Makamu
ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan, akipata
maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka kampuni ya
usambazaji na uuzaji wa gas ya Oryx Mohamed Mohamed (kushoto)
alipotembelea banda hilo wakati wa
kuadhimisha wiki ya mazingira yaliyofanyika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
kuadhimisha wiki ya mazingira yaliyofanyika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
ORYX GAS “Rafiki wa Mazingira”
Dar es Salaam, June 2018; Katika kuadhimisha wiki ya mazingira mwaka huu nchini Tanzania
kampuni mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya ORYX ijulikanayo
kama ORYX ENERGIES LTD imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali
ili kuhakikisha nishati mbadala inatumika badala ya mkaa ambao umeonekana kuwa na gharama kubwa sana.
ORYX GAS kwa nyakati tofauti wamekuwa
wadau muhimu sana katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kutunza mazingira, na kwa muda mrefu wamekuwa
na kampeni yao ya ORYX GAS “Rafiki wa
Mazingira”. Katika kuhadhimisha wiki ya mazingira wameamua kuchukua fursa kujiunga na wadau wengine kushirikiana katika
kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya
gesi ya kupikia kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo
inachochea uharibifu wa miti na mazingira kwa ujumla.
Akizungumza
katika maonyesho hayo
eneo la mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha mauzo
kampuni ya gesi ya ORYX Bw. Jeffrey Nasser amesema kuwA; ORYX GAS
amekuwa rafiki mkubwa sana wa mazingira pale tulipoamua
kuwaletea nishati mbadala ya gesi, na haikuishia hapo tuu bali
tuliwawezesha
wananchi wengi sana nchi nzima kuipata kwa gharama ndogo na hata yale
maeneo ya
wananchi wa hali ya chini tumewawezesha kupata gesi yetu. Na Tunaamini
tumeokoa
miti mingi ambayo ingekatwa kwa matumizi ya kupikia.
Ili kuhakikisha
kuwa watu wote wanatumia nishati ya gesi,kampuni ya ORYX imewekeza kwa kiwango
kikubwa sana kwenye maghara ya uhifadhi na mitambo ya kujaza gesi nchi
nzima.Hatutarajii kusikia tena uhaba wa gesi ya kupikia nchini na hatutarajii
kabisa watumiaji wa gesi wanarejea kwenye mkaa na kuni kwa kukosa nishati hii
ya gesi hapa nchini. Aliongezea Afisa Huyo wa ORYX .
Akielezea kaulimbiu ya mwaka huu ya
Mkaa ni gharama sana; Bwana Bw. Jeffrey amesema kuwa Mkaa ni gharama sana hasa
kwa wakazi wa mijini. Sasa hivi gunia la mkaa kwa wakazi wa Dar es salaml
imefikia shilingi 70,000 na wengi wanalalamika kuwa mkaa haumalizi mwezi.Sisi
tunawapa mtungi wa gesi wa kilo 15 ambao kwa familia ya watu saba wanaotumia
gesi pekee huweza kutumia kati ya siku 30 hadi 40. Mbali na faida za gharama
ndogo,gesi yetu pia ni salama kwa afya ya mtumiaji na usafi wa mazingira ambapo
tusingeanza usambazaji mkubwa wananchi wangepaswa kuweka bajeti nyingine za
matibabu ya madhara ya moshi mwilini na ukarabati wa nyumba ambazo huchafuka
sana kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.
Kampuni ya ORYX imetoa shukurani sana kwa wananchi kwa muitikio
mkubwa sana wa matumizi ya gesi kila siku inayoenda. Muitikio mkubwa umeonekana
hasa pale ongezeko la watumiaji wengi
wapya nchi nzima wakinunua mitungi mipya ya gesi ya ORYX kwa matumizi yao. Mbali
na hapo wengiwamerudisha mrejesho kuwa
walichelewa kuanza kutumia ges hiyo na wamehuakikishia uongozi wa kampuni ya
ORYX kuwa hawatarudi tena kutumia kuni na Mkaa.
Kampuni ya ORYX inatoa wito kwa jamii
yote kwenda na mabadiliko ya matumizi ya nishati ya kupikia, Oryx Gas kama wasambazaji
wakubwa sana nchini wameona muitikio mkubwa sana kwa jamii mbalimbali nchi
nzima hususani pembezoni mwa nchi.
Kampuni ya ORYX pia wametoa wito kwa serikali kuzidi kushirikiana
nao katika kuhamasisha wananchi katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia
nishati mbadala ya gesi. Na pia wameiomba serikali kusimamia Sheria za
mazingira kwa ukamilifu ili watu waelewe na waone umuhimu wa kutunza misitu kwa
vizazi vilivyopo na vijavyo.
0 comments:
Post a Comment