A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Saturday, May 19, 2018

Barclays giving a lesson on financial risk management

Barclays Africa Group Limited (BAGL) Strategic Markets Origination Africa, Mohamed Sayed giving a lesson on financial risk management during a workshop organized by Barclays Bank Tanzania in Dar es Salaam recently .
Barclays Bank Tanzania Director of Markets,  Esther Maruma  (right), chats to some banks customers during a one day financial risk management  workshop organized by BBT for its clients in Dar es Salaam  recently.
Barclays Bank Tanzania Director of Markets, Corporate and Investment Banking,  Esther Maruma  (right), shares a light moment with Barclays Africa Group Limited (BAGL) Strategic Markets Origination Africa, Mohamed Sayed during a one day financial risk management  workshop organized by BBT for its clients. Looking is a bank customer, Emmanuel Matalu.
A cross section of Barclays bank customers during a workshop on Financial Risk Management in Dar es Salaam recently.
Barclays Bank Tanzania   Head of Markets Sales, Irene Rwegalulira (second right), shares a light moment with some Barclays customers during a workshop on financial risk management hosted by the bank in Dar es Salaam recently.
Share:

Tuesday, May 15, 2018

Sanlam na Maxcom kuwawezesha wateja wa bima kufanya malipo kwa njia ya simu za mkononi

01%2B%25281%2529
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wa pili kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa, Jameson Kasati, wakisaini  hati za makubaliano ya ushirikiano utakaowawezesha ulipaji rahisi wa bima mbalimbali kupitia simu za mkononi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani ni maofisa wa Sanlam na wa Maxcom.
02

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wa tatu kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa, Jameson Kasati, wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano utakaowawezesha ulipaji rahisi wa bima mbalimbali kupitia simu za mkononi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani ni maofisa wa Sanlam na wa Maxcom.
03

Baadhi ya maofisa wa Maxcom  wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na viongozi wa Sanlam Life Insurance katika hafla hiyo.
04

 Baadhi ya maofisa wa Sanlam Life Insurance  wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na viongozi wa Maxcom katika hafla hiyo.

WATANZANIA watapata fursa ya kufanya malipo ya bima mbalimbali kwa njia rahisi zaidi kupitia simu zao za mikononi baada ya kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance na Maxcom kuingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara.


Akizungumza katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman alisema kwamba sheria ya bima imebadilika hivyo kuwataka wateja wa bima kuweza kufanya malipo yao  moja kwa moja kwenye kampuni za bima.

“Sheria ya bima huwa zinabadilika mara kwa mara kwa sasa sheria inamtaka mteja wa bima kuweza kufanya malipo bila kupitia kwa dalali au mawakala wa bima na tumegundua njia rahisi ya kuwawezesha wateja wetu ni hii ya kuweza kufanya malipo ni kupitia simu zao za mikononi,” aliongeza Suleiman.

Aliongeza kwamba utaratibu huo wa kulipa malipo ya bima kwa njia ya simu za mikononi unalenga kupanua wigo wa kulipa malipo na kuimarisha makusanyo ya michango na kumsaidia mteja wao kufanya malipo kwa njia rahisi zaidi ndani na nje ya nchini.

Aliongeza kwamba kwa takwimu za hivi karibuni takribani asilimia 62 ya watanzania wana miliki simu za mikononi ambapo ni sawa na watu milioni 20 lakini wanaofanya malipo ya bima  hawazidi laki moja.
“kwahiyo tumeamua kuungana na hawa ndugu zetu wa Maxcom ili kuweza kuwarahisishia wateja wetu kuweza kufanya malipo ya bima kwa njia ya simu za mkononi” aliongeza Suleiman

Kwahiyo alisisitiza umuhimu wa kuingia kwenye malipo kwa njia ya simu kwa kuwa kwa mwaka watanzania wanaofanya malipo kwa njia ya simu za mkononi ni wengi na takribani shs bilioni 1.4 kwa mwaka miamala kwa njia ya simu hufanyika.

Suleiman alisema ni muhimu kuweza kuingia kwenye soko hilo ili kuweza kuongeza wigo wa soko lake ambalo kwa sasa alisema kampuni hiyo ina asilimia 62 kwenye soko la bima nchini na kwa mwaka jana pekee kampuni yao ililipa madai kwa wateja wake kiasi cha shs billion 14.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Jameson Kasati alifafanua kwamba mfumo wa kampuni yao wa kielectroniki ni imara na salama kwa wateja wa bima nchini kuweza kufanya malipo mbalimbali kama michango na kulipa ada kwa wakati wakiwa mahali popote.

“tumejiunga na ulipaji wa njia ya kieletroniki na serikali ambapo pia watu na makampuni binafsi wanaweza kupata fursa hiyo ya kufanya malipo yao kwa njia ya simu za mkononi katika juhudi za kuboresha ulipaji wa huduma mbalimbali nchini,” alisema Kasati
Aliongeza kwamba uzinduzi wa huduma hiyo ni wakati muafaka wa watanzania kuweza kufanya malipo yao ya bima kwa njia ya simu za mkononi kwa mawakala mbalimbali ndani ya nchini.
Share:

ULEGA APOKEA MIFUKO 200 YA SARUJI

1
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akipokea mifuko 200  saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la bima la Taifa,Elisante Maleko yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya zahanati na madarasa.
02
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akipokea kava la tairi la gari kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la bima Taifa,Elisante Maleko  leo mkoani Pwani.
03
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na  Mbunge wa Mkuranga  Uvuvi,Abdullah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

MBUNGE na Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdallah Ulega leo Mei amepokea mofuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni tatu kutoka shirika la bima la Taifa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.

Akizungumza na waandishi wa habari Ulega ameeleza kuwa saruji hizo zitatumika katika ujenzi wa zahanati katika vijiji mbalimbali kama Kibamba, kazole, Yavayava  na Mkanonge Wilayani humo.

Ulega ameeleza kuwa kazi hii ni yetu sote katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli na kuifikisha Tanzania mbele zaidi.

Pia ulega ameeleza kuwa ujenzi wa miundombinu hasa ya madarasa na Zahanati unaendelea katika vijiji mbalimbali na hii ni katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za msingi.

Aidha Ulega ameshukuru shirika hilo kwa msaada huo wa kusaidia Wilaya ya Mkuranga kwa ujenzi wa shule na zahanati.

Kwa upande wake  Meneja Masoko wa Shirika la bima la taifa Elisante Maleko ameeleza kuwa utoaji wa mifuko hiyo ya saruji ni kutokana na mahusiano mazuri baina yao hivyo wakaona faida wanayopata kutoka kwa wananchi hao ambao ni wateja wazuri ni kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa na zahanati katika vijiji mbalimbali vya Mkuranga.

Mkurugenzi wa Shirika hilo tawi la Ubungo Segeja Mabulla amemshukuru mbunge na mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwakutanisha na kutoa elimu ya kuwasaidia wananchi kuhusiana na masuala ya bima pia amewapongeza wakazi wa Wilaya hiyo kwa kuwa wateja wazuri wa bima za halmashauri na bima za maisha.
Share:

Barclays Bank Tanzania promises better and innovated services to its customers

Barclays Bank Tanzania (BBT) Managing Director, Abdi Mohamed, addresses BBT  Business Banking Customers at a function hosted by Barclays to address the bank’s plans and strategies for delivering  highly-innovated products and services that meet customer satisfaction  and also get feedback on services offered and how to improve them. The brief event was held in Dar es Salaam at the weekend.  
Barclays Tanzania Head of Business Banking, Melvin Saprapasen, speaks to some of BBT Business Banking Customers at a function hosted by Barclays to attend to the bank’s plans and strategies for offering highly-innovated products and services that satisfy customer taste and also draw feedback on service delivery quality and how to improve it. The brief occasion was held in Dar es Salaam at the weekend.

Barclays Bank Tanzania (BBT) Managing Director, Abdi Mohamed (right), talks to  some  BBT Business Banking Customers at a function hosted by Barclays to deal with the bank’s plans and strategies for delivery of highly-innovated products and services that meet customer satisfaction  and also as a forum for drawing feedback from customers on services quality received and room for improvement. A brief occasion was held in Dar es Salaam at the weekend.
Barclays Bank Tanzania (BBT) Board Chairman, Simon Mponji (centre), and BBT Managing Director, Abdi Mohamed (left), talks to the bank’s customer, TOL Gases Managing Director  Daniel Warungu, during  a function hosted by Barclays for its Business Banking Customers to share the bank’s plans and strategies for offering highly-innovated products and services  that meet customers satisfaction,  and also as a means for soliciting feedback from customers on services delivery level and suggestions for improvement. The brief event took place in Dar es Salaam over the weekend.
Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left), listens to the bank’s customer,   Tanconsult Executive Chairman Hadji George Ally, during a function hosted by Barclays for its Business Banking Bustomers to address the bank’s plans and strategies for delivering highly-innovated products and services that meet customer satisfaction and also as a forum for get feedback on quality of services offered and how to improve that. The brief occasion was held in Dar Salaam over the weekend.  Looking on is Barclays Tanzania Head of Business Banking, Melvin Saprapasen.
Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left), salutes the Director for African Power Machinery, Hussein Hamadi, during a function hosted by Barclays to its Business Banking Customers in Dar es Salaam over the weekend. Second left is Barclays Assistant Relationship Manager, Jane Kalumuna.
Mar-kim Chemicals Managing Director, Akif Kara (left) shares a light moment with some Barclays Bank officials and other invitees at a function hosted by Barclays to its Business Banking Customers in Dar es Salaam over the weekend.
African Muslim Finance Manager, Mohamed Ezzat (right), chats with some Barclays Bank officials during  a function hosted by Barclays to its Business Banking Customers to address the bank’s  plans and strategies for delivery of highly-innovated products and services  that meet customer satisfaction  and at the same time solicit feedback on services offered and how to improve them. The brief event took place in Dar es Salaam over the weekend.
Share:

Monday, May 14, 2018

HALOTEL YAFANYA KUFURU YAZINDUA SUPER HALO.

3-12

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kifurushi ambacho kimepewa jina la Super Halo, kitakuwa hakina kikomo, ambacho kitakuwa kitafanya wateja wa mtandao huo kunufaika na huduma hiyo.

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua kifurushi kisichokuwa na kikomo cha muda kitakacho wawezesha wateja wa mtandao huo kufanya mawasiliano bila kikomo cha muda wa vifurushi vilivyopewa jina la Super Halo.

Wateja wa mtandao wa Halotel watakao jiunga na kifurushi hicho wataweza kupiga simu au kutumia intaneti hadi pale vifurushi vitakapokwisha na mteja hatokuwa na hofu ya kuisha kwa muda wa kifurushi chake.

6-7

Ofisa Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo

Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, uzinduzi huo wa vifurushi vya Super Halo ni mapinduzi mengine makubwa katika sekta ya mawasiliano kwa kuondoa ukomo wa muda katika vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti.


“Hii ni hatua nyingine kubwa ya ubunifu wa hali ya juu katika utoaji wa huduma zetu ili kuwawezesha wateja  wetu wote walioko  nchi nzima kunufaika na huduma za mawasiliano bila ya kuwa na wasiwasi wa kuisha kwa muda wa matumizi ya mawasiliano hayo pamoja na kukidhi mahitaji yao katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi kupitia kifurushi hiki” Alisema Semwenda na Kuongeza.
2-9

“Kifurushi hiki kinawapa fursa kubwa watanzania wote ambao ni wateja wa Halotel walioko nchi nzima kuweza kujiunga na kufurahia dakika nyingi za muda wa maongezi za kuweza kupiga Halotel kwenda Halotel na Halotel kwenda mitandao mingine pamoja na MB za intaneti za kutosha ambavyo vifurushi vyote hivi wateja watavitumia  bila kikomo, cha muda wa maongezi Aliongeza Semwenda.

“Mteja wa Halotel anaweza kujiunga kwa kuanzia shilingi 500 na kupata dakika 17 za  kupiga Halotel bila kikomo cha muda na kwa shilingi 500 hiyo hiyo mteja anaweza kujiunga na kupata MB 110 za intaneti za kutumia bila kikomo. Lengo kubwa katika kifurushi hiki ni kumwezesha mteja kuona thamani ya pesa yake na kuweza kufurahia mawasiliano ya kupiga simu na kutumia MB za intaneti bila kikomo cha muda,” alisisitiza Semwenda.

5-8

Baadhi ya wateja wa Mtandao wa simu wa  Halotel wakifuatilia huduma mbalimbali zinazotolewa na mtandao huo.

Mbali na Kifurushi hicho cha SUPER HALO, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo alipata fursa ya kuzindua huduma nyingine mpya  ya Facebook Bure, ambapo kuanzia sasa wateja wote wa Halotel nchi nzima wataweza kuperuzi mtandao wa Facebook bure.

“Tutaendelea kuhakikisha wateja wetu walioko mijini na vijijini wanapata huduma bora inavyoendana na uhalisia wa maisha yao, na kuhakikisha hili linaendana na uhalisia, pamoja na kifurushi cha SUPER HALO, leo tunazindua huduma nyingine mpya ya Facebook Bure itakayowawezesha wateja wetu nchi nzima kuweza kulike, kukomenti, kuchat na rafiki na ndugu zao kokote walipo nchini pamoja kuperuzi  taarifa mbalimbali kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook bila gharama yoyote,” Aliongeza Semwenda.
Share:

Friday, May 11, 2018

WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA WANUFAIKA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko (wapili kushoto) akizungumza na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na wakazi wa mtaa huo jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Vijana wajasiriamali waosha magari wa Kikundi cha  Msingi Mikwanja Car Wash yenye thamani ya shilingi milioni 1 iliyotoka katika fedha ya mfuko wa jimbo la Ukonga.Ni mwendelezo wa kutimiza ahadi ambazo Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara aliziahidi kwa wakazi wa jimbo hilo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),John Mrema.
Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto) akizungumza jambo na wakazi wa Mtaa wa Guruka Kwalala uliopo katika kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili katika mtaa huo leo kwa ajili ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa vijana wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash ikiwa ni mwendelezo wa kutimiza ahadi za Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko,Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto,Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo.
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto),Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala,   Dorcas Rukiko, Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo wakikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash, Ally Mfaume (Wapili kulia) na Katibu Wake,Yasini Omary jijini Dar es Salaam leo.Uongozi wa Kata na mtaa pamoja Viongozi kutoka Chadema wamekabidhi mashine mbili za kuosha magari kwa Vikundi  vya Vijana wajasiamali waosha magari wa Mtaa wa Guruka Kwalala.
Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko (kushoto) akizungumza jijini Dar es Slaam leo na Vijana wa Kikundi kingine cha Vijana wajasiriamali kitwaacho Nyamachoma kinachofanya kazi ya kuosha magari maeneo ya Gongo la  mboto Mwisho wa lami katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya shilingi Milioni 1 iliyotoka katika fedha ya Mfuko wa jimbo la Ukonga ikiwa  ni Mwendelezo wa kutimiza ahadi alizoahidi Mbunge wa Jimbo hilo,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Nyamachoma Car Wash,Juma Sungamizi,Katibu wa kikundi,Jimmy Vitalis na Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema.
    Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi(watatu kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.
Mashine ya Kuosha magari iliyokabidhiwa leo kwa Kikundi cha Nyamachoma Car wash kilichopo Gongo la Mboto mwisho wa lami jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akizungumza jijini Dar es Salaam leo na Vijana wajasiriamali wa Kikundi cha Kuosha magari kiitwacho Nyamachoma Car Wash katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa kikundi hicho yenye thamani ya shilingi Milioni 1 kutoka katika Mfuko wa Jimbo la Ukonga.
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Katibu wa Kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha magari kiiitwacho Nyamachoma Car Wash,Jimmy Vitalis (wapili kulia) na Mwenyekiti wa kikundi hicho,Juma Sungamizi jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akipeana mikono ya pongezi na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo baada ya kukabidhi mashine mbili za kuosha magari na pikipiki kwa Vikundi viwili vya waosha magari Nyamachoma Car Wash na Msingi Mkwanja Car Wash vilivyopo katika Mtaa wa Gruruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive