Friday, January 27, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KATA YA GOWEKO
Thursday, January 26, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 150 YA CEMENT KUBORESHA MADARASA
Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala Edward Mwoleka, (wa tatu kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilamba iliyopo Mbagala Charambe iliyotolewa na TCB kwa ajili ya kufanya maboresho ya madarasa ya shule hiyo. Kutoka kulia ni Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta, Diwani wa Kata ya Charambe Twahil Shabani, pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga.
Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala, Edward Mwoleka, (wa tatu kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga, iliyotolewa na TCB kwa ajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya shule ya msingi Kilamba iliyopo Charambe. Kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Leah Masaba, Diwani wa Kata ya Charambe, Twahil Shabani pamoja na Mjumbe wa shule.
Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Gloria Mutta (wa tatu kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement, kwa Mtendaji kata ya Charambe, Theodora Malata iliyotolewa na TCB kwa ajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya Shule ya Msingi Kilamba iliyopo Charambe.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilamba, Leah Masaba, akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mifuko 150 ya Cement iliyotolewa na TCB kwa ajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya shule hiyo.
Mtendaji kaya ya Charambe, Theodora Malata akitoa shukrani kwa niaba ya shule ya Msingi Kilamba kwa uongozi wa TCB baada ya kupokea msaada wa mifuko 150 ya Cement iliyotolewa na TCB kwa ajili ya kufanyia maboresho ya madarasa ya shule hiyo iliyopo Charambe jijini Dar es Salaam.
Sunday, January 22, 2023
MATUKIO YA MAUAJI WILAYA YA MANYONI WANANCHI WAMLILIA RC SERUKAMBA AWASAIDIE
Thursday, January 19, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKI UZINDUZI UJENZI WA RELI YA KISASA KUTOKA TABORA HADI ISAKA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Phillip Mpango akisikiliza maelezo ya ushiriki wa benki ya Tanzania Commercial Bank TCB katika ujenzi wa Reli ya kisasa(SGR) kutoka kwa Mkurugenzi wa wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adolphina William wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adolphina William wakati (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Phillip Mpango.Tanzania Commercial Bank (TCB) Imeendelea kushiriki zoezi endelevu la ujenzi wa kipande cha nne cha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165.
TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165..
TCB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali na kuhakikisha kuwa inatoa huduma stahiki kila kona ya Tanzania na kuhakikisha inaunga mkono kwa asilimia zote maendeleo ya nchi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa wateja wakubwa wa Tanzania Commercial Bank Adolphina William wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya nne leo Mkoani Shinyanga.
Adolphina amesema, Tanzania Commercial Bank ni Benki ya Wananchi na wamejitoa na wameshiriki kwa hatua kubwa katika kuhakikisha shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanikisha mradi wa SGR kwa mafanikio makubwa.
“Tanzania commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC wanafanya kazi nzuri sana kuhakikisha wanaunganisha wananchi kwa njia ya usafiri wa reli hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio makubwa hapa nchini.
Adolphina ameeleza kuwa kwa Sasa Tanzania Commercial Bank ina matawi kila pembe ya Tanzania hivyo imejipanga vyema kutoa huduma kwa watanzania pamoja na wageni kutoka nje hivyo amewasihi watanzania ambao bado hawajafungua akaunti na benki ya TCB wakafungue akaunti ili kunufaika na huduma zinazopatikana katika Benki hiyo.