkurugenzi Mipango na Uendeshaji wa Taasisi hiyo Baraka Koukara pamoja na Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Saluna Ally haflaya uzinduzi huo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala wa Taasisi ya Coconut Foundation, Saluna Ally (katikati)akizungumza na waandishi wa habari watika wa ufunguzi wa mashindano ya tahajia katika Shule za Msingi Tanzania (kushoto) ni Mkurugenzi Mipango na Uendeshaji wa Taasisi hiyo Baraka Koukara pamoja na Meneja Mradi Anna Mwalongo haflaya uzinduzi huo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
UFUNGUZI WA MASHINDANO YA TAHAJIA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI TANZANIA. (TANZANIA NATIONAL SPELLING BEE COMPETITIONS 2018)
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Coconut Foundation kwa kushirikiana na wizara ya elimu na TAMISEMI, imeanzisha mashindano ya kutamka herufi za maneno magumu ya lugha ya kiingereza, yenye lengo la kukuza elimu bora, uwezo wa kujieleza na stadi muhimu za maisha kwa wanafunzi wa shule za msingi Tanzania katika kuwaanda wawe nguvukazi sahihi ya uchumi wa viwanda.
Kwa mwaka 2018, zaidi ya shule 100 kutoka mikoa ya Dar es salaam na Lindi zitashiriki kuanzia ngazi ya shule mpaka kitaifa kuanzia mwezi huu Agosti mpaka kilele chake mwezi Novemba, na washindi 10 bora wakitarajia mialiko ya kimataifa. Shindano hili linahusisha shule zote za umma na binafsi, wadau mbalimbali wa elimu na umma kwa ujumla.
Kwa mwaka 2018, Mashindano haya yanaanzia ngazi ya shule ambapo washindi 21 hupatikana kufuzu ngazi ya kimkoa. Kutokana na uwingi wa shule, mkoa wa Dar es salaam manispaa zake 5 yaani Ubungo, Temeke, Ilala, Kigamboni na Kinondoni zitafanya mashindano ya kimkoa hivyo kufanya mikoa 6 pamoja na Lindi. Washindi 50 kutoka kila mkoa watafuzu mashindano ya kitaifa ili kupata washindi 10 bora kutoka makundi mawili kulingana na ngazi za madarasa. Mwaka jana 2017 washindi wa juu walipata nafasi ya kwenda kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki nchini Uganda na mashindano ya Afrika nzima nchini Afrika Kusini. Mipango zaidi kuhusu mwaka huu itatangazwa pindi itakapokamilika. Aidha, zawadi mbalimbali hutolewa kwa washindi.
Mashindano haya yenye kuifikia mikoa yote hapo mapema baadae, yatahusisha lugha za kiswahili na kiingereza lakini kwa mwaka 2018 ni kiingereza peke yake; yana lengo la kumuwezesha mwanafunzi kutawala kutawala mawasiliano katika kujieleza binafsi, kujiamini, kujua misamiati mingi ya lugha, kuzungumza katika halaiki za watu wengi, kukuza usikivu yakinifu, kusoma, kuandika, kumudu muda na kufanya mambo kwa wakati, kuishi katika timu na kupata utajiri wa maarifa na stadi mbalimbali ambazo hutunzwa katika fasihi mbalimbali na wataalamu.
Taasisi ya COCONUT FOUNDATION imesema kuwa Mashindano haya yamefanyiwa utafiti na kubaini kiini cha vijana wengi kutoibuka washindi katika soko shindani la ajira baada ya kuhitimu masomo, siyo elimu mbovu bali kukosa uwezo wa ndani kuzikabili changamoto bila woga, na uwezo wa kuitafsiri elimu waliyoipata kutoka nadharia kwenda kwenye matokeo ya kivitendo katika kuzitatua changamoto hizo. Tangu mwaka 2011 kutoka kwenye mwanzo mgumu mpaka kufikia mwaka jana 2017 ambapo shindano la kwanza la majaribio lilifanyika kwa mkoa wa Dar es salaam pekee, taasisi imesema uzoefu ulioonekana ni kuwa madhara ya kisaikolojia ya utotoni na mafunzo au malezi ya awali na msingi, humuathiri mwanadamu maisha yake yote ikiwa hakuna jitihada za utambuzi.
Kuwajengea wanafunzi haiba ya ushindi na kujitawala kuanzia ngazi za utotoni wawe vinara hapo baadae katika ulimwengu wa ajira, biashara na maendeleo mapana ya taifa na dunia kwa ujumla, ndilo lengo kuu la mashindano haya na kwa upekee kabisa taasisi hiyo imejikita kuleta chachu inayohitajika lakini haipo katika mtaala wa kawaida.
Taasisi inazikaribisha shule mbalimbali kujisajili, wadau mbalimbali wa maendeleoya elimu kuunga mkono jitihada hizi na vijana waliohitimu elimu hasa katika fani za lugha kuomba nafasi ya kujitolea ili kukuza ueledi wao na nafasi za ajira.
Aidha, taasisi inaomba ushirikiano kwa vyombo mbalimbali vya habari ili kukuza ufanisi wa shindano hili lenye kuendana na sera ya viwanda, katika kumjenga kijana mtanzania tangu hatua za awali.
Taasisi ya Coconut (Coconut Foundation) ni asasi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa mwaka mwaka 2015 chini ya wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, ,wazee na watoto; yenye lengo wa ukuzaji kiwango cha elimu ya kimatokeo kwa kuchagiza stadi muhimu zisizo katika mtaala wa kawaida bila kuuharibu mtaala uliopo bali kushirikiana na wizara husika; kwa kuwafanya wanafunzi wapende kujifunza na kujitegemea zaidi. Taasisi ina makao yake Kijitonyama, Dar es salaam.
Tunawatakia wote utendaji mwema wa maendeleo ya elimu Tanzania na ujenzi wa uchumi wa viwanda.
.........................
.........................
Coconut Foundation
DATE EVENT VENUE 9th July -21st September
2018
Training/Instructions on Spelling
guideline to students
At a respective participating school
21st July 2018 Teachers/facilitators envisioning
(T.O.T)
Coconut Foundation offices
4th August 2018 On-stage facilitators training
(judges/callers/Child carers etc)
Coconut Foundation offices
18th August 2018 Endorsement event(stakeholders
forum)
At one of the schools (to be advised soon
22nd-29th September 2018 School competitions At a respective participating school
1st October 2018
Strictly deadline at 1600
hours
End of submitting names of school
winners for regional BEE competitions
Submission at info@coconutfoundation.or.
6th October 2018 Temeke Regional competition National Museum Theatre, Posta-Dar es sala 13th October 2018 Kigamboni Regional Competition National Museum TheatrePosta-Dar es salaa 20th October 2018 Ubungo Regional Competition National Museum Theatre, Posta-Dar es sala 27th October 2018 Lindi Regional Competition Hall- Lindi 3rd November 2018 Ilala Regional Competition National Museum Theatre, Posta-Dar es sala 10th November 2018 Kinondoni Regional Competition National Museum Theatre, Posta-Dar es sala 15th November 2018 Lindi regional winners travel to Dar
es salaam for national competition
Dar es salaam-Mtwara road
16th November 2018 Orientation for all national
contestants
JNICC Hall (Julius Nyerere International Convention Centre) ,Posta-Dar es sal 17TH November 2018 Grand Finale Tanzania National Spelling Bee Competition
JNICC Hall (Julius Nyerere Internation Convention Centre) ,Posta-Dar e salaam 18th November 2018 Lindi regional winners traveling
back to Lindi
Dar es salaam-Mtwara road.
0 comments:
Post a Comment