A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, January 24, 2022

WANANCHI WA KATAVI WAIPOKEA KWA SHANGWE TANZANIA COMMERCIAL BANK

 .com/img/a/

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mh. Mwamvua Mrindoko (kushoto),  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank (TCB) katika Manispaa ya Mpanda  mjini mkoani Katavi,  kulia ni  Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu  Meneja wa Tawi la Mpanda Julius Mlang'a  pamoja na maofisa wa kamati ya ulinzi ya mkoa..com/img/a/Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mh. Mwamvua Mrindoko wa  (kushoto),  akipokea kadi ya ATM kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB,  Sabasaba Moshingi, alipofungua akaunti alipoalikwa kuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank  lililofunguliwa katika Manispaa ya Mpanda  mjini mkoani Katavi jana  wengine pichani ni Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu  Meneja wa Tawi la Mpanda Julius Mlang'a  pamoja na maofisa wa wengite kutoka TCB

.com/img/a/

Tanzania Commercial Bank (TCB)  imezindua tawi jipya Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mpanda ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma za kibenki kwa wateja na Wananchi kwa ujumla.

Tawi hilo la kwanza kwa taasisi za fedha kuzinduliwa Mkoa Katavi Wilaya ya Mpanda, limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko .

 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi alisema huo ni mwendelezo wa Tanzania Commercial Bank katika kusogeza huduma kwa wateja wake.

 

Alisema tawi hilo jipya la Mpanda litarahisisha utoaji huduma za kibenki kwa wateja wake hali ambayo itapunguza mzunguko wa wananchi kuzifuata huduma za kibenki maeneo mengine ya mbali

Aliongeza kuwa Tanzania Commercial Bank (TCB) imezingatia shughuli za kiuchumi zinazoendeshwa Wilayani humo kwa  wafanyabiashar  wafugaji na wakulima wa na kufungua tawi hilo hivyo wateja hawatalazimika kwenda mjini kupata huduma za kibenki kama hapo awali

 

AlisemaTanzania Commercial Bank sio kwamba tu ni benki kubwa nchini, bali inatoa mchango mkubwa katika shughuli za kijamii  hasa kuinua elimu pamoja na Afya.

Kwa kuona umuhimu wa kusongeza huduma kwa wateja hasa maeneo ya vijijini Tanzania Commercial Bank (TCB) inaendelea kuwawezesha mawakala watakaosaidia kutoa huduma hizo jambo ambalo litasaidia kusogeza huduma kwa wateja wetu nchi mzima.

 

Aliongeza, kwa sasa Benki hiyo ina matawi  82 Mawakala tunao zaidi 3,800  mashine zakutolea pesa ATM zetu tunazojitegemea Kama TanzaniaCommercial Bank ni 84 lakini zile ATM ambazo tupo chini ya Umoja Switch ni zaidi ya 250.

 

Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank  Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko  ameupongeza uongozi wa Tanzania CVommercial Banki  kwa kuja kuwekeza katika  Mkoa huu na anaamini kwa wingi wa watu waliojitikeza katika tukio hili watakwenda kufungua akaunti.

 

Mrindoko pia ameipongeza  Tanzania Commercial  Banki (TCB)  kwa kufika Mkoani Katavi na kuwakaribisha kwani fursa zipo nyingi katika mkoa huo zikiwemo za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara pamoja na mazao mengine  ya kimkakati.

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliuhakikishia uongozi wa Tanzania Commercial  Banki (TCB)  kwamba Katavi ni mkoa unaokua kwa kasi sana kutokana na shughuli za uzalishaji na za kimaendeleo hivyo huduma ya  Tanzania Commercial Bank kwakfungua tawi hilo limekuja wakati muafaka

 

“Kuzinduliwa kwa Tawi la Tanzania Commercial Bank (TCB)  hapa Katavi maana yake ni kwamba huduma za kibenki zitapatikana kwa urahisi zaidi hivyo wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara wa Katavi jitokezeni kwa wingi wenu kuchangamkieni  fursa hii na kuja kufungua akaunti na kufanya miamala mengine kama kulipa kodi alisisitiza Mrindoko

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive