Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 420 kwaajili ya udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia (kulia) ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chillo pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo Boniface Wambura.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario (wapili kulia) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia wakisaini Mkataba wa makubaliano ya Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni 420 zilizotolewa na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. (Kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo Boniface Wambura pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chillo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Wallace Karia (katikati),akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya makubaliano ya Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni 420 zilizotolewa na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo Boniface Wambura
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario (kulia),akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya makubaliano ya Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni 420 zilizotolewa na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. (katikati) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo Boniface Wambura
Mkuu wa kitengo cha Masoko na mawasiliano wa benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chillo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Wallace Karia , wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa KCB Bank na TFF.
KCB Bank Tanzania imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kudhamini Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) kwa msimu wa mwaka 2018/2019. Mkataba huo wenye thamani ya shilingi za Kitanzania 420,000,000 ulitiwa saini leo na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank, Nd. Cosmas Kimario na Rais wa TFF Nd. Wallace Karia katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
KCB Bank Tanzania imeongeza thamani ya udhamini wake kwenda ligi hiyo kutoka kiasi cha shilingi za Kitanzania 325,000,000 msimu wa 2017/18 mpaka shilingi 420,000,000 msimu wa 2018/19 ongezeko la ziadi ya milioni 90,000,000, ongezeko linaloashiria dhamira ya benki hiyo kutaka kunyanyua vipaji na kuendeleza ushindani katika mpira wa miguu nchini Tanzania.
Hafla ya kutia saini makubaliano hayo ilihudhuriwa pia na Kaimu Mwenyekiti wa Bodiya KCB Bank Tanzania, Bi.Fatma Chillo, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Nd. Boniface Wambura, Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi KCB Bank Tanzania, wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, Nd. Cosmas Kimario alisema kwamba mchango wa kiuchumi unaoletwa na soka ni mmoja sababu kubwa zilizopelekea KCB Bank Tanzania kutaka kudhamini ligi hiyo kwa Mwaka wa pili mfululizo. “Tunaamini kuwa sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini kwani ni chanzo cha ajira kwa watanzania hasa vijana.” alisema Nd. Kimario.
Kaimu Menyekiti wa Bodi ya KCB Bank Tanzania, Bi.Fatma Chilloalisema kuwa ni fursa ya kipekee kuweza kudhamini Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa pili. “Lengo letu ni kuleta hamasa kwa timu na mashabiki wa mpira wa miguu kwa kuzijengea timu, hata zile ndogo uwezo wa kifedha ili kuziwezesha kushindana kikamilifu hivyo kuongeza ushindani ndani ya ligi.” Alieleza Bi. Chillo.
Rais wa TFF, Ndg. Wallace Karia aliishukuruKCB Bank Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Tanzania jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2018/19. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.
Kuhusu Benki ya KCB
Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki.
Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba,Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.
Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment