A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, February 16, 2026

Akiba Commercial Bank Plc Washirikiana na Vyombo vya Habari Kueneza Elimu ya Kifedha


Dar es Salaam, Tanzania; 16 Februari 2026 – Akiba Commercial Bank Plc (ACB) imeendelea kuimarisha ushirikiano wake na wadau wa vyombo vya habari kama sehemu ya juhudi zake za kuendeleza Elimu ya Fedha na kukuza huduma jumuishi za kifedha. 
Kwa kutambua mchango wa vyombo vya habari kama daraja muhimu kati ya taasisi za kifedha na umma, Benki inathamini na kutambua umuhimu  wa vyombo vya habari  katika kueneza ujumbe wa elimu ya fedha. Kupitia magazeti, runinga, redio na majukwaa ya kidijitali, vyombo vya habari vina uwezo wa kufikia hadhira mbalimbali na kueneza Elimu ya Fedha na hivyo kuwezesha jamii 

 kufanya maamuzi sahihi ya maswala ya kifedha.
Akizungumza wakati wa kikao na vyombo mbali mbali  vya  habari, Dora Saria, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, alisisitiza kuwa elimu ya fedha ni kipaumbele cha kimkakati kinacholenga.


 kuiwezesha jamii kuwa na uelewa wa maswala ya  akiba, ukopaji na uwajibikaji, huduma za kifedha za kidijitali, fursa za uwekezaji na mbinu bora za usimamizi wa fedha. Aliongeza kuwa kwa kukuza utoaji wa Elimu za Fedha na kuhimiza matumizi makini ya huduma za kibenki jamii itaweza kunufaika kiuchumi na kimaendeleo.

Alibainisha zaidi kuwa kadiri taswira ya kifedha nchini Tanzania inavyobadilika, hasa kupitia  kuongezeka kwa matumizi ya kidijitali, umuhimu wa elimu ya kifedha unaongezeka sambamba na mabadiliko hayo na hivyo kupelekea kuongezeka kwa juhudi na kipaumbele cha  kuelemisha jamii katika uelewa wa Elimu ya Fedha.


Kupitia mkutano huo, Benki pia ilishirikisha vyombo vya habari vipaumbele vyake vya kimkakati kwa mwaka 2026, kwa kuainisha  ukuzaji na upanuzi wa huduma za Kidijitali kwa ajili ya kuleta ufanisi  na  kuimarisha uzoefu wa wateja na viwango vya uridhikaji katika utoaji huduma.
Akiba Commercial Bank Plc itaendelea  kushirikiana kwa karibu na wadau wa vyombo vya habari ili kuimarisha uwazi, kujenga imani ya umma katika sekta ya kifedha na kutoa ya elimu ya kifedha nchini.


Kuhusu Akiba Commercial Bank Plc (ACB)
Akiba Commercial Bank Plc ni benki ya kibiashara inayolenga  kuhudumia watu kutoka makundi  mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wateja binafsi, SMEs,Makampuni makubwa  na taasisi za Serikali, ikizingatia  uwezeshaji wa tabaka la wajasiriamali (SMEs) ili kukuza  biashara, ajira na maendeleo jumuishi.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive