A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, February 20, 2023

Wateja wa Benki ya Absa kununua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa kupitia mkopo wake ulioboreshwa

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed wafurahi katika hafla ya utiaji saini makubaliano yatakayowawezesha wateja wa Absa kununua nyumba za NHC kwa mkopo. Ilikuwa ni katika hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Absa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed (kulia), wakiangalia wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (katikati) akisaini makubaliano yatakayowawezesha wateja wa Benki ya Absa kununua nyumba za NHC kwa mkopo. Ilikuwa ni wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Absa jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed (kulia), akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu (kulia), wakiangalia wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed akisaini makubaliano yatakayowawezesha wateja wa benki hiyo kununua nyumba za NHC kwa mkopo kutoka benki hiyo. Ilikuwa ni wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Absa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya Absa pamoja na wahudhuriaji wengine wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mkopo wa nyumba ulioboreshwa wa Benki ya Absa katika hafla iliyofanyika pamoja na utiaji saini makubaliano yatakayowezesha wateja wa Absa kununua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mkopo.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive