A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, August 27, 2024

ORYX GAS TANZANIA YAMTUA MZIGO WA KUNI NA MKAA MAMA NA BABA LISHE MKOANI MBEYA


MAMA na BABA LISHE MKOANI mbeya wameingia Kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta mpushi bora anaeweza  kutumia gesi ya Kampuni ya Oryx Gas huku  lengo la mashindano hayo ni kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia  kama ambavyo Rais Dk.Samia amedhamiria kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania iwe inatumia nishati hiyo.
Akizungumza na wana habari mkoani hapa leo Agosti 27,2024 jijini Mbeya , Meneja Miradi ya Nishati Safi kutoka Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba amesema mashindano hayo yanatija kubwa kwa Mama Lishe na Baba Lishe kwani wanatambua kundi hilo ndilo linaloathirika kiafya kutokana na kutumia kuni na mkaa kwa muda mrefu.

"Mama baba Lishe anakaa muda mrefu anapokua anapopika kwa kutumia  mkaa kwani  tunaambiwa wananchi wengi wa Tanzania wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na matatizo ya kupumua au matatizo ambayo yanatokana na madhara ya kuni na mkaa.

"Sasa katika kundi hilo tunaweza kusema Mama na Baba Lishe ndio waathirika wakubwa , hivyo ni jamii ambayo sasa hivi sisi Oryx tunamkakati wa kuhamasisha iachane na matumizi ya Kuni na mkaa. na kuni  na mkaa kwasababu wao ndio wanakaa jikoni muda mrefu katika kupika kila siku ndani ya siku 365,"amesema Ndomba.

Amesisitiza kwa hiyo Mama Lishe na Baba Lishe waanze kubadilika na kuanza kutumia nishati safi hivyo kutawasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya na kuokoa maisha yao, mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx kunalenga kuliepusha kundi hilo dhidi ya madhara yanayotokana na matumizi  ya kuni na mkaa.
"Lengo la mashindano haya ni katika muendelezo  ambao Oryx tumeuanza muda mrefu wa kuhamasisha na kusaidia kuhakikisha  matumizi ya nishati safi ya kupikia katika mapishi.


Kwa hiyo ujumbe wetu kwa watu watumie gesi katika kupika mapishi.Tunaamini nishati safi ya kupikia ni suluhisho la changamoto nyingi hasa za kiafya,kimazingira na kiuchumi,"amefafanua.
Share:

Thursday, August 15, 2024

TCB YAKUTANA NA SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA KUJADILI NAMNA BORA YA KUKUZA SEKTA YA FEDHA.

Katika jitihada za kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi za kifedha na mihimili ya Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw. Adam Mihayo, amemtembelea na kuzungumza na Spika wa Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Tulia Ackson.  

Bw. Mihayo ameambatana na Mkurugenzi wa Biashara za Wateja Wadogo na wa Kati wa benki hiyo Bi. Lilian Mtali, katika ziara hiyo ambayo inafungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya Benki ya TCB na Bunge la Tanzania katika kuwainua wajasiriamali wadogo na wa kati nchini.  

Mazungumzo na kiongozi huyo wa Bunge linaloundwa na wabunge 393 kutoka majimbo 239 yamejikita katika masuala nyeti yanayohusu majimbo mbalimbali katika jitihada za kuendelea kuwainua wajasiriamali wadogo na wa kati. 

Wakitambua mchango mkubwa wa kundi hili katika ukuaji uchumi na uzalishaji wa ajira mpya, mazungumzo yao yamejikita katika mpango wa utoaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali. Miradi hii itasaidia kukuza na kuchochea mazingira ya biashara kwa wajasiriamali pamoja na biashara zao. 

“Lengo letu sio kutoa jibu moja kwa nchi nzima. Huwezi kuwa na suluhisho moja kwa watu wote, ndiyo maana ni muhimu kuwasikiliza wadau wengi iwezekanavyo. Njia hii itatusaidia kutoa majibu yatakayokidhi mahitaji ya wajasiriamali kulingana maeneo wanayoishi hata wale walioko vijijini,” amesema Bw. Mihayo. 

Kwa upande wake, Mheshimiwa Tulia Ackson amebainisha umuhimu wa ushirikiano huo na kusisitiza wajibu wa Bunge katika kutunga sera zinazowezesha maendeleo ya wajasiriamali na kuhakikisha kwamba biashara zao zinapata rasilimali zinazohitajika ili kukua. “Maendeleo ya wajasiriamali ni muhimu kwa ukuaji uchumi wa taifa letu, kupitia ushirikiano huu na Benki ya TCB, tunaweza kutengeneza mazingira yatakayowezesha ukuaji wa biashara,“ amesema. 

Kikao hicho kimehitimishwa kwa azimio la ushirikiano wa pamoja na kuendelea kubuni nyanja mbalimbali za ushirikiano lengo likiwa kuinua sekta ya wajasiriamali.




Share:

ZAIDI YA WANAHISA 5000 WA MWANGA HAKIKA BANK WASHIRIKI MKUTANO MKUU WA NNE WA WANAHISA.

Mwenyekiti  wa Bodi ya  Wakurugenzi ya Mwanga Hakika Benki, Mhandisi Rithuan Mringo (watatu kushoto), akizungumza na wanahisa wa benki hiyo wakati wa Hafla ya Mkutano Mkuu wa nne wa wanahisa wa Benki hiyo uliyofanyika Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Jagjit Singh, Makamo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mwanga Hakika benki  Mhandisi Raymond Thadeus , Pamoja na viongozi wengine wa bodi hiyo.
Makamo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mwanga Hakika benki  Mhandisi Raymond Thadeus (wapili kushoto), akizungumza na wanahisa wa benki hiyo wakati wa Hafla ya Mkutano Mkuu wa nne wa wanahisa wa Benki hiyo uliyofanyika Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Jagjit Singh, Mwenyekiti  wa Bodi ya  Wakurugenzi ya Mwanga Hakika Benki, Mhandisi Rithuan Mringo Pamoja na viongozi wengine wa bodi hiyo.
Wanahisa wa Mwanga Hakika Bank wakiwa katika usahili kwaajili ya kushiriki Mkutano huo.
Wanahisa wa Mwanga Hakika Bank wakifuatilia Mkutano huo.


Benki ya Mwanga Hakika Imefanya mkutano mkuu wa nne na wanahisa wa benki hiyo yaani AGM (Annual General Meeting) wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro.
Mkutano huu una lengo la kutimiza matakwa ya serikali inavyoagiza kila kampuni kufanya mkutano mkuu na wanahisa wao kila mwaka.


Akizungumza wakati ,mkutano huo  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi  wa Mwanga Hakika Benki Mhandisi Ruthuan Mringo ameeleza kuwa mkutano huo ulikuwa na lengo la kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri  yaliyopo baina ya wanahisa na benki yao, ili kuwataarifu wanahisa  kuhusu benki ilipoanza ilipo sasa na mwendelezo wake ili kuweza kupata taarifa kamili na Ili wanahisa hao waweze kutathmini maendeleo ya benki hiyo na kubaini kama Kuna changamoto ziweze kutatuliwa. 

 Pia wanahisa  wanayo nafasi kubwa ya kutoa ushauri juu ya maswala ya kimaendeleo yatakayo ikuza benki hiyo ili iendelee kuwa imaara siku hadi siku.


Mkutano huu ni mkutano wa nne na wanahisa wa benki ya Mwanga Hakika, ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka  (2021) na kuhudhuriwa na wanahisa mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha uhusiano wao na wanahisa wa benki hiyo. Amesema Mringo.


Mbali na hayo, benki ya Mwanga Hakika imekuwa ni desturi yetu kufanya mkutano huo wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro kwasababu benki hiyo ch

Benki hiyo imeendelea kuimarika siku hadi siku na kwamba tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020 kumekuwepo ongezeko la amana za wateja kutoka Sh80.06 bilioni kwa mwaka 2022 hadi kufikia Sh142.19 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 78.

Aidha amesema ukuaji wa mikopo kwa wateja umeongezeka kutoka Sh80.69 bilioni hadi kufikia Sh131.44 bilioni.

"Ukuaji huu unaonyesha uwezo wetu wa kusaidia wateja wetu kufikia malengo yao ya kifedhabkwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu,"amesema Mringo 

Amesema jumla ya mali za benki hiyo zimeongezeka na kufikia Sh208.93 bilioni, ikilinganishwa na Sh116.95 bilioni mwaka 2022 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 79.

"Mapato yetu ya Benki yamefikia Sh20.06 bilioni kutoka Sh 13 .41 bilioni mwaka 2022, ongezeko la asilimia 50 , ukuaji huu unatokana na juhudi zetu za kuboresha huduma na kuongeza Wigo kwa wateja wetu,"amesema Mringo
Share:

Monday, August 5, 2024

USAID Technical Adviser visits beneficiaries of USAID Afya Yangu Southern and USAID Kizazi Hodari Southern projects.

The United States Agency for International Development (USAID) Technical Adviser Sarah Dastur pictured with some pupils of the JJ Mungai Primary in Iringa who are beneficiaries of the USAID Kizazi Hodari (Brave Generation) Southern Zone Project when she made a visit to inspect the project beneficiaries over the weekend.

Iringa Monday 5 August 2024 - The United States Agency for International Development (USAID) Technical Adviser Sarah Dastur conducted a joint visit to the USAID Afya Yangu (My Health) Southern and USAID Kizazi Hodari (Brave Generation) Southern Zone projects in Iringa. This visit involved representatives from USAID Tanzania and Washington. The visit assessed and supported ongoing Orphans and Vulnerable and Children (OVC) and pediatric HIV/TB activities, showcasing collaborative efforts between the projects to improve health outcomes in the region. The two projects are both implemented by Deloitte Consulting Limited aiming at improving the health status of the thriving youth, children and communities.

The USAID Technical Adviser Sarah Dastur visited JJ Mungai Primary School within Iringa Municipal, Isakalilo center which cares for children living with HIV and Tosamaganga hospital which has been provided care and counselling for people living with HIV.

During the visit, beneficiaries of the projects commented USAID for coming up with the projects that helped Tanzanians especially low-income earners saying that the projects has brought back smiles to them.

One of the project beneficiaries, Omary Juma (not his real name) who has been diagnosed with HIV and burdened by financial hardships said the project has really helped to bring back his smile. ‘My health has well improved through this project comprehensive support which includes health monitoring and education about reproductive health and HIV/Aids’, said Juma.

He added, ‘The project has helped me a lot. I learned most things from my community care workers and that has changed my life. I now have hopes with my life and I can now accomplish my dreams. I feel happy and courageous.

Speaking after visiting the beneficiaries, the USAID Technical Adviser Sarah Dastur said ‘Our commitments are aligned with the Government of Tanzania strategic priorities which involves close collaboration with Ministry of Health, Ministry of Community Development, Gender, Women and Special Groups and the President’s Office-Regional Administration and Local Government (PO-RALG)’.
Dr Stella Mtera (left) who is the CTC in charge of Tosamaganga Hospital in Iringa, listens to the United States Agency for International Development (USAID) Technical Adviser Sarah Dastur when she made a visit to inspect beneficiaries of the USAID Afya Yangu (My Health) Southern Project over the weekend.
Share:

Sunday, August 4, 2024

Benki ya DCB yaunga mkono jitihada za serikali ujenzi wa Reli ya SGR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, akihutubia mkoani humo jana, katika hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa huo kabla hawajaondoka Kwa treni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na Benki ya Biashara ya DCB kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na utalii kupitia Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.

Katika kuunga mkono juhudi zilizofanywa na serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR pamoja na kukuza utalii kupitia Royal Tour, Benki ya Biashara ya DCB imedhamini safari ya walimu zaidi ya 1000 kutumia treni ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kisha Mikumi ili kukuza utalii wa ndani na kujifunza mambo yatakayowasaidia wanafunzi wao wawapo madarasani.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga walimu hao kutoka Jiji la Dar es Salaam, katika Stesheni ya SGR, jijini humo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema taasisi yao imeshirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kuwapa nafasi walimu hao kutembelea mbuga za wanyama ya Mikumi ili kujionea vivutio vya utalii vitakavyowasaidia kuwafundisha wanafunzi wa mashuleni.

Alisema DCB inamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambalo ndiko wanakotoka walimu hao hivyo akawashauri kutumia huduma zilizoboreshwa za benki hiyo kama vile kuweka amana, bima mbalimbali na mikopo yenye masharti nafuu ili kuboresha maisha yao na kuacha kuangukia katika taasisi zinazotoa mikopo inayowaumiza na yenye masharti magumu.

Naye Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Bw. Ramadhan Mganga alisema DCB ndio mkombozi halisi wa watanzania kwani wanazo huduma na bidhaa tofauti zinazokidhi mahitaji ya kibenki ya watanzania hivyo kutoa hamasa kwa walimu hao na kwa watanzania kwa ujumla kuchangamkia huduma hizo.

Aidha alisema ili kufanikisha safari hiyo wamedhamini mabasi 30 yatakayowasafirisha walimu hao kutoka Morogoro kwenda Mikumi ikiwa pia ni kutambua mchango wa walimu hao katika maendeleo ya benki yao.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila aliipongeza DCB Kwa kufanikisha safari hiyo ya walimu akisema ofisi yake itaendelea kuandaa safari kwa makundi mengine ikiwa ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuitangaza treni ya SGR.

Ziara hii sio tu itaongeza maarifa kwa walimu kupitia ziara ya Mikumi, bali pia itaongeza chachu ya kampeni inayoendelea ya Royal Tour,”alisema.

Benki ya Biashara ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikitokana na wito wa Rais wa awamu ya tatu, Hayati, William Benjamin Mkapa, kufuatia kilio cha mitaji cha wananchi wenye kipato cha chini na cha kati wa Jiji la Dar es Salaam kukosa mikopo katika benki nyingi za kibiashara kwa kutokidhi vigezo vilivyokuwa vikiweka na benki hizo.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Bw. Ramadhan Mganga akizungumza kuhusu udhamini wa benki hiyo Kwa ziara ya walimu 1000 wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ziara yao kwenda Mikumi kwa kutumia treni ya SGR kutokea mkoani humo jana. Benki ya imedhamini mabasi 30 Ili kusafirisha walimu hao kutoka Morogoro kuelekea Mikumi Ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na utalii kupitia Royal Tour.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila (katikati), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw. Sabasaba Moshi mkoani humo jana, wakati wa hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa huo kabla hawajaondoka katika stesheni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na DCB kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila, mkoani humo jana, wakati wa hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa wa Dar es Salaam, kabla hawajaondoka kwa treni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na Benki ya Biashara ya DCB ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.
Baadhi ya walimu kutoka jijini Dar es Salaam wakiwasili kwa treni ya SGR mjini Morogoro jana, wakiwa safarini kuelekea katika mbuga za wanyama ya Mikumi. Benki ya Biashara ya DCB ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour imedhamini safari hiyo Kwa kutoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi mbugani huko kutoka Morogoro.
Share:

Saturday, August 3, 2024

TCB YAINGIA MKATABA WA MAKUBALIANO NA ZEEA KUWEZESHA MIKOPO VIKUNDI MAALUM

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Mihayo (Kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kusaini mikataba wa makubaliano (MOU) na wakala wa uwekezaji wananchi kiuchumi Zanzibar (ZEEA) unsolenga kuanzisha mpango maalum wa kutoa mikopo  itakayonufaisha makundi maalum, hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya TCB jijini Dar es Salaam. wengine pichani ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na uwekezaji Zanzibar Bi. Mariyam Abdallah, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa uwekezaji wananchi kiuchumi Zanzibar (ZEEA) Juma Burhan Mohamed.

Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa uwekezaji wananchi kiuchumi Zanzibar (ZEEA) Juma Burhan Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kusaini mikataba wa makubaliano (MOU) na Benki ya Biashara Tanzania TCB unaolenga kuanzisha mpango maalum wa kutoa mikopo  itakayonufaisha makundi maalum, hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya TCB jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na uwekezaji Zanzibar Bi. Mariyam Abdallah (katikati), akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mikataba hiyo.

Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidigital na Ubunifu, Jesse Jackson (kulia), akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mikataba hiyo.


 
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) leo imesaini mkataba wa makubaliano (MOU) naWakala wa serikali wa uwezeshaji wananchi kiuchumi zanzibar ( ZEEA) Makubaliano haya ya kimkakati yanalenga kuanzisha mpango maalum wa mikopo utakaonufaisha makundi maalum wakiwemo wanawake na vijana wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi visiwani Zanzibar. Mpango huu unakusudia kuchochea ukuaji wa biashara, ongezeko la ajira, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Akishuhudia kusainiwa kwa hati hizo jijini Dar es salaam Katibu mkuu ofisi ya Raisi kazi uchumi na Uwekezaji zanzibar Mariam amesema tayari shilingi bilioni 2 zimeshakusanywa na halmashauri visiwani humo ili kuanza uwezeshaji akiitaka benki ya TCB kuhakikisha inafanya tathmini ya mikopo wanayotoa kwa makundi hayo ili ziweze kurejeshwa kwa wakati na wengine waweze kukopa .

Ameeleza kuwa mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali,kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao. Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha
uchumi wa ndani, kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupambana na ukosefu wa ajira na kuleta maendeleo na kuwa Kupata fursa ya mikopo ni muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa biashara
ndogondogo na za kati



Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TCB ADAM MIHAYO amesema Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla na kwamba Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha
uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla. 

Amesema  mkataba huo utawezesha  kutoa mikopo nafuu kwa makundikiasi cha shilingi milioni 30 kwa kikundi, huku wakipewa muda miezi 24 sawa na
miaka miwili Kwa kutoa mikopo nafuu
kwa makundi hayo, TCB na ZEEA watawasaidia wajasiriamali kupanua biashara zao, kutengeneza fursa mpya za ajira, na hivyo kupunguza uhaba wa ajira.


Mpango huu pia utazisaidia biashara kujiendesha, kukabiliana na mfumuko wa bei, pamoja na kuwekeza katika vitendea kazi, na kuzipa ustahimilivu,Tuna furaha kushirikiana na ZEEA kuwainua wajasiriamali wanawake, vijana na makundi mengine maalum yaliyomo visiwani Zanzibar,” alisema Adam Mihayo,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB. 




Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA Juma Burhan Mohamed amesema wanalenga kuipatia benki ya TCb kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ili waanze utoaji wa mikopo hiyo  na kwamba Mpango huu unaendana na lengo  la kuwezesha maendeleo ya kiuchumi kwa kujenga uchumi jumuishi Kwa
kuyawezesha makundi maalum, wanaziinua biashara binafsi, pamoja na kuimarisha mfumo mzima wa uchumi na kutengeneza mazingira imara ya
kiuchumi.” alisema 

Mbali na kuchangia maendeleo ya kiuchumi, makubaliano haya pia yanakusudia kuimarisha uchumi wa buluu visiwani Zanzibar. Kupitia mikopo hii itakayoinua biashara ndani katika sekta hii, TCB na ZEEA wanapigia chapuo eneo hili nyeti la
shughuli za kiuchumi lenye uwezo wa kuchangia maendeleo kwa kiasi kikubwa.


Mchango wa Benki ya TCB katika kuunga mkono jitihada za Serikali katik na kupokea maombi ya mkopo yanayofikia wastani wa Mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha biashara na uchumi



Share:

Friday, August 2, 2024

UINGEREZA KUENDELEA KUFADHILI MIRADI YA UKIMWI NCHINI

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki wenye umri mdogo wa Kampeni ya kupanda mlima kilimanjaro ya GGM Kili Challenge, Regina Enos Baraka (kulia), mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda na kushuka mlima huo, mjini Moshi, Kilimanjaro, hivi karibuni. Kampeni hiyo ya kila mwaka ina lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki. Regina anaishi katika Kituo cha Moyo wa Huruma cha Geita kilichoanzishwa kwa msaada kutoka Mfuko wa Kili Challenge.

Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi Ili kutimiza malengo ya Kimataifa ya muda wa kati na mrefu ili kuona hakuna maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vinavyohusiana na VVU .

Balozi Concar aliyasema hayo wakati wa mapokezi ya wapanda mlima Kilimanjaro 71 walikuwa wakishiriki Kampeni ya kila mwaka ya GGM Kili Challenge mjini Moshi, Kilimanjaro, inayoandaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kupambana na Ukimwi (TACAIDS)

Njia kuu ambayo Uingereza inafanya ni kuwa mmoja wachangiaji wakubwa wa Mfuko wa Kimataifa wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, kwa miaka mitatu kutoka 2024 hadi 2026, Uingereza itatoa pauni bilioni 1 kwa mfuko huo, ambao kwa jumla utatoa dola milioni 602 kwa Tanzania."

Nitoe pongezi kwa AngloGold Ashanti na Bodi ya Wadhamini ya Geita Gold Mining Limited Kilimanjaro Challenge dhidi ya HIV/AIDS pamoja na TACAIDS kwa kuifanya Kili Challenge kuwa tukio la kila mwaka la kupendeza likileta ujumbe wa nguvu kwa wanaoishi na VVU”, alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi ukutoka Geita Gold Mining, Mhandisi Nzuamkende alisema kampeni hiyo inayofanyika Kwa mwaka wa 22, inalenga kukusanya fedha kuchangia jitihada za Serikali ya Tanzania kufikia malengo ya sifuri tatu ( Maambukizi mapya Sifuri, Unyanyapaa Sifuri na vifo vinavyohusiana na UKIMWI Sifuri).

Tunapokusanyika hapa ili kusherehekea mafanikio yenu, ninatoa shukrani zangu za dhati kwa kila mmoja wenu kwa kukabiliana na hofu zenu, na kushinda mojawapo ya milima mirefu zaidi na yenye changamoto duniani."

Juhudi zenu, kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro na kwenye njia tambarare za baiskeli, hazijadhihirisha tu nguvu ya uamuzi na umoja lakini pia zimeleta athari kubwa katika dhamira yetu ya pamoja ya kupambana na VVU na UKIMWI, mmetuonyesha kwamba hakuna changamoto isiyoweza kuzuilika tunapokutana kwa sababu moja na kwa hilo, nawapongeza nyote”, alisema.

Aidha aliwashukuru wafadhili na washiriki wote kutokana na michango yao inayoendelea kufanikisha Kampeni hiyo hadi kuufanya Mfuko wa Kili Challenge Against HIV/AIDS Trust kuwa mfuko wa kimataifa, unaohusisha wapanda mlima na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela alisema Tanzania inafanya vizuri kueleka malengo ya kimataifa ya muda mrefu na wa kati ambayo ni kufikia 95 tatu kufikia mwaka 2025 ambazo kama tawimu za karibuni zinavyoonesha kuwa kuna watu milioni 1.7 wanaishi na VVU, hivyo 95 ya kwanza ni kuona watu hao wanatambuliwa na kujua hali zao ambapo sasa imefika asilimia 83, huku 95 ya pili ni wale wanaoishi na VVU watumie dawa za kufubaza makali ya ukimwi (ARV) ambapo Tanzania imevuka lengo kwa kufikisha asilimia 98 na 95 ya tatu wale wanaotumia ARV asilimia 95 wawe wamefubaza virusi, utafiti wa mwisho unaonyesha maambukizi mapya yakipungua.

Nao baadhi ya washiriki wenye umri mdogo waliopanda Mlima Kilimanjaro, Regina Baraka na Baraka Erasto, kutoka kituo cha Moyo wa Huruma cha mkoani Geita, kilichoanzishwa kupitia mfuko wa Kili Challenge walielezwa kufurahishwa kwa uzoefu walioupata Kwa mara ya kwanza wakipanda mlimani hivyo kutoa hamasa Kwa vijana wadogo wenye umri kama wao kujitokeza kushiriki katika Kampeni hiyo Ili kuweza kuleta mabadiliko kwa wenye VVU.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki wenye umri mdogo wa Kampeni ya kupanda mlima kilimanjaro ya GGM Kili Challenge, Baraka Erasto (kulia), mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda na kushuka mlima huo, mjini Moshi, Kilimanjaro, hivi karibuni. Kampeni hiyo ya kila mwaka ina lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki. anaishi katika Kituo cha Moyo wa Huruma cha Geita kilichoanzishwa kwa msaada kutoka Mfuko wa Kili Challenge.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akihutubia katika hafla ya kuwapokea wapanda mlima Kilimanjaro waliokuwa wakishiriki kampeni ya kila mwaka ya GGM Kili Challenge yenye lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi. Kampeni hiyo imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki zoezi hilo lilioanza Julai 19 kufikia tamati yake mjini humo hivi karibuni.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive