Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Uzalishaji Mbegu Bora za Miti na Vipando wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), SACC Caroline Malundo (katikati), akiwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Green Village Estate, Bwana Reeves Ngalemwa (kulia kwake), wakati akiwasili kijijini hapo akimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, CC Prof. Dos Santos Silayo, kuhitimisha kilele cha kampeni ya upandaji miti 1000 iliyokuwa na malengo ya kuhamasisha wakazi wa Green Village na maeneo jirani umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa njia ya upandaji miti. Mti hiyo 1000 ilipatikana kwa ufadhili wa TFS Ofisi ya Kinondoni. Kushoto kabisa ni mwakilishi kutoka Shirika la Watumishi Housing Investment (WHI), Bwana Valentine Arra wamiliki wa kijiji hicho.
Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Uzalishaji Mbegu Bora za Miti na Vipando wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), SACC Caroline Malundo (katikati), akielezea namna bora ya upandaji miti alipoenda kuhitimisha kilele cha kampeni ya upandaji miti 1000 iliyokuwa na malengo ya kuhamasisha wakazi wa Green Village na maeneo jirani umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa njia ya upandaji miti.
Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Uzalishaji Mbegu Bora za Miti na Vipando wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), SACC Caroline Malundo, akipanda miti kuhitimisha kilele cha kampeni ya upandaji miti 1000 iliyokuwa na malengo ya kuhamasisha wakazi wa Green Village na maeneo jirani umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa njia ya upandaji miti. Mti hiyo 1000 ilipatikana kwa ufadhili wa TFS Ofisi ya Kinondoni. Naibu Kamishna alimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, CC Prof. Dos Santos Silayo.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Mabwepande Colle Mohamed Senkondo, akipanda mti katika hafla ya kuhitimisha kampeni ya upandaji miti 1000 katika Kijiji cha Green Village Estate, Bunju Mabwepande, Kinondoni, Dar es Salaam hivi karibuni.
Kiongozi wa kiroho wa Kanisa la KKKT Mabwepande, Anna Mbaga, naye alipata heshima ya kupanda mti wa kumbukumbu katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Green Village Estate, Bwana Reeves Ngalemwa akizungumza katika hafla hiyo pamoja na mambo mengine alitoa taarifa ya maendeleo ya kijiji pamoja mkakati endelevu wa kampeni ya utunzaji wa mazingira kijijini hapo. Alisema tuzo licha ya tuzo iliyozinduliwa kushindanisha wanakijiji ili kumpata mtunza mazingira bora lakini mipango imo mbioni ya kuwa na tuzo yenye wigo mpana wa washiriki wake itakayowashirikisha watu kutoka nje ya kijiji.
Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Uzalishaji Mbegu Bora za Miti na Vipando wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), SACC Caroline Malundo akihutubia kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, CC Prof. Dos Santos Silayo katika hafla hiyo kuhitimisha kampeni ya upandaji miti 1000 iliyopatikana kwa uwezeshaji wa TFS. Katika hotuba yake, Naibu Kamishna alitoa hamasa kwa watanzania kuona umuhimu wa kupanda miti kwani takwimu zinaonyesha kuna uharibifu wa misitu wa takribani hekta 412,000 kwa mwaka huu unaosababishwa na shughuli za kibinadamu.
Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Uzalishaji Mbegu Bora za Miti na Vipando wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), SACC Caroline Malundo (wa pili kulia), akipokea Tuzo ya Mazingira ya Green Village Estate Mazingira Award 2023 kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, CC Prof. Dos Santos Silayo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira, Afya na Miundombinu ya kijiji hicho, Dk. Rehema Simba (wa tatu kushoto), wakati akizindua rasmi tuzo hiyo itakayotolewa kila mwaka. Mshindi wa tuzo hiyo atakapatikana kutokana na vigezo vilivyowekwa na kamati hiyo. Lengo ikiwa ni kuhamasisha wanakijiji na wakazi wa maeneo ya jirani umuhimu wa kutunza mazingira kwa njia ya kupanda miti.
Katibu wa Kamati ya Mazingira, Afya na Miundombinu wa Green Village Estate, Bwana Andrew Tarimo (kulia), akimkaribisha Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Mabwepande, OCD Colle Mohammed Senkondo, ambapo yeye pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mabwepande, ASP Goodluck Lema (wa pili kushoto), wakiwa baadhi ya wageni maalumu walioalikwa katika hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni, Bi. Tumaini Masako, mjumbe wa kamati ya mazingira, Mwenyekiti wa Kijiji, Bwana Reeves Ngalemwa na Mjumbe wa Kamati ya Burudani, Bwana Swalehe Kweka (wa pili kulia).
Ni shangwe tu….Mwenyekiti wa Green Village Estate, Bwana Reeves Ngalemwa (kulia), Katibu wa Kijiji, Bwana Pantaleo Shoki (kushoto), wakimlaki Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Uzalishaji Mbegu Bora za Miti na Vipando wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), SACC Caroline Malundo mara baada ya kuwasili kuhitimisha kilele cha kampeni ya upandaji miti 1000 zoezi lililoratibiwa kwa ufanisi na Kamati ya Mazingira, Afya na Miundombinu ya kijiji hicho. Wa pili kulia ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Mabwepande, OCD Colle Mohammed Senkondo.
Timu ya ushindi! Wanakamati wa Kamati ya Mazingira, Afya na Mazingira chini ya uenyekiti wa Dk. Rehema Simba wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi, viongozi wa Green Vilage pamoja na baadhi ya wageni maalumu walioalikwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Green Village Estate pamoja na mwakilishi kutoka Watumishi Housing wakipozi mbele ya wapiga picha pamoja na mgeni rasmi na wageni wengine waalikwa mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment