A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Sunday, June 12, 2022

BENKI YA NBC YAPONGEZWA KWA HUDUMA BORA ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mh. Hemed Suleiman Abdulla (kulia) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Theobald Sabi (kushoto) walipokutana Zanzibar. Pamoja na mambo mengi, Mh. Abdulla ameipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kutoa huduma bora za kifedha kwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania bara na Taifa kwa ujumla hapa nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, MH. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi na Maofisa wengine kutoka benki hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Benki ya NBC kwa kuendelea kutoa huduma bora za kifedha kwa wananchi wa Zanzibar na taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Abdulla aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi kutoka Benki ya Taifa ya Biashara NBC alipokutana nao katika ofisi ya Spika mjini Unguja, mara baada ya viongozi hao kuhudhuria kikao cha Baraza la Wawakilishi wakiwa ni wageni wa Spika wa Zanzibar, Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid.

“Nawapongeza sana NBC kwa kuendelea kuwa mdau muhimu hapa Zanzibar na pia Tanzania bara kwa uwezeshaji wa kiuchumi kwa watu wa Zanzibar.

Endeleeni kuongeza wigo wa kutoa huduma kwa kuongeza matawi na mawakala ili muweze kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawaahidi kutoa ushirikiano na kuendelea kuweka mazingira bora ya kufanyia biashara” alisema.

Kwa upande wake Spika wa Zanzibar, Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid aliishukuru Benki ya NBC kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo akitolea mfano misaada mbalimbali kwa jamii ambayo benki hiyo imekuwa ikitoa kila mwaka.

Spika Zubeir alipongeza pia udhamini wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC katika ligi ya mpira wa miguu nchini, NBC Premier League kuwa ni wenye tija kwa taifa kwa kutoa vipato na kuibua vipaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Abdulla na Spika wa Zanzibar Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid kwa mkutano huo wenye lengo la kuboresha mahusiano ya pande zote ili kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hasa katika kukuza uchumi wa nchi yetu.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive