Programu inalenga kuboresha biashara zinazoongozwa na wanawake kwa kuwapa ujuzi katika usimamizi wa zabuni, uboreshaji wa bidhaa, usalama wa chakula, na mbinu za masoko.
• Uzinduzi huu unaendana na dhamira ya Stanbic ya kukuza maendeleo endelevu na kuwawezesha wajasiriamali wa ndani.
Dar es Salaam, Tanzania — Jumatano, 30 Oktoba 2024: Benki ya Stanbic Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuboresha Lishe (GAIN) kupitia Mtandao wa Biashara wa Kuongeza Lishe Tanzania (SBN), wamezindua kikundi cha saba cha Programu ya Maendeleo ya Wafanyabiashara chini ya kituo cha ukuzaji biashara cha Stanbic (BSI). Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha Biashara Ndogo na za Kati (SMEs), hasa zile zinazoongozwa na wanawake katika sekta ya chakula na lishe, kujenga mifano ya biashara inayozingatia maendeleo endelevu, kuchangia malengo ya ukuaji wa kiuchumi wa Tanzania kwa ujumla.
Ushiriki wa GAIN unaonesha dhamira yake ya kuboresha usalama wa chakula na lishe nchini Tanzania kwa kuwawezesha wafanyabiashara wa ndani kufuata viwango bora vya usalama na ubora wa chakula. Kwa kuunganisha mafunzo juu ya lishe na usalama wa chakula, GAIN inalenga kuhakikisha kuwa wazalishaji wa chakula wa Tanzania wanakidhi viwango vya sekta na kukuza mazoea bora ya lishe. Msaada wa GAIN utasaidia sio tu kuimarisha biashara hizi bali pia kuboresha ubora wa lishe wa bidhaa zinazopatikana kwa jamii za Kitanzania, hivyo kuchangia taifa lenye afya bora.
Dkt. Winfirda Mayilla, Mkuu wa Programu wa GAIN Tanzania, alisema, “Ushirikiano wetu na Stanbic haujalenga tu kuboresha ushindani wa SME za Tanzania bali pia kuinua jamii kwa kuongeza athari chanya za lishe kutoka kwa biashara hizi. Ushirikiano huu ni hatua kuelekea kufanikisha malengo ya GAIN ya kufanya upatikanaji wa vyakula vyenye virutubishi na unafuu kwa wote.”
Washiriki wa kundi hili la saba wamepata mafunzo maalumu ambayo yanakwenda zaidi ya ujuzi wa msingi wa biashara ili kushughulikia maeneo muhimu yanayoathiri biashara zao moja kwa moja. Mtaala ulioimarishwa ulijumuisha masomo ya juu katika usimamizi wa zabuni, uundaji na uboreshaji wa bidhaa, usalama wa chakula, na masoko ya kimkakati. Haya yote yamewapatia washiriki maarifa ya kuboresha ubora wa uzalishaji wao, kuboresha mazoea ya usalama wa chakula, kuuza bidhaa zao kwa ufanisi, na kushiriki katika fursa za zabuni za wauzaji.
Kupitia juhudi za pamoja za Stanbic na GAIN, washiriki wamepata zana zinazohitajika kutekeleza mazoea salama na yenye lishe katika uzalishaji wa chakula, kuhakikisha biashara zao zinakidhi viwango vya afya na ubora. Maarifa haya ya msingi juu ya usalama wa chakula ni muhimu kwa kujenga uaminifu miongoni mwa watumiaji. Zaidi ya hayo, programu hii imewasaidia washiriki kuimarisha mbinu zao za masoko, hivyo kuwawezesha kufikia masoko mapana na kushindana kwa ufanisi zaidi ndani ya sekta hii.
Aidha, washiriki wamejifunza kujenga mifano ya biashara yenye uthabiti inayozingatia maendeleo endelevu na kuingiza maudhui ya ndani, jambo ambalo linaongeza hamasa ya ushirikishwaji wa kiuchumi. Mbinu hii inasaidia sio tu mafanikio yao ya muda mrefu bali pia inachangia mazingira ya kiuchumi yanayozingatia usawa na uendelevu nchini Tanzania.
Programu hii inatoa miezi sita ya ushauri maalumu, ikiwapatia washiriki mwongozo wa kuendelea ambao unawasaidia kukabiliana na changamoto za soko na kukuza biashara zao kuwa uendelevu. Kwa kuongezea, wahitimu watajiunga na mtandao mpana wa wajasiriamali ndani ya kituo cha ukuzaji biashara cha Stanbic na mtandao wa SUN Business, kuwapatia ufikiaji wa miunganisho ya thamani na uwezekano wa ushirikiano.
Kai Mollel, Mkuu wa Kitengo cha Ukuaji Biashara kutoka Benki ya Stanbic Tanzania, alisema, “Kituo cha ukuaji biashara cha Stanbic siyo tu mahali pa mafunzo—ni jukwaa ambalo biashara za ndani hupata rasilimali, mitandao, na mwongozo wanaohitaji ili kukuza biashara zao. Kupitia ushirikiano kama huu na GAIN, tunaunda fursa endelevu zinazowezesha biashara na kujenga Tanzania yenye nguvu na yenye afya.”
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2022, kituo cha ukuaji biashara cha Stanbic kimekuwa nguzo muhimu ya dhamira ya Benki ya Stanbic Tanzania katika kusaidia biashara za ndani. Programu za BSI zinalenga kuwawezesha SME kwa njia za kujenga uwezo maalum, hivyo kuwawezesha kushiriki kwa manufaa katika sekta muhimu kama kilimo, viwanda, na sasa chakula na lishe.
Zaidi ya SME 200 wamepata mafunzo na zaidi ya ajira 500 zimeanzishwa hadi sasa kupitia rogramu ya Maendeleo ya Wauzaji ya BSI, ambayo imeonesha athari chanya katika mfululizo wa vikundi sita vilivyopita, ikichangia kwa kiasi kikubwa kwenye uhimilivu wa uchumi na uundaji wa ajira nchini Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Incubator kutoka Benki ya Stanbic Tanzania, Kai Mollel na Mkuu wa miradi kutoka Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN), Winifrida Mayilla wakitia saini ya Makubaliano (MOU) kwa ajili ya kushirikiana katika mafunzo ya awamu ya 7 ya Supplier Development Program. Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wanawake na vijana 50, wamiliki na waendeshaji wa biashara ya chakula. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na wafanyakazi wa Stanbic Bank Tanzania pamoja na GAIN Tanzania.