A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Wednesday, February 19, 2025

YAS NA SAMSUNG WAZINDUA SAMSUNG S25 YENYE UWEZO WA KUTUMIA AKILI MNEMBA

Dar es Salaam 18 Februari 2025: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Yas, pamoja na Samsung Tanzania zimezindua simu mpya aina ya S25 ambayo imekuja na teknolojia ya akili mnembayaani Artificial intelligence (AI).

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha simu za mkononi wa Samsung, Mgope Kiwanga amesema wao kama Samsung wanayofuraha kutambulisha bidhaa hiyo hapa nchini ambapo kupitia simu hiyo Watanzania wataweza kuona mabadiliko makubwa kupitia simu hizo.

Aidha Mgope amesema mbali na toleo hilo la S25 pia kuna matoleo mengine mawaIi ambayo ni Samsung ultra na base ambapo kila moja litakuwa na waranti ya mwaka mmoja, ambapo kupitia ushirikiano huo na Yas mteja atapata mambo mazuri ikiwemo kupata GB96 kutoka Yas Tanzania, amesema Mgope.

Kwa upande wake Meneja Huduma za Ziada ya Yas, Bi.Ikunda Ngowi amesema wao kama Yas wanayofuraha kushirikiana na Samsung kupitia bidhaa zao ambapo wao kwa kunogesha uzinduzi huo wameamua kutoa GB 96 kwa mwaka

Share:

Tuesday, February 18, 2025

Benki ya Absa ya endelea kusambaza upendo wa Siku ya Wapendanao kwa wajasiriamali

Meneja wa Masuala Endelevu na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi, akichagua maua, wakati baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakitembelea eneo maarufu la biashara ya maua, Mbuyuni, Namanga jijini Dar es Salaam jana, Ili kuendelea kusambaza upendo wa Siku ya Wapendanao kwa wajasiriamali hao, na pia kuwaelezea huduma mbalimbali za kibenki zitolewazo na Absa.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIKA kile kilichoelezwa kuwa ni kujali stori za maisha ya wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na uchuuzi wa maua, Benki ya Absa Tanzania imewatembelea wafanyabiashara hao, kuzungumza nao na kuwapa motisha mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wapendanao iliyoadhimishwa duniani kote hivi karibuni.

Akizungumza katika hafla hiyo katika eneo maarufu kwa biashara hiyo la Mbuyuni, Namanga jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Masuala Endelevu na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi, alisema Absa imeamua kuwatembelea wajasiriamali hao kama njia ya kusambaza upendo, kwa kuwa ni kati ya makundi yanayosahaulika, wakati wanahusika kwenye kusambaza upendo kwa kuuza maua.

“Kama mnavyofahamu ahadi mpya ya chapa yetu isemayo ‘stori yako ina thamani’, ndiyo maana Absa tukaamua kuendelea kusambaza upendo wa Siku hii ya Wapendao kwa kipekee kabisa kwa kuwatembelea hawa wafanyabiashara wadogowadogo hapa Mbuyuni kuonesha kuwa stori za wafanyabiashara hawa wa maua zina thamani sana na zina umuhimu kwetu."

“Hawa wafanyabiashara ndio watu muhimu sana katika kusambaza upendo, lakini mara nyingi husahaulika, hutumia siku yao nzima katika kuuza maua na kusambaza upendo kwa wengine, lakini wao wenyewe wanasahaulika, kwa hiyo Absa imeamua kuwatembelea ili wasijisikie wapweke bali wajisikie kuguswa na upendo”, alisema Bi. Abigail.

Mmoja wa wafanyabiashara hao wa maua, Robert Mwita Nyamkama, huku akiishukuru benki hiyo kwa kuwatembelea, alisema biashara ya mwaka huu imeshamiri ikilinganishwa na mwaka jana, hali inayotokana na watu wengi zaidi kuwa na mwamko wa kupeleka zawadi ya maua kwa wapendwa wao.

“Tunaishukuru Absa kwa kutukumbuka na kuja kututembelea tukiwa kwenye biashara zetu, hii imetuthibitishia kuwa benki hiyo inatuthamini, na ni ishara thabiti kuwa kauli ya benki hiyo ya stori yako ina thamani kwetu ni ya ukweli kabisa,” alisema.

Siku ya Wapendanao, ambayo hujulikana sana kama Valentine, huadhimishwa tarehe 14 Februari kila mwaka, ambapo hutiwa nakshi na utamaduni maarufu wa wapendanao kupelekeana zawadi za vitu mbalimbali vikiwemo kadi na maua yenye rangi mekundu.
Mchuuzi wa maua, Bw. Robert Byamukama akikabidhi Kwa mmoja wateja, Vivian mwamanda, wakati baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakitembelea eneo maarufu la biashara ya maua, Mbuyuni, Namanga jijini Dar es Salaam jana, Ili kuendelea kusambaza upendo wa Siku ya Wapendanao kwa wajasiriamali hao, na pia kuwaelezea huduma mbalimbali za kibenki zitolewazo na Absa.
Mmoja wa wateja wa maua, Daniel Mgedule (kulia), akipokea ua kutoka Kwa mmoja wa wachuuzi wa maua katika eneo maarufu la biashara ya maua, Mbuyuni, Namanga, Dar es Salaam jana, wakati baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakitembelea eneo hilo, kuendelea kusambaza upendo wa Siku ya Wapendanao kwa wajasiriamali hao, na pia kuwaelezea huduma mbalimbali za kibenki zitolewazo na Absa.
Share:

Saturday, February 15, 2025

TCB YAPELEKA TABASAMU KWA WASHINDI WA KAMPENI YA MAHABA KISIWANI








Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB)imewazawadia washindi wawili safari ya kwenda Zanzibar na malazi waliofanya miamala mingi katika msimu wa wapendanao kupitia kampeni iliyoendeshwa na benki hiyo ijulikanayo kwa jina la Mahaba Kisiwani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Adam Mihayo, Mkurugenzi wa Biashara za Wateja Wadogo na Kati, Lilian Mtali amesema TCB imefanikiwa kukuza uelewa na matumizi ya bidhaa zake za kidijitali kwa kuwazawadia wateja hao waliofanya miamala mingi katika msimu wa wapendanao.

Amesema kampeni ya Mahaba Kisiwani inadhihirisha malengo ya kimkakati ya TCB kutumia teknolojia kukuza matumizi ya njia za kidijitali katika kufanya malipo.

Mtali amesema mbali na kuwakabidhi zawadi hizo washindi hao pia TCB inaadhimisha hatua muhimu ya miaka 100 ya huduma na ubora wa benki tangu kuanzishwa kwake.

Amewapongeza wafanyakazi wa benki hiyo kwa juhudi na mchango wao katika mafanikio ya benki hiyo. “Mafanikio ya benki yetu katika kipindi cha miaka 100 iliyopita ni matokeo ya juhudi na bidii za kila mmoja wetu.

“Tunadhamiria kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ambayo kila mmoja anathaminiwa, anaungwa mkono na kuwezeshwa tunapoendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu,”amesema

Amesema TCB inaendelea kuahidi kuwekeza katika uvumbuzi wa kidijitali na kuongeza ubora kwa wafanyakazi wake ili kuhakikisha mustakabali wenye mafanikio kwa wateja pamoja na wafanyakazi wake

'HomeHabariTCB yawazawadia washindi wa kampeni ‘Mahaba Kisiwani.'
Share:

Thursday, February 13, 2025

AKIBA COMMERCIAL BANK AWARDS WINNERS "TWENDE KIDIJITALI" CAMPAIGN


Six customers from various branches of Akiba Commercial Bank Plc have been awarded cash prizes and other rewards after emerging as winners in the "Twende Kidijitali – Tukuvushe Januari" campaign. The winners were recognized for their high usage of the bank’s digital services, including ACB Mobile, Internet Banking, and VISA card.


Speaking during the prize-giving ceremony, Akiba Commercial Bank’s Chief Commercial Officer, Ms. Wezi Olivia Mwazani, congratulated the winners and thanked them for their participation. She emphasized that the campaign was designed to encourage customers to embrace digital banking solutions, which enhance financial accessibility and improved transaction security.


"We congratulate our winners for being part of our digital transformation journey. Through services such as ACB Mobile, Internet Banking, and VISA card, our customers have been able to conduct transactions quickly, securely, and conveniently. We encourage more customers to continue using these services for their benefit," said Ms. Wezi.

Some of the campaign winners expressed their excitement and appreciation, stating that they were delighted to be recognized and rewarded for using digital banking services. They also affirmed their commitment to continuing to use these services due to their ease and convenience.

The Twende Kidijitali – Tukuvushe Januari campaign is part of Akiba Commercial Bank’s strategy to promote digital banking adoption, offering customers modern and efficient financial solutions.
Share:

Absa Bank Tanzania Unveils the Absa Group Savings Account – A Unique Solution for Collective Savings

Absa Bank Tanzania Director of Retail Banking, Ms. Ndabu Swere (centre), addresses a media conference, during the official launch of the bank's group saving account in Dar es Salaam today. Looking on are, Absa's Citizenship Manager, Ms. Abigail Lukuvi (left), and the bank's Head of Retail Products and Strategy, Mr Heristraton Genesis.

Dar es Salaam, 13 February 2025 – Absa Bank Tanzania has officially launched the Absa Group Savings Account, a versatile financial solution designed to help groups achieve their shared goals while enjoying both transactional and savings benefits. Whether for vacations, social events, emergencies, or long-term investments, this account provides an easy, profitable, and secure way for savings groups to manage their funds.

Speaking at the launch event, Ms. Ndabu Swere, Director of Retail Banking at Absa Bank Tanzania, emphasized the significance of the new product. "At Absa Bank Tanzania, we recognize that financial goals are not always individual – sometimes, they are shared. Whether it’s a family, an alumni association, a neighborhood group, or an investment club, we understand the importance of collective financial management. That is why we have introduced the Absa Group Savings Account – to ensure that groups can access financial services easily, securely, and with great benefits."

The Absa Group Savings Account allows both registered and unregistered groups of at least three members to save together while earning competitive interest rates and benefiting from seamless digital banking access. Account holders will enjoy:
  • A cheque book for easy transactions.
  • Free unlimited cash deposits at Absa branches, ATMs, or through Absa Wakala.
  • Competitive interest rates calculated daily and paid quarterly.
  • Zero monthly maintenance fees for groups maintaining an average balance of TZS 1 million and above.
  • Free mobile and internet banking access for seamless financial management.
  • Enhanced trust and transparency in group financial management.
On his part, Mr. Aron Luhanga, Head of Marketing and Corporate Affairs at Absa Bank Tanzania, spoke about the bank’s broader mission and brand commitment. "At Absa, we are driven by our purpose: “Empowering Africa tomorrow, together, one story at a time.” This new product is a reflection of that purpose, ensuring that Tanzanians can work together toward their financial aspirations. Our brand promise, “Your story matters,” or in Swahili, “Stori yako ina thamani,” is not just a slogan – it is our commitment to supporting our customers at every step of their journey."

With the launch of the Absa Group Savings Account, Absa Bank Tanzania continues to reinforce its commitment to providing innovative and customer-centric financial solutions. The bank invites families, investment clubs, and community groups to open an Absa Group Savings Account and begin their journey towards shared success.
Head of Retail Products and Strategy at Absa Bank Tanzania, Mr. Heristraton Genesis (right), addresses a media conference, during the official launch of the bank's group saving account in Dar es Salaam today. Looking on are, Absa's Citizenship Manager, Ms. Abigail Lukuvi (left) and the bank's Head of Retail Banking, Ms. ndabu Lilian Swere.
Some members of the media at work, during the official launch of the bank's group saving account in Dar es Salaam today. The media was addressed by the bank's Director of Retail Banking, Ms. Ndabu Lilian Swere.
Share:

Tuesday, February 4, 2025

Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar

Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar over the weekend. Centre is the company’s CEO Gina Washington and Miguel Pilgram, CEO of Pilgram Group, a property development company based in the Isles.

By GUARDIAN Reporter

ZANZIBAR Ministry of Labour, Economy, and Investment has said that it will continue to expedite the issuance of investment permits without bureaucracy so that investors can start doing business with ease for the economic development of the Isles.


Speaking during the launch of international real estate investment company Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar Real Estate which has a presence in more than 20 countries in the world, Minister Shariff  Ali Shariff said that investment in the property market has huge potential to foster Zanzibar’s economic growth.


The company’s Chief Executive Officer (CEO), Gina Washington, echoed a similar opinion, adding that the market has the potential to provide more employment opportunities for young people.


According to the Zanzibar Investment Promotion Authority (ZIPA), 30 percent of the authority’s registered projects are in real estate, making it a promising area for further investments.


He said that the official launch of the company is a milestone that signifies not only the growth of a world-class real estate brand in our region but also the vast opportunities Zanzibar offers in the investment and property market. 


“Zanzibar is experiencing a transformative era, driven by strategic economic reforms, increased investor confidence, and a forward-thinking government agenda.

 This event is a testament to our collective commitment to fostering a business-friendly environment that attracts global players while ensuring sustainable development that benefits both local and international stakeholders,” he said.


He added that the investment landscape has never been more promising with the government positioning investment as a key pillar for economic diversification and long-term prosperity. 


“The rapid development of infrastructures, streamlined regulatory frameworks, and enhanced ease of doing business has made Zanzibar an attractive destination for investors across various sectors, including real estate,” he noted.


With tourism, and blue economy initiatives driving growth, the real estate sector remains a critical enabler of the vision to provide high-quality residential, commercial, and mixed-use developments that cater to our growing economy and international market demand, he said.


“In the last four years under the 8th Phase of the Revolutionary Government of Zanzibar, Zanzibar Investment Promotion Authority (ZIPA) has registered more than 430 investment projects account for a staggering 5.9 billion US dollars’ worth of capital and are expected to create more than 22,000 direct jobs to the locals. 


With tourism projects leading the charts which accounts for more than 38 percent of all registered projects followed by real estate sector which accounts for more than 22 percent of all registered project. About 78 percent of real estate registered projects was registered in the last four years, this shows the readiness and willingness of our government in supporting the real estate business in Zanzibar.


For her part, Washington said that for over 119 years, Coldwell Banker has been a global leader in real estate, known for trust, integrity, and innovation. 


“Today, as we establish Coldwell Banker in this region, our mission is clear—we are here to bring a new level of professionalism and transparency to the market, helping investors, developers, and agents to thrive,” she said.


Naimah Kunambi, Associate Broker and Sales Manager | Coldwell Banker Islemark Realty said that the launch is more than just the opening of a real estate brokerage but the beginning of a new standard in real estate, one built on excellence, professionalism, and a commitment to serving our clients, agents, and community at the highest level.


“I want to take a moment to acknowledge and sincerely thank everyone who has played a role in making today possible—our dedicated team, our partners, our clients, and all of you here today. Your support and belief in our vision mean everything,” she said
Share:

Friday, January 24, 2025

FEZA BOYS YANG'ARA UFAULU WA KIDATO CHANNE WAPATA ALAMA A,,

SHULE Sekondari Feza Boys imejivunia uwekezaji iliyofanya katika kumuandaa mwanafunzi kuwa bora baada ya kufaulisha wanafunzi wote kwa kupata daraja la kwanza katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne ulifanyika mwaka 2024, huku zaidi ya asilimia 65 wakipata division 1.7.

Hayo ameyasema Makamu Mkuu wa Shule ya FEZA Boys, Shabani Mbonde wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23,2025 katika shule hiyo iliyopo Kunduchi Dar es Salaam mara baada ya Baraza la Mitihani kutangaza matokeo ya kidato cha nne.

Mbone ameleeza kuwa matokeo hayo hajatokea tu kirahisi bali ni uwekezaji na mazingira ya shule yanayomtengeza mwanafunzi kuwa bora na walimu wa kutosha ambapo kila mwalimu ana wastani ya kufundisha wanafunzi 10.

" FEZA SHOOLS haitoi mwanafunzi bora katika A tu, bali katika nyanja zote.Sisi katika elimu hatumjengi mwanafunzi kupata A tu lakini pia katika kukabiliana na hali zote katika maisha kulingana na wakati uliopo.

"Hii yote inatokana na jitihada mbalimbali za wanafunzi wenyewe na walimu. Mwanafunzi wetu anakuwa ni kama ametoka kwenye mashine au kiwanda kilichomjenga katika kupambana na changamoto mbalimbali katika mtihani na maisha.Tunajivunia wanafunzi wetu na walimu wetu," amesema Makamu Mkuu huyo.

Aidha Mbonde amesema kama sekta binafsi wanashukuru serikali kwa kusisitiza suala la elimu na wanaiunga mkono Serikali katika kuhakikisha elimu inakuwa bora.

Naye Mkuu wa taaluma msaidizi wa kidato cha tatu na nne, Abdallah Juma ameeleza mbinu wanazotumia kuwafundisha wanafunzi hao kuwa ni progamu mbalimbali walizonazo shuleni hapo.

" Sio kwamba sisi vijana wote tunaowachukua ni wale 'cream' tu bali wanakuja hata wenye uwezo mdogo tunawatengeneza na wanakiwa sawa na wenzao na wanafaulu kwa pamoja.

" Matokeo haya yamepatikana kwa njia tofauti, pande zote tatu zina mchango yaani wazazi, walimu na wanafunzi, pia tuna programu mbalimbali za masomo kuanzia asubuhi, jioni na hata usiku, pia wanapata muda wa kucheza", amesema.

Kwa upande mmoja wa wanafunzi wa FEZA BOYS waliofanya vizuri kwa kupata division one 1.7, Moses Francis, amesema anamshukuru Mungu kwani mafanikio hayo hayakuja kirahisi ya kupata A masomo yote 10 ila mazingira ya shule yamechangia ikiwamo kusoma kwa bidii kama mwanafunzi.

Amefafanua kuwa kutokana na ratiba za shule zilivyopangiliwa wanapata muda wa kutosha wa kupumzika lakini kuna kipindi kigumu unatakiwa kusoma sana ili kufaulu mtihani.

"Hii haipatikani kirahisi, mtu kufaulu lazima kuwe na motisha kuanzia kwa mwanafunzi wenyewe na mzingira mazuri ya kujifunzia pamoja na kumtanguliza Mungu.Kila wiki tunafanya mazoezi ya masomo kwa kufanya test," amesema Moses.

Katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ufaulu umeongezeka ambapo jumla ya watahiniwa wa shule 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo sawa na asilimia 92.32 wamefaulu kwa kupata madaraja ya I,II,III,IV.

Makamu mkuu wa shule ya sekondari ya Feza Boys ,Shabani Mbonde akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa matokeo ya kidato cha nne na shule hiyo kupata ufaulu wa alama A kwa wanafunzi waoote kwenye atokeo ya kidato cha nne.Kulia ni mmoja ya mwanafunzi aliyepata ufaulu wa A. Mosses Mwaijande na Kushoto ni Mtaalumu Abdalla Juma
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza Boys wakishangilia kwa kumbeba mwanafunzi mwenzao,Allan Masaka aliyefanya viziuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa kupata ufaulu wa alama A.7 jumla ya wanafuzi woote katika shule hiyo wamepata ufaulu wa alama A .Na,mpiga picha maalumu
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza Boys wakishangilia kwa kumbeba mwanafunzi mwenzao,Moses Mwaijande aliyefanya viziuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa kupata ufaulu wa alama A.7 jumla ya wanafuzi woote katika shule hiyo wamepata ufaulu wa alama A
Share:

Wednesday, January 22, 2025

Absa Bank Tanzania concludes Spend & Win campaign with great success, third Subaru Forester winner applauds service excellence

The final winner of Absa Bank Tanzania's three-month Spend & Win campaign, Ms. Amalia Lui Shio (center), receives the ignition key to a brand-new 2024 Subaru Forester from the bank’s Head of Retail Banking, Ms. Ndabu Lilian Swere, during a ceremony held in Dar es Salaam yesterday. The campaign aimed to encourage more Tanzanians to adopt digital banking solutions, such as debit and credit cards, which offer safety, convenience, and access to a wide range of banking services. Also present were senior officials from Absa Bank.
The final winner of Absa Bank Tanzania’s three-month Spend & Win campaign, Ms. Amalia Lui Shio, is seen in a jovial mood shortly after receiving her brand-new 2024 Subaru Forester from the bank’s Head of Retail Banking, Ms. Ndabu Lilian Swere, during a ceremony held in Dar es Salaam today. The campaign aimed to encourage more Tanzanians to adopt digital banking solutions, such as debit and credit cards, which offer safety, convenience, and access to a wide range of banking services.
Some members of Absa Bank Tanzania’s staff celebrates with Ms. Amalia Lui Shio, the third winner of the bank’s three-month Spend & Win campaign, shortly after she received her brand-new 2024 Subaru Forester during a ceremony held in Dar es Salaam today. The campaign aimed to encourage more Tanzanians to adopt digital banking solutions, such as debit and credit cards, which offer safety, convenience, and access to a wide range of banking services.
Ms. Amalia Lui Shio, the third winner of the Absa Bank Tanzania Spend & Win three-month campaign, drives off in her brand-new 2024 Subaru Forester shortly after receiving it at a function held in Dar es Salaam today.
The final winner of Absa Bank Tanzania's three-month Spend & Win campaign, Ms. Amalia Lui Shio (center), dances alongside traditional ngoma artists during the handover ceremony of a brand-new 2024 Subaru Forester. The vehicle was presented to her by the bank’s Head of Retail Banking, Ms. Ndabu Lilian Swere, in Dar es Salaam yesterday. The campaign aimed to encourage more Tanzanians to adopt digital banking solutions, such as debit and credit cards, which offer safety, convenience, and access to a wide range of banking services.
Share:

Sunday, January 19, 2025

Benki ya Akiba yakabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni ya 'Twende Kidigitali'


Benki ya Akiba imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni 'Twende Kidigitali' na kuwahimiza kuendelea kutumia huduma zake za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet Banking, ACB VISA Card na ACB Wakala ili kufurahia uzoefu wa kipekee wa huduma za kibenki.


Shukrani hizo zimetolewa jijini Dar es salaam Januari 2025 na Mkuu wa Kitendo cha Biashara wa benki hiyo, Dkt. Danford Muyango wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya hiyo ambapo wateja kadhaa kutoka Dar es Salaam na mikoani wamekabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha zilizowekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao kupitia Benki ya Akiba.


"Kampeni ya 'Twende Kidijitali' ilizinduliwa mwezi Desemba 2024 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kibenki kwa wateja wakati wa msimu wa sikukuu na pia kuwasaidia wateja kushinda changamoto za kifedha mwezi huu wa Januari kupitia zawadi mbalimbali" amesema Danford.
Wateja walionyesha furaha na shukrani kwa Benki ya Akiba kwa jitihada zake za kuimarisha huduma za kidijitali ambazo zimeboresha uzoefu wao wa kibenki kwa kuwapatia urahisi na wepesi wa kupata huduma za kifedha wakiwa mahali popote na wakati wowote.


Mmoja wa wateja wa waliokabidhiwa zawadi na Benki ya Akiba ni Alfayo Zephania ambaye alieleza jinsi alivyopokea furaha habari njema za kuibuka mshindi wa kampeni hiyo.


"Nilifurahishwa sana na tarifa ya ushindi wangu na ninaishukuru Benki ya Akiba kwa kujali wateja wake na kutoa huduma bora. Natoa rai kwa wateja wengine kujiunga na Benki ya Akiba ili kunufaika na huduma bora ikiwemo mikopo ambayo imenivusha pakubwa katika biashara zangu” alisema Zephania.


Mteja mwingine, Ezekiel Willium alielezea furaha yake kwa zawadi aliyoshinda, akisema ushindi huo umempa hamasa zaidi ya kushiriki kwa bidii ili kupata zawadi kubwa zaidi katika droo kuu ya mwisho wa kampeni hiyo ya 'Twende Kidigitali'.


Pia Benki ya Akiba imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni hiyo na kuwasihi waendelee kutumia huduma za kidijitali za benki hiyo ili kunufaika zaidi.


Meneja Mwandamizi Benki ya Akiba, Magreth Mwasumbi (kulia) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo walioibuka washindi wa kampeni ya 'Twende Kidigitali'.
Share:

Wednesday, December 18, 2024

Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu ya Kampeni ya "Spend and Win" na hafla ya kukabidhi Subaru Forester kwa mshindi wa pili, Bi. Alyshah Bharwani (wa tatu kushoto), katika hafla jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Masoko wa Absa, Beda Buswalo. Mteja wa benki hiyo, Bi. Amalia Lui Shio, alitangazwa mshindi wa tatu.
Mshindi wa pili wa Kampeni ya "Spend and Win" ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. Alyshah Bharwani (wa tatu kushoto), akionesha funguo za Subaru Forester mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), katika hafla jijini Dar es Salaam leo. Tukio hilo pia lilihusisha droo ya tatu ya kampeni, ambapo mteja wa benki hiyo, Bi. Amalia Lui Shio, alitangazwa mshindi. Kulia ni Bw. Jamil Kanji, mmoja wa wanafamilia wa Alyshah.

Benki ya Absa Tanzania imehitimisha rasmi Kampeni yake ya "Spend & Win" kwa mafanikio makubwa, kupitia droo ya tatu na ya mwisho iliyofanyika leo, ambayo imeashiria mwisho wa miezi mitatu ya msisimko, ubunifu, na zawadi kwa wateja.

Hafla hiyo ilipambwa na kutangazwa kwa mshindi wa tatu na wa mwisho, Bi. Amalia Lui Shio, ambaye atapokea zawadi yake—Subaru Forester ya mwaka 2014, Januari 2025.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ndabu Swere, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja Binafsi katika Benki ya Absa Tanzania, alimtangaza mshindi na kuwapongeza washindi wote watatu waliotangazwa katika kampeni hiyo.

'“Tunayo furaha kumtangaza Bi. Amalia Lui Shio kama mshindi wa droo ya tatu na ya mwisho ya Kampeni ya ‘Spend & Win’,” alisema Bi. Swere. “Stori yako ni muhimu, na kupitia kampeni hii, tumepata fursa ya kuwawezesha wateja wetu kubadilisha maisha yao. Bi. Amalia Lui Shio atapokea rasmi gari lake mwezi ujao, na tunasubiri kwa shauku kusherehekea tukio hili la kusisimua pamoja naye.”

Wakati wa hafla hiyo, Bi. Ndabu pia alikabidhi funguo za Subaru Forester ya mwaka 2014 kwa mshindi wa pili, Bi. Alyshah Aminmohamed Bharwani, ambaye alitoa shukrani za dhati kwa Benki ya Absa kwa zawadi hiyo ya kubadilisha maisha.

“Ninawashukuru sana Benki ya Absa kwa kampeni hii. Kushinda gari hili ni jambo kubwa sana kwangu na familia yangu, na nimefurahi sana kuwa sehemu ya safari hii,” alisema Bi. Bharwani.

Kampeni ya "Spend & Win" ambayo ilizinduliwa tarehe 10 Septemba 2024, iliwapa wateja wa Benki ya Absa Tanzania fursa ya kushinda moja kati ya magari matatu ya Subaru Forester kwa kufanya miamala kwa kutumia kadi zao za Absa au majukwaa ya kidijitali. Wateja walikidhi vigezo vya kuingia kwenye droo kwa kufanya angalau miamala 20 ya kadi yenye jumla ya TZS milioni 5 au zaidi kwa mwezi, huku miamala ya kidijitali ikiongeza nafasi zao za kushinda.

Akiongelea mafanikio ya kampeni hiyo, Bi. Ndabu aliwashukuru wateja wote waliopata nafasi ya kushiriki na kusisitiza dhamira ya benki hiyo ya kutoa suluhisho za kibunifu na uzoefu mzuri kwa wateja wake.

“Kwa niaba ya Benki ya Absa Tanzania, napenda kuwashukuru wateja wetu wote walioshiriki kampeni hii na kuwapongeza washindi wetu watatu: Bw. Rashid Nassoro Said, Bi. Alyshah Aminmohamed Bharwani, na Bi. Amalia Lui Shio,” alisema Bi. Ndabu. “Katika Absa, tumejizatiti kuwawezesha wateja wetu na jamii, na kampeni kama hii ni mojawapo ya njia tunazotumia kuonyesha shukrani zetu huku tukitimiza dhamira yetu ya ‘Kuiwezesha Kesho Afrika ya kesho, Pamoja, Hatua moja baada ya nyingine."

“Tunapohitimisha kampeni hii, nataka kuwahakikishia wateja wetu kuwa huu sio mwisho. Absa itaendelea kuanzisha kampeni na fursa za kusisimua za kuwazawadia na kuwaunga mkono wateja wetu wanapofanikisha malengo yao.”

Hitimisho la Kampeni ya "Spend & Win" linaimarisha nafasi ya Benki ya Absa Tanzania kama benki ya kidijitali inayoongoza na mshirika wa kuaminika katika safari za kifedha za wateja wake.
Share:

Saturday, December 14, 2024

Benki ya Absa Tanzania Yashinda Tuzo 11 za Heshima Mwaka 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akizungumza na waandishi wakati akitangaza mafanikio ya benki kwa Mwaka 2024 kupitia Tuzo mbalimbali 11 ilizopata. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.

• Kutambuliwa kwake kunadhihirisha, Ufanisi katika Ubunifu wa Kifedha, Uongozi na kujali Wateja.

Benki ya Absa Tanzania inajivunia kutangaza mafanikio yake makubwa ya kushinda tuzo 11 za heshima mwaka 2024. Tuzo hizi zinatambua mchango mkubwa wa benki katika uwezeshaji wa kifedha, uvumbuzi, utawala bora, na huduma kwa wateja.

Tuzo muhimu ambazo benki imeshinda mwaka huu ni pamoja na:

• Chapa ya Benki Inayokua Haraka Zaidi 2024, iliyotolewa na World Brand Magazine.

• Benki ya Wateja rejareja na Wateja Wadogo na wa Kati inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 zilizotolewa na World Economic Magazine Awards.

• Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha Tanzania, iliyotolewa na Tanzania Women Industrial Awards.

• MD/CEO Bora wa Mwaka, iliyotolewa na Top 100 Executive List Awards.

• Hatifungani Bora ya Mwaka, iliyotolewa na Soko la Hisa la Dar es Salaam.

• Muwasilishaji Bora wa Ripoti ya Taarifa za Fedha 2023, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)

• Mwajiri Bora anayeinukia na Mwajiri Bora katika Usimamizi na Maendeleo ya Vipaji, zilizotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

• Benki inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu za Mikopo Tanzania, iliyotolewa na Consumer Choice Awards Afrika 2024.

• Benki inayopendwa zaidi na kufikika zaidi Kusini mwa Afrika, iliyotolewa na Consumer Choice Awards Afrika 2024.

Utendaji bora wa Benki ya Absa Tanzania mwaka 2024 umeoneshwa kupitia matokeo yake mazuri ya kifedha kwa nusu ya kwanza ya mwaka. Mapato ya jumla yaliongezeka kwa 25% kufikia TZS bilioni 105, huku faida kabla ya kodi ikipanda kwa 65% kufikia TZS bilioni 54. Amana za wateja ziliongezeka kwa 21%, zikionesha uimara wa benki hiyo na uwezo wake wa kutoa ukuaji endelevu.

Tuzo ya Chapa ya Benki Inayokua haraka zaidi inaadhimisha maendeleo makubwa ya Benki ya Absa Tanzania tangu ilipoanzishwa mwaka 2020. Ndani ya miaka minne tu, Absa imepata kiwango sawa cha imani na kutambuliwa kama benki za ndani na kimataifa zenye karibu karne moja ya historia nchini Tanzania. Tuzo hii inaonyesha ahadi ya chapa ya Absa: 'Stori yako ina Thamani', inadhihirisha kujitolea kwa benki hiyo katika kuthamini Stori za kipekee za wateja wake, kuunda suluhisho za kibunifu, na kuiwezesha jamii.

Tuzo ya Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha inaonyesha dhamira ya Absa katika kukuza ujumuishi wa kifedha. Kupitia bidhaa kama Akaunti ya Absa She Business, benki hiyo imewawezesha wanawake wajasiriamali kupata huduma za kibenki bila gharama, msaada wa ushauri, na programu za kujenga uwezo.

Katika sekta ya SME, suluhisho maalum za Absa na ushirikiano wa kimkakati zimesaidia benki kushinda tuzo ya Benki inayotoa huduma Kwa wateja wadogo na wa Kati (SME) inayokua haraka zaidi Tanzania 2024.

Tuzo ya Benki ya Wateja Rejareja inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 inaonyesha msisitizo wa benki hiyo katika mabadiliko ya kidijitali na urahisi wa wateja, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa huduma za uwakala na suluhisho za kibunifu kama jukwaa la malipo la Mobi Tap.

Kutambuliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji kama MD/CEO wa Mwaka na tuzo ya Ripoti Bora za Kifedha 2023 kunathibitisha kujitolea kwa Absa kwa utawala bora, uwazi, na uongozi wa mfano wa kuigwa.

Tuzo kutoka Consumer Choice Awards, kama Benki Inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu wa Mikopo Tanzania, zinaonyesha dhamira ya Absa ya kuwapa wateja nafasi ya kwanza katika shughuli zake.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alisema: "Tuzo hizi ni ushahidi wa nguvu ya ushirikiano wetu na wateja na wadau wetu. Tunaheshimika kutambuliwa katika nyanja nyingi, na tutaendelea kujitolea kuimarisha Afrika ya Kesho kupitia suluhisho za kibenki zenye ubunifu, ujumuishi, na athari chanya.”

Benki ya Absa Tanzania inapoendelea na safari yake ya ukuaji na mabadiliko, inabaki imara katika dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwawezesha jamii. Tuzo hizi ni kielelezo cha kujitolea kwa benki hiyo kwa uvumbuzi, uwazi, na kuridhisha wateja wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akionesha Moja ya tuzo waliyoshinda wakati akizungumza na waandishi wa habari kutangaza mafanikio ya benki kwa Mwaka 2024 kupitia tuzo mbalimbali 11 walizipata. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), pamoja na baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa benki hiyo, wakionesha kwa waandishi wa habari, tuzo mbalimbali 11 ambazo benki hiyo imeshinda kwa mwaka 2024, alipokutana nao, jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Monday, December 2, 2024

Benki ya Absa Tanzania yang'ara tuzo za Chaguo la Walaji

  

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora rafiki za Mikopo nchini Tanzania kwa Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Sengati Giattas, wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya Benki Bora inayopendwa Zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kushoto) akionesha tuzo ya Benki Bora inayopendwa zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser na Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Sengati Giattas (katikati), wakionesha tuzo za Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora rafiki za Mikopo nchini Tanzania na Benki Bora inayopendwa zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika, mara baada ya kukabidhiwa, wakati wa hafla ya kila mwaka ya Tuzo za Chaguo la Walaji, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Share:

Saturday, November 30, 2024

Benki ya Absa Tanzania yashinda tuzo ya uandaaji bora wa taarifa za fedha

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri (wa pili kulia), akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA. Pius Maneno.

BENKI ya Absa Tanzania imeibuka kidedea kwa kuibuka na ushindi wa kwanza wa Uandaaji Bora wa Taarifa za Fedha kwa Mwaka 2023 katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati wa tuzo za kila mwaka zinazoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo za mwaka 2023 zilishuhudia mchuano mkali ukihusisha washiriki 86 kutoka katika vitengo tofauti waliokidhi vigezo vilivyowekwa na NBAA ambapo washindi wake walikabidhiwa tuzo za na mgeni rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri.

Akizungumza muda mfupi baada ya kupokea tuzo hiyo, Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Muhsin Kaye alisema ushindi huo unaonesha ni kwa jinsi gani benki yao imebobea na kuwa na uzoefu, pamoja na watu wenye ujuzi wa kutosha katika uandaaji wa taarifa hizo.

“Ushindi huu ni ishara ya uwajibikaji sisi kama benki lakini pia uadilifu na uwazi katika uwasilishaji wa taarifa zetu, natoa ahadi kwa wateja wetu na kwa watanzania kuwa tutaendelea kujitahidi kuandaa taarifa sambamba na vigezo na kanuzi zinazohitajika na ni fahari kwetu sisi benki lakini ni fahari pia kwa wateja wetu wote.

“Ningependa kuishukuru Bodi ya NBAA kwa kuweka chachu ya uandaaji wa taarifa za kifedha kwa kuzingatia vigezo vilivyo sahihi kabisa, sisi kama benki tumefarijika kupata tuzo hii ikiwa ni muendelezo kwani tumeshapata tuzo hii miaka kadhaa iliyopita”, alisema Bw. Kaye.

Pamoja na hayo alisema, ushindi huo unaenda sambamba na lengo kuu la benki hiyo ambalo ni Kuiwezesha Afrika na Tanzania ya Kesho Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, huku ikitiwa nguvu na ahadi ya chapa isemayo, ‘Story yako Ina Thamani.

“Sisi kama Absa Tanzania tunaamini ushindi huu utaendelea kuongeza ari na hamasa zaidi kwa benki yetu kufanya vizuri zaidi katika kuziwesha Story za mafanikio ya wateja wetu na watanzania kwa ujumla”, alisema Bw. Kaye
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno (wa pili kushoto) akimpongeza Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye, mara baada ya benki hiyo kutangazwa mshindi wa kwanza kwanza wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri.
Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye (kulia), akipozi kwa picha ya kumbukumbu na pamoja na wawakilishi wa taasisi zilizoibuka na ushindi wa kwanza katika vitengo mbalimbali wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa tuzo a Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha zinazoandaiwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), jijini Dar es Salaam jana. Wengine katika picha ni mgei rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA. Pius Maneno.
Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha (wa pili kushoto ), Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi, Bw. Heristraton Genesis (kushoto), Mdhibiti wa Masuala ya Fedha, Muhsini Kaye na Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi, wakionesha tuzo ya Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), muda mfupi baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive