Monday, January 31, 2022
Dr. Ngozi Okonjo-Iweala, Director General of the World Trade Organization, Joins the Group of Thirty
Sunday, January 30, 2022
Benki ya DCB kupitia mfuko wake wa kuisaidia jamii wa DCB FOUNDATION wasaidia kampeni ya usafi wa mazingira Temeke.
DCB KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI
Monday, January 24, 2022
WANANCHI WA KATAVI WAIPOKEA KWA SHANGWE TANZANIA COMMERCIAL BANK
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mh. Mwamvua Mrindoko (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank (TCB) katika Manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi, kulia ni Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu Meneja wa Tawi la Mpanda Julius Mlang'a pamoja na maofisa wa kamati ya ulinzi ya mkoa.Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mh. Mwamvua Mrindoko wa (kushoto), akipokea kadi ya ATM kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB, Sabasaba Moshingi, alipofungua akaunti alipoalikwa kuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank lililofunguliwa katika Manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi jana wengine pichani ni Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu Meneja wa Tawi la Mpanda Julius Mlang'a pamoja na maofisa wa wengite kutoka TCB
Tanzania Commercial Bank (TCB) imezindua tawi jipya Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mpanda ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma za kibenki kwa wateja na Wananchi kwa ujumla.
Tawi hilo la kwanza kwa taasisi za fedha kuzinduliwa Mkoa Katavi Wilaya ya Mpanda, limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko .
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi alisema huo ni mwendelezo wa Tanzania Commercial Bank katika kusogeza huduma kwa wateja wake.
Alisema tawi hilo jipya la Mpanda litarahisisha utoaji huduma za kibenki kwa wateja wake hali ambayo itapunguza mzunguko wa wananchi kuzifuata huduma za kibenki maeneo mengine ya mbali
Aliongeza kuwa Tanzania Commercial Bank (TCB) imezingatia shughuli za kiuchumi zinazoendeshwa Wilayani humo kwa wafanyabiashar wafugaji na wakulima wa na kufungua tawi hilo hivyo wateja hawatalazimika kwenda mjini kupata huduma za kibenki kama hapo awali
AlisemaTanzania Commercial Bank sio kwamba tu ni benki kubwa nchini, bali inatoa mchango mkubwa katika shughuli za kijamii hasa kuinua elimu pamoja na Afya.
Kwa kuona umuhimu wa kusongeza huduma kwa wateja hasa maeneo ya vijijini Tanzania Commercial Bank (TCB) inaendelea kuwawezesha mawakala watakaosaidia kutoa huduma hizo jambo ambalo litasaidia kusogeza huduma kwa wateja wetu nchi mzima.
Aliongeza, kwa sasa Benki hiyo ina matawi 82 Mawakala tunao zaidi 3,800 mashine zakutolea pesa ATM zetu tunazojitegemea Kama TanzaniaCommercial Bank ni 84 lakini zile ATM ambazo tupo chini ya Umoja Switch ni zaidi ya 250.
Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko ameupongeza uongozi wa Tanzania CVommercial Banki kwa kuja kuwekeza katika Mkoa huu na anaamini kwa wingi wa watu waliojitikeza katika tukio hili watakwenda kufungua akaunti.
Mrindoko pia ameipongeza Tanzania Commercial Banki (TCB) kwa kufika Mkoani Katavi na kuwakaribisha kwani fursa zipo nyingi katika mkoa huo zikiwemo za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara pamoja na mazao mengine ya kimkakati.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliuhakikishia uongozi wa Tanzania Commercial Banki (TCB) kwamba Katavi ni mkoa unaokua kwa kasi sana kutokana na shughuli za uzalishaji na za kimaendeleo hivyo huduma ya Tanzania Commercial Bank kwakfungua tawi hilo limekuja wakati muafaka
“Kuzinduliwa kwa Tawi la Tanzania Commercial Bank (TCB) hapa Katavi maana yake ni kwamba huduma za kibenki zitapatikana kwa urahisi zaidi hivyo wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara wa Katavi jitokezeni kwa wingi wenu kuchangamkieni fursa hii na kuja kufungua akaunti na kufanya miamala mengine kama kulipa kodi alisisitiza Mrindoko
Wednesday, January 19, 2022
Tanzania Commercial Bank yakabidhi majengo ya kisasa shule ya msingi kitunga, wilaya ya muleba mkoani kagera
Monday, January 17, 2022
NAIBU KATIMU MKUU WIZARA YA NISHATI ATEMBELEA SOKO LA KARUME
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, ametembelea soko la Karume lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia Januari 16 jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika soko hilo, alikagua na kushuhudia athari mbalimbali zilizotokana na moto huo ambao umeathiri miundombinu mbalimbali ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kusababisha baadhi ya sehemu kukosa umeme.
Akizungumza mara baada ya kutembelea soko hilo Naibu Katibu Mkuu Mahimbali amesema kuwa kazi ya kuhakikisha huduma ya umeme inarejea katika Mikoa ya Ilala na Temeke inaendelea ambapo mafundi tayari wapo katika maeneo hayo.
Moto huo ulianza majira ya saa 9 usiku ambapo jitihada za kuuzima moto huo zilifanyika ili kudhibiti moto usienee katika makazi ya wananchi lakini kutokana na miundombinu ya soko hilo kazi ya kuzima ilikuwa ngumu na kusababisha na kuteketea kwa soko lote.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (katikati) akimsiliza Meneja wa Tanesco Kanda ya Mashariki Dar es Saalam na Pwani, Keneth Boimanda (kulia) wakati alipotembelea soko la Karume na kukagua miundombinu ya TANESCO iliyoathirika na moto huo, Januari 16, 2022.
Tuesday, January 4, 2022
Rais Samia Ateua watatu, Dk Baghayo Saqware ndani arejeshwa TIRA
Na Mwandishi Wetu
RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi tatu tofauti nchini.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, ilisema Rais amemteua Dk Baghayo Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).
Dk. Saqware ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), aliwahi kuongoza taasisi hiyo kwa mafanikio lakini aliondolewa na Rais wa Serikali ya awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli.
Baadhi ya mafanikio aliyoyapata ni kuongezeka kwa mapato ya Serikali kupitia tozo za kibima kutoka sh. Bilioni 10.1 mwaka 2015 hadi sh bilioni 12.1 mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 11;
Mafanikio mengine ni kuzuia ubadhirifu kwa kuimarisha mfumo wa kieletroniki wa TIRA MIS wenye kuzuia na kuhakiki bima zote za magari nchini. Hatua hii imesaidia kupunguza ubadhirifu na kuwalinda watumiaji wa huduma za bima ya magari na vyombo vingine vya moto.
Mafanikio mengine ni kupanua wigo wa utoaji huduma za bima kwa kuanzisha na kutekelezwa kwa kanuni za kusimamia huduma za bima kupitia mabenki (Bancassurance Regulations 2019) ambazo zilipitishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philipo Mpango wakati huo Machi 2019.
Kanuni hizi zimelenga kuongeza upatikaji wa huduma za bima nchini kwa urahisi na ufanisi kupitia mtandao wa matawi ya benki Tanzania. Utekelezaji huu ulileta uhasama baina ya Kamishna wa Bima na madalali wa bima (Insurance Brokers) ambao waliamini uanzishwaji wa kanuni hizi zinalengo la kuua biashara ya udalali, jambo ambalo si sahihi.
Kuondoa kero kwa wateja na wafanyabiashara ya bima ni moja ya mafanikio wakati ule baada ya kutekeleza kwa vitendo mabadiliko ya sheria namba 10 ya mwaka 2009 kifungu namba 72 kinachoelekeza ada za bima kulipwa moja kwa moja kwa kampuni ya bima bila kupitia kwa mtu wa kati (insurance intermediaries).
Mafanikio mengine ni kuthibiti utoroshwaji wa tozo za bima kwa kuanzisha utaratibu wa ithibati (“accreditation”) kwa makampuni na madalali wa nje ya nchi wanaofanya biashara ya bima mtawanyo na kampuni zilizosajiliwa nchini.
Mengine ni kuongeza uwezo wa kubakiza tozo nchini (Retention Level) kulinda wateja wa bima kwa mfumo bora wa malipo ya fidia, kulinda ajira za Watanzania, kuweka utaratibu wa kuratibu wataalamu bima nchini.
Mbali na Dk Saqware, Rais Samia pia amemteua Charles Itembe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalumu la Mauzo ya Nje (EPZA). Itembe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, Rais Samia pia amemteua Ernest Mchanga kuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC).
Mchanga ni Katibu Msaidizi, Fedha na Utawala, Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango. Uteuzi huo ulianza Januari mosi mwaka huu