Zaidi ya wakazi 500 wa Bagamoyo wenye matatizo mbalimbali ya macho wanatarajia kupata matibabu bure katika kambi maalum ya matibabu ya macho Bure katika hospital ya Wilaya Bagamoyo, chini ya ufadhili wa Lions Club ya Dar es Salaam-Mzizima.
Kambi maalum ya kupima na kufanya upasuaji wa macho Bure imeanza jana katika hospitali ya wilaya bagamoyo na mpaka sasa zaidi ya wakazi 300 wamejitokeza kupima na 50 kati yao wamefanyiwa upasuaji.
“Tunashukuru sana watu wote waliofanyiwa upasuaji sasa hivi wanaona vizuri. Kambi hii ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa Bagamoyo, hasa ukizingatia kuwa karibu asilimia 50 ya watu wa Bagamoyo wana matatizo ya mtoto wa jicho,” amesema Mkurugenzi wa Wilaya Bagamoyo, Bw. Shauri Selenda, wakati wa uzinduzi rasmi wa kambi ya zaidi watu
Imefadhiliwa na Lions Club ya Dar es Salaam- Mzizima
Zaidi ya 300 wakazi bagamoyo wamejitokeza kufanyiwa vipimo vya matatizo ya macho na 50 kati yao wamefanyiwa operation na sasa wanaona vizuri.
"Wakazi wengi wenye matatizo ya macho wanaendelea kujitokeza, na katika zooezi lengo letu ni kifanya upasuaji kwa watu zaidi ya 200...." amesema Mkurugenzi wa Wilaya Bagamoyo , Shauri Selenda, wakati ufungizi rasmi wa kambi ya siku 3 ya kutuo huduma bure ya upimaji wa macho na upasuaji kwa wakazi wilayani huyo.
Mkurugenzi huyo ameishukuru Club ya Lions- Mzizima kwa kufadhili utoaji ya huduma hiyo bure, na kuwataka wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano wa Lions Club mzizima, ili kuwakwamua watanzania wengi wanakabiliwa na matatizo ya macho—wilaya Bagamoyo na nchi nzima kwa ujumla.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo, ametoa wito kwa Taasisi ya Lions Club Mzizima, awamu ijayo huduma hiyo ipanuliwe hadi katika mashule ya sekondari na msingi, ili kuwasaidia “watoto wetu wenye matatizo ya macho"
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Bagamoyo, Bi. Kandi Lusingu, amesisitza kuwa awamu ijayo zoezi la upimaji wa macho liende sambamba na utoaji wa miwani kwa watu waliugulika kuwa na matatizo ya kuona, na kuongeza kuwa hatua hiyo itafanya zoezi hili kuwa na tija na manufaa kwa watu wenye matatizo hayo.
"Pia naunga mkono zooezi hili kufanyika mashuleni , kwani itasaidia sana kuboresha uwezo wa vijana wetu, kuongeza ufualu, na pia kuongeza nguvu kazi ambayo ni nguzo mihimu kwa maendeleo taifa letu,” amesema Bi. Lusingu.
Nae Raisi wa Lions Club Mzizima, Baruani Muslim "Katika zoezi hili, taasisi yetu inalenga kuwasaidia wakazi zaidi 500 wa Bagamoyo wenye matatizo mbalimbali ya macho.. mbali na macho, Lions Club tunasaidia jamii katika maeneo mbalimbali—upimaji wa kisukari, utunzaji wa mazingira na mengine mengi."
"Lions Club Mzizima itaendelea kushirikiana na serikali, katika wasaidia watanzania wenye matatizo mbalibali, lengo kuu likiwa ni kuboresha maisha ya watanzania na kulewezesha Taifa kupiga hatua kubwa za maendeleo.
Mmoja wa wanufaika wa kambi ya macho Bagamoyo, Omary Shukuru amesema ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi wanasikia huduma kama hizi za bure, na kuongeza kuwa “katika hali ya kawaidia huduma hizi zina gharama kubwa ambazo mwananchi wa kawaidia hawezi kumudu.”